Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,203
- 44,240
.Well the way CCM primaries are supposed to work toward getting candidates for different political offices in the General Elections. Watch this:
Well.. what the heli is wrong with this people.. if they don't trust their own voters why vote? Why don't they just announce who who on Sunday or Monday so we get over with it.. but for 15 days they are still discussing the same thing.
What suprise me, some people who are considered to be educated are willing to participate in this illusion of democracy! Am I wrong to call this arrangement bordering stupidity?
.
Mzee MKJJ, huo ndio utaratibu waliona unafaa kwa chama chao. Wamejifunza kwa makosa yaliyofanyika Zanzibar mwaka 2000 pale Kamati Maalum (CCM), Zanzibar ilipompa alama juu kabisa Dr. Bilal na za chini kabisa Karume, majina yalipoletwa NEC panga likamshukia Bilal na Karume akabebwa na NEC Bara, na aliposhinda tuu, akaiweka kando timu nzima ya Komandoo, isipokuwa yule Mzee wa TISS, (Mwakanjuki). Kilichofuatia sote tunakielewa.
Huu utaratibu ni kura za maoni tuu, mwenye uamuzi wa kutangaza ni vikao vya juu vya kufanya uteuzi ili kuzuia vilio vya kutotendewa haki na kudhibiti makundi, mathalani mgombea fulani ndio kipenzi cha wengi, nyinyi mpigieni tuu kura na hapo ndio mwisho wa kazi yenu na kusubiri maamuzi ya vikao vya uteuzi.
Matokeo yakitangazwa baada ya kura, watu wataanza kusherehekea ushindi kabla, halafu panga la NEC likiwashukia, nani huku chini atawaelewa. Hiyo process wanayoitumia ni kwa lengo la " Consolidation of Party Unity" na sio lack of transparence.
Wale ambao hamkuujua mlolongo huu, uko wazi kwenye website ya CCM, wale wapenzi tembeleeni kama wenzenu, ila hata wale wengine kama kina sisi, tunapita pita kote tuu for information seach, tuwe tunapenda au laa, kama alivyofanya Mzee Mwanakijiji na hapa ametufungua macho.
Wameweka mlolongo huo makusudi ili watakaokuwa wameshinda kwenye kura za maoni na kupigwa panga kwenye vikao vya uteuzi wasipate muda wa kutimkia kwenye vyama vya upinzani.
Mani, nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani. Lakini kumbuka kuwa, hawa wanaokuwa wameshinda kura za maoni (kihalali) ndio chaguo la wakaazi wa eneo husika. Kama itakujakutokea huko mbele wakaondolewa kwa mizengwe ya vikao vya juu(mafisadi) na kumpitasha mwingine ambaye alikataliwa na hao hao wapiga kura, na endapo eneo husika halijamsimamisha mgombea makini wa chama cha upinzani, basi huyu aki-cross huwa anashinda kirahisi sana. Mfano mzuri ni huyu huyu Dr. Slaa alipokataliwa na ccm. Kwa kubana muda hadi dk za mwisho, watu wa jinsi hii huwa wanakuwa wamepotea moja kwa moja kwenye ulingo wa siasa.