CCM sasa wamtumia Warioba kuimaliza CHADEMA?

Huyu mzee ni wa kuonea huruma tu. Ila comments zake zinapaswa kuchukuliwa kwa msimamo chanya!! Hakuna cham kisafi kama bafaru!! Ni mawazo yake!!
 
Hapa my friend hujawa neutral kama unavyopenda uonekane.
You cant stand out kwa kusema you aint one of them.
hebu tuambie Warioba alipendekeza CHADEMA ifanye nini isiwe 'nguvu ya soda' anayo-claim? Na kwa nn ni 'nguvu ya soda'?
Kila anayejaribu kushauri, kuonya, kukemea baadhi ya mapungufu ya CHADEMA mtasema anatumiwa na CCM. Hivi kama mtu au chama unakipenda utakaa kimya tu na kukisifia hata kama unaona kinakoelekea siko? Sasa hivi Jaji Warioba anajaribu kuwa juu kidogo ya siasa za vyama. Jana alivikosoa vyama vyote ikiwemo CCM yake. Wewe umeyaona maoni haya ya CHADEMA tu. Kwa namna ulivyoleta, utaungwa mkono sana tu humu JF. Umeongea lugha ya wengi humu.
 
kushindana kwa sera. Sera zipi? Ninachojua ni kwamba chadema wamaekuwa tu wakosoaji bila kueleza ni kipi walichoandaa ambacho watawaletea wananchi iwapo wataingia madarakani. Ni kulia lia na kulalamika wakati kwenye majimbo wanayoyaongoza hali ni hoi bin taabani na wala huoni kama kuna kitu kinachoweza kuipambanua chadema na ccm na kuwapa watu matumaini kwamba chama hicho ni mbadala wa ccm.
si mlisema chama cha msimu!
Wacha moto uwake!
 
Hakuna mwana ccm mwenye mapenzi mema na chama cha upinzani.....labda kiwe ccm-b.
Just b'coz Warioba amesema ccm wa chllenges au sio kisafi, hakimfanyi yeye kuwa anayekitakia chama cha upinzani mema.
 
Ama Kweli Chadema mnaonesha ni jinsi gani heshima Huyo unaye mtukana na Sawa na baba yako na pia aliwahi kuwa kiongozi Wa nchi hii. Hivi nikweli hakuna alichokifanya alipokuwa madarakani? Au umezaliwa juzi hujuwi tulikotoka? Achani siasa za chuki

Hapa hatuangalii umri wa mtu bali busara zake,matamko na matendo yake.Ina maana kwa kuwa yeye ana umri kama wa baba/babu/bibi/mama zetu ndio tusimpe ukweli wake wakati anaongea vitu vya KIJINGA. MTU MZIMA OVYOO
 
Nimesoma habari ya Jaji Warioba katika gazeti la Raia Mwema la leo, nikagundua kuwa CCM bado inafikiri kuwa Watanzania kuwa ni wajinga kiasi hicho, wanachofikiri wao ni kuwa bado kuna watu wanaweza kufikiri vizuri kwa ajili ya watu wengine.

Kingine nilichogundua ni kuwa CCM wanaweweseka, na CCM ndio itakayoleta vurugu nchi hii kwa kuwa haiko tayari kushindwa kidemokrasia yamejidhihirisha katika mazungumzo hayo ya Jaji Warioba.

Lingine nililojifunza ni kuwa CCM sasa wanatumia mbinu zozote zile zidi ya CHADEMA kuwa kuwa haiwezi tena kushindana na CHADEMA kisera imebakia kuropoka, sasa wamebuni mbinu za kuwatumia watu maarufu kama Warioba kujifanya wanazunguzia mustakabali wa nchi bila upendeleo huku wakiingiza maoni ya kuiponda CHADEMA.

Warioba anasema Chadema kule igunga wasifikiri wanapanda chati ile inaweza kuwa nguvu ya soda halafu anaingiza propaganda za CCM za udini na kuwa CHADEMA si chama cha watu.

Tumuulize Warioba atupe data zinazoonyesha kuwa kule si kupanda chati bali ni nguvu za soda si kuzungumza kisiasa na kinadharia. Wengine sisi si wanasiasa tunataka analysis and fact.

Angalizo kwa CHADEMA ni kuwa kuna nguvu iliyo nyuma ya pazia ya kuiangamiza ambayo ni kubwa sana, sasa hivi wanawatumia wakongwe hao wameanza na Warioba, atafuata Salim, gazeti la Raia Mwema limeshachukuliwa! Kumbuka Warioba na Jenerali na Mkapa walikuwa marafiki wakubwa sana kabla ya wawili wao hawajagombana.

Mimi nimefanya kazi kwa Jenerali Ulimwengu wakati wanaanzisha gazeti la Mtanzania nawafahamu vizuri.

Watanzania tusikubali kuruhusu watu kufikiri kwa niaba yetu, CCM hawako tayari kuona chama kingine kwa kuwa wanaogopa utawala mwingine kwa kuwa wanajua katika CCM hakuna aliyemsafi kamili. Watajifanya kujikosoa wenyewe ili wabaki madarakani ili kulinda madhambi yao. Tuendelee kupambana mapaka ukombozi kamili upatikane.

Mungu ibariki Tanzania.

Bahati nzuri mimi nasoma MWANAHALISI
 
Raia Mwema a.k.a jambo leo a.k.a uhuru aka Tazama a.k.a Hoja a.k.a Mzalendo a.k.a Annuur a.k.a Habari leo.Niendelee zaidi? Hakuna gazeti lolote makini lingeweza kuandika upupu huu.Raia mwema sasa hivi ni gazeti la propaganda la Magamba.
 
Hawa wazee watulie wale hizo hela zetu za kodi wanazolipwa kila mwezi. Mimi simpende kwa sura wala hotuba zake. Pumzika kwa amani mzee.
 
Yawezekana fedha za meremeta zimeisha
kuna wakati alikua anajifanya kuwasema mafisadi wakamkumbusha pesa za meremeta Hana la kufanya ili apone inabidi aungane nao na si kuwapinga maana hatA yeye ni fisadi mzee!.KUNA MAONI YA MTU MMOJA KASEMA UKIINGIA CCM KUTOKA NI VIGUMU.
 
We chizi kweli, unaweza kumpa adui mbinu???sera zipo na kukuakikishia hilo ndo maana graph ya cdm inapanda alafu magamba inashuka! Kutoka wabunge 5 hadi 48 ni ongezeko zaidi ya silimia 400, ssm kutoka 81% hadi 61% ni kushuka kisiasa na hizi nitakwimu za haraka sana!hii yote ni kukuakikishia kuwa chama kinakubalika na kina watu makini sio magamba!!!!
 
Hawa wazee wanadhani sisi tunaangalia uzee wao, tunachokiangalia ni madini wanayotema au sumu!wapo watu makini pamoja na uzee wao lakini katika hili warioba umechemka, lazima upime fikra na mwendo kasi wa wananchi wako, upime hali ya maisha ya watanzania, uupime uongozi na uzalendo ulivokufa, upime mienendo ya viongozi wetu!kapime hata mapokeo ya wananchi juu ya uongozi na falsafa yao siri kuibia umma, upime maendeleo yaliyoletwa na chama hiki tangu kiingie madarakani kikiwa kama tanu na kuunganisha nguvu na asp kuzaa mwanaharamu anaitwa ccm!no way mzee!we are in the 21st century, we need fresh blood with fresh idea kwani pamoja na kukaa kwao madarakani kwa muda bado hakuna chochote hali nchi walizozisaidia kupata uhuru!wote wameendelea zaidi yetu!huu ni nini kama sio ujinga!!!!!!!!!!!!
 
Anaposema chadema si chama cha watu mwambieni asife mapema na kwashakoo yake,ili aje ajionee kama sisi ni watu au si watu.
 
CCM ya sasa haina mtu anayeweza kuzijibu HOJA za CDM na watanzania wakamwelewa, na hii tabia ya CCM kutumia wastaafu ndiyo itawamaliza zaidi, hawa wazee wamelitumikia taifa na muda wao umeshaisa waacheni wapumzike - mnaweza kuwafuata kwa ushauri tu ila si kuwapandisha tena majukwaani wakidodoka je?

We just want solutions to our problems, kipindi cha ahadi na maneno matamu matamu na longo longo kibao kimeshaisha - thats why kila chaguzi ndogo zinapokuja CCM wanahaha mno.

Tunawaheshimu sana wastaafu wetu, na kama kweli wana uchungu na nchi mbona hawakemei maovu? Hatutaki yaliyomtokea Mchugaji Mtikila kule Tarime akiwa jukwaani kuongea mambo ya uongo kuufanya ukweli ili hali watu wameshajichokea.
 
Back
Top Bottom