Makala kama kweli ni mkweli yeye alitakiwa kuwapa waandishi wa habari hizi risiti wazione na awape copy waweke hadharani maana si siri ila alitaka ukweli . Tutajuaje kama risiti hizo ni za magari yaliyo bandarini ? Why idadi inapungiua tena na wakati wakubwa wake walisema ni 200 ? Je baada ya kumwita Slaa muongo ndiyo hawaendi mahakamani kama walivyo tamka ? Bado kuna siri kubwa ukweli mwingi umefichwa.Ngojeeni Slaa akiibuka .
Lunyungu,
Mpeni Dr. Slaa data za ukweli. Akikosea mara mbili au tatu kama alivyofanya kweli hili la magari, tayari mnakuwa mmewapa CCM ngao ya kummaliza. Kumbuka ya Mrema, alikuwa analipua mabomu ya kweli lakini baada ya muda CCM wakaanza kumpelekea data fake ili aumbuke na kuonekana mwongo.
Ni mategemeo yangu hatutaenda huko na Dr. Slaa. Hii habari sio siri Dr. Slaa ameongea kitu ambacho sio ukweli.