CCM ni chama kipya?

Eunda

Member
May 2, 2008
60
11
Kama kweli CCM kimefanya vizuri kwa wananchi kipindi chote cha uongozi wake ni kwanini wanatumia nguvu kubwa na pesa nyingi kuwanadi wagombea wao kana kwamba ni chama kipya? Kielelezo cha mafanikio kama wanavyodai ingekuwa siraha kubwa ya kupata kura nyingi katika chaguzi zao.
Kwa kutumia pesa nyingi na nguvu kubwa kwa ajili ya kuwashawishi wananchi ili waweke madarakani ni kilelezo tosha kwamba CCM haijafanya lolote kwa wananchi licha ya kutamba kuwa kimefanya mengi toka uhuru na hali hakuna ukweli ndani yake.

Tuachane na ushabiki, ni ukweli usiofichika CCM maji yako shingoni.
 

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,743
3,036
Hawana jipya, sasa hivi wamebaki kuwatumia "BAKWATA" kuleta fitina kwa wanachi ndo wabaki madarakani.
 

KIHENGE

JF-Expert Member
Sep 20, 2011
339
98
Wamenichekesha saana eeeti mzeee namgula aliyeshindwa kuingia kwenye kamati kuu leo amekuwa na mvutooo! Hahahah!
 

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,039
CCM siyo chama halali au mkuu u dnt know this...kwahiyo lazima kitumie nguvu kubaki madarakani.
 

mwana wa africa

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
548
128
ukitaka kujua ccm ni chama cha wafanyakazi na wakulima ulizia dukani bei ya sukari, unga, mafuta ya taa, gunia la mkaa, chumvi, nk ndo utajua kama ccm ni chama kipya au....!
 

Capitalist

Senior Member
Feb 3, 2011
164
27
Ccm ilishakufa kufa siku nyingi wana jikongoja tu, lazima watumie nguvu nyingi, ubabe nk ili kuhakikisha kinabaki madarakani.
 

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,173
3,330
Shida kubwa ya CCM ni kuwa kuna watu maarufu kuliko chama na hivyo kuondoa discpline katika chama. kutokana na hilo, ndani ya chama kumezuka siasa za chuki, matabaka na fitna na hivyo kupoteza mwelekeo. Lingine ni kushindwa kusimamia maamuzi yake kichama, mfano mzuri ni maamuzi ya kujivua gamba.
 
Nov 28, 2010
31
5
CCM imekwisha haikubariki, ili ishinde Igunga ni lazima itumie nguvu nyingi sana kama chama kipya, Walipeleka Wanasheria wameshindwa! Wakapeleka wana habari, wamechemsha, walipeka wastaafu haijasaidia, wamepeleka mawaziri wanalala huko huko kama wafanyavyo kule bungeni sasa wanapeleka Wakandarasi wataalamu wa kuongea kisukuma! hayo ni matusi, wana Igunga hawahitaji msemaji mzuri wa kisukuma wala kujua Hijab/Mtandio ulitolewa makusudi au katika harakati za kumtia nguvuni muarifu kitambaa kikachojoka! Wanataka mbunge bora anayetoka katika chama chenye mwelekeo.
 

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,039
Hivi hiki nyinyiem kilijisari wapi?Wadhamini waliwatoa wapi.?Tendwa twambie cku ambayo ccm ilijisajiri na kwanini hakikubadisha jina wakati sheria inasema 1992 pluralism system chama kisitumie jina la chama ambacho kiliwai kuwepo.ccm is a monster
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom