CCM na kuvua gamba: Vita ya makundi na chuki kuelekea urais 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na kuvua gamba: Vita ya makundi na chuki kuelekea urais 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Aug 7, 2011.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Chama cha CCM kiliwataka wanachama wake wanaotuhumiwa kwa kasha Mbali Mbali za Kifisadi wajichunguze halafu wapime na Wachukue Maamuzi ya Kujivua Gamba.

  Msingi wa Tamko la Kujivua gamba la CCM ni tuhuma ambazo zilianzia katika Viwanja vya Mwembe Yanga tarehe 15 September 2008 Pale Katibu mkuu wa CHADEMA alipotoa orodha Maarufu kabisa iliyobadilisha hali ya Kisiasa katika Nchi ya Tanzania, orodha aliyoiita List of Shame . Katika Orodha hiyo Dr. Slaa aliorodhesha Majina ya Makada 11 ambao aliwaita kwamba waemlisababishia taifa hili hasara kubwa sana. Hebu tujikumbushe Orodha hiyo

  1. Dr. Daudi Balali
  2. Andrew J Chenge
  3. Basil P Mramba
  4. Grey S Mgonja
  5. Patrick Rutabanzibwa
  6. Nimrod Mkono
  7. Nazir Karamagi
  8. Rostam Aziz
  9. Edward Lowasa
  10. Benjamin Mkapa
  11. Jakaya Kikwete

  Tokea Tamko hilo litolewe ni watu watatu tu kati ya Kumi na moja wanaotakiwa Kijivua Gamba ( Kwa Maslahi ya Chama) na ni Edward, Rostam na Andrew.

  Tangia watu hao waombwe kuachia ngazi zao vimeripotiwa vikao mbalimbli kati ya hao watatu na viongozi wa CCM wakiwaomba wajiuzulu kwa Maslahi ya Chama. Ikumbukwe kwamba Niliandika huko Nyuma kwamba CCM haina uwezo wa kuwafukuza hao isipokuwa wataondoka wakitaka na nikasema kwamba Kujivua Gamba kwa hao itategemea zaidi huruma yao na si nguvu za CCM ( Rostam ameamua kujitoa mwenyewe baada ya kusengenywa sana, sasa amejiuzulu CC inampongeza Gademu unampongeza Mwizi?)

  Sio lengo langu kuzungumzia mambo ya Kujua Gamba lakini nataka nieleze Mtazamo wangu juu ya Kujuvua gamba

  1. Why Lowasa, Chenge and Rostam?

  Lowasa ni kikwazo kikubwa sana kwa Kundi la akina Sitta ambalo lina hasira ya kuukosa Uwaziri Mkuu na wanatambua kwamba Wasipopambana na Lowasa sasa Safari ya Sitta ya kuingia Ikulu 2015 itakuwa Ngumu sana.

  2. Why Richmond alono and not other like Kagoda, Epa and IPTL?

  Waanajua wakigusa IPTL wanagusa maslahi ya mkuu wao na Kagoda EPA iliwaingiza CCM madarakani 2005

  Kwa hiyo kinachoendelea sasa hivi ni Sarakasi za makundi ya Uraisi kuelekea 2015 ila wakiendelea hivi hakika CCM itafika 2015 vipande vipande
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Chama cha CCM kiliwataka wanachama wake wanaotuhumiwa kwa kasha Mbali Mbali za Kifisadi wajichunguze halafu wapime na Wachukue Maamuzi ya Kujivua Gamba.

  Msingi wa Tamko la Kujivua gamba la CCM ni tuhuma ambazo zilianzia katika Viwanja vya Mwembe Yanga tarehe 15 September 2008 Pale Katibu mkuu wa CHADEMA alipotoa orodha Maarufu kabisa iliyobadilisha hali ya Kisiasa katika Nchi ya Tanzania, orodha aliyoiita List of Shame . Katika Orodha hiyo Dr. Slaa aliorodhesha Majina ya Makada 11 ambao aliwaita kwamba waemlisababishia taifa hili hasara kubwa sana. Hebu tujikumbushe Orodha hiyo

  1. Dr. Daudi Balali
  2. Andrew J Chenge
  3. Basil P Mramba
  4. Grey S Mgonja
  5. Patrick Rutabanzibwa
  6. Nimrod Mkono
  7. Nazir Karamagi
  8. Rostam Aziz
  9. Edward Lowasa
  10. Benjamin Mkapa
  11. Jakaya Kikwete

  Tokea Tamko hilo litolewe ni watu watatu tu kati ya Kumi na moja wanaotakiwa Kijivua Gamba ( Kwa Maslahi ya Chama) na ni Edward, Rostam na Andrew.

  Tangia watu hao waombwe kuachia ngazi zao vimeripotiwa vikao mbalimbli kati ya hao watatu na viongozi wa CCM wakiwaomba wajiuzulu kwa Maslahi ya Chama. Ikumbukwe kwamba Niliandika huko Nyuma kwamba CCM haina uwezo wa kuwafukuza hao isipokuwa wataondoka wakitaka na nikasema kwamba Kujivua Gamba kwa hao itategemea zaidi huruma yao na si nguvu za CCM ( Rostam ameamua kujitoa mwenyewe baada ya kusengenywa sana, sasa amejiuzulu CC inampongeza Gademu unampongeza Mwizi?)

  Sio lengo langu kuzungumzia mambo ya Kujua Gamba lakini nataka nieleze Mtazamo wangu juu ya Kujuvua gamba

  1. Why Lowasa, Chenge and Rostam?

  Lowasa ni kikwazo kikubwa sana kwa Kundi la akina Sitta ambalo lina hasira ya kuukosa Uwaziri Mkuu na wanatambua kwamba Wasipopambana na Lowasa sasa Safari ya Sitta ya kuingia Ikulu 2015 itakuwa Ngumu sana.

  2. Why Richmond alono and not other like Kagoda, Epa and IPTL?

  Waanajua wakigusa IPTL wanagusa maslahi ya mkuu wao na Kagoda EPA iliwaingiza CCM madarakani 2005

  Kwa hiyo kinachoendelea sasa hivi ni Sarakasi za makundi ya Uraisi kuelekea 2015 ila wakiendelea hivi hakika CCM itafika 2015 vipande vipande
   
 3. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Chama cha magamba,mafisadi na matapeli,hakuna jipya tusubiri siku kitakapo kufa.
   
 4. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kuna CCM ya Sitta
  Kuna CCM ya Lowasa
  Kuna CCM ya Membe

  Urais 2015 unawatoa Macho hawaaminiani hao ha ha ha
   
 5. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Utajizungusha wee lakini nia yako hasa ni kumtetea fisadi mkuu LOWASSA,... kwa taarifa yako the writting is on the wall, either ajiuzulu mwenyewe walau abaki na kachembe ka heshma au asubiri kusukumwa nje na kupoteza punje ndogo ya heshma aliyobaki nayo.
  Si umeshasikia Interpol wako nchini towards the build up ya NEC ijayo... Hatutaki mabaka uchumi wa nchi waendelee kufikiria wanaweza kuhodhi nafasi za mamlaka ya juu zaidi.

  Kwangu mimi LOWASSA - NO na FREEMAN MBOWE - NO. Wote ni tabaka la kibepari zaidi. Hulka ya kibepari ni kujilimbikizia mali!!!

  Atleast cdm wana a credible standby presidential material, ingawa sijui wanafanya nini kuhakikisha wanamtunza na kumlea kiafya ili abaki fit mpaka 2015. Ingekua ni nchi za wenzetu, hii hazina angeajiriwa mtu mahsusi wa kufuatilia afya yake tu kuanzia anachokula mpaka ratiba za mazoezi.
   
 6. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  hawa magamba watauana sana mwaka huu,mara wamuonye sita kuwa anaikosoa serikali.huku jairo anaboronga,nape naye anadai wanambeza yaani ni shida tupu,uraisi unawamaliza.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,412
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]CCM gamba jipya
  • Idadi ya watuhumiwa yaongezeka kila kukicha
  na Salehe Mohamed, Dodoma
  Tanzania Daima


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  TUHUMA mpya za ufisadi zinazolizunguka Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), zimezidi kuongeza idadi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaokabiliwa na kuhusishwa na tuhuma za ufisadi, Tanzania Daima Jumapili limebaini.

  Ongezeko hilo la watuhumiwa wa ufisadi ambao takriban wote ni viongozi au makada wa chama hicho tawala, kunazidi kukiweka chama hicho katika hatua ngumu ya kuweza kujisafisha kutoka katika dimbwi la tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu wa fedha na mali ya umma na matendo mengine yenye mwelekeo wa uhujumu wa uchumi.

  Kuibuka kwa tuhuma hizo mpya za ufisadi ndani ya Shirika la UDA zinazoyagusa majina mapya ya makada wa CCM kunakuja wakati chama hicho kikiwa katika hatua ya kipropaganda waliyoipa jina la kujivua gamba.
  Hadi wakati tuhuma mpya za UDA zilipoibuka, majina ya makada wa CCM waliokuwa wakitajwa kuwa katika orodha rasmi ya magamba yanayopaswa kuvuliwa na ambayo yamekuwa yakipigiwa chapuo kubwa ndani ya vyombo vya habari yalikuwa ni matatu tu.

  Majina ya makada hao ni lile la Mbunge wa Monduli na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Mbunge wa Bariadi Magharibi ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa zamani, Andrew Chenge na la mwisho ni la aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.

  Hata hivyo, idadi hiyo ilipungua na kubakiza majina mawili, baada ya Rostam kuamua kujiuzulu nafasi zake zote za kisiasa ndani ya chama hicho katika mazingira ambayo wadadisi wa mambo bado wanaendelea kufuatilia kiini chake. Wakati CCM ikihangaika kutafakari namna ya kumalizana na makada wengine wawili waliobaki katika orodha hiyo, tuhuma mpya za ufisadi zinazogusa majina ya makada wake wapya zimeibuka na kuzusha mtafaruku mkubwa ndani ya chama hicho na pengine serikalini.


  Miongoni mwa majina mapya ya kwanza kutajwa katika orodha hiyo mpya ya makada wanaotajwa katika tuhuma mpya za ufisadi unaoigusa UDA ni lile la aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, Iddi Simba.

  Mbali ya Simba, jina jingine la mwana CCM ambalo limetajwa ndani ya Bunge katika tuhuma mpya za ufisadi wa UDA ni lile la Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya.

  Ukiwaacha makada hao wawili, mwingine anayetajwa katikati ya tuhuma hizo ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam anayetokana na CCM, Dk. Didas Masaburi, ambaye alikuwa ni mtu wa kwanza kuliibua sakata hilo wakati alipotangaza uamuzi wa kumuachisha kazi, Meneja wa UDA, Victor Milanzi.

  Kutajwa kwa Masaburi katika sakata hilo la UDA ambalo mwenyewe anasema ndiye aliyeliibua na kulikemea, kumesababisha kuibuka kwa tuhuma nyingine mpya za ufisadi katika Jiji la Dar es Salaam zinazowagusa makada wengine wa CCM ambao pia ni wabunge wa jiji hilo.

  Aliyeibua majina mapya ya makada hao wa CCM ni Masaburi mwenyewe ambaye alikuwa akijibu tuhuma za ufisadi wa UDA ambazo zimelizonga jina lake ndani ya Bunge kwa siku kadhaa sasa.

  Masaburi ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Arusha, alisema baadhi ya wabunge wa Dar es Salaam ambao walikuwapo tangu Bunge lililopita wanamhusisha katika ufisadi wa UDA kama mbinu ya kukwepa kubambwa katika tuhuma za namna hiyo hiyo zinazoelekea kuwagusa wao.

  Akitoa mifano, Masaburi alisema kumekuwa na tuhuma za ufisadi zinazogusa soko la wafanyabiashara ndogogo lililopo maeneo ya Ilala, maarufu kwa jina la Machinga Complex, ambalo mwenyekiti wake wa bodi alikuwa ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan ‘Zungu'.

  Kutokana na hali hiyo, meya huyo wa Jiji la Dar es Salaam, alieleza kutoshangazwa na tuhuma zinazoelekezwa kwake na wabunge wa Dar es Salaam hususan wale wa CCM.

  Mbali ya hilo, Masaburi alilitaja jina la Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu kuwa aliloliweka katika orodha ya kuchunguzwa kutokana na kuwapo kwa tuhuma nyingi za ufisadi katika Shirika la Uchumi na Maendeleo Dar es Salaam (DDC).
  Kwa mujibu wa Masaburi, kutokana na ukweli kwamba, Mtemvu yuko katika bodi ya DDC na Zungu katika Machinga Complex, ambazo ameshatangaza kuelekeza harakati zake za kusafisha ufisadi, hakushangazwa na kitendo cha wabunge hao wawili wa Dar es Salaam kuungana na wenzao wengine kumshambulia na kumtuhumu kwa ufisadi wa UDA ilhali wakijua fika kwamba hausiki kwa namna yoyote.

  Madai hayo ya Masaburi yanakuja wakati kukiwa na taarifa kwamba katika kikao cha wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam kilichokaa mjini Dodoma hivi karibuni kujadili suala la UDA, mbunge mmoja wa CCM aliwajia juu wenzake kwa kubeba hoja za wapinzani katika suala hilo.

  Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kwamba mbunge huyo (jina tunalo) aliwashambulia wabunge wenzake akiwahusisha katika tuhuma kadha wa kadhaa za ufisadi.

  Mtoa habari zetu anaeleza kwamba mbunge huyo wa CCM alifikia hatua ya kuwaeleza wabunge wenzake kwamba wakati wakishabikia masuala ya UDA wao wenyewe walikuwa katika vitanzi vya kupoteza nyadhifa zao, iwapo tuhuma zao zitafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

  Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumapili umebaini kwamba tuhuma za ufisadi zinazoendelea kukichafua chama hicho zimesababisha kuibuka kwa hasira miongoni mwa wabunge wa chama hicho wa maeneo ya nje ya Dar es Salaam.

  Baadhi ya wabunge wa CCM waliozungumza na gazeti hili kwa masharti ya majina yao kutoandikwa waliweka bayana msimamo wao kuwa wamechoshwa na vitisho wanavyovipata kutoka kwa viongozi wao wa chama na hivi sasa wapo tayari kujiengua ndani ya chama hicho na kujiunga na upinzani.
  Walibainisha kuwa tabia ya kufumbia macho vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma ndiyo unaokifanya chama hicho kupoteza imani kwa wananchi ambao kadiri siku zinavyokwenda ndivyo wanatumbukia kwenye lindi la umasikini.

  Walisema mchawi wa CCM si vyama vya upinzani ila ni watendaji wa serikali na vigogo wa chama hicho ambao wameamua kugawana rasilimali za taifa kwa masilahi yao.

  Walimbebesha lawama Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kuwa ndiye mwenye kukwamisha kuchukuliwa hatua kwa baadhi ya vigogo wa chama hicho kwa madai ya kutaka sheria zifuatwe na wengine kuwasamehe kwa vigezo anavyovijua mwenyewe.
  Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka, alisema tatizo kubwa linalowakabili wabunge wa chama hicho ni kujipendekeza kwa viongozi wa serikali pamoja na kutofahamu kile kinachopingwa na wabunge wenzao wasiotaka rasilimali za umma zitumike kwa upendeleo au ubadhirifu.

  Alisema baadhi ya wabunge wamekuwa wakimuona yeye ni kikwazo na anayetoa kauli za ubaguzi wa kimaeneo mara kwa mara anapopinga ugawaji wa rasilimali lakini hawataki kuchunguza kwa undani kile anachokisema.

  "Hatuwezi kukiimarisha chama na serikali kama tutaendelea kuwa waoga kwa viongozi wetu na watu wanaotumia rasilimali za taifa kwa faida ya kikundi fulani au eneo fulani," alisema.

  Sendeka alisema ni lazima wabunge watambue kuwa masilahi ya taifa ndiyo yanapaswa kupewa kipaumbele halafu ndio yafuatie ya chama kilichotoa ridhaa kwa mbunge husika kuwania wadhifa wake.

  Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Ismail Aden Rage, wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Uchukuzi alisema kuwa tatizo kubwa la serikali ya CCM ni kuvumilia makada wake wanaoshiriki kwenye ubadhirifu badala ya kuwachukulia hatua ikiwemo kufilisi mali zao.

  Deo Filikunjombe, Mbunge wa Ludewa (CCM) anasema umefika wakati kwa serikali ya chama hicho kutoa adhabu kali kwa makada wake na watendaji wa serikali wanaobainika kushiriki katika ubadhirifu ikiwezekana wanyongwe.
  Mbunge huyo alisema CCM inajimaliza kwa kutumia muda na nguvu nyingi za kupambana na CHADEMA inayoratibu maandamano ya kupinga ugumu wa maisha badala ya nguvu hizo kuzielekeza kuboresha maisha ya wananchi pamoja na kupambana na mafisadi.

  Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM), anasema watu walioingia mikataba mibovu inayolifilisi taifa bado wapo bungeni, chamani na serikalini badala ya kuwepo magerezani.

  Lembeli alisema hakuna sababu ya Rais Kikwete na serikali ya chama hicho kujali sheria katika kuwaadhibu vigogo wanaotafuna rasilimali za taifa na kusababisha maisha magumu kwa wananchi.

  Wakati wabunge hao wakiona hatari ya chama chao kuanguka kwa sababu ya kuwalinda wabadhirifu, Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) (Uchumi na Fedha Taifa) Mwingulu Nchemba, anahofia chama chao kupinduliwa na CHADEMA inayofanya maandamano ya kupinga ugumu wa maisha na upandaji wa gharama za bidhaa mbalimbali.

  Juzi Nchemba, alivitaka vyombo vya dola kuingilia kati maandamano yanayofanywa na CHADEMA kwa madai kuwa yanalenga kufanya mapinduzi ya serikali iliyopo madarakani.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 8. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii imekaa vizuri.
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]CCM: Mbio za urais, makundi vinatutesa[/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 26 November 2011 07:45[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG] Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, jana, juu ya maazimio yaliyotolewa kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho uliofanyika kwa siku mbili mkoani Dodoma.Kulia ni Makamu Mwenyekiti Bara Pius Msekwa Picha na Edwin Mjwahuzi

  CHASEMA KUJIVUA GAMBA,VITA YA UFISADI VIKO PALEPALE
  Neville Meena na Habel Chidawali, Dodoma
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kwa mara ya kwanza kimekiri hadharani kuwa mbio za Urais wa mwaka 2015 ni miongoni mwa mambo yanayokitikisa na sasa kinachukua hatua za kuwadhibiti makada wake wenye nia hiyo ili harakati zake zisikiathiri.Kadhalika, CCM kimesema dhana ya kujivua gamba kiliyoiasisi iko palepale na kwamba utekelezaji wake unaanza mara moja kwa kuwachukulia hatua wanachama wake wote wanaotuhumiwa kwa rushwa na ufisadi.

  Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama aliwaambia waandishi wa habari jana Mjini Dodoma kuwa si vibaya makada wa chama hicho kuanza kufikiria urais wa 2015 lakini tatizo ni njia ambazo zinatumika katika harakati hizo.

  “Sisi hatuna shida na watu hao kwa kuwa ni haki yao, lakini lazima watumie njia sahihi ambazo hazitaleta shida kwa chama na tumeona iko haja ya kutengeneza mfumo mzuri wa kupata mgombea urais ambaye hatatokana na fedha isipokuwa akubalike kwa uwezo wake wa kujenga hoja, itikadi yake na kile anachokiamini,” alisema Mukama.

  Mukama alikiri kuwa mbali na mbio za urais 2015, pia CCM kinateswa na siasa za makundi ambayo yamekuwa yakitumika kushambuliana, kinyume cha maadili yake.

  Alisema CCM kinachukua hatua za kukabiliana na makundi ambayo misingi yake hujengwa katika chaguzi za ndani ya chama, na kwamba watahakikisha hilo halitokei wakati wa uchaguzi wake unaotarajiwa kufanyika mwakani.

  “Kwa maneno ambayo tuliyatumia tulisema, hii kansa ya kupangana safu inaweka mtu ambaye hata sifa wala hana habari kabisa na matatizo ya wananchi, wala haumii lakini anapanga safu… lazima tuondokane na kansa hii ili tupate viongozi wanaojali na wanaohangaika na maisha ya wavuja jasho wa nchi hii,” alisema.

  Kujivua gamba

  Kuhusu suala la kujivua gamba, akimaanisha kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa makosa mbalimbali ukiwemo ufisadi na rushwa, Katibu Mkuu huyo alisema kati ya maazimio 26 yaliyotolewa na NEC Aprili mwaka huu, Azimio namba 27 “linahitaji kutekelezwa haraka iwezekanavyo.”

  “Dhana hiyo ya kukipatia chama chetu sura mpya ndiyo iliyopewa jina la kujivua gamba na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa imekwishatengeneza mpango wa utekelezaji wa uamuzi huo,’’ alisema Mukama.

  Alisema katika kikao chake kilichomalizika juzi, NEC imeamua kuwa viongozi wa CCM wanaotuhumiwa kwa ufisadi ndani ya chama walipaswa kujipima na kujitafakari wenyewe na ikibidi wachukue hatua jambo ambalo halijatekelezwa hadi sasa.

  Alisema Azimio hilo liliwalenga viongozi katika ngazi zote za chama kuanzia taifa hadi tawi na kilichokusudiwa ni kujenga utamaduni wa kusimamia maadili ya viongozi na wanachama wake.

  “Takriban miezi saba baada ya Azimio hilo kupitishwa, bado hatujapata mwitikio wa kuridhisha kutoka kwa viongozi wa ngazi yoyote wa chama chetu ambao ni walengwa wa azimio,’’ alisema na kuongeza:

  “Bila shaka sasa wakati umefika wa chama kutekeleza ile sehemu ya pili ya azimio husika kwa kuwawajibisha wahusika, lakini utekelezaji wake hauna budi ufanyike kwa kufuata utaratibu uliowekwa ndani na kanuni za CCM za uongozi na maadili.’’

  Msingi wa mpango wa kujivua gamba umejengwa katika azimio la NEC linalosema: “Viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi watafakari, wajipime na kuchukua hatua wao wenyewe kwa maslahi ya chama, wasipofanya hivyo, chama kiwawajibishe bila kuchelewa.”

  Lakini tangu kupitishwa kwa mpango huo Aprili mwaka huu, ni kada mmoja tu, Rostam Aziz aliyechukua hatua za kujiuzulu Ubunge wa Jimbo la Igunga na Ujumbe wa NEC huku wengine wakiwa kimya.

  Mukama alisema sehemu ya pili ya azimio hilo inayosema: “Wasipofanya hivyo chama kiwawajibishe bila kuchelewa,” ndiyo msingi wa NEC kurejesha suala hilo kwa Kamati Kuu na kwamba sasa litafanyika katika ngazi zote.
  Alisema NEC imeziagiza kamati za siasa kupitia kamati za ulinzi usalama na maadili kwa ngazi zote kuanza mara moja, mchakato wa kutekeleza azimio hilo kwa mujibu wa kanuni na taratibu za chama.

  Alisema NEC iliagiza kazi hiyo kufanyika haraka bila kuchelewa na baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, taarifa zipelekwe kwenye vikao vya kikatiba vya uamuzi kwa hatua za utekelezaji.

  Alisema chama hicho kitahakikisha kwamba ajenda hiyo haitekwi na makundi yanayokinzana na kwamba lengo zima ni kuhakikisha kwamba CCM kinaongeza uwezo wa kusimamia mambo yake na Serikali zake zote.

  “Lazima kifike mahali (CCM), kiwe na uwezo wa kuzisimamia na kuhakikisha kwamba Serikali zinatekeleza matakwa ya wananchi na siyo vinginevyo, ndiyo maana watu wanajiunga na vyama kwani huwa wanatarajia watapata utetezi,” alisema Mukama.

  Kuhusu vurugu na migomo ya vyuo vikuu CCM kiliagiza Serikali kuchukua hatua za haraka kukabiliana na hali hiyo na kuitaka kusimamia sheria inayokataza uendeshaji wa shughuli za kisiasa katika taasisi za elimu nchini. Kimetaka wanafunzi na watumishi wabanwe ili waendeshe shughuli hizo nje ya taasisi husika.

  Kuhusu suala la Nishati nchini, Mukama alisema NEC imeiagiza Serikali kuhakikisha kuwa inapunguza bei za mafuta na hasa ya taa ambayo yanatumiwa na wananchi wengi wenye kipato cha chini.

  Juzi, Mawaziri Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, waliwashambulia kwa maneno makali wajumbe wawili wa Sekretarieti ya CCM kwamba wamekuwa wakikivuruga chama na kusababisha mgawanyiko uliopo kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakisimamia mpango wa kujivua gamba.

  Lowassa aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu, kutokana na kashfa ya Richmond ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumzia suala hilo wakati wa mjadala wa hali ya siasa, pale alipowataja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, John Chiligati kwamba wamekuwa wakitukana watu ovyo kwa fedha wanazopewa na CCM.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, Lowassa alitumia zaidi ya dakika saba kumshambulia Nape kwamba amekuwa akifanya mambo nje ya utaratibu na kwamba mwenendo huo umekuwa ukikibomoa chama badala ya kukijenga.

  Sumaye alisimama na kuhoji sababu za chama hicho kunyamazia ukiukwaji wa taratibu ambao umekuwa ukifanywa na watendaji hao.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...