MKUU NI KWELI KABISA HAYO ULIYOWATAARIFU KURUTA WATARAJIWA.MIMI NILIKUWA KAMBI YA JKT MGAMBO ILIYOPO KABUKU WILAYA YA HANDENI.SIKU MOJA NILIMTOKA MP ALIYETAKA KUNIPA DRILL NIKAJONGOMEA KWENYE SHAMBA LA michungwa nikawa nashindia na kulalia machungwa (yaani kula lunch na diner ya machungwa tu) kwa siku mbili mfululizo.
Hapa umeua mwana wane!
Yaani nimecheka pamoja na kwamba niko peke yangu kwenye computer! Lunch na dinner ya Machungwa hii ni noma mwanangu sijawahi kuisikia. Ilikuwaje mkuu hiyo lunch na dinner? Yaani huu uhondo niliukosa kwa ncha ya sindano Nyamb..f zao waliopitisha maamuzi ya kufuta JKT kipindi cha mwaka 1994. Niliishia kujaza fomu na kupokea joining instructions nikiwa nimepangiwa MLALE JKT. Kitisho kikubwa ilikuwa mnaenda kwenye shamba la mahindi linaloitwa DUNIA. Mkuu nilikuwa nimejiandaa kikamilifu.
Tunajiandaa Januari tuende kulipoti shenzi wakafuta JKT aaaagh!!! Hao vijana ngoja waende. Wallah hata mimi umri ungekuwa bado unaruhusu ningejiandikisha. HONGERA ZENU WAKUU MLIOPITIA HUKO!!
Mwisho wa umri ni 45 Mwalimu Baba wa Taifa, Mzee Kawawa, Mzee Kahama et al.. walienda wakiwa watu wazima zaidi.
In fact wabunge wote ambao hawajapita JKT inafaa waende labda wata behave inavyostahili huko Bungeni.
Pia nadhani ingekuwa ni sifa mojawapo kwenye CV kwamba ni COMPULSORY kuwa umepita JKT ndipo ugombee ubunge, udiwani, etc.
MKUU NI KWELI KABISA HAYO ULIYOWATAARIFU KURUTA WATARAJIWA.MIMI NILIKUWA KAMBI YA JKT MGAMBO ILIYOPO KABUKU WILAYA YA HANDENI.SIKU MOJA NILIMTOKA MP ALIYETAKA KUNIPA DRILL NIKAJONGOMEA KWENYE SHAMBA LA michungwa nikawa nashindia na kulalia machungwa (yaani kula lunch na diner ya machungwa tu) kwa siku mbili mfululizo.
Mkuu hawa jamaa wa sasa hivi hawawezi kutuvunja miguu? Miaka 45 mbona ni kasheshe? Ila hawa wabunge kwa kweli inastahili wapelekwe huko. Hayo matusi yakina Lusi labda yatapungua. Ila nina wasiwasi na hao jamaa wa gheshi letu kama hawatatoa upendeleo! Utakuta jamaa wanapangiwa vitengo vizuri vizuri ili wapumue. Huyu Mr. DHAIFU naye si ashauri watu wote ambao hawakupitia JKT warudi huko japo kwa miezi 6 tu kama alivyofanya baba wa Taifa miaka ile.