GE2025 CCM ni Baba wa siasa za kimkakati Afrika

GE2025 CCM ni Baba wa siasa za kimkakati Afrika

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Pengine unafuatilia siasa za Afrika Kusini juu juu sana, zuma muda huu yuko wapi? yupo Gerezani?
Siyo lazima awe gerezani.Hata kumtoa mtu kwenye kiti cha URAIS kupitia chama chake ni hatua nzuri.Siyo sera za Zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa ccm kwenye taifa la watu zaidi ya milioni 60.Huo ni ujinga hata wewe unayejisifu bila shaka una element za ujinga.
 
Zile Narratives za Lissu dhidi ya Mbowe zilipikwa vizuri sana! No reform No election ilikua propaganda iliyofanikiwa sana kuchomekwa CDM!!

The Only thing Samia alikua anakosa usingizi ni ushiriki wa CDM mwaka huu!!
CCM haijawahi kuhofia chama chochote kwenye uchaguzi kwa sababu, hakuna chama chenye uwezo kwenye jambo lolote kuishinda CCM.
 
Kwa hoja zako tu, sio lazima useme.
Kanyonyeshe kwanza ndiyo urudi
Screenshot_20250725-185609~2.png
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni urithi wa kihistoria na kisiasa wa Tanzania, lakini pia ni somo la uthabiti barani Afrika. Kimekuwa chama pekee cha ukombozi ambacho hadi leo bado kinaendelea kushika hatamu za uongozi kwa amani na utulivu.

Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan umeleta upeo mpya wa mageuzi ya kimfumo, kuifanya CCM kuwa taasisi yenye misingi ya kidemokrasia na mkakati thabiti wa kuishi kwa vizazi vingi.

Mageuzi ya CCM chini ya Rais Samia

Rais Samia Suluhu amelifanya CCM kuwa chama chenye uhai na uimara zaidi kwa kuzingatia mageuzi yanayolenga wananchi. Ametekeleza mabadiliko ya katiba ya chama ili kuongeza nafasi za vijana na wanawake kushiriki kwenye uongozi.

Kwa mfano, katika chaguzi za ndani za mwaka 2022, idadi ya vijana waliojitokeza kugombea nafasi za chama iliongezeka kwa zaidi ya 30% kulinganisha na miaka ya nyuma. Hii ni ishara kwamba CCM imegeuka kuwa chombo cha kuwashirikisha wananchi wote bila kubagua umri, jinsia au nafasi ya kijamii.

Idadi ya Wanachama imeimarika zaidi

Kwa sasa CCM kina wanachama takribani milioni 13 kote nchini, jambo linalokifanya kuwa chama kikubwa zaidi barani Afrika. Tofauti na vyama vingine ambavyo hujikita mijini pekee, CCM inawigo mpana kuanzia kijijini hadi mijini. Kwa mfano, wanachama wake wameenea katika kila kata, kijiji na mtaa, hali inayokifanya chama kuwa karibu na maisha ya wananchi wa kawaida. Hii ndiyo sababu, kila uchaguzi unapofanyika, CCM hubaki na mtandao thabiti wa kisiasa.

Mabadiliko ya chama

Mojawapo ya hatua muhimu chini ya Rais Samia ni mabadiliko ya katiba ya CCM yaliyofanyika ili kulifanya chama kuwa na uwazi zaidi. Mabadiliko haya yameweka msisitizo kwenye nidhamu ya viongozi na uwajibikaji kwa wananchi. Aidha, yameweka mfumo unaolinda uwakilishi wa makundi maalumu, hususan wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Hatua hii imeongeza imani ya wanachama na kuimarisha uhalali wa chama kama taasisi ya kidemokrasia.

CCM na Urithi wa vyama vya ukombozi Afrika

Wakati vyama vya ukombozi barani Afrika kama UNIP (Zambia) na KANU (Kenya) vilipoanguka na kupoteza mvuto, CCM kimeendelea kudumu. Sababu kubwa ni uwezo wake wa kujirekebisha na kuendana na mahitaji mapya ya jamii. Kwa mfano, wakati vyama vingine vilishindwa kuvumilia ushindani wa kidemokrasia, CCM kiliamua kufungua milango ya mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 bila kulazimishwa na mapinduzi au vita. Hatua hii inaonesha upeo wa kimkakati wa chama hiki katika kulinda amani na mustakabali wa taifa.

Ulinzi wa Amani na Umoja wa Kitaifa

Tanzania ni moja ya nchi chache barani Afrika ambazo hazijawahi kushuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe. CCM kimekuwa nguzo kuu ya mshikamano huo. Kupitia sera zake, chama kimehakikisha Watanzania wa makabila zaidi ya 120 wanaishi kwa mshikamano na mshikikano.

Kwa mtazamo wa historia na hali ya sasa, CCM si chama cha kawaida bali ni taasisi yenye mchango mkubwa wa kisiasa na kijamii. Kupitia mageuzi ya Rais Samia Suluhu Hassan, chama kimeendelea kujipambanua kama nguzo ya amani, mshikamano na maendeleo.

Ndiyo maana leo hii CCM kinahesabiwa kama Baba wa siasa za kimkakati Afrika, kielelezo cha uthabiti, ushawishi na dira endelevu.
Kama ulisoma shule ulipoteza muda Bure. Msomi yoyote na mwenye akili timamu hawezi kushangilia wizi wa kutisha kwenye nchi yake. Na Silaha ya matapeli ni mjinga kama wewe. Jinga kabisa
 
Niliwahi kuandika katika kipindi kilichopita naomba na Leo pia nirudie UCHAWA na UCHAWI tofauti yake ni ndogo sana kama ambavyo maneno yake yamepishana kidogo sana ndivyo hata hao watu walivyo fanana kwenye mioyo Yao
 
Back
Top Bottom