CCM na refarii aliyepoteza kadi na filimbi

Mpambano unaendelea. Katikati ya mchezo,refa anagundua kuwa amepoteza kadi-ya njano na nyekundu pamoja na filimbi. Kutokana na kasi ya mchezo, anauchuna. Haisikiki filimbi wala haionekani kadi hata pale inapohitajika.

Wachezaji wanakatana mitama ya kiama lakini kimya. Wachezaji wanatukana na vikumbo kupigana lakini kimya. Mpira unatoka na kurushwa tena bila filimbi kupigwa.

Wachafu wanacheza rafu na wasafi wanachafuliwa. Wachezaji wanatamba kila namba na kujigamba. Refarii yuko kimya huku akionekana dhahiri shahiri kuwa kasi ya mchezo inamshida.

Anajikaza kisabuni tu. Anaendelea kukimbia hapa na pale akiomba tu mchezo uishe salama. Itasikika filimbi gani goli likifungwa? Atasemaje kuwa ni goli halali au haramu? Mpambano hauna mfano.

Refarii anafanya siri. Hasemi ukweli kama amepoteza filimbi na kadi. Anakufa na tai yake shingoni. Hata mchezaji kibaka naye kajichanganya mpirani na anakaribia kutangazwa 'man of the match'. CCM iko njia panda!

Mzee Tupatupa (kwasasa Dodoma)

Tutaheshimiana tu...CC lizaboni n cowards
 
Natamani nikuone make maandiko yako huwa yananikosha roho. Yeye Mwenyewe hakuwa mchezaji mzuri. ndo maana unaona hata uwezo wake wa kuchezesha ni mdogo tu.

Picha.png
 
Mzee @Vuta-Nikuvute huyu MUSSA ALLAN amechanganyikiwa kusikia kwamba Mtalichinjia mbali jina la Mgombea wake

Lakini kwa post yake mbona anaonekana kukata tamaa na Refarii,hana filimbi wa kadi zote njano na nyekundu,kwa hiyo mchezaji mwenye nguvu ndio anatamba uwanjani.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom