Kuhusu nadharia kadhaa za sababu ya muungano huu ikiwemo suala la Usalama wa Zanzibar baada ya Mapinduzi, Hofu ya Ukomunisti na mengine ambayo leo sio mada za mjadala huu, tunabaki kuiona nafasi ya ASP na baadae CCM katika kuidhoofisha hadhi ya Zanzibar kwenye Muungano.
Tuanzie hapo. Baada ya kuundwa Muungano ambao uhalali wake ulitiliwa mashaka na baddhi ya viongozi wa Zanzibar wa waKATI HUO KWA TARATIBU KUTOKAMILISHWA KUPATA BARAKA kWENYE BARAZA LA MAPINDUZI AU CHOMBO CHA UWAKILISHI CHA WANANCHI.
Kuliibuka zogo la mkataba wa Muungano na uhalali wake na ulivyotafsiriwa. Kuliibuka zogo la kuongezwa mambo ya Muungano kinyemela, kumeibuka sintofahamu mara kadhaa kwa kuandamwa wanaohoji muungano kwa kupata vitisho mbali mbali na kutokea matukio yasiyo majibu hadi leo.
Yaliyopita kabla mwaka 1977 ilipoundwa CCM tuyaache, tuanze hapo. CCM iliundwa mwaka huo kwa kuungana ASP na TANU. Kazi ya CCM sasa ni kuunganisha itikadi ya chama kuwa moja baada ya kufanikiwa Serikali mbili kuungana. CCM ilitumika kuuwa itikadi za ASP na TANU. Makao Makuu yakawa DODOMA.
Kuongezeka kwa mambo ya Muungano yalifanywa kipindi cha CCM hii hii kuwa madarakani. Kuondolewa nafasi ya Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais hapo miaka ya 1990 kulifanywa na CCM ikiwa ndio yenye maamuzi Bungeni.
Rais wa Zanzibar kuwa Waziri wa JMT asiye na Wizara Maalumu kulifanywa na kuridhiwa na CCM.
Kuendelea kunyanganywa nguvu za kimaamuzi kwa Zanzibar ndani ya Bunge kumefanywa na CCM hii hii leo inayotawala.
DHANA YA UKOLONI NDANI YA MUUNGANO.
Kuna hii dhana ambayo inapata mashiko. Zanzibar maamuzi yote kuhusu nani atawale yanafanywa Dodoma kupitia maamuzi ya CCM na kuwekewa kinga ya kiulinzi na Jamuhuri ya Muungano kwa kutumia Jeshi na vyombo vya Muungano.
Uraisi wa Zanzibar ni kilemba cha ukoka ambapo wazanzibari hawana maamuzi ya kumuweka Rais wao lazima Baraka zipite kutoka JMT. Serikali ya JMT ndio yenye jukumu la Ulinzi wa Jamuhuri na Usalama, Vyovyote iwavyo wanawajibika kuhakikisha yule wanayemtaka ndio anasdhika hatamu ( rejea chaguzi zote kuanzia 1995 hadi 2015) Licha ya kukiukwa kote kule kwa taratibu wao ndio wamehakikisha Uongozi uliopo unaendelea.
Zanzibar imebanwa kupitia taratibu za kuwa na maamuzi huru ya kiuchumi na mapato ya ndani, Inalazimika kuomba ridhaa Bara.
Dhana ya Ukoloni inakuja vile vile kwa kupandikizwa migogoro baina ya watu wa Zanzibar kwa Uongozi wa JMT kutumia Nyenzo zake kuchaguwa upande wa kufanya nao kazi na wala sio kusimamia haki kutendeka kila unapokuja uchaguzi. sio hayo tu kuna tetesi za kupandikizwa Viongozi kutoka Bara kushika nafasi za kichama na kiserikali huko Zanzibar.
Yaani Maslahi ya Bara yanapitia ndani ya CCM kisha ndani ya SMZ kuhakikisha azma inafikiwa.
Huu ni mkakati wa muda mrefu wa kuidhoofisha Zanzibar kwenye Muungano kuhakikisha kile kitu kinaitwa Serikali mbili kuelekea moja kinafikiwa ( a Matter of Time)
Bara inatumia mwanya wa Muungano kupandikiza watu wake kwenye CCM kushika nafasi za Uongozi Zanzibar na Serikalini na kuifanya Serikali ya Zanzibar kushindwa kuwa na msimamo wa kujisimamia MASLAHI YAKE KWENYE MUUNGANO ( TWO IN ONE)
Serikali ya JMT kutokuwa tayari kulitatuwa tatizo la Malalamiko ya muungano kutoka Zanzibar na badala yake kutumia vitisho na kauli kali kwa yoyote anayehoji Muungano ni ushahidi wa wazi kuwa Muungano una ajenda zake kuhusu kuipoteza Zanzibar na hapo ndipo hoja ya Ukoloni inapopata Nguvu kule Zanzibar.
Ikumbukwe kuwa ni CCM hii hii iliyofanya figisu kuharibu mapendekezo ya Katiba mpya ya Warioba ambayo walau iliyoonesha njia ya kutaka kuuweka sawa Muungano wetu.
CCM inabaki ndio injinia wa kuidhoofisha Zanzibar kwenye Muungano huu kwa njia tofauti.
Tujenge Muungano wa Haki kwa Maslahi ya Wote. Muungano ulianzia mahali fulani kamwe hiwezekani kusiwe na mahali pa kunzia kuondowa changamnoto zake na utatuzi wa migogoro yake.
Ukiona hayo yanafirigiswa ujue hao walioshikilia kunyamazisha watu ndio wakoloni wenyewe ikiwemo CCM ambae ndio mpishi mkuu.
Kishada.