CCM na refarii aliyepoteza kadi na filimbi

CCM na refarii aliyepoteza kadi na filimbi

Nafumbua kwa kusema Kikwete amewaomba viongozi wa dini kuwapuuza wanaonunua Urais kwa pesa hivi yeye ameshindwaje kuwachukulia hatua?wakati filimbi anayo na kadi anazo? huyu ndie anayesemwa na mtoa mada
 
Nimekupenda sana leoo mzee tupatupa wa lumbamba kwa sasa Dodoma
 
Mzee wangu kweli una makengeza!!!!!! yaani haujaona jinsi refalii alivyovalia viatu! "amepiga kulwa na doto" huku NIKE kule REEBOK, ilimradi katupia tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Utenzi maridadi sana! Asante gwiji Shaaban Bin Robert II

Jana refa kakimbila kanisani Tanga kuomba Rehema za mwenyezi Mungu "filimbi ipatikane"; tena kutoka kwa wale wale anaosema ziku zote wasijihusishe na maswala ya kisiasa watayumbisha NJI; Alahaula Alahkwata!!
 
Mkuu @VUTANKUVUTE Refa wa chama cha mapinduzi hakuingia na filimbi,kadi ya manjano au nyekundu tangu mapema,alijua anayoenda kukabiliana nayo. Kwa sasa anachoombea ni mchezo uishe salama kwa mazingira ambayo hakuyatengeneza.
 
Mkuu umenikumbusha Enzi zile tunacheza mpira wa mchangani Enzi za utoto... kama huna viatu lwako,mwenye njumu sawa, mwenye fwato (viatu vya matairi)sawa, mwenye kuvua shati sawa, yaani kila mtu na anavyojiskia na mpira unachezwa hadi nyuma ya goli...golikipa anabadilishwa kila goli likiingia anabadilishana na mchezaji wa ndani anayembadili ukipa... mwenye mpira tu ndio mbabe...mkimzingua anabeba mpira huyoooo anaondoka zake na mechi inaishia hapo...sanasana mnabadili mchezo, wenye kuruka sarakasi haya, wenye kudaka panzi haya, wenye kurudi makwao haya.... Kweli CCM imenikumbusha mbali maana kumbe bado inacheza ile michezo ya kitoto na ukubwa wote huu

Yani ilikuwa balaa, ilikuwa ikibaki dakika 15 tunasema sasa tunafanya yale ya Nyota nyekundu (Red Star) ilikuwa unakimbia na mtu huku ukimlambisha njumu kwenye miguu.
 
Hivi kampeni hii ya watangaza nia wa ccm ingefanya na NLD ingekuwa vip au ndiyo strategy mpya 2015 kuanza kampeni kwa Hugo refa
 
walio cheza rafu za mwaka 2005,wakamshangaza mzee wetu mkapa, ndio watakao cheza rafu hiyohiyo
tuambiane ukweli tu ,kwamba ccm walichelewa kutafuta m badala wa huyo jamaa,sasa huyu waliomleta hawezi kumfunika jamaa huyo alieanza safari muda mrefu, NA PILI WAMEKOSEA KUMTUO KULE AMBAPO HAWATUTAKI na niwaambie kitu kwa manufaa yenu kuwa anaye ondoka madarakani hana nguvu kama anaetaka kuingia madarakani na kundi la waliokula nchi kipindi cha aliopo ni ndogo sana kuliko kundi la wanaotaka nao waonje matunda ya taifa hili kunawatu wapo chamani toka nyerere hawaujui unaibu wala uwaziri ccm hakuna makundi mengi kuna kundi la wanaotaka kubaki kwenye system ambao ni wachache,na kundi la wanaotaka kuingia ambalo ndio kundi kubwa na dalili ni kwamba wakikosea kumweka mtu ambae wengi wanamtaka msitarajie wakaungana mkono itakuwa ni ile statement ya chagua jiwe tukose wote. ,mwaka 2005 ilijidhihirisha pale mzee wetu jembe langu ever mzee benjamini mkapa alivyo baki akishangaa, NARUDIA KUSEMA ATAWASHANGAZA TENA MWAKA HUU.
 
Mimi naona hajapoteza filimbi wala kadi. Zote anazo ila kaamua kuuchuna kwa kukosa sifa ya kuchezesha. Hataki kuonekana kwamba hatua yoyote aliyoichukua kwenye mchezo iwe halali ama haramu imechangia kuanguka ama kushinda kwa aliyeshindwa ana kushinda.

Lakini kinachompa nguvu ya kufanya hivyo na kuendeleza mchezo kinyume na kanuni ni dharau kwa wachezaji, mashabiki na wadau wote wa mchezo kwamba hawana uwezo wa kumfanya lolote. Liwalo na liwe. Ni kama vile anasema, "walinichaguaje nichezeshe mchezo wakati wanajua sina uwezo?, Watajiju!, muda uishe, niende zangu nkajiandae kwa outing yangu".

Kosa linarudi kwa waliompa urefa huku wakijua mchezo siyo wake. Wayaone wenyewe!.
Big up sana mkulu.Hapa umenena
 
Nafumbua kwa kusema Kikwete amewaomba viongozi wa dini kuwapuuza wanaonunua Urais kwa pesa hivi yeye ameshindwaje kuwachukulia hatua?wakati filimbi anayo na kadi anazo? huyu ndie anayesemwa na mtoa mada


Yeye hana tofauti na joka la kibisa...lile joka kubwa la maigizo lisilo nga'ata
 
Utenzi maridadi sana! Asante gwiji Shaaban Bin Robert II

Jana refa kakimbila kanisani Tanga kuomba Rehema za mwenyezi Mungu "filimbi ipatikane"; tena kutoka kwa wale wale anaosema ziku zote wasijihusishe na maswala ya kisiasa watayumbisha NJI; Alahaula Alahkwata!!


Maisha yangu na baada ya miaka 50
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Swali langu kuhusu huyo refarii attamalizaje mpira kama hana filimbi?

Itabidi ale maharage, mayai, tende, maziwa mtindi akiachia moja tu kila mtu anatafuta njia yake na mpira utapasuka.😉
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom