CCM na magari ya uchaguzi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na magari ya uchaguzi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Dec 22, 2009.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Dec 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Kuna taarifa za ndani kuwa kuna zaidi ya magari 200 yameingia jijini Dar es Salaam kupitia bandari hiyohiyo, wasiwasi wangu ni kama yamelipiwa ushuru...

  Tetesi nilizo nazo tayari yamezua mzozo mkubwa ndani ya wakuu TRA na issue mpaka imemfikia Dr. Slaa ambaye anasisitiza patachimbika... Kama hayajalipiwa ushuru, kuna msamaha wanastahili kama chama? Chini ya sheria gani? Ni applicable kwa vyama vyote?
   
 2. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  hawa jamaa ni wasanii! Hata wakibanwa kulipa, zitatoka huko huko (TRA) kulipia....
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Here we go again.....
   
 4. A

  AmaniKatoshi Senior Member

  #4
  Dec 22, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Dk. Slaa ailipua CCM

  • Serikali mkoani Tanga yahaha kuizuia helikopta ya Mbowe isiruke
  na Waandishi Wetu, Tanga

  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, jana alifichua ufisadi mkubwa uliofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuingiza magari 200 aina ya Land Cruiser ‘mkonga' bila ya kulipia sh milioni 600 za ushuru wa forodha kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

  Dk. Slaa aliyasema hayo jana katika mkutano mkubwa wa hadhara wa muendelezo wa Operesheni Sangara uliofanyika katika Kijiji cha Kilole wilayani Korogwe. Alisema amepokea taarifa hiyo jana kutoka kwa msiri wake ndani ya TRA.

  Alisema hana ugomvi na CCM kuingiza magari 200 kwa ajili ya kupata ushindi mwaka 2010, lakini ugomvi wake mkubwa ni chama hicho kutoyalipia magari hayo ushuru wa sh milioni 600 ambazo zingewasaidia Watanzania katika kujenga nchi kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo.

  Akizungumza kwa kujiamini, alisema suala hilo lina ukweli usiokanushika. Alimtaka na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kama anaweza akanushe.

  "Taarifa hii nimeipata leo, na ina ukweli ndani yake. Hivi ninavyoongea yanaweza kutolewa muda wowote bandarini. Kama suala hili ni uongo, Pinda akanushe. Na wakilipa leo waandike tarehe risiti ya leo kwa kuwa hadi ninavyoongea hayajalipiwa," alisema Dk. Slaa.

  Alisema huo ni ufisadi mkubwa ambao unafanywa na CCM wakati vyama vingine vinalipa ushuru.

  Dk. Slaa alisema kuwa mwaka 2005 CCM ilifanya ufisadi kama huo kwa kumtumia mfanyabishara mwenye asili ya Kiasia, Jeetu Patel, na kufanikiwa kuingiza magari 235 bila kulipia ushuru pia.

  Alisema viongozi wote wa CCM wamewekana katika nafasi za uongozi, ndiyo sababu maadili katika nafasi za uongozi wa kiserikali na taasisi zake yamemong'onyoka.

  Katika hatua nyingine, Dk. Slaa ameeleza kushangazwa na kitendo cha Mbunge wa Jimbo la Mlalo, Brigedia Jenerali Mstaafu Hassan Ngwilizi, kutowaeleza wapiga kura wake matumizi ya fedha za miradi zinazotolewa na wahisani mbalimbali.

  Akihutubia katika mkutano wa hadhara wa Operesheni Sangara, katika Kijiji cha Lukozi wilayani Lushoto juzi, Dk. Slaa alielezea wasiwasi wake kuhusu matumizi mabaya ya fedha hizo zinazotolewa kwa maendeleo ya vijijini mara baada ya kupewa taarifa na wananchi wa kijiji hicho.

  Alisema kushindwa kutoa taarifa ya matumizi na kiasi cha fedha zinazotolewa na wahisani kwa wananchi ni ufisadi unaofanywa na viongozi, hususan mbunge wa jimbo hilo, ambaye ni mmoja wa wahusika wakubwa wa kusimamia miradi ya maendeleo vijijini.

  Akifafanua kuhusu baadhi ya fedha zinazotolewa na wahisani kwa maendeleo ya wananchi vijijini kupitia halmashauri za wilaya alisema ni pamoja na zinazotolewa na Mfuko wa Capital Development Fund (CDF) na Local Gavernment Programme (LGCP), ambazo hutolewa kwa kila mtu anayeishi vijijini.

  "Mnataka kuniambia kuwa hamjui kama kuna fedha zinatolewa na wahisani kwa ajili ya maendeleo ya vijijini na wala hamjawahi kuzisikia? Kama ni kweli muulizeni mbunge wenu, huyo ndiyo anajua ziliko, maana mimi ni mbunge kama yeye najua zinatolewa fedha hizo na kama hamjaziona basi ziko mfukoni mwake," alifafanua.

  Alisema kuwa wahisani mbalimbali hutoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo zinaelekezwa kwa wananchi kupitia halmashauri za wilaya, hatimaye kuwasilishwa kwa uongozi wa vijiji ambao nao hupanga matumizi na kuyawasilisha kwa halmashauri kuu.

  Katika ufafanuzi wake kwa wananchi kuhusu fedha hizo, Dk. Slaa alibainisha kuwa, wahisani hutoa kiasi cha dola za Kimarekani 1.5 kwa kila kichwa, kwa maana ya kila mtu hata mtoto mchanga.

  "Nataka mfahamu wazi kwamba, kila mtu aliyepo hapa hupata dola za kimarekani 1.5 kila siku ambazo hutolewa na wahisani, ambazo ni sawa na sh 3,050 kwa kila mtu kwa siku. Jiulizeni, ni fedha kiasi gani hizo kwa miezi sita? Kama hamjui au hamjawahi kusikia kitu kama hicho, basi mafisadi wanazitafuna," alisema.

  Awali wananchi wa kijiji cha Lukozi walimweleza Dk. Slaa katika mkutano huo kuwa, hawajawahi kuelezwa au kusikia fedha zinazoletwa kwao kutoka kwa wahisani, jambo ambalo limezidi kuwaongezea hofu kubwa kwa uongozi wa CCM na serikali yake katika kuendeleza wimbi la ufusadi.

  Akielezea zaidi kuhusu mwenendo wa mbunge wa jimbo hilo, Dk. Slaa aliongeza kuwa, mbunge huyo amekuwa akijihusisha na masuala ya ufisadi ikiwemo kutetea makandarasi wabovu hata kama hawakubaliki na vyombo vinavyosimamia sheria za nchi kama Bunge.

  "Nawambieni huyu mbunge wenu mimi namfahamu kuliko mnavyomfahamu nyinyi, aliwahi kumtetea bungeni mkandarasi anaitwa Martin Thomas, ili aendelee na ujenzi wa barabara yenu, jambo ambalo mimi nilipinga vikali. Hata katika hili naanza kupata wasiwasi kuwa kuna ufisadi hapa, muulizeni hizi fedha ziko wapi?"

  Katika hatua nyingine Dk. Slaa ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Karatu kupitia CHADEMA, aliwataka wananchi wa Mkoa wa Tanga, hususan wa Wilaya ya Lushoto kuwahoji Ngwilizi na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kuhusu sh bilioni 40 zilizoibwa kutoka Benki Kuu na Kampuni ya Kagoda.

  "Hivi mnajua kuwa kuna wizi wa mabilioni ya fedha yaliyochotwa na viongozi wa CCM, mimi ni mmoja wa viongozi wa kwanza kutaja majina ya mafisadi waliochota mabilioni hayo, kama hamjui waulizeni Ngwilizi na Makamba, wanajua, ni fedha nyingi sana ambazo akipewa mtu mmoja sh bilioni 155 na akawa anatumia sh milioni moja kila siku, atazitumia kwa miaka 465," alisema.

  Wakati huo huo, serikali mkoani Tanga inahaha kuizuia CHADEMA kurusha helikopta kwa madai kuwa inahatarisha amani na usalama wa watu.

  Habari za uhakika kutoka ndani ya CHADEMA zimeeleza kuwa tayari uongozi wa Mkoa wa Tanga umeiandikia barua Mamlaka ya Mawasiliano nchini kuitaka kuzuia helikopta inayotumiwa na viongozi wa ngazi ya juu ya chama hicho isitue katika mikutano ya Operesheni Sangara inayoendelea mkoani hapa kwa sasa.

  "Tunazo taarifa hizo, na tayari uongozi wa mkoa kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa umeiandikia barua Tume ya Mawasiliano kwa lengo la kuzuia matumizi ya helikopta katika mikutano yetu, wakidai kuwa inahatarisha amani na usalama wa watu jambo ambalo si kweli, ni hofu ambayo imewakumba viongozi wa CCM na serikali yake, tunajua Operesheni Sangara inawaumiza vichwa sana, ndiyo sababu kubwa," alifafanua Mkurugenzi wa shughuli za Bunge wa chama hicho, John Mrema, alipoulizwa na Tanzania Daima.

  CHANZO: Tanzania Daima
   
 5. A

  AmaniKatoshi Senior Member

  #5
  Dec 22, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Haya sasa, wanafiki akina Mrema, REDET na wengineo watasemaje tena...wakanushe CCM kuwa MAFISADI wa KODI ZA WANANCHI!!

  MH SLAA (a.k.a NO DATA NO RIGHT TO SPEAK) ameshachafua tena hewa ya CCM kwa kufichua ukwepaji kodi,,,,,na kwa kuiamini....."KAMA PINDA ANAWEZA AKANUSHE HILI"

  Wanajamii wenzangu, haswa kama wewe ni maskini mwenzangu....tumuombee Dr Slaaa afya njema.....
   
 6. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  CCM si ndo inaongoza serikali? Lazima wajipendelee!
   
 7. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hahaha, keki ya taifa lazima waonje wao kwanza! Au vipi?
   
 8. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duuh..anyway..But MM atasema hoja ya Chadema ni ufisadi tu...?? co do u want them to keep Quite for the foolishness like this.....I dont understand you...which side you are..!!!?
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,996
  Trophy Points: 280
  msamaha ni kwa sisiemu tu...
  Wengine lieni hamna chenu
   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ubabe ubabe!
   
 11. S

  Sumaku Member

  #11
  Dec 22, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dk. Slaa ailipua CCM

  • Serikali mkoani Tanga yahaha kuizuia helikopta ya Mbowe isiruke
  na Waandishi Wetu, Tanga

  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, jana alifichua ufisadi mkubwa uliofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuingiza magari 200 aina ya Land Cruiser ‘mkonga’ bila ya kulipia sh milioni 600 za ushuru wa forodha kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

  Dk. Slaa aliyasema hayo jana katika mkutano mkubwa wa hadhara wa muendelezo wa Operesheni Sangara uliofanyika katika Kijiji cha Kilole wilayani Korogwe. Alisema amepokea taarifa hiyo jana kutoka kwa msiri wake ndani ya TRA.

  Alisema hana ugomvi na CCM kuingiza magari 200 kwa ajili ya kupata ushindi mwaka 2010, lakini ugomvi wake mkubwa ni chama hicho kutoyalipia magari hayo ushuru wa sh milioni 600 ambazo zingewasaidia Watanzania katika kujenga nchi kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo.

  Akizungumza kwa kujiamini, alisema suala hilo lina ukweli usiokanushika. Alimtaka na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kama anaweza akanushe.

  “Taarifa hii nimeipata leo, na ina ukweli ndani yake. Hivi ninavyoongea yanaweza kutolewa muda wowote bandarini. Kama suala hili ni uongo, Pinda akanushe. Na wakilipa leo waandike tarehe risiti ya leo kwa kuwa hadi ninavyoongea hayajalipiwa,” alisema Dk. Slaa.

  Alisema huo ni ufisadi mkubwa ambao unafanywa na CCM wakati vyama vingine vinalipa ushuru.

  Dk. Slaa alisema kuwa mwaka 2005 CCM ilifanya ufisadi kama huo kwa kumtumia mfanyabishara mwenye asili ya Kiasia, Jeetu Patel, na kufanikiwa kuingiza magari 235 bila kulipia ushuru pia.

  Alisema viongozi wote wa CCM wamewekana katika nafasi za uongozi, ndiyo sababu maadili katika nafasi za uongozi wa kiserikali na taasisi zake yamemong’onyoka.

  Katika hatua nyingine, Dk. Slaa ameeleza kushangazwa na kitendo cha Mbunge wa Jimbo la Mlalo, Brigedia Jenerali Mstaafu Hassan Ngwilizi, kutowaeleza wapiga kura wake matumizi ya fedha za miradi zinazotolewa na wahisani mbalimbali.

  Akihutubia katika mkutano wa hadhara wa Operesheni Sangara, katika Kijiji cha Lukozi wilayani Lushoto juzi, Dk. Slaa alielezea wasiwasi wake kuhusu matumizi mabaya ya fedha hizo zinazotolewa kwa maendeleo ya vijijini mara baada ya kupewa taarifa na wananchi wa kijiji hicho.

  Alisema kushindwa kutoa taarifa ya matumizi na kiasi cha fedha zinazotolewa na wahisani kwa wananchi ni ufisadi unaofanywa na viongozi, hususan mbunge wa jimbo hilo, ambaye ni mmoja wa wahusika wakubwa wa kusimamia miradi ya maendeleo vijijini.

  Akifafanua kuhusu baadhi ya fedha zinazotolewa na wahisani kwa maendeleo ya wananchi vijijini kupitia halmashauri za wilaya alisema ni pamoja na zinazotolewa na Mfuko wa Capital Development Fund (CDF) na Local Gavernment Programme (LGCP), ambazo hutolewa kwa kila mtu anayeishi vijijini.

  “Mnataka kuniambia kuwa hamjui kama kuna fedha zinatolewa na wahisani kwa ajili ya maendeleo ya vijijini na wala hamjawahi kuzisikia? Kama ni kweli muulizeni mbunge wenu, huyo ndiyo anajua ziliko, maana mimi ni mbunge kama yeye najua zinatolewa fedha hizo na kama hamjaziona basi ziko mfukoni mwake,” alifafanua.

  Alisema kuwa wahisani mbalimbali hutoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo zinaelekezwa kwa wananchi kupitia halmashauri za wilaya, hatimaye kuwasilishwa kwa uongozi wa vijiji ambao nao hupanga matumizi na kuyawasilisha kwa halmashauri kuu.

  Katika ufafanuzi wake kwa wananchi kuhusu fedha hizo, Dk. Slaa alibainisha kuwa, wahisani hutoa kiasi cha dola za Kimarekani 1.5 kwa kila kichwa, kwa maana ya kila mtu hata mtoto mchanga.

  “Nataka mfahamu wazi kwamba, kila mtu aliyepo hapa hupata dola za kimarekani 1.5 kila siku ambazo hutolewa na wahisani, ambazo ni sawa na sh 3,050 kwa kila mtu kwa siku. Jiulizeni, ni fedha kiasi gani hizo kwa miezi sita? Kama hamjui au hamjawahi kusikia kitu kama hicho, basi mafisadi wanazitafuna,” alisema.

  Awali wananchi wa kijiji cha Lukozi walimweleza Dk. Slaa katika mkutano huo kuwa, hawajawahi kuelezwa au kusikia fedha zinazoletwa kwao kutoka kwa wahisani, jambo ambalo limezidi kuwaongezea hofu kubwa kwa uongozi wa CCM na serikali yake katika kuendeleza wimbi la ufusadi.

  Akielezea zaidi kuhusu mwenendo wa mbunge wa jimbo hilo, Dk. Slaa aliongeza kuwa, mbunge huyo amekuwa akijihusisha na masuala ya ufisadi ikiwemo kutetea makandarasi wabovu hata kama hawakubaliki na vyombo vinavyosimamia sheria za nchi kama Bunge.

  “Nawambieni huyu mbunge wenu mimi namfahamu kuliko mnavyomfahamu nyinyi, aliwahi kumtetea bungeni mkandarasi anaitwa Martin Thomas, ili aendelee na ujenzi wa barabara yenu, jambo ambalo mimi nilipinga vikali. Hata katika hili naanza kupata wasiwasi kuwa kuna ufisadi hapa, muulizeni hizi fedha ziko wapi?”

  Katika hatua nyingine Dk. Slaa ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Karatu kupitia CHADEMA, aliwataka wananchi wa Mkoa wa Tanga, hususan wa Wilaya ya Lushoto kuwahoji Ngwilizi na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kuhusu sh bilioni 40 zilizoibwa kutoka Benki Kuu na Kampuni ya Kagoda.

  “Hivi mnajua kuwa kuna wizi wa mabilioni ya fedha yaliyochotwa na viongozi wa CCM, mimi ni mmoja wa viongozi wa kwanza kutaja majina ya mafisadi waliochota mabilioni hayo, kama hamjui waulizeni Ngwilizi na Makamba, wanajua, ni fedha nyingi sana ambazo akipewa mtu mmoja sh bilioni 155 na akawa anatumia sh milioni moja kila siku, atazitumia kwa miaka 465,” alisema.

  Wakati huo huo, serikali mkoani Tanga inahaha kuizuia CHADEMA kurusha helikopta kwa madai kuwa inahatarisha amani na usalama wa watu.

  Habari za uhakika kutoka ndani ya CHADEMA zimeeleza kuwa tayari uongozi wa Mkoa wa Tanga umeiandikia barua Mamlaka ya Mawasiliano nchini kuitaka kuzuia helikopta inayotumiwa na viongozi wa ngazi ya juu ya chama hicho isitue katika mikutano ya Operesheni Sangara inayoendelea mkoani hapa kwa sasa.

  “Tunazo taarifa hizo, na tayari uongozi wa mkoa kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa umeiandikia barua Tume ya Mawasiliano kwa lengo la kuzuia matumizi ya helikopta katika mikutano yetu, wakidai kuwa inahatarisha amani na usalama wa watu jambo ambalo si kweli, ni hofu ambayo imewakumba viongozi wa CCM na serikali yake, tunajua Operesheni Sangara inawaumiza vichwa sana, ndiyo sababu kubwa,” alifafanua Mkurugenzi wa shughuli za Bunge wa chama hicho, John Mrema, alipoulizwa na Tanzania Daima.

  CHANZO: Tanzania Daima
   
 12. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  naona inabidi ukubaliane na INVISIBLE ili muwe na thread ya pamoja!ingawa yeye amekuwahi kwakweli
   
 13. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #13
  Dec 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Nilishahisi tutafika huku mapema tu... Haya si 'USED' hivyo thamani yake lazima ipo juu sana.

  Hivi kwa bei yake kwa sasa ni kiasi gani kwenye soko? Ukichukua thamani kwa kila moja ukazidisha kwa 200 utapata kiasi gani? Kwa miaka 5 kiasi hicho cha fedha kingewasaidia watanzania wangapi? What are our priorities?
   
 14. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,190
  Likes Received: 996
  Trophy Points: 280
  Hakuna shughuli au harakati yeyote inayofanikiwa bila pesa. Sasa kama serikali ya chama tawala itakomba pesa zote kifisadi maendeleo yatapatikana wapi? Uzuri wa vyama pinzani ndio kama huu wakutuonyesha nyani mla mahindi mabichi shambani. Kazi ina baki kwetu katika maamuzi kwenye sanduku la kura na wala sii kwa viongozi wa kisiasa tena. HEKO OPERATION SANGARA VIVA DR SLAA
   
 15. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  We need guys like DR. Slaa to make us move.... its real SHAME to our nation, nafikiri napata picha mtu akisema "nchi ipo uchi"
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na hapo ndipo penye tatizo kubwa, kama tumerogwa vile
   
 17. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Ni watanzania wachache sana wanaelewa hi philosophy, na itachukua muda kueleweka, ila hakuna chochote chenye haki kinachoshindikana. nimekusoma Mkuu.
   
 18. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani umeambiwa pesa imetoka CCM??? AU Serikalini??? pengine chama kimepata ufadhili. Hii ni changamoto kwa vyama pinzani je wataweza kushindana na hawa??? kama wenzetu wanakosa hata vibendera vya kupeperusha!!!!
   
 19. A

  Albano Member

  #19
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kwa muono wangu nadhani hii ni propaganda ya Slaa. Kwa uelewa wangu gari likishafika bandarini kama halina msamaha wa kodi litabaki bandarini mpaka lilipiwe.

  Slaa anakiri kwa maneno yake kuwa magari bado yapo bandarini na hayajalipiwa ushuru. Sasa hawa CCM watakwepaje kodi ili hali bado magari yapo bandarini? Alichotakiwa kukifanya kujustfy anachokisema ni kusubiri yatolewe ndipo aseme wamekwepa kodi.

  Ukiingiza magari 200 siyo siri ndani ya bandari kila mmoja atajua hivyo nadhani hii stori ya Slaa ni ya kuunga unga kwa sababu kila mmoja anajua kuna magari bandari hayajalipiwa na hayajatolewa. Slaa ninamheshimu sana kwa hoja zake. Lakini katika hili amepotoka na hajafanya analysis zake vizuri. Angesubiri kwanza yatolewe.

  Haya mambo ya kuwa nimeambiwa na mtu wangu wa siri hayapaswi kuchukuliwa na mtu kama yeye! Nadhani sasa anaanza kutokutofautiana na wanaporojo wengine wengi wanaozusha mambo bila data.
   
 20. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Du, kiboko, lakini, how credible could the funds source be? Hata hivyo kwa sababu hawa jamaa wajanja watakuwa wana mobilize ma don wao kulipia hayo magari; ie

  Manji shs. 200mil
  Jeetu shs. 200mil
  Tanil shs. 200mil

  KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
   
Loading...