CCM ndio wameondoa hadhi ya Zanzibar kwenye Muungano. Kuna ukoloni unaendelea

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,097
2,000
Kuhusu nadharia kadhaa za sababu ya muungano huu ikiwemo suala la Usalama wa Zanzibar baada ya Mapinduzi, Hofu ya Ukomunisti na mengine ambayo leo sio mada za mjadala huu, tunabaki kuiona nafasi ya ASP na baadae CCM katika kuidhoofisha hadhi ya Zanzibar kwenye Muungano.

Tuanzie hapo. Baada ya kuundwa Muungano ambao uhalali wake ulitiliwa mashaka na baddhi ya viongozi wa Zanzibar wa waKATI HUO KWA TARATIBU KUTOKAMILISHWA KUPATA BARAKA kWENYE BARAZA LA MAPINDUZI AU CHOMBO CHA UWAKILISHI CHA WANANCHI.

Kuliibuka zogo la mkataba wa Muungano na uhalali wake na ulivyotafsiriwa. Kuliibuka zogo la kuongezwa mambo ya Muungano kinyemela, kumeibuka sintofahamu mara kadhaa kwa kuandamwa wanaohoji muungano kwa kupata vitisho mbali mbali na kutokea matukio yasiyo majibu hadi leo.

Yaliyopita kabla mwaka 1977 ilipoundwa CCM tuyaache, tuanze hapo. CCM iliundwa mwaka huo kwa kuungana ASP na TANU. Kazi ya CCM sasa ni kuunganisha itikadi ya chama kuwa moja baada ya kufanikiwa Serikali mbili kuungana. CCM ilitumika kuuwa itikadi za ASP na TANU. Makao Makuu yakawa DODOMA.

Kuongezeka kwa mambo ya Muungano yalifanywa kipindi cha CCM hii hii kuwa madarakani. Kuondolewa nafasi ya Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais hapo miaka ya 1990 kulifanywa na CCM ikiwa ndio yenye maamuzi Bungeni.

Rais wa Zanzibar kuwa Waziri wa JMT asiye na Wizara Maalumu kulifanywa na kuridhiwa na CCM.

Kuendelea kunyanganywa nguvu za kimaamuzi kwa Zanzibar ndani ya Bunge kumefanywa na CCM hii hii leo inayotawala.

DHANA YA UKOLONI NDANI YA MUUNGANO.
Kuna hii dhana ambayo inapata mashiko. Zanzibar maamuzi yote kuhusu nani atawale yanafanywa Dodoma kupitia maamuzi ya CCM na kuwekewa kinga ya kiulinzi na Jamuhuri ya Muungano kwa kutumia Jeshi na vyombo vya Muungano.

Uraisi wa Zanzibar ni kilemba cha ukoka ambapo wazanzibari hawana maamuzi ya kumuweka Rais wao lazima Baraka zipite kutoka JMT. Serikali ya JMT ndio yenye jukumu la Ulinzi wa Jamuhuri na Usalama, Vyovyote iwavyo wanawajibika kuhakikisha yule wanayemtaka ndio anasdhika hatamu ( rejea chaguzi zote kuanzia 1995 hadi 2015) Licha ya kukiukwa kote kule kwa taratibu wao ndio wamehakikisha Uongozi uliopo unaendelea.

Zanzibar imebanwa kupitia taratibu za kuwa na maamuzi huru ya kiuchumi na mapato ya ndani, Inalazimika kuomba ridhaa Bara.

Dhana ya Ukoloni inakuja vile vile kwa kupandikizwa migogoro baina ya watu wa Zanzibar kwa Uongozi wa JMT kutumia Nyenzo zake kuchaguwa upande wa kufanya nao kazi na wala sio kusimamia haki kutendeka kila unapokuja uchaguzi. sio hayo tu kuna tetesi za kupandikizwa Viongozi kutoka Bara kushika nafasi za kichama na kiserikali huko Zanzibar.

Yaani Maslahi ya Bara yanapitia ndani ya CCM kisha ndani ya SMZ kuhakikisha azma inafikiwa.

Huu ni mkakati wa muda mrefu wa kuidhoofisha Zanzibar kwenye Muungano kuhakikisha kile kitu kinaitwa Serikali mbili kuelekea moja kinafikiwa ( a Matter of Time)
Bara inatumia mwanya wa Muungano kupandikiza watu wake kwenye CCM kushika nafasi za Uongozi Zanzibar na Serikalini na kuifanya Serikali ya Zanzibar kushindwa kuwa na msimamo wa kujisimamia MASLAHI YAKE KWENYE MUUNGANO ( TWO IN ONE)

Serikali ya JMT kutokuwa tayari kulitatuwa tatizo la Malalamiko ya muungano kutoka Zanzibar na badala yake kutumia vitisho na kauli kali kwa yoyote anayehoji Muungano ni ushahidi wa wazi kuwa Muungano una ajenda zake kuhusu kuipoteza Zanzibar na hapo ndipo hoja ya Ukoloni inapopata Nguvu kule Zanzibar.

Ikumbukwe kuwa ni CCM hii hii iliyofanya figisu kuharibu mapendekezo ya Katiba mpya ya Warioba ambayo walau iliyoonesha njia ya kutaka kuuweka sawa Muungano wetu.

CCM inabaki ndio injinia wa kuidhoofisha Zanzibar kwenye Muungano huu kwa njia tofauti.

Tujenge Muungano wa Haki kwa Maslahi ya Wote. Muungano ulianzia mahali fulani kamwe hiwezekani kusiwe na mahali pa kunzia kuondowa changamnoto zake na utatuzi wa migogoro yake.

Ukiona hayo yanafirigiswa ujue hao walioshikilia kunyamazisha watu ndio wakoloni wenyewe ikiwemo CCM ambae ndio mpishi mkuu.
Kishada.
 
KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,097
2,000
Mkuu kutawaliwa kwa Zanzibar kunatokana na CCM zanzibar, watu Kama jecha hawataki muwe huru
Unaambiwa CCM Zanzibar sasa hawana tena nguvu za kuipigania Zanzibar ndani ya Muungano. Walishafanya makosa ambayo kujirudi ni vigumu. Wamebaki wakipewa vinafasi vya peremende ikiwa ni malipo ya ukibaraka. Waliuwa Afro Mama leo wanaendekeza matumbo.

Ukipata stori za wazee wa Zanzibar walivyolia siku ilipounganishwa ASP na TANU mara na wewe machozi yanakutoka. Njama za kuivuruga Zanzibar hazikuanzxa juzi. " Ni Ukoloni juu ya Ukoloni tu". Hizi ndizo lugha zilizoko Zanzibar.
 
Kwa wasiojuwa siasa za Zanzibar, Mzee Jumbe ndio alipigilia msumari wa kuimaliza Zanzibar kwa kusimamia kuunganishwa ASP na TANU, Wazalendo wa Zanzibar walimuona mtu mbaya sana. Baadae zilipokuja siasa za Serikali tatu ndio maana alipingwa na baadhi ya wazanzibari ambao walijua azma yake haikuwa ya kweli. Ukichimbuwa sana utagunduwa mengi.
 
Bobwe2

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
2,427
2,000
Kuna huu mfumo kristo umeusahau mtoa mada,kina lukuvi walisema bila ya waswas kuwa mfumo kristo ndio koti lao la huu muungano wa kikoloni

Sent using tecno tochi
 
KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,346
2,000
Huu muungano ukivunjika utaiongezea Tanganyika gharama ya kuwahifadhi wakimbizi wa Zanzibar watakaozalishwa kila mwaka kutokana na machafuko yasiyoisha
 
Abunwasi

JF-Expert Member
Jun 25, 2009
5,491
2,000
Kuhusu nadharia kadhaa za sababu ya muungano huu ikiwemo suala la Usalama wa Zanzibar baada ya Mapinduzi, Hofu ya Ukomunisti na mengine ambayo leo sio mada za mjadala huu, tunabaki kuiona nafasi ya ASP na baadae CCM katika kuidhoofisha hadhi ya Zanzibar kwenye Muungano.

Tuanzie hapo. Baada ya kuundwa Muungano ambao uhalali wake ulitiliwa mashaka na baddhi ya viongozi wa Zanzibar wa waKATI HUO KWA TARATIBU KUTOKAMILISHWA KUPATA BARAKA kWENYE BARAZA LA MAPINDUZI AU CHOMBO CHA UWAKILISHI CHA WANANCHI.

Kuliibuka zogo la mkataba wa Muungano na uhalali wake na ulivyotafsiriwa. Kuliibuka zogo la kuongezwa mambo ya Muungano kinyemela, kumeibuka sintofahamu mara kadhaa kwa kuandamwa wanaohoji muungano kwa kupata vitisho mbali mbali na kutokea matukio yasiyo majibu hadi leo.

Yaliyopita kabla mwaka 1977 ilipoundwa CCM tuyaache, tuanze hapo. CCM iliundwa mwaka huo kwa kuungana ASP na TANU. Kazi ya CCM sasa ni kuunganisha itikadi ya chama kuwa moja baada ya kufanikiwa Serikali mbili kuungana. CCM ilitumika kuuwa itikadi za ASP na TANU. Makao Makuu yakawa DODOMA.

Kuongezeka kwa mambo ya Muungano yalifanywa kipindi cha CCM hii hii kuwa madarakani. Kuondolewa nafasi ya Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais hapo miaka ya 1990 kulifanywa na CCM ikiwa ndio yenye maamuzi Bungeni.

Rais wa Zanzibar kuwa Waziri wa JMT asiye na Wizara Maalumu kulifanywa na kuridhiwa na CCM.

Kuendelea kunyanganywa nguvu za kimaamuzi kwa Zanzibar ndani ya Bunge kumefanywa na CCM hii hii leo inayotawala.

DHANA YA UKOLONI NDANI YA MUUNGANO.
Kuna hii dhana ambayo inapata mashiko. Zanzibar maamuzi yote kuhusu nani atawale yanafanywa Dodoma kupitia maamuzi ya CCM na kuwekewa kinga ya kiulinzi na Jamuhuri ya Muungano kwa kutumia Jeshi na vyombo vya Muungano.

Uraisi wa Zanzibar ni kilemba cha ukoka ambapo wazanzibari hawana maamuzi ya kumuweka Rais wao lazima Baraka zipite kutoka JMT. Serikali ya JMT ndio yenye jukumu la Ulinzi wa Jamuhuri na Usalama, Vyovyote iwavyo wanawajibika kuhakikisha yule wanayemtaka ndio anasdhika hatamu ( rejea chaguzi zote kuanzia 1995 hadi 2015) Licha ya kukiukwa kote kule kwa taratibu wao ndio wamehakikisha Uongozi uliopo unaendelea.

Zanzibar imebanwa kupitia taratibu za kuwa na maamuzi huru ya kiuchumi na mapato ya ndani, Inalazimika kuomba ridhaa Bara.

Dhana ya Ukoloni inakuja vile vile kwa kupandikizwa migogoro baina ya watu wa Zanzibar kwa Uongozi wa JMT kutumia Nyenzo zake kuchaguwa upande wa kufanya nao kazi na wala sio kusimamia haki kutendeka kila unapokuja uchaguzi. sio hayo tu kuna tetesi za kupandikizwa Viongozi kutoka Bara kushika nafasi za kichama na kiserikali huko Zanzibar.

Yaani Maslahi ya Bara yanapitia ndani ya CCM kisha ndani ya SMZ kuhakikisha azma inafikiwa.

Huu ni mkakati wa muda mrefu wa kuidhoofisha Zanzibar kwenye Muungano kuhakikisha kile kitu kinaitwa Serikali mbili kuelekea moja kinafikiwa ( a Matter of Time)
Bara inatumia mwanya wa Muungano kupandikiza watu wake kwenye CCM kushika nafasi za Uongozi Zanzibar na Serikalini na kuifanya Serikali ya Zanzibar kushindwa kuwa na msimamo wa kujisimamia MASLAHI YAKE KWENYE MUUNGANO ( TWO IN ONE)

Serikali ya JMT kutokuwa tayari kulitatuwa tatizo la Malalamiko ya muungano kutoka Zanzibar na badala yake kutumia vitisho na kauli kali kwa yoyote anayehoji Muungano ni ushahidi wa wazi kuwa Muungano una ajenda zake kuhusu kuipoteza Zanzibar na hapo ndipo hoja ya Ukoloni inapopata Nguvu kule Zanzibar.

Ikumbukwe kuwa ni CCM hii hii iliyofanya figisu kuharibu mapendekezo ya Katiba mpya ya Warioba ambayo walau iliyoonesha njia ya kutaka kuuweka sawa Muungano wetu.

CCM inabaki ndio injinia wa kuidhoofisha Zanzibar kwenye Muungano huu kwa njia tofauti.

Tujenge Muungano wa Haki kwa Maslahi ya Wote. Muungano ulianzia mahali fulani kamwe hiwezekani kusiwe na mahali pa kunzia kuondowa changamnoto zake na utatuzi wa migogoro yake.

Ukiona hayo yanafirigiswa ujue hao walioshikilia kunyamazisha watu ndio wakoloni wenyewe ikiwemo CCM ambae ndio mpishi mkuu.
Kishada.
Mmekuwa mkipata taabu sana na mnaendelea kupata ta abu sana kuzungumzia kitu ambacho wala hamkifahamu vizuri. Hizo kelele za uhalali wa muungano zimeelezwa na hivi sasa watu wanapiga kazi tu na kwa taarifa yenu ni kwa zanzibar ya juzi siyo ya leo. Nadhani itakuwa busara sana kama mtalalamikia mheshimiwa Trump wa US of A maana kwa sasa yeye ndiye mmbabe wa dunia.
 
KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,097
2,000
Mmekuwa mkipata taabu sana na mnaendelea kupata ta abu sana kuzungumzia kitu ambacho wala hamkifahamu vizuri. Hizo kelele za uhalali wa muungano zimeelezwa na hivi sasa watu wanapiga kazi tu na kwa taarifa yenu ni kwa zanzibar ya juzi siyo ya leo. Nadhani itakuwa busara sana kama mtalalamikia mheshimiwa Trump wa US of A maana kwa sasa yeye ndiye mmbabe wa dunia.
Aliyefahamu haya maelezo ajitokeze atufahamishe kwa njia inayoeleweka.
 
LIKE

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
4,533
2,000
Unaambiwa CCM Zanzibar sasa hawana tena nguvu za kuipigania Zanzibar ndani ya Muungano. Walishafanya makosa ambayo kujirudi ni vigumu. Wamebaki wakipewa vinafasi vya peremende ikiwa ni malipo ya ukibaraka. Waliuwa Afro Mama leo wanaendekeza matumbo.

Ukipata stori za wazee wa Zanzibar walivyolia siku ilipounganishwa ASP na TANU mara na wewe machozi yanakutoka. Njama za kuivuruga Zanzibar hazikuanzxa juzi. " Ni Ukoloni juu ya Ukoloni tu". Hizi ndizo lugha zilizoko Zanzibar.''..story za wazee wa Zanzibar walivyolia..''

itakuwa wanalipia madhila waliyomtenda John Okello

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MIMI BABA YENU

Senior Member
Mar 1, 2019
181
500
Bila shaka umeridhika kuhusu nafasi ya CCM kuidhoofisha Zanzibar kwenye Muungano.
CCM kushika dola bara na visiwani isikusumbue coz Kuna mafanikio mengi ya Muungano yanayozinufaisha nchi zote mbili kiuchumi na kisiasa na yamefanikishwa kwa juhudi za viongozi wa taifa na waasisi wa muungano (CCM na ASP chini ya Nyerere na Karume) ambapo mpaka sasa Zanzibar na Tanganyika zinatawaliwa na amani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom