CCM na Mategemeo yao JKT

CCM na Mategemeo yao JKT

OH YES

1.MWINGULU MCHEMBA
2.ALI MWINYI
3.NAPE NNAUYE
4.WILLIAM MALECELA
5.JANUARY MAKAMBA

Yes, Na zaidi Hawa watoto wa wakubwa AZIMIO la ZANZIBAR LILIWACHUNGA na Kuvunja JKT sasa wanaona

Ubaya wake? Too late President Mwinyi; Oh Kikwete Riz1 atakwenda?

We nawewe sijui upo Nchi gani!!Nape aka Vuvuzela naye ni Mbunge?
 
This is bullshit. Hatuwachagui wabunge kupiga kwata bali kutunga sheria, na kulinda katiba. Mbona mnachanganya apples and oranges? Sijawahi kuona hii eti watunga sheria waende jeshini. Kweli CCM imeishiwa sera. Hili swala inabidi lipingwe kwa nguvu zote. Kujiunga jeshi inabidi iwe ihari na sio lazima otherwise we have an emergency.

Hizo pesa si bora zitumike kwa mambo mengine muhimu kama shule, madawati, vitabu, maji na umeme.

Again, this is bullshit-
 
Tatizo la Nchi hii sio vijana kutopita JKT na kamwe Jkt haiwezi kusaidia lolote...Nchi imeoza kwa ufisadi na wizi wakutisha kuanzia kwa viongozi wa jeshi hadi kwa wakuu wa Serikali,eti leo mnakuja na habari zakupeleka vijana jkt kuleta uzalendo ivi huwa mnafikirisha bongo zenu kweli!!Uzalendo utakuwepo pale tu hiki chama cha mafisadi kitaondoshwa madarakani na mijizi yote kufikishwa mahakamani,kufilisiwa nakufungwa bila kujali cheo chake na mali zake alizoliibia Taifa.
 
We nawewe sijui upo Nchi gani!!Nape aka Vuvuzela naye ni Mbunge?[/QUOTE

Haukumbuki Aligombea UBUNGE wakamtoa ki-vuvuzela? Unajuaje hana Mpango wa kugombea tena?

Acha kuwa na fikra fupi... kuwa na historia na UJUE ALIANZIA WAPI KWANZA
 
Mbunge kijana ndo ana umri gani?

Jamani hawa waandishi wa habari na Wabunge wanamatatizo gani lakini hata kukubali taarifa zisizokamilifu?
 
Dah! Naitamani sana hii programme bt unfortunately form six nlimaliza 2007.......
 
OH YES

1.MWINGULU MCHEMBA
2.ALI MWINYI
3.NAPE NNAUYE
4.WILLIAM MALECELA
5.JANUARY MAKAMBA

Yes, Na zaidi Hawa watoto wa wakubwa AZIMIO la ZANZIBAR LILIWACHUNGA na Kuvunja JKT sasa wanaona

Ubaya wake? Too late President Mwinyi; Oh Kikwete Riz1 atakwenda?

Vipi ni VITU malumu wapya au?
 
Malelea akatafutwe nasikia bado hajapatikana. kuruta wakavae green vest za njano au kijani. Pia wajichunge sana na ugonjwa wa osmosis, test tube etc,
 
kwanza itawafanya wawe fiti hata wanapofuatiliwa na majasusi na watakua sio waoga
napendekeza wapewe na mafunzo ya kijeshi kuwaimarisha zaidi kiulinzi
 
Hii imenikumbusha mbali sana, miezi sita hadi kufika rank ya uservice ilikuwa kama miaka. Kuna maafande wengi walikuwa wanapenda kusimamisha milingoti na makuruta usiku jambo la kujihadhari sana. Hii intake ya kwanza na hao jamaa wana kiu mbovu.
Ni baada tu ya kuhitimu kidato cha sita, wanafunzi wote baada ya paper ya mwisho tunaanza kupitia list nani kachaguliwa kwenda kambi ipi. Mimi nasoma nakuta natakiwa kureport MAKUTUPORA –Dom.

Naangalia list zaidi nakuta na rafiki yangu naye kapangwa makutupora – Tunapanga tukutane Dom ili tupange safari wote, tunaagana kwa likizo fupi majumbani kuaga wazazi wetu maana tuendako ni pagumu.

Wakati ule hakuna simu za mkononi, ila tunaitikia ahadi tunakutana Dodoma stend ile tarehe husika ilipofika, mimi namshauri rafiki yangu (ambaye kwa sasa ni Meja wa Jeshi) tuende Jpili na si leo ijumaa, Jumapili ni siku ya mapumziko kwa hiyo tutapata muda wa kuzoea kambi kabla ya kuanza mafunzo Jtatu asubuhi – tunakubaliana tunaondoka wote kwa mjomba wangu for two days rest.

Jumapili saa nane tunapanda gari tayari safari ya kuanza maisha ya JESHI. Mimi na yeye na mabegi yetu madogo mwili ukiwa tayari kwa lolote lile, ndani yamoyo wangu ni wasiwasi tu hivi kukuje huko? Mara konda anapita oyaa mnaenda wapi? Natamka tunaenda Makutupora JKT, watu kwenye basi wanageuka kutuagalia moyo unazidi kudunda mmhh kulikoni watu kuhamaki.

Nyie wa JKT haya mmeshafika, nauli tafadhali!! Tunalipa nauli tunachukua mabegi yetu gari inaondoka natamani irudi tuondoke nayo; Mbele naona Nembo ya jeshi,
JESHI LA KUJENGA TAIFA
MAKUTUPORA JKT.
UTII NA UKAKAMAVU ( Sikumbuki maandishi yote)

Tunatembea kwa tahadhali kubwa, hakuna anayeongea na mwenzake – ndani ya kambi naona kwa mbali watu wanakimbia kimbia nikahisi basi wale ni wenzetu ila wamepewa vibukta na Tshet za kijani, Mara tunasikia sauti ya juu ---
Kruta chuchumaa Chini—(hapo najua mziki sasa umeanza, huku najiuliza mbona leo ni jumapili hawa hawana weekend?)
Weka begi mgongoni – haya ruka kichura mpaka hapa tulipo (huyo alikuwa askari wa zamu lango kuu la kuingilia kambini)
Tulitii amri ile tukaruka kichura hadi main gate ---
Simama juu --- chuchumaa – amri hii ilidumu kama dakika tano aisee nikahisi ugali niliokula home unaanza kurudi kwenye koromeo taratibuu)

Baada ya hapo ni kupewa sheria za kambi ---1. Kila kitu unachoambiwa lazima ujibu – NDIYO AFANDE 2. Marufuku kutembea sababu Kruta hujafundiswa 3. Kila uendako hakikisha una Mestin (bakuli la msosi). Kanuni zingine mtazipata kombania – wewe (mimi) umepangiwa D copy na wewe A coy. Hapo ndiyo ukawa mwisho wetu maana tayari tumetenganishwa na rafiki yangu – kweli maisha mapya nitaweza kuumaliza mwaka mzima humu. Najiuliza nikiwa nimepoteza matumaini.

Naondoka na begi langu mwendo ni wa mbwa, yaani kukimbia hadi Kombania namkuta Sajenti pamoja na Kopro – haya Kruta chukua vifaa – hapo napewa Bukta, Fulana, zote za kijani Buti na mestini. Hawa jamaa mbona hawaangali size? Najiuliza kwa mshangao, kweli nimepewa bukta na fulana kubwa mno lakini nimeambiwa hakuna kuuliza swali hapa.

Nafika Hangani ( bweni ) nakutana na kuruta wenzengu, najitahidi kuwazoea kwa haraka hasa wale waliotoka kidato cha sita – nakutana na baadhi tuliosoma nao o’level Napata moyo wa maisha mapya, kabla hata sijaweka vitu vyangu nasikia filimbi – jamaa wananiambia kimbia twenda kombania afande kaja, aisee maisha naona magumu mno. Kombania nakutana na wasichana wengi tu, duh aisee moyo unaanza kuwa na imani, wote wamevaa vibukta na Tshit za kijani, kasoro mimi kwani sikupata muda wa kuvaa. Mara nasikia KRUTA WA DANGER –Jamaa wote wanajibu AFANDEEEEE!!!; Nawapa dakika 20 nikirudi nikute vyura wanalia kwenye hayo maua --- Wanajibu na mimi najitahidi kuzoea -- NDIYO AFANDEEE!!! Cha kushangaza hakuna ndoo, bomba ni moja maji yanatoka kidogo sana, sasa tumwagilie bustani hadi vyura walie --- naona mambo ya ajabu haya ila wenzangu waliofika mapema wameshazoea, wanachukua mestini zao foleni kukinga maji. hilo ndilo Jeshi -- Hakuna kuhoji hakuna Kutafakari ni Kutii amri.

Inafika saa tatu naambiwa jiandae tunaenda DISCO, duh kuna disko huku? nakumbuka aaahh leo ni Jpili kumbe ni Disco day -- kabla hata sijamaliza kufikiri zaidi naambiwa si DISCO la kucheza ni DISCO la kuimba kwa hiyo kumbuka wimbo wowote ule maana wewe lazima utachaguliwa na afande uimbishe - aisee maisha mapya kabisa.
Kweli zilikuwa Nyimbo za kupeana matumaini, nyimbo za ujasiri na hata nyimbo za kushekesha kama mabata madogo madogo yanaogelea......nk.


Wakuu hiyo ndiyo ilikuwa siku ya kwanza JKT – kwa hiyo wabunge vijana mnaotaka kuandika majina yenu kwenda kulitumia Taifa (JKT) hakuna mwongozo wa spika kule, kule kila kitu unachoambiwa jibu ni NDIYO AFANDE – hakuna kuhoji wala kutafakari na hiyo ndiyo amri ya JESHI. Kwa hiyo kina Mnyika, Nasari, Zitto, Mchemba, Kafulila, Mdee, Makamba, Sugu na wengineo mkiandika majina basi msisahau kwenda kuaga makwenu maana lazima mrudi na alama unless muwe treated kama waheshimiwa kitu ambacho hakitakuwa na maana yoyote.

Otherwise ni sehemu ya kufurahia na uzuri wa jeshi Siku ikiisha basi imeisha, Hakuna mambo ya Jana ulitoroka NO; na kazi kubwa ya kutumia ubongo kule ni jinsi ya kumtoroka Afande wakati anapanga kazi ila uhakikishe unakula bila kukushika, akikushika utakula chakula vizuri ila utaanza doso kafie kwenu ambapo lazima msosi wote uliokula utokee mdomoni bila mpangilio.

Ni maisha mapya ya kufurahisha ingawa kuna siku utalia na kukumbuka wazazi wako.

Baadhi ya misemo kuje JESHINI
Kalinyekalinye - adhabu
Songombigo – adhabu kali
Doso kafie kwenu – hii lazima upimwe afya kwanza kabla hujaanza kuitumikia
Usawa wa Gudulia – Kwenye sufuria la msosi
Kujongomea –kutoroka
,Kichele – Kipindi hicho tulikuwa tunapata mshahara kwa mwezi – sikumbuki bei gani ila ilikuwa kidogo sana

OPERATION VYAMA VINGI – MAKUTUPORA JKT.
Kwa wale mnaokumbuka tulicheza gwalide la kufuzu kwa niamba ya kambi zote nchini – Mgeni rasmi alikuwa Mzee J. Malecela – wakati huo waziri mkuu. something to remember in life time. Go and Enjoy!!!
 
mwaka 2005 wakati jk ana miaka takribani 52 tuliambiwa ni kijana kwa hiyo lusinde anaingia humu,lukuvi naye ndani
 
Yaani Mheshimiwa Waziri hakuna kitu kingine kizuri kwa Watanzania ukiachilia mbali kujiunga JKT nikiwa MP??

Na hii ni kwa mujibu wa sheria au ni kwa mujibu wa sera za CCM?

Plse lets know?? Kama kuwafanya wazalendo hata hao walioenda ndo mafisadi namba one and lets fear God men and women of God of this nation. Wazalendo gani wakati hamsemi 4bln for clearance of tractors from the Port??

Don mislead us.
 
Wabunge wa CDM wawe makini sana na hii programu ya JKT. Kama inawezekana wasijiunge na mafunzo hayo; wanaweza potezewa mbali kabisa halafu watasingizia mafunzo
 
Mimi naomba waanze na wabunge hawa Vijana, vinginevyo CDM msikubali kwenda huko JKT
1. Dr. Hussein Mwinyi
2. Dr. Emmanuel Nchimbi
3. Dr. mathayo David Mathayo
4. Ummi Mwaalim
5. Angela Kairuki
6. January Makamba
7. Wliiam Ngereja
8. Steven Massele
9. George Simbachawene
10. Mwigulu Nchemba
11. Amos Makalla
12. Lazaro Nyalandu
13. Adamu Malima
14. Janeth Mbena

Waanze mawaziri na manaibu wote ambao hawakupitia JKT. Kama ni kisima CCM mlikuwa mnachimba mtatumbukiwa wenyewe!
 
Kwa CCM JK ni kijana. Kwa kipimo hicho hakuna atakayebaki pale mjengoni. Wasira naye ndani.
 
Back
Top Bottom