Mkasa wa Mobutu Seseseko na Timu ya Taifa ya Zaire Kombe la Dunia mwaka 1974

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,783
66,962
Fainali za Kombe la Dunia la mwaka 1974 lilifanyika pale Ujerumani Magharibi ambapo wenyeji walifanikiwa kushinda kombe hilo kwa kuwafunga Uholanzi 2-1 katika mchezo wa fainali. Ujerumani waliongozwa na Franz Backenbeur Kaizer walistahili ushindi kwa 100%.

Katika Fainali hizo zilishiriki timu kadhaa ikiwemo Zaire ambayo ilikuwa ikishiriki Fainali hizo kwa mara ya kwanza huku ikiweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kushiriki Fainali hizo kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kabla kufuzu kwa Fainali hizo, Zaire walikuwa wametoka kutwaa ubingwa wa Afrika wakiongozwa na golikipa mahiri kuwahi kutokea nchini Zaire, Kazadi Mwamba, Kiungo hodari Ricky Mavuba na Straika matata Mulamba Ndaye ambaye mpaka leo anbakia na rekodi inayosimama ya kufunga magoli mengi zaidi (9) kwenye Afcon ya 1974. Kwahiyo Zaire ilikuwa imejengwa kwa kuwategema wachezaji hao watatu ambao ndio walikuwa mwanga wa timu.

Punde tu baada ya Zaire kufuzu Kombe la Dunia la Mwaka 1974, Rais wa Nchi hiyo Dikteta Mobutu Sesseeko Kuku Ngbendu Wa Zabanga alikiita kikosi cha Zaire katika kasri lake na kuwapa zawadi mbalimbali ikiwa ni motisha ya kutambua mchango wao katika kuliletea heshima Taifa hilo changa barani Afrika. Baadhi ya zawadi walizopewa wachezaji hao ni nyumba za kifahari pamoja na magari ya volkswagen ambayo kwa wakati huo yalikuwa ni magari ya kifahari sana. pia ripoti nyingine zinasema kuwa wachezaji hao waliishi kama wafalme.

Zaire (1).jpg

Muda wa mashindano ulipofika Zaire iliiagwa kwa heshima zote na kuahidiwa zawadi nono endapo tu ingefika walau raundi ya pili ya mashindano hayo (yaani ivuke hatua ya makundi tu). Timu iliondoka Zaire ikiwa na watu wengi sana pengine kuliko timu yoyote ile iliyoshiriki michuano hiyo. Licha ya wachezaji, makocha na benchi la ufundi, katika msafara huo pia walikuwepo baadhi ya Mawaziri katika kuhakikisha mambo yanakuwa sawa, pia walikuwepo maofisa wa jeshi la nchi hiyo na makachero wa idara ya usalama katika msafara huo.


Tuhuma za Uwepo wa Waganga 12 wa Jadi katika Msafara wa Timu
Kuna baadhi ya tuhuma zinadai wakati timu ya Zaire ikipanda pipa kuelekea Ujerumani, katika Msafara huo kulikuwa na waganga 12 ambao walitumwa na Rais Mobutu ili kwenda kufanya ndumba zao ambazo zingeweza kuwasaidia Zaire kufanya vizuri katika mashindano hayo. Mpaka leo tuhuma hizo hazikuwahi kuthibitishwa.

tribal-witch-doctors-cameroons-west-africa-circa-1935-RJRKYA.jpg

Wakati wa Mashindano
Michuano ilianza mapema tarehe 13 June mwaka 1974 ambapo Zaire ilikuwa kundi namba 2 ikiwa pamoja na timu ya Brazil (Bingwa mtetezi wa michuano), Scotland pamoja na Yugoslavia.

Mechi ya kwanza, June 14, Zaire alicheza na Scotland akaishia kupokea kichapo cha magoli 2-0. Kikosi cha Scotland kilikuwa na nyota kama Kenny Dalglish staa wa Liverpool kwa wakati huo, Dennis Law nyota wa Man Utd nk.

Mechi dhidi ya Yugoslavia
Mnamo Juni 18, Zaire iliyokuwa chini ya Kocha kutoka Yugoslavia, Blagoje Vidinic walikuwa wanashuka dimbani kucheza mchezo wao wa pili dhidi ya Yugoslavia. Kabla ya mechi hii, wachezaji wa Zaire waligomea mazoezi wakishinikiza walipwe pesa walizoahidiwa na serikali yao. FIFA ilibidi iingilie kati kwa kuwalipa Zaire ili waweze kucheza mchezo wao dhidi ya Yugoslavia. FIFA walifanya vile ili taswira y mashindano isiharibike.

Mechi ikafanyika katika jiji la Gilsenkichern, dakika ya 20 Zaire tayari alikuwa kashakula goli tatu. Dakika ya 21 tu, Kocha Bladoje Vidinic akaamua kumtoa mlinda mlango chaguo la kwanza Kazadi Mwamba na kumuingiza golikipa chaguo la tatu, Dimbi Tubilandu ambaye urafiki wake na mmoja wa wasaidizi wa Rais Mobutu ulimfanya apewe nafasi ya kucheza mchezo huo. Zaire ikapokea kipigo cha fedheha kutoka kwa Yugoslavia, mechi ikaisha Yugoslavia 9-0 Zaire.

Matokeo hayo yaliishtua Dunia, yakamshtua na Dikteta Mobutu ambaye yeye hakusafiri na timu alibaki tu nyumbani. Akahoji uwepo wa wale Waganga? Kwanini hawakupunguza idadi ya magoli? Waganga wakawa na kesi ya kujibu kwa Rais. Pia alimshutumu kocha wa Zaire ambaye ni mwenyeji wa Yugoslavia kwa kuisaidia nchi yake ya Yugoslavia kushinda kwa kishindo.

Haikuishia hapo, Dikteta Mobutu akawatuma wanajeshi wake waliokuwa kwenye msafara na timu kuwa mechi ya mwisho, Zaire Vs Brazil timu ya Zaire haitakiwi kuruhusu magoli zaidi ya matatu kwani kushindwa kufanya hivyo wachezaji wangeiingia matatani.

Mechi ya tatu na ya mwisho ilipigwa Juni 22, Zaire alipigwa 3-0, dakika ya 79 Brazil walipata faulo, wachezaji wa Zaire wakaweka ukuta, wakati refarii alipopuliza filimbi kuashiria Brazil wapige faulo ile ghafla beki Ilunga wa Zaire akatoka kwenye ukuta wao akaenda kuubutua ule mpira, kitendo kilichowashangaza wengi na akazawadiwa kadi ya njano, lakini wengi hawakujua kuwa alikuwa anapoteza muda ili Brazil wasipate goli la nne ambalo lingeweza kuwaweka matatani kikosi cha Zaire kutoka kwa Dikteta Mobutu aliyewaagiza wasifungwe zaidi ya goli 3.


Bahati ikawa kwao, mechi ikaisha 3-0, Zaire akatupwa nje ya mashindano kwa rekodi ya aibu katika historia ya Kombe la Dunia na hawakuwahi kufuzu tena mashindano hayo.

Baada ya Mashindano
Kocha wa Zaire raia wa Yugoslavia, Blagoje Vidinic akapewa ushauri na baadhi ya wadau kuwa asirudi nchini Zaire kwani angeenda kukumbana na mateso ya dikteta Mobutu. Hivyo akabaki hukohuko Ujerumani na baadae alirudi kwao. Wachezaji walipelekwa jeshini kwa adhabu zaidi kama hukumu ya kulidhalilisha Taifa. Wachezaji wale walipokonywa mali zao zote wakaishia kuishi katika lindi la umaskini wa kutupwa.

Ikawa mwisho kwa Rais Mobutu kuwekeza katika soka, akahamishia mapenzi yake katika mchezo wa ngumi ambapo aliandaa pambano maarufu la ngumi kati ya Muhamad Ali Vs George Foreman pambano ambalo pia hujulikana kama Rumble in the Jungle.

MWISHO
 

Attachments

  • zaire.jpg
    zaire.jpg
    110.2 KB · Views: 21
Nipo mkuu, Corona ndio baba lao siku hizi, ukifanya mchezo inakutwanga gwala. Tuombe iishe ili tuwe huru
Kabisa maana hali sio shwari kaka mie nimekambia mjini nipogo zangu Sangusangu huku taratibuu
 
Back
Top Bottom