CCM ndiyo imetufikisha hapa sio upinzani

Hapa tulipo panatosha au wewe unataka pale? Kama ni pale nenda peke yako.
 
watawala wa ccm wamekula wakavimbiwa hadi wakajisahau,wamekuwa waropokaji na kauli zao za kikoloni.wanadhani hii nchi ni mali yao binafsi.kiufupi tu wametufikisha hapa tulipo,hatuna kitu chochote cha kujivunia kama taifa.wakati umefika wa kusema no imetosha sasa na kila mtu akahakikisha 2015 tunawapiga chini.
Nchi haitatawalika,hapata kalika,hakuna kulala hizo ni kauri za mzee wako slaa wala huna haja ya kuwaza nani mwenye kauri mbaya hapa tanzania.
 
Wadau Salaam.
Leo asubuhi nilipata wasaa wa kuangalia udondozi wa magazeti kwenye luninga.Taarifa tatu kati ya nyingine nyingi zimenisukuma kuweka haya machache.Matarajio yangu ni kuwa yatasaidia kuibua fikra pana na mjadala chanya juu ya mustakabali wa nchi yetu baada ya kufikishwa hapa tulipo na chama tawala hasa hiki cha miongo miwili iliyopita.
Taarifa ya kwanza ni kuhusu tamko la Mh.Spika Anna Makinda kuhusu haja ya kuwaongezea wabunge mishahara kwa vile wabunge wa zamani wana hali mbaya mithili ya ombaomba.Kwamba Anna Makinda anahusisha kushindwa maisha kwa waheshimiwa hawa na viwango vya jumla vya mishahara ya wabunge sio dhamira ya uzi huu.
La pili ilikuwa taarifa ya hali mbaya ya shule ya sekondari mbagala ya hapa hapa Dar es salaam ambapo taarifa zinasema wanafunzi hawana madawati,wanaketi chini au kwenye ndoo,madarasa hayana sakafu na huduma ya maji na hali ya majengo ya shule hiyo ni duni sana.
La tatu ni taarifa kuwa serikali hii ya CCM imefanikiwa kuwakopa wakulima mazao yao yanayofikia kiasi cha Tshs 1.7 BILIONI!
Nikiwa njiani kuelekea kibaruani nikawa natafakari!
Hivi inakuwaje nchi moja hii hii,ikawa na pengo kubwa la uhalisia wa maisha kiasi hiki?kwamba wakati waheshimiwa wakiwakilishwa na mheshimiwa mkubwa wao (Spika)anaona vimshahara vya milioni saba na ushee,jumlisha na posho ya vikao ya Tshs 330,000/=kwa SIKU,na vijipesa vya Mafuta,Mfuko wa jimbo,ujumbe wa kamati na bodi mbalimbali na posho zake,msamaha wa kodi kwa wateule hawa bado ni kidogo sana kiasi kwamba wanashindwa kumudu ukali wa maisha na wanahitaji kuongezewa!Wakati huo huo,siku hiyo hiyo,nchi hiyo hiyo Tanzania kuna wanafunzi ambao wanakosa madawati ya kukalia!hawana hata maji ya KUNYWA!wanakalia ndoo kwenye madarasa yasiyo na sementi!
Halafu tena,Katika nchi hiyo hiyo,inayo ongozwa na serikali hiyo hiyo ya CCM,Kuna wakulima baada ya kuvuja jasho na damu kwa kilimo cha kujikimu kisicho na tija na kuvuna walichovuna serikali hiyo hiyo imeenda kuchukua mazao yao kwa MKOPO!Tena si kidogo.....BILIONI 1.7!
Nikatafakari zaidi kuwa hali hii iko kila mahali.....Kwenye huduma za afya ambapo watawala wanaenda kufanya check up Africa ya kusini,Amerika na India wakati wakina mama wajawazito wanalala wawili katika kitanda kimoja au chini sakafuni,Kwenye Elimu ambapo watoto wa watawala wanasoma English medium na Cambridge syllubus huku watawaliwa wakisoma kayumba et al,Kwenye uongozi na ajira,kwenye fursa na ushawishi....kila mahali!
Nikatafakari zaidi kuwa haya ni matokeo ya mfumo rasmi ambapo Taifa moja.....la watawala na wapambe wao,wanao nufaika na kuneemeka na utawala huu....na taifa jingine......la watawaliwa.....ambao wao kazi yao ni kuwachumia hawa watawala,kuwa neemesha kwa jasho lao na nguvu zao!wanaishi katika nchi moja!
Angalia bodi ya mikopo ya elimu ya juu,wanao pigana vikumbo kule si watoto wa watawala, ni watoto wa taifa hili la watawaliwa ambao wanakatwa kodi wasiyo itumia...watawala hawakatwi kodi....kuanzia kinara wa utawala mwenyewe!Na kwa vile sisi ni mataifa mawili tofauti katika nchi moja watawala hawawajibiki kwa watawaliwa!ila watawaliwa wanawajibika kwa watawala.
Ndiyo maana watawala wamejipa hali ya kuwa miungu watu,ambapo wanaona kila kitu ni stahili yao.Dhamira zao haziwasuti tena kuona wao wanakula na kusaza wakati jirani zao wanalala na njaa!Hawasumbuki tena na umaskini uliokithiri wa watu wetu kwa vile hauwahusu!Wanashughulika zaidi na matumbo yao kuliko kelele zetu.
Nikatafakari zaidi kuwa hawawezi kusikia kilio chetu kwa vile maumivu yetu hayawahusu,Tukiongeza kelele wao wanasikia "Uchochezi",Tukihoji wao wanaona "Chuki binafsi za wasionacho dhidi ya wenye nacho",Tukijitutumua kujitambua wao wanaona "Uhaini"!
Nilipo endelea kutafakari,Nikakumbuka maneno ya mwandishi Benjamin Disraeli katika kitabu chake Sybil. "Two nations between whom there is no intercourse and no sympathy; who are ignorant of each other's habits, thoughts and feelings, as if they were dwellers in different zones or inhabitants of different planets; who are formed by different breeding, are fed by different food, are ordered by different manners, and are not governed by the same laws ... THE RICH AND THE POOR."
Vinginevyo,Utauelezeaje ulafi huu unao endelezwa na CCM?
Mkuu umechafua jukwaa kwa kuandika kitu kisicho kichwa wala miguu.
 
Watu nyegeee zikiwapanda wanaonge lolote, mishahara ya MP ni midogo??? lazima uwe unaugua kichaa, kwa hali ya sungura mdogo mtu anakunja mil 7 na marupurupu kibao eti anaombaomba, hata sitaki kusikia. Kwa hiyo tuwafanyeje??? wengine ni mila zao kuombaomba
 
In a country/state where there is a GAP between THE HAVES AND HAVENOT,what's next is (according to KARL MARX)THE OVERTHROW OF THE EXISTING SYSTEM which is CCM in our case.It is high tIME that the TANZANIANS especially WE-THE OPPRESSED should LIBERATE OURSELVES from the CCM REGIME.the education that we acquire should act as a stepping stone towards achieving our goal(to remove CCM from POWER).
 
Wadau Salaam.
Leo asubuhi nilipata wasaa wa kuangalia udondozi wa magazeti kwenye luninga.Taarifa tatu kati ya nyingine nyingi zimenisukuma kuweka haya machache.Matarajio yangu ni kuwa yatasaidia kuibua fikra pana na mjadala chanya juu ya mustakabali wa nchi yetu baada ya kufikishwa hapa tulipo na chama tawala hasa hiki cha miongo miwili iliyopita.
Taarifa ya kwanza ni kuhusu tamko la Mh.Spika Anna Makinda kuhusu haja ya kuwaongezea wabunge mishahara kwa vile wabunge wa zamani wana hali mbaya mithili ya ombaomba.Kwamba Anna Makinda anahusisha kushindwa maisha kwa waheshimiwa hawa na viwango vya jumla vya mishahara ya wabunge sio dhamira ya uzi huu.
La pili ilikuwa taarifa ya hali mbaya ya shule ya sekondari mbagala ya hapa hapa Dar es salaam ambapo taarifa zinasema wanafunzi hawana madawati,wanaketi chini au kwenye ndoo,madarasa hayana sakafu na huduma ya maji na hali ya majengo ya shule hiyo ni duni sana.
La tatu ni taarifa kuwa serikali hii ya CCM imefanikiwa kuwakopa wakulima mazao yao yanayofikia kiasi cha Tshs 1.7 BILIONI!
Nikiwa njiani kuelekea kibaruani nikawa natafakari!
Hivi inakuwaje nchi moja hii hii,ikawa na pengo kubwa la uhalisia wa maisha kiasi hiki?kwamba wakati waheshimiwa wakiwakilishwa na mheshimiwa mkubwa wao (Spika)anaona vimshahara vya milioni saba na ushee,jumlisha na posho ya vikao ya Tshs 330,000/=kwa SIKU,na vijipesa vya Mafuta,Mfuko wa jimbo,ujumbe wa kamati na bodi mbalimbali na posho zake,msamaha wa kodi kwa wateule hawa bado ni kidogo sana kiasi kwamba wanashindwa kumudu ukali wa maisha na wanahitaji kuongezewa!Wakati huo huo,siku hiyo hiyo,nchi hiyo hiyo Tanzania kuna wanafunzi ambao wanakosa madawati ya kukalia!hawana hata maji ya KUNYWA!wanakalia ndoo kwenye madarasa yasiyo na sementi!
Halafu tena,Katika nchi hiyo hiyo,inayo ongozwa na serikali hiyo hiyo ya CCM,Kuna wakulima baada ya kuvuja jasho na damu kwa kilimo cha kujikimu kisicho na tija na kuvuna walichovuna serikali hiyo hiyo imeenda kuchukua mazao yao kwa MKOPO!Tena si kidogo.....BILIONI 1.7!
Nikatafakari zaidi kuwa hali hii iko kila mahali.....Kwenye huduma za afya ambapo watawala wanaenda kufanya check up Africa ya kusini,Amerika na India wakati wakina mama wajawazito wanalala wawili katika kitanda kimoja au chini sakafuni,Kwenye Elimu ambapo watoto wa watawala wanasoma English medium na Cambridge syllubus huku watawaliwa wakisoma kayumba et al,Kwenye uongozi na ajira,kwenye fursa na ushawishi....kila mahali!
Nikatafakari zaidi kuwa haya ni matokeo ya mfumo rasmi ambapo Taifa moja.....la watawala na wapambe wao,wanao nufaika na kuneemeka na utawala huu....na taifa jingine......la watawaliwa.....ambao wao kazi yao ni kuwachumia hawa watawala,kuwa neemesha kwa jasho lao na nguvu zao!wanaishi katika nchi moja!
Angalia bodi ya mikopo ya elimu ya juu,wanao pigana vikumbo kule si watoto wa watawala, ni watoto wa taifa hili la watawaliwa ambao wanakatwa kodi wasiyo itumia...watawala hawakatwi kodi....kuanzia kinara wa utawala mwenyewe!Na kwa vile sisi ni mataifa mawili tofauti katika nchi moja watawala hawawajibiki kwa watawaliwa!ila watawaliwa wanawajibika kwa watawala.
Ndiyo maana watawala wamejipa hali ya kuwa miungu watu,ambapo wanaona kila kitu ni stahili yao.Dhamira zao haziwasuti tena kuona wao wanakula na kusaza wakati jirani zao wanalala na njaa!Hawasumbuki tena na umaskini uliokithiri wa watu wetu kwa vile hauwahusu!Wanashughulika zaidi na matumbo yao kuliko kelele zetu.
Nikatafakari zaidi kuwa hawawezi kusikia kilio chetu kwa vile maumivu yetu hayawahusu,Tukiongeza kelele wao wanasikia "Uchochezi",Tukihoji wao wanaona "Chuki binafsi za wasionacho dhidi ya wenye nacho",Tukijitutumua kujitambua wao wanaona "Uhaini"!
Nilipo endelea kutafakari,Nikakumbuka maneno ya mwandishi Benjamin Disraeli katika kitabu chake Sybil. "Two nations between whom there is no intercourse and no sympathy; who are ignorant of each other's habits, thoughts and feelings, as if they were dwellers in different zones or inhabitants of different planets; who are formed by different breeding, are fed by different food, are ordered by different manners, and are not governed by the same laws ... THE RICH AND THE POOR."
Vinginevyo,Utauelezeaje ulafi huu unao endelezwa na CCM?
Anna makinda is a leader who does not fear god nor respect human sufferings!she has turned aside from the way our union constitution has pointed out her! I do not approve of her way of supporing legislators loveless demands of pay rise while all tanzanian's primary schools do not have a morden flash toilets.
 
Mkuu umechafua jukwaa kwa kuandika kitu kisicho kichwa wala miguu.
Kwa hakika ningestaajabu kama ungeweza kubaini kichwa na miguu ya chapisho hili....sidhani kama ufahamu huo unatolewa huko Lumumba!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Mkuu umechafua jukwaa kwa kuandika kitu kisicho kichwa wala miguu.
uraia wako uko mashakani maana kama ungekuwa raia wa tanzania, unge soma Luka:1-13 au 16:10-13 most jesus proclamation of 😀ishonest worker.
 
mambo haya ya aliyasema yesu miaka 2000 iliyopita: Luka 16:19-31 Maskini na Lazaro. Anna makinda, ni Lazaro na sisi ni maskini. Anatwanya mapesa kwa washikaji huku shule hazina vyoo vya kuvuta!
 
Hapa tulipo panatosha au wewe unataka pale? Kama ni pale nenda peke yako.

Lumumba project mishipa yenu ya akili ilishaharibiwa siku nyingi, mmebakia kushabikia upumbavu wa serikali bila kujali utu wenu. shame on you
 
Nilimshangaa huyu mama anayewatetea watu wanaopata mshahara wa milioni 7 kwa mwezi kuwa na maisha magumu badala ya wananchi wa jimbo lake ambao kila kitu ni kigumu kwao kwa siku zote! Mheshimiwa Makinda anashindwa kuwatetea waalimu ambao mishahara yao ni midogo, wafanya kazi wa afya na hata wakulima ambao elimu ya watoto wao ni duni kila mwaka, anawatetea wabunge kwa kuwa naye yumo! Du....!

Lakini huyu mama najiuliza katika kumbukumbu yangu kama kawahi kufundisha hivi! By professional ualimu ndo kazi yake, sasa machungu ya walimu anawasahau vipi?
 
Mungu ibariki Tanzania na sisi watu wake pia utupe ufahamu wa kina na moyo wa kuwa wazalendo kwa Taifa letu.

Mheshimiwa Rais Magufuli naomba utambue kwa kina na mapana yake kuwa tumefika hapa kwa sababu ya Chama Cha Mapinduzi.

Ikumbukwe kuwa nchi hii toka inapata uhuru imekuwa chini ya utawala wa serikali ya CCM. Awamu ya kwanza Mwl Nyerere alikuwa mchungu na maliasili za taifa hili pia alijitahidi kuweka misingi thabiti ya utawala bora na uwajibikaji kwenye serikali yake.

Lakini hizi awamu nyingine tumeshuhudia madudu mengi sana yanayosababishwa na vigogo wa CCM na washirika wake katika kulinyonya taifa na kuliingiza matatani.

Hivyo mheshimiwa Magufuli tuwe wakweli mbele za Mungu adui yetu na taifa hili ni CCM na serikali zake hasa awamu ya pili,tatu na nne.

Na hizi awamu zimekuwa zikitofautiana katika kutuletea maumivu sisi wanyonge wa taifa hili. Nashukuru sana kwa Mwenyezi Mungu kwakuwa unaomba watu wote kwa dini zetu tukuombee kwa Mungu akusaidie kuliongoza taifa.

Lakini ili watu tukuombee lazima Mh Rais utambue ukweli huo. Kwani kweli humweka mtu huru. Hivyo ni lazima tutambue kuwa adui wa taifa hili ni CCM na serikali zake na hii ndio kweli ili tuwe huru.

Najua hadi sasa unatumbua majibu, Mungu akusaidie kwani kama ni majipu ni mengi sana.

Tujiulize majipu haya nani kayasababisha? Jibu jepesi kabisa bila kumung'unya ni CCM na baadhi ya serikali zake. Hivyo Mheshimiwa Rais unapotumbua majipu unatumbua majipu ya wanachama wenzako ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa viongozi wako na kwa wakati mwingine umekuwa kiongozi wao.

Mungu akusaidie sana kuikana dhamila ya CCM ya zamani na uijenge CCM mpya yenye kujali utu,haki,utawala bora na uwajibikaji. Pia katika serikali yako wapo wengi sana waliotufikisha hapa tulipo hivyo uwe makini nao.

Mwisho Mungu akusaidie usimame peke yako kutenda haki pasipo kuingiliwa na tawala zilizoshindwa na kutufikisha hapa tukiwa na mjipu mengi.
 
Acha habar yako mkuu,kwani hyo ni ccm tu ilitawala hakuna vyama vinginevyo vilishika utawala katika ngazi mbali mbali,,au kwako wewe uongozi ni urais tu,grow up acha kulalamika..fanyeni kazi ccm ccm kina mnyika,sugu,mdee au Nao ni ccm.huu sio wakati wa kampeni cjui chama gani hapa ni kazi tu ue kashasema jipu popoye lilipo atalikamua...
 
Nadhani wewe pia ni jipu kubwa sana kwa taifa hili. Gari haliwezi kwenda uelekeo unaotakiwa kama usukani umekatika. Hivyo Rais ni usukani (steering) hivyo vyama vingine vimewahi kutupatia Rais. Rais Magufuli akiwasikiliza wajinga kama wewe taifa litarudi kulekule kwenye majipu kuongezeka
 
Ukishaona mtu anakomaa na uchama muda huu nae jipu tambazi,we umeona raisi kadeal na uchama?fanya kazi kijana,we unadhani Ana muda kusikiliza hizo pumba zako..kwani yy hajui washirika wa majipu ni kina nani..endelea kupaza sauti ka mwehu kwenye issue ya uchama this time..
 
Amakweli taifa limefika hapa kwa kuwa na kundi la wajinga kama wewe. Ili taifa lisongembele linatakiwa kutathimini wapi limetoka na nichangamoto gani limezipata na nini kilisababisha hizo changamoto. Hivyo taifa litasonga mbele sasa wewe mbugila unataka twende kichwa kichwa kama unavyokwenda wewe pasipo kushirikisha akili.
 
Habali wana jamii kuna haka kamusemo kaa ccm imetufikisha hapa mimi huwa sikaelewi kwan zaman tulikua wap na tulikua na nan na saiv tuko wap na tuko na nan mara nyingi husikia tumefikishwa hapa na ccm kama siyo ccm tusingefika hapa tulipo nini maana yake
 
Naomben ufafanuzi kwani tulipofikishwa hapa na hiyo ccm ni pazur au ni pabaya
 
Mbona ni simple tu, yaani imetudumaza! Kwa umli tulionao kimaendeleo tumedumaa, miaka 55 ya Uhuru, bado tunahangaika na MAJI, barabara na UMEME. Wenzetu wenye umri huu, wako mbali kimaendeleo. Hivi kinatushinda hata kiwanda cha toothpicks! Hapa ndio ilipotufikisha! Upo?
 
Back
Top Bottom