Ni baada tu ya kuhitimu kidato cha sita, wanafunzi wote baada ya paper ya mwisho tunaanza kupitia list nani kachaguliwa kwenda kambi ipi. Mimi nasoma nakuta natakiwa kureport MAKUTUPORA –Dom.
Naangalia list zaidi nakuta na rafiki yangu naye kapangwa makutupora – Tunapanga tukutane Dom ili tupange safari wote, tunaagana kwa likizo fupi majumbani kuaga wazazi wetu maana tuendako ni pagumu.
Wakati ule hakuna simu za mkononi, ila tunaitikia ahadi tunakutana Dodoma stend ile tarehe husika ilipofika, mimi namshauri rafiki yangu (ambaye kwa sasa ni Meja wa Jeshi) tuende Jpili na si leo ijumaa, Jumapili ni siku ya mapumziko kwa hiyo tutapata muda wa kuzoea kambi kabla ya kuanza mafunzo Jtatu asubuhi – tunakubaliana tunaondoka wote kwa mjomba wangu for two days rest.
Jumapili saa nane tunapanda gari tayari safari ya kuanza maisha ya JESHI. Mimi na yeye na mabegi yetu madogo mwili ukiwa tayari kwa lolote lile, ndani yamoyo wangu ni wasiwasi tu hivi kukuje huko? Mara konda anapita oyaa mnaenda wapi? Natamka tunaenda Makutupora JKT, watu kwenye basi wanageuka kutuagalia moyo unazidi kudunda mmhh kulikoni watu kuhamaki.
Nyie wa JKT haya mmeshafika, nauli tafadhali!! Tunalipa nauli tunachukua mabegi yetu gari inaondoka natamani irudi tuondoke nayo; Mbele naona Nembo ya jeshi,
JESHI LA KUJENGA TAIFA
MAKUTUPORA JKT.
UTII NA UKAKAMAVU ( Sikumbuki maandishi yote)
Tunatembea kwa tahadhali kubwa, hakuna anayeongea na mwenzake – ndani ya kambi naona kwa mbali watu wanakimbia kimbia nikahisi basi wale ni wenzetu ila wamepewa vibukta na Tshet za kijani, Mara tunasikia sauti ya juu ---
Kruta chuchumaa Chini-(hapo najua mziki sasa umeanza, huku najiuliza mbona leo ni jumapili hawa hawana weekend?)
Weka begi mgongoni – haya ruka kichura mpaka hapa tulipo (huyo alikuwa askari wa zamu lango kuu la kuingilia kambini)
Tulitii amri ile tukaruka kichura hadi main gate ---
Simama juu --- chuchumaa – amri hii ilidumu kama dakika tano aisee nikahisi ugali niliokula home unaanza kurudi kwenye koromeo taratibuu)
Baada ya hapo ni kupewa sheria za kambi ---1. Kila kitu unachoambiwa lazima ujibu – NDIYO AFANDE 2. Marufuku kutembea sababu Kruta hujafundiswa 3. Kila uendako hakikisha una Mestin (bakuli la msosi). Kanuni zingine mtazipata kombania – wewe (mimi) umepangiwa D copy na wewe A coy. Hapo ndiyo ukawa mwisho wetu maana tayari tumetenganishwa na rafiki yangu – kweli maisha mapya nitaweza kuumaliza mwaka mzima humu. Najiuliza nikiwa nimepoteza matumaini.
Naondoka na begi langu mwendo ni wa mbwa, yaani kukimbia hadi Kombania namkuta Sajenti pamoja na Kopro – haya Kruta chukua vifaa – hapo napewa Bukta, Fulana, zote za kijani Buti na mestini. Hawa jamaa mbona hawaangali size? Najiuliza kwa mshangao, kweli nimepewa bukta na fulana kubwa mno lakini nimeambiwa hakuna kuuliza swali hapa.
Nafika Hangani ( bweni ) nakutana na kuruta wenzengu, najitahidi kuwazoea kwa haraka hasa wale waliotoka kidato cha sita – nakutana na baadhi tuliosoma nao o'level Napata moyo wa maisha mapya, kabla hata sijaweka vitu vyangu nasikia filimbi – jamaa wananiambia kimbia twenda kombania afande kaja, aisee maisha naona magumu mno. Kombania nakutana na wasichana wengi tu, duh aisee moyo unaanza kuwa na imani, wote wamevaa vibukta na Tshit za kijani, kasoro mimi kwani sikupata muda wa kuvaa. Mara nasikia KRUTA WA DANGER –Jamaa wote wanajibu AFANDEEEEE!!!; Nawapa dakika 20 nikirudi nikute vyura wanalia kwenye hayo maua --- Wanajibu na mimi najitahidi kuzoea -- NDIYO AFANDEEE!!! Cha kushangaza hakuna ndoo, bomba ni moja maji yanatoka kidogo sana, sasa tumwagilie bustani hadi vyura walie --- naona mambo ya ajabu haya ila wenzangu waliofika mapema wameshazoea, wanachukua mestini zao foleni kukinga maji. hilo ndilo Jeshi -- Hakuna kuhoji hakuna Kutafakari ni Kutii amri.
Inafika saa tatu naambiwa jiandae tunaenda DISCO, duh kuna disko huku? nakumbuka aaahh leo ni Jpili kumbe ni Disco day -- kabla hata sijamaliza kufikiri zaidi naambiwa si DISCO la kucheza ni DISCO la kuimba kwa hiyo kumbuka wimbo wowote ule maana wewe lazima utachaguliwa na afande uimbishe - aisee maisha mapya kabisa.
Kweli zilikuwa Nyimbo za kupeana matumaini, nyimbo za ujasiri na hata nyimbo za kushekesha kama mabata madogo madogo yanaogelea......nk.
Wakuu hiyo ndiyo ilikuwa siku ya kwanza JKT – kwa hiyo wabunge vijana mnaotaka kuandika majina yenu kwenda kulitumia Taifa (JKT) hakuna mwongozo wa spika kule, kule kila kitu unachoambiwa jibu ni NDIYO AFANDE – hakuna kuhoji wala kutafakari na hiyo ndiyo amri ya JESHI. Kwa hiyo kina Mnyika, Nasari, Zitto, Mchemba, Kafulila, Mdee, Makamba, Sugu na wengineo mkiandika majina basi msisahau kwenda kuaga makwenu maana lazima mrudi na alama unless muwe treated kama waheshimiwa kitu ambacho hakitakuwa na maana yoyote.
Otherwise ni sehemu ya kufurahia na uzuri wa jeshi Siku ikiisha basi imeisha, Hakuna mambo ya Jana ulitoroka NO; na kazi kubwa ya kutumia ubongo kule ni jinsi ya kumtoroka Afande wakati anapanga kazi ila uhakikishe unakula bila kukushika, akikushika utakula chakula vizuri ila utaanza doso kafie kwenu ambapo lazima msosi wote uliokula utokee mdomoni bila mpangilio.
Ni maisha mapya ya kufurahisha ingawa kuna siku utalia na kukumbuka wazazi wako.
Baadhi ya misemo kuje JESHINI
Kalinyekalinye - adhabu
Songombigo – adhabu kali
Doso kafie kwenu – hii lazima upimwe afya kwanza kabla hujaanza kuitumikia
Usawa wa Gudulia – Kwenye sufuria la msosi
Kujongomea –kutoroka
,Kichele – Kipindi hicho tulikuwa tunapata mshahara kwa mwezi – sikumbuki bei gani ila ilikuwa kidogo sana
OPERATION VYAMA VINGI – MAKUTUPORA JKT.
Kwa wale mnaokumbuka tulicheza gwalide la kufuzu kwa niamba ya kambi zote nchini – Mgeni rasmi alikuwa Mzee J. Malecela – wakati huo waziri mkuu. something to remember in life time. Go and Enjoy!!!