CCM na PIPI kwa watoto, kulikoni?

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,062
Inaonekana CCM wameanza kamchezo ka kuwagawia sana pipi watoto kila wanapokwenda.....

Je hii inaonyesha ni upendo kwa watoto hao au kuna nia nyingine maana hawa watoto hata kura hawapigi kwa hiyo siwezi kusema wanafanya hivyo ili wapigiwe kura.

Vitoto vyote viko hoi si kawaida. Heri hata ya vile vinaletwa kwa Rais maana vinakuwa vimeandaliwa ila hivi vya Nape, nywele kipilipili kama AVATAR ya Nyani Ngambu...... Nakaribisha wachambuzi wa picha.....

165681_10150357294655405_474836185404_16246385_5374759_n.jpg
 
Nape nayeye...... Ila yeye hapa alisababisha mtafaruku baada ya watoto kuanza kugombea Pipi. Yaani ukiona watoto wanagombea pipi na ukiwaangalia watoto wenyewe, ina maana hawana uwezo kabisa wa kununua Pipi hizo..... Waya mkali sanasana.

attachment.php
 
Mgawo wa umeme unaende..........ahhh samahani ni Pipi bado zinaendelea.

images
 
angewagawia walau na vitana,manake nywele vipilipili hizo wasipozizoesha kuzichana wakiwa masharobaby ndo mambo ya nywele za maiti! my poor country!
 
King'asti,

Halafu jamaa hata huruma halina. Unaona kabisa dogo amezidiwa nguvu na dogo mwenzie ambaye ni mkubwa kwake. Wananyang'anyana hizo pipi na yeye badala ya kusema STOP na afanye mgawo vizuri, LINACHEKELEA.....

Ni kitendo cha kusikitisha sana. Inabidi kutengeneza picha na kuwarushia Wazazi wao.

ONENI JAMAA ANAVYOWACHEKA WATOTO WENU KUGOMBEA PIPI.
 
Did u really mean that? Mzazi wa mtoto kama huyo hiyo picha unamrushia kwa njia ipi? email?skype?facebook?posta?fax?
Na hata ukimpelekea kwa mikono..mzazi wa mtoto kama huyo anaweza kuchukua hatua gani!??
 
Kwani unadhani wazazi wao hao watoto ni Mabwege? Ndiyo maana Mwakyembe akasema "Watanzania si mabwege tena......"

Ukiwaambia Watanzania wanaelewa. Wengi somo la uraia linaanza kuwaingia vema kichwani.

Ukiwapa hiyo picha na maelezo kidogo......... Picha inasema zaidi ya maneno milioni ngapi vile?

Mie nilishashuhudia jamaa aliyekuwa kaweka Picha la Kikwete nyumbani kwake kijijini kwetu. tulipompa somo jinsi wenzake wanavyokula nchi hii, jamaa asubuhi tunaenda tukakuta Posta lote kalichoma moto kwa hasira.......

Back
Top Bottom