CCM na refarii aliyepoteza kadi na filimbi

CCM na refarii aliyepoteza kadi na filimbi

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Mpambano unaendelea. Katikati ya mchezo,refa anagundua kuwa amepoteza kadi-ya njano na nyekundu pamoja na filimbi. Kutokana na kasi ya mchezo, anauchuna. Haisikiki filimbi wala haionekani kadi hata pale inapohitajika.

Wachezaji wanakatana mitama ya kiama lakini kimya. Wachezaji wanatukana na vikumbo kupigana lakini kimya. Mpira unatoka na kurushwa tena bila filimbi kupigwa.

Wachafu wanacheza rafu na wasafi wanachafuliwa. Wachezaji wanatamba kila namba na kujigamba. Refarii yuko kimya huku akionekana dhahiri shahiri kuwa kasi ya mchezo inamshida.

Anajikaza kisabuni tu. Anaendelea kukimbia hapa na pale akiomba tu mchezo uishe salama. Itasikika filimbi gani goli likifungwa? Atasemaje kuwa ni goli halali au haramu? Mpambano hauna mfano.

Refarii anafanya siri. Hasemi ukweli kama amepoteza filimbi na kadi. Anakufa na tai yake shingoni. Hata mchezaji kibaka naye kajichanganya mpirani na anakaribia kutangazwa 'man of the match'. CCM iko njia panda!

Mzee Tupatupa (kwasasa Dodoma)
 
Mzee tupatupa funguka, usiongee kwa mafumbo.Mwaga mtama.
 
Mimi naona hajapoteza filimbi wala kadi. Zote anazo ila kaamua kuuchuna kwa kukosa sifa ya kuchezesha. Hataki kuonekana kwamba hatua yoyote aliyoichukua kwenye mchezo iwe halali ama haramu imechangia kuanguka ama kushinda kwa aliyeshindwa ana kushinda.

Lakini kinachompa nguvu ya kufanya hivyo na kuendeleza mchezo kinyume na kanuni ni dharau kwa wachezaji, mashabiki na wadau wote wa mchezo kwamba hawana uwezo wa kumfanya lolote. Liwalo na liwe. Ni kama vile anasema, "walinichaguaje nichezeshe mchezo wakati wanajua sina uwezo?, Watajiju!, muda uishe, niende zangu nkajiandae kwa outing yangu".

Kosa linarudi kwa waliompa urefa huku wakijua mchezo siyo wake. Wayaone wenyewe!.


VUTA-NKUVUTE
 
Last edited by a moderator:
Ndiyo matatizo ya kumpa uongozi wa chama fisadi. Anajijua yeye ni mchafu kishawahi kutishwa kuhusu uchafu wake kuanikwa hadharani. Sasa hana uwezo wa kukemea lolote lile yupo yupo tu anaomba Mungu miezi hii michache ikatike haraka bila ya kutokea balaa lolote lile.
VUTA-NKUVUTE
 
Last edited by a moderator:
Mkuu umenikumbusha Enzi zile tunacheza mpira wa mchangani Enzi za utoto... kama huna viatu lwako,mwenye njumu sawa, mwenye fwato (viatu vya matairi)sawa, mwenye kuvua shati sawa, yaani kila mtu na anavyojiskia na mpira unachezwa hadi nyuma ya goli...golikipa anabadilishwa kila goli likiingia anabadilishana na mchezaji wa ndani anayembadili ukipa... mwenye mpira tu ndio mbabe...mkimzingua anabeba mpira huyoooo anaondoka zake na mechi inaishia hapo...sanasana mnabadili mchezo, wenye kuruka sarakasi haya, wenye kudaka panzi haya, wenye kurudi makwao haya.... Kweli CCM imenikumbusha mbali maana kumbe bado inacheza ile michezo ya kitoto na ukubwa wote huu
 
Mzee Tupa tupa,tatizo siyo filimbi wala kadi,tatizo Referii ni DHAIFU.Ukweli ni mchungu lakini inabidi kuusikia.

Ninasikitika huko kwenye maeneo yetu ,hatuna kijana wa kaliba ya JJ Mnyika,mwenye uwezo wa kupaza sauti na kusema jamani hiki siyo kijiko kikubwa bali ni chepeo!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom