CCM na Hatima Ya Bunge La Katiba

CCM na Hatima Ya Bunge La Katiba

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,434
Siku sio nyingi zijazo, Bunge la katiba litakutana mjini Dodoma kufanyia kazi rasimu ya pili ya Katiba. Iwapo “kila kitu kitaenda sawa”, Katiba hii itakuwa ni ya kwanza itokanayo na umma/wananchi tangia uhuru (1961). Katika mchakato wa maoni ya katiba mpya kwenye umma, sehemu kubwa ya mjadala ilihusisha suala la Muungano, na hii ni kwa mujibu wa tume ya Jaji Warioba. Kwahiyo kuelekea bunge la Katiba, nadhani kuna haja yetu kujikita Zaidi katika suala la muundo wa muungano, hasa ikizingatiwa kwamba katika hili, wajumbe wa CCM wanaenda kulisimamia kama kwa vile ni moja ya masuala machache ambayo CCM inayasimamia “kisera”.

Ni muhimu tukumbuke kwamba mjadala juu ya muundo wa muungano uliingizwa kwenye sheria ya mabadiliko ya katiba bila ya matakwa ya viongozi kadhaa wa CCM na serikali yake. Ilikuwa ni wananchi (hasa wa Zanzibar) ambao ndio walilazimisha suala la muungano liingie kwenye sheria ya mabadiliko ya Katiba. Sote tunakumbuka jinsi gani wananchi wa Zanzibar walivyopinga muswada wa awali wa serikali kwa kuchoma moto hadharani rasimu waliyopelekewa. Isingekuwa ni busara za Waziri Samwel Sitta ambae ndiye aliyeiwakilisha serikali katika hafla ile, pengine leo tungekuwa tunazungumza mengine. Matukio mengine mengi yalifuatia baada ya hapo, lakini muhimu kuelekea bunge la katiba ni kwamba:

Licha ya WANANCHI wengi kuwasilisha maoni yao kwa tume ya Katiba juu ya mfumo wa muungano wanaopendelea, “bado kuna viongozi wa CCM na wafuasi wao” wasiolitakia mema taifa letu ambao wanaendelea “kukaidi” matakwa ya wengi juu ya mfumo wa muungano wanaoona unawafaa.

Licha ya MWENYEKITI WA CCM TAIFA (Rais Kikwete) kuwaelimisha viongozi wa CCM juu ya umuhimu wa “kujiandaa Kisaikolojia” na mfumo wa serikali Tatu baada ya Kikwete kusoma alama za nyakati kufuatia mgogoro usiokwisha kwa miaka 50, “bado kuna baadhi ya viongozi wa CCM na wafuasi wao” wanaoendelea kukaidi ushauri wa mwenyekiti wao wa CCM (Taifa). Viongozi hawa wa CCM wanataka Mwenyekiti wa CCM taifa afuate matakwa ya chama (CCM) badala ya wao kufuata ushauri wake wenye busara ambao unalenga kuwaamsha kwa nia ya kuepusha mgogoro mkubwa ndani ya taifa letu.

Licha ya MWENYEKITI WA CCM TAIFA (Rais Kikwete) kuhimiza kwa viongozi wa vyama vya siasa juu ya umuhimu wa vyama hivi kuweka mbali itikadi zao katika kipindi hiki na badala yake kuweka mbele maslahi ya taifa, “bado kuna viongozi wa CCM na wafuasi wao” wanaoendelea kukaidi wito huu kutoka kwa Mwenyekiti wao (Taifa). Kwa mfano rejea tamko la UVCCM hivi karibuni kuhusiana na muundo wa muungano. Ukaidi huu unatuacha na maswali mengi kuliko majibu juu ya nini itakuwa ni hatima ya bunge la katiba linalotarajiwa kukutana hivi karibuni, lakini muhimu Zaidi, nini itakuwa ni hatima ya muungano wetu na taifa letu.

Licha ya ukweli kwamba mshirika mwingine wa muungano tayari ameshafanya maamuzi ambayo kimsingi, Katiba yake inapindua mambo mengi yaliyomo ndani ya Katiba ya JMT (1977). Kwa mfano, Zanzibar imebadili katiba yake na kuchukua madaraka ya Jamhuri ya Muungano, kama vile kuelekeza sheria za muungano zilizopitishwa na bunge la muungano kupelekwa kwenye baraza la wawakilishi. Maana yake ni kuwa, Katiba ya Zanzibar sasa ipo juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Licha ya haya yote, bado viongozi hawa wa CCM wanakaidi hoja za watanganyika na wao kuja na serikali yao na katiba yao.

Mienendo na matamshi ya viongozi hawa wa CCM hasa yanayokaidi matakwa ya wengi juu ya mfumo wa muungano yatafanya tuamini kwamba, katika suala la muungano, matokeo ya bunge la Katiba yanaweza chukua sura kuu tatu zifuatazo:

Scenario ya kwanza:
Wajumbe wa CCM wataunga mkono matakwa ya wananchi walio wengi kwa mujibu wa rasimu ya katiba, ingawa kwa kufanya hivyo, hao watakuwa wameenda kinyume na sera rasmi ya CCM ambayo ni muungano wa serikali mbili.

Kuna mambo matatu muhimu ya kuyaangalia hapa. Kwanza, ikumbukwe kwamba hadi leo hakuna ushahidi wowote unao onyesha kwamba wananchi/umma ulishirikishwa katika kufikia maamuzi ya sera ya serikali mbili. Pili, utaratibu/Mchakato wa chama (CCM) wa kutunga au kubadili sera zake upo wazi – kwa maana ya kwamba mabadiliko yoyote ya kisera ni lazima yahusishe NEC na baadae kupata Baraka za mkutano mkuu wa ccm (taifa). Na tatu, sote tunajua kwamba kufikia tarehe ya bunge la katiba kuanza, hakuna kikao cha namna hiyo ambacho kitakuwa kimekaa. Na kitendo cha CCM kuamua kutofanyia mabadiliko ya sera ya muungano wa serikali mbili hadi tarehe ya bunge la katiba, maana yake ni kwamba CCM imeamua kufa kiume na sera yake hii. Kwa mantiki hii, iwapo wajumbe wa CCM wataamua kufanya maamuzi ambayo yatapingana na sera rasmi ya chama chao (CCM) ya “serikali mbili”, hiyo itakuwa ni political suicide kwa CCM kuelekea 2015.

Mtu anaweza kujenga hoja kwamba iwapo wajumbe wa CCM watakabiliwa na upinzani mkali bungeni katika kusimamia sera ya CCM ya “muungano wa serikali mbili”, CCM itaweza kujinasua kwa kuhusisha Kamati ya wabunge wa CCM ambayo itaweza kukutana kwa dharura na hatimaye wajumbe wa CCM kuja na msimamo na mshikamano unaounga mkono matakwa ya wananchi walio wengi (kwa mujibu wa rasimu ya katiba). CCM ingeweza kufanya hivyo katika masuala mengine lakini kwa suala la muungano, CCM ina maslahi yake, lakini muhimu Zaidi ni kwamba, suala hili linagusa sera ya chama kwa mujibu wa katiba ya chama. Kwa hali hii, itakuwa ni vigumu sana kwa kamati ya wabunge wa CCM kufanya maamuzi kinyume na sera rasmi ya chama chao (CCM), vinginevyo watarajie kukivunja chama. Katiba ya CCM haiwapi wajumbe wa CCM katika bunge hilo mamlaka ya kubadili sera za chama, badala yake wanatarajiwa kwenda katika bunge hilo kutetea muungano wa serikali mbili. Mamlaka ya kubadili sera lazima yapitie NEC (CCM) na kubarikiwa na Mkutano Mkuu wa Taifa, vikao ambavyo ni dhahiri kwamba CCM ilishaamua kutouviitisha kuelekea bunge la Katiba.

Hivyo basi, chini ya scenario hii ya kwanza, iwapo wajumbe wa CCM wataamua kuunga mkono muungano wa serikali tatu, basi hiyo itakuwa ni hatua ya kwanza kwa CCM kuvunjika vipande vipande kuelekea uchaguzi mkuu (2015).

Scenario ya pili ni kwamba:
Kutokana na wingi wao, wajumbe wa CCM (pamoja na wengine ambao CCM itafanikiwa kuwashawishi ndani ya bunge husika watafanya kila wanaloweza kuhakikisha kwamba bunge la Katiba linakwama iwapo misimamo/sera za CCM kama vile juu ya muungano zitakwama. Hali hii itapelekea bunge la Katiba kuvunjika. Iwapo itatokea hivyo, itajengwa hoja kwamba Katiba ya sasa ya JMT (1977) iendelee kutumika hadi baadae muafaka utakapopatikana. Kwa maana nyingine, itajengwa hoja kwamba Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania (1977) iendelee kutumika mpaka maelezo Zaidi yatakapotoka baadae. Hoja hii itaongezewa nguvu Zaidi na hoja kwamba, “pamoja na mapungufu kadhaa ya Katiba ya sasa (1977), Katiba hii bado ni “Katiba halali”.

Bila ya kujalisha wajumbe wa CCM watajenga hoja gani juu ya haja ya nchi kuendelea kuwa chini ya Katiba ya sasa mpaka hapo baadae kwa vile ni Katiba ya JMT (1977) bado ni halali, ukweli utaendelea kubakia kwamba, ili taifa lisonge mbele kwa amani na utulivu, suala la katiba mpya haliwezi kwepeka tena. Umuhimu wa taifa kuhitaji Katiba mpya haraka upo katika maeneo makuu matatu ya hoja kama ifuatavyo:

Kwanza – on the practical level (KIVITENDO), Katiba ya JMT (1977) kwa sasa “is no longer irrelevant”. Na hii ni kwa sababu, msingi wa Katiba ya JMT (1977) ulijengwa juu ya nguzo kuu mbili ambazo ni:
· Nguzo ya kwanza ni Mfumo wa Chama Kimoja Cha Siasa (CCM).
· Nguzo ya pili ni Mfumo wa Muungano wa Serikali Mbili.

Hakuna mjadala kwamba nguzo zote mbili kwa sasa zimesha momonyoka. Ama tutakavyoona, kilichokuwa kinaupa muungano pamoja na sera husika ya CCM uhalali ilikuwa ni masuala mengine. Vinginevyo, katika kipindi chote cha miaka 50 ya muungano, umma haukuwahi shirikishwa juu ya mfumo wanaopendelea, na pia umma haukuruhusiwa kujadili suala la muungano. Matokeo yake ni kwamba, Mlinzi wa muungano huu ikawa ni ‘vyombo vya ulinzi na usalama’ badala ya wananchi ambao, katka hali ya kawaida, ndio hutakiwa kuwa walinzi wa muungano. Hata Mwalimu aliwahi jadili kwamba hatowapiga mabomu wananchi ambao wataukataa muungano. Miaka 50 baadae, kwa mujibu wa rasimu ya katiba, hatimaye wananchi wamepara fursa ya kutoa maoni yao juu ya muungano, na walio wengi wameonyesha jinsi gani hawaridhiki na mfumo wa sasa wa serikali mbili.

Hoja ya pili juu ya umuhimu wa taifa kupata katiba mpya ipo ‘on a very basic principle’. Inaonekana kwamba Viongozi wa CCM wanaopinga mfumo wa serikali tatu ambao ni matakwa ya wananchi walio wengi wanashindwa kuelewa kwamba Katiba sio tu ni nyaraka ya kisheria au kitaalamu (it is not simply a legal or/and technical document), bali muhimu Zaidi ni kwamba Katiba ni nyaraka ya kisiasa (a political document). Ili Katiba ipate uhalali wa kisiasa (political legitimacy) na kustahili utiifu na uaminifu (obedience and loyalty) kwa pande zote mbili za jamii – (rulers) watawala na (the ruled) watawaliwa, ni lazima katiba ya nchi iwe na maridhiano kitaifa (national consensus). Ndani ya Katiba kwa kawaida huwa kuna kanuni za msingi ambazo kwa ujumla wake, hutoa mwongozo juu ya jinsi gani jamii inataka kuji ‘organize’ naku ‘behave’, relative to the use of political power ndani ya taifa. Vile vile katiba ya nchi kwa kawaida huwa ina ‘determine’ na kutoa taswira ya jinsi gani mahusiano baina ya serikali (state) na jamii (society) yanatakiwa yawe. Ni kwa misingi hii, kuna ulazima wa maridhiano mapana (broad consensus) ndani ya taifa ili Katiba ya nchi iweze kupata uhalali (legitimacy) mbele ya umma.

Katiba isiyotokana na ‘national consensus’ pia huwa inakosa uhalali wa kisiasa (political legitimacy). Katiba ya namna hii huwa ni Katiba ambayo hulazimishwa kwa wananchi, na matokeo yake huwa - sio watawala (rulers) wala watawaliwa (ruled) ambao huijali na kuiheshimu. Baada ya kusema hayo, niseme pia kwamba - haina maana kwamba serikali inayoongoza chini ya katiba ya namna hii huwa haina uhalali wa kuongoza nchi/taifa. Serikali husika inaweza kupata ‘uhalali’ wa kuliongoza taifa, lakini UHALALI huo hutokana na vyanzo vingine, na SIO KATIBA YA NCHI, na katika hili ningependa wajumbe wa bunge la Katiba (hasa CCM) waelewe kwamba:

Iwapo bunge la Katiba litavunjika bila ya muafaka juu ya katiba mpya, na iwapo uamuzi utakaofuatia utakuwa kwamba taifa liendelee kutumia Katiba iliyopo (1977) kwa vile ni Katiba “HALALI”, ni muhimu kwa wajumbe husika kuelewa kwamba Serikali ya awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere chini ya mfumo wa chama kimoja, serikali ambayo ndio iliyotunga Katiba ya sasa JMT (1977), chanzo (source) cha Uhalali wake haikuwa ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) bali chanzo cha uhalali huo ilikuwa ni haya yafuatayo:

· Kwanza - Historia ya TANU (na ASP) ya kupambana kutokomeza ukoloni na kutetea wanyonge.
· Pili – Uwepo wa ‘a popular and Charismatic Leaders’, hasa Baba wa Taifa, J.K Nyerere.
· Tatu - itikadi ya Ujamaa chini ya Azimio La Arusha.

Katika mazingira haya, wananchi wengi hawakujali sana kuhusu “content and practice” ya Katiba ya JMT (1977). Pia hawakujali sana iwapo Katiba ya nchi ilikuwa inafuatwa au inakiukwa. Badala yake wananchi walio wengi waliona serikali yao ni serikali halali kutokana na sources tajwa hapo juu. Uhalali wake haukutokana na Katiba ya JMT (1977). Lakini katika mazingira ya sasa, hali imebadilika, kwani:

· Uhalali wa kihistoria wa TANU/ASP/CCM kama vyama vilivyopigania uhuru na kutetea wanyonge walio wengi, uhalali huu umeshafifia.
· Taifa (na CCM) haina tena charismatic leaders wa mifano ya Mwalimu Nyerere, Karume na wengine wanaofanana nao.
· Itikadi ya Ujamaa haipo tena, na hata rasimu ya Katiba imeifuta ingawa CCM inaenda kwenye bunge la katiba kama chama cha ‘kijamaa’.

Maswali yanayofuatia ni kwamba - iwapo haya matatu yote yametoweka, Je:

· Maridhiano ya kitaifa (national consensus) yatajengwa na kitu gani?
· Ni kitu gani kitafanya pawepo na “loyalty na obedience” miongoni mwa “watawala” (rulers) na “watawaliwa” (ruled) bila ya kujalisha itikadi za vyama vya siasa?

Jibu dhahiri ni “KATIBA MPYA” ambayo itatokana na umma/wananchi.

Umuhimu wa Taifa kupata Katiba mpya unazidi kuwa na nguvu kwa kuzingatia kwamba katika nyakazi za sasa, taifa halipo tena chini ya mfumo wa chama kimoja bali vyama vingi vya siasa, na kwa hoja hii peke yake, umuhimu wa Katiba yenye uhalali wa kisiasa bila ya kujalisha itikadi za vyama unazidi kuwa mkubwa. Vinginevyo tukiendelea kuwa na katiba inayopendelea chama kimoja cha siasa, basi chama chochote kitakachoingia madarakani baada ya CCM kitashawishika kubadilisha katiba itakayokuwepo ili kukidhi mahitaji ya chama husika. Hali hii itatupeleka kwenye machafuko makubwa. Njia pekee ya kuepusha balaa hili ni kwa vyama vilivyopo kuweka mbali itikadi zao pembeni na kujadili katiba yenye maslahi ya taifa.

Scenario ya tatu na mwisho ni kwamba:
Bunge la Katiba litaridhia kuendelea na mfumo wa muungano wa serikali mbili. Hii itatokana na wajumbe wanaotetea mfumo wa serikali tatu kushindwa na wenzao wa serikali mbili “kwa hoja za kisiasa” Zaidi, kwa mfano:

· Hoja kwamba serikali tatu zitapelekea kutoweka kwa amani na utulivu nchini.
· Hoja kwamba serikali tatu zitapelekea kuvunjika kwa muungano.
· Hoja kwamba serikali tatu itakuwa ni mzigo kwa walipa kodi.
· Na hoja mpya iliyobuniwa hivi karibuni kwamba – “idadi ya wananchi”waliofikiwa na tume ya katiba kutoa maoni yao juu ya mfumo wa muungano ni idadi ndogo sana ikilinganishwa na jumla ya watanzania ambao ni Zaidi ya watu milioni 40.

Ø Tukianza na hoja juu ya amani na utulivu:
Masuala yanayopelekea taifa lolote lile kuingia katika vurugu ni pamoja na ukandamizaji wa haki na demokrasia, ubadhirifu wa fedha za walipa kodi (ufisadi) na matumizi mabaya ya rasilimali za taifa. Katika muktadha wa muungano wetu, vurugu za upande wa Zanzibar zimetokana na wazanzibari kupigania haki ‘autonomy’ na ‘identity’ ya kama moja ya nchi shiriki za muungano. Hoja kwamba chanzo cha machafuko husika ni udini ni hoja za kisiasa zenye mapengo maalum to justify mambo Fulani Fulani. Kwa upande wa “Tanzania Bara”, wengi walikuwa wamefumbwa macho na “kiini macho”. Na isitoshe wananchi walizuiwa kujadili suala la muungano, na matokeo yake ikawa kwamba – walinzi wa Muungano ikawa ni “vyombo vya ulinzi na usalama” badala ya “wananchi”. Katika muungano wowote ule duniani, Walinzi wa kweli na wa Kuaminika wa muungano inatakiwa kuwa ni WANANCHI, sio vyombo vya ulinzi na usalama. Sasa kwa vile wananchi walio wengi wamependelea muungano wa serikali tatu, basi ni dhahiri kwamba ni wananchi hao hao ndio watakaoulinda muungano wanaoupenda kwa hali na mali. Nje ya hapo, tutaendelea na mfumo wa kulazimisha, ambao utachochea machafuko ndani ya taifa letu. Kwa mantiki hii, hoja kwamba Serikali Tatu zitapelekea uvunjifu wa amani na utulivu ‘ goes straight to the dustbin’.

Ø Tukija kwenye hoja ya pili kwamba “serikali tatu” zitavunja muungano:
Viongozi wa CCM ambao wanapinga serikali tatu, wengi wao ni wale wale ambao wana msimamo na na maoni ambayo yanavunja badala ya kuimarisha. Kwa mfano, kwa mujibu wa taarifa zilizopo, baadhi ya viongozi wa CCM waliotoa maoni yao mbele ya tume huku wakisimamia serikali mbili, pia walitaka kuwepo na mabadiliko makubwa kwenye katiba ambayo kimsingi yanadhoofisha muungano. Kwa mfano:

· Viongozi hawa wanaopendelea mfumo wa serikali mbili, pia wanataka Zanzibar iwe na kiti chake Umoja wa Mataifa, mabadiliko ambayo ni dhahiri yatapelekea kuvunjika kwa muungano. Lakini kwa mtazamo wao, haya yataimarisha muungano wa serikali mbili. Ni vigumu kuelewa nia yao kwa Tanganyika ni nini hasa. Hakuna lengo lingine hapa Zaidi ya ulafi wa madaraka. Pia:
· Viongozi hawa wa CCM pia wanataka Zanzibar iwe na Benki Kuu yake, Sarafu yake, Usalama wa taifa, Jeshi, Polisi na rais wake kutambulika kama amiri jeshi mkuu. Kwa mtazamo wao, haya yataimarisha muungano wa serikali mbili. Katika hili, pia ni vigumu kuelewa nia ya kwa Tanganyika ni nini hasa. Hakuna lengo lingine hapa Zaidi ya ulafi wa madaraka.

Muungano ambao unampa mshirika mmoja (Zanzibar) ‘autonomy na identity’ anayostahili huku mshirika mwingine (Tanganyika) akinyimwa haya, ni dhahiri kwamba muungano wa ain ahiyo hautadumu. Kwa maana nyingine, viongozi wa aina hii ndani ya CCM ndio watakawa ni sababu ya kuvunjika kwa muungano.

Ø Tukija kwenye hoja kwamba serikali tatu itakuwa ni mzigo kwa walipa kodi:
Hoja hii tumeshaifafanua vya kutosha, lakini pia tume ya warioba imefanya kazi nzuri katika hilo. Pamoja na hayo, bado wapo viongozi ndani ya CCM na wafuasi wao waliendeleza ‘hoja za kisiasa’ kuwatishia wananchi. Lakini habari njema ni kwamba wananchi wengi wanazidi kuwa waelewa na wameangalia suala la muungano “over and above politics”, na ndio maana juhudi za baadhi ya viongozi wa CCM kuwashawishi waendelee kuishi chni ya kiini macho, juhudi hizo zimegonga mwamba kwani 34% ndio wameitikia wito wa viongozi hawa huku 61% wakipinga hoja za viongozi hawa wa CCM.

Na mwisho ni hoja mpya ya “kisiasa” kwamba wananchi waliofikiwa na tume ya warioba kutoa mapendekezo ya serikali tatu ni wachache mno ikilinganishwa na jumla ya watanzania ambao ni karibia milioni 45. Hoja hii ni mufilisi, na mjumbe yoyote wa bunge la katiba ambae ni msomi na mwelewa hawezi thubutu kusimamia hoja hii. Mimi sio “statician” lakini kwa upeo wangu mdogo katika hili (wataalam wengine watanisaidia Zaidi):

Idadi ya watanzania waliosikilizwa na tume ya warioba ni ‘sample’ kati ya watanzania Zaidi ya milioni 40. Ni muhimu wanasiasa wa CCM watakaoenda kujadili hoja hii kwenye bunge la katiba wakafahamu kwamba hata kama idadi ya watanzania wote ingekuwa haijulikani, kuchukua sample ya 37,00 bado isingekuwa tatizo kwani “Mathematics of probability” zina prove for us kwamba size of population doesn’t matter unless size ya sample yako exceeds a few percentage ya total population unayoitafiti. Kwa mantiki hii, hata sample ya watu (500) mia tano tu is equally useful kutafiti maoni katika idadi ya watu hata milioni kumi na tano, as it would kwa population ya watu laki moja. Na ndio maana ni kawaida kwa ‘survey systems’ ku ‘ignore’ the population size, kama size ya population ni kubwa sana au kama haijulikani. Population size becomes a factor only if unahusisha idadi ndogo sana ya watu au una ‘deal’ na idadi ya wanachama au wajumbe wa chombo Fulani ambao wajulikana wapo wangapi, kwa mfano “idadi ya wanachama wa CCM ambao inaodaiwa kwamba wapo “milioni sita”.
Ni matumaini yetu kwamba tutawakilishwa na wajumbe wenye uelewa wa “mathematics of probability”, ili wanasiasa uchwara wasiende bungeni kupotosha umma kwa kukejeli matokeo ya utafiti wa tume ya jaji warioba.

Bila Tanganyika, Tanzania Haiwezekani. Tusemezane.

Cc Nguruvi3, Mag3, Candid Scope, Jasusi, Pasco, Mzee Mwanakijiji, JokaKuu, Zinedine, MTAZAMO, zumbemkuu, Mkandara, Kichuguu, Bongolander, Nape Nnauye, ZeMarcopolo, zomba, chama, Ritz, MwanaDiwani, Kimbunga, JingalaFalsafa, Kobello, EMT, Ngongo
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi, kabla sijaanza kusoma post yako, la muhimu, haraka, na dharura zaidi, wanaohusika waboreshe daftari la kudumu la wapiga kura. Hii kitu ni muhimu kuliko hilo Bunge la Katiba au hata Katiba yenyewe. Bila watu (wapiga kura) Bunge na Katiba havina maana yoyote.

.... naanza sasa kusoma huu uzi.
 
Mchambuzi Jifunze kuelewa wasomaji wengi wanatumia simu, na hapa ni mgongano wa mawazo. Hivyo basi jitahidi uwe unafupisha article with the same meaning. Asante kwa uliowatag maana ndio umewakusudia
 
As far as I know katiba yetu itapita kwa urahisi sana... kitu kinachokosekana kabla ya Bunge la Katiba ni elimu ya why rasimu is the way it is today... Hivyo niombe vyombo vya habari makini viendelee kuwa-engage akina Warioba, Jaji Ramadhani and team extensively ili wajumbe waelewe kwa nini rasimu iko hivyo kabla wao wenyewe hawajajadili.
 
Mchmbuzi ki utaratibu kabisa bunge linatakiwa kuipitisha rasimu ya pili kama ilivyo kwa ajili ya kuipa legal legitimacy hwatakiwi kufanya mabadiliko kwa hayo ni mawazo ya mabosi wao wananchi hawana mamlaka ya ku question mawazo halali ya wananchi kwa maana ya namna ambavyo wanataka watawaliwaje full stop. Mchambuzi namba ya mil.6 walioko ccm umeipata wapi walipata kura mil.5 watakuwa na BAHATI km hao watakuwa wamebakia labda milioni2 kwa hivi sasa
 
Maneno meeengi lakini point yako hapa tukubali serikali tatu.lakini haya mambo huwezi kulazimisha,litakoloamliwa na wengi ndo hilohilo.
 
Siku sio nyingi zijazo, Bunge la katiba litakutana mjini Dodoma kufanyia kazi rasimu ya pili ya Katiba. Iwapo "kila kitu kitaenda sawa", Katiba hii itakuwa ni ya kwanza itokanayo na umma/wananchi tangia uhuru (1961). Katika mchakato wa maoni ya katiba mpya kwenye umma, sehemu kubwa ya mjadala ilihusisha suala la Muungano, na hii ni kwa mujibu wa tume ya Jaji Warioba. Kwahiyo kuelekea bunge la Katiba, nadhani kuna haja yetu kujikita Zaidi katika suala la muundo wa muungano, hasa ikizingatiwa kwamba katika hili, wajumbe wa CCM wanaenda kulisimamia kama kwa vile ni moja ya masuala machache ambayo CCM inayasimamia "kisera".

Ni muhimu tukumbuke kwamba mjadala juu ya muundo wa muungano uliingizwa kwenye sheria ya mabadiliko ya katiba bila ya matakwa ya viongozi kadhaa wa CCM na serikali yake. Ilikuwa ni wananchi (hasa wa Zanzibar) ambao ndio walilazimisha suala la muungano liingie kwenye sheria ya mabadiliko ya Katiba. Sote tunakumbuka jinsi gani wananchi wa Zanzibar walivyopinga muswada wa awali wa serikali kwa kuchoma moto hadharani rasimu waliyopelekewa. Isingekuwa ni busara za Waziri Samwel Sitta ambae ndiye aliyeiwakilisha serikali katika hafla ile, pengine leo tungekuwa tunazungumza mengine. Matukio mengine mengi yalifuatia baada ya hapo, lakini muhimu kuelekea bunge la katiba ni kwamba:

Licha ya WANANCHI wengi kuwasilisha maoni yao kwa tume ya Katiba juu ya mfumo wa muungano wanaopendelea, "bado kuna viongozi wa CCM na wafuasi wao" wasiolitakia mema taifa letu ambao wanaendelea "kukaidi" matakwa ya wengi juu ya mfumo wa muungano wanaoona unawafaa.

Licha ya MWENYEKITI WA CCM TAIFA (Rais Kikwete) kuwaelimisha viongozi wa CCM juu ya umuhimu wa "kujiandaa Kisaikolojia" na mfumo wa serikali Tatu baada ya Kikwete kusoma alama za nyakati kufuatia mgogoro usiokwisha kwa miaka 50, "bado kuna baadhi ya viongozi wa CCM na wafuasi wao" wanaoendelea kukaidi ushauri wa mwenyekiti wao wa CCM (Taifa). Viongozi hawa wa CCM wanataka Mwenyekiti wa CCM taifa afuate matakwa ya chama (CCM) badala ya wao kufuata ushauri wake wenye busara ambao unalenga kuwaamsha kwa nia ya kuepusha mgogoro mkubwa ndani ya taifa letu.

Licha ya MWENYEKITI WA CCM TAIFA (Rais Kikwete) kuhimiza kwa viongozi wa vyama vya siasa juu ya umuhimu wa vyama hivi kuweka mbali itikadi zao katika kipindi hiki na badala yake kuweka mbele maslahi ya taifa, "bado kuna viongozi wa CCM na wafuasi wao" wanaoendelea kukaidi wito huu kutoka kwa Mwenyekiti wao (Taifa). Kwa mfano rejea tamko la UVCCM hivi karibuni kuhusiana na muundo wa muungano. Ukaidi huu unatuacha na maswali mengi kuliko majibu juu ya nini itakuwa ni hatima ya bunge la katiba linalotarajiwa kukutana hivi karibuni, lakini muhimu Zaidi, nini itakuwa ni hatima ya muungano wetu na taifa letu.

Licha ya ukweli kwamba mshirika mwingine wa muungano tayari ameshafanya maamuzi ambayo kimsingi, Katiba yake inapindua mambo mengi yaliyomo ndani ya Katiba ya JMT (1977). Kwa mfano, Zanzibar imebadili katiba yake na kuchukua madaraka ya Jamhuri ya Muungano, kama vile kuelekeza sheria za muungano zilizopitishwa na bunge la muungano kupelekwa kwenye baraza la wawakilishi. Maana yake ni kuwa, Katiba ya Zanzibar sasa ipo juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Licha ya haya yote, bado viongozi hawa wa CCM wanakaidi hoja za watanganyika na wao kuja na serikali yao na katiba yao.

Mienendo na matamshi ya viongozi hawa wa CCM hasa yanayokaidi matakwa ya wengi juu ya mfumo wa muungano yatafanya tuamini kwamba, katika suala la muungano, matokeo ya bunge la Katiba yanaweza chukua sura kuu tatu zifuatazo:

Scenario ya kwanza:


Kuna mambo matatu muhimu ya kuyaangalia hapa. Kwanza, ikumbukwe kwamba hadi leo hakuna ushahidi wowote unao onyesha kwamba wananchi/umma ulishirikishwa katika kufikia maamuzi ya sera ya serikali mbili. Pili, utaratibu/Mchakato wa chama (CCM) wa kutunga au kubadili sera zake upo wazi – kwa maana ya kwamba mabadiliko yoyote ya kisera ni lazima yahusishe NEC na baadae kupata Baraka za mkutano mkuu wa ccm (taifa). Na tatu, sote tunajua kwamba kufikia tarehe ya bunge la katiba kuanza, hakuna kikao cha namna hiyo ambacho kitakuwa kimekaa. Na kitendo cha CCM kuamua kutofanyia mabadiliko ya sera ya muungano wa serikali mbili hadi tarehe ya bunge la katiba, maana yake ni kwamba CCM imeamua kufa kiume na sera yake hii. Kwa mantiki hii, iwapo wajumbe wa CCM wataamua kufanya maamuzi ambayo yatapingana na sera rasmi ya chama chao (CCM) ya "serikali mbili", hiyo itakuwa ni political suicide kwa CCM kuelekea 2015.

Mtu anaweza kujenga hoja kwamba iwapo wajumbe wa CCM watakabiliwa na upinzani mkali bungeni katika kusimamia sera ya CCM ya "muungano wa serikali mbili", CCM itaweza kujinasua kwa kuhusisha Kamati ya wabunge wa CCM ambayo itaweza kukutana kwa dharura na hatimaye wajumbe wa CCM kuja na msimamo na mshikamano unaounga mkono matakwa ya wananchi walio wengi (kwa mujibu wa rasimu ya katiba). CCM ingeweza kufanya hivyo katika masuala mengine lakini kwa suala la muungano, CCM ina maslahi yake, lakini muhimu Zaidi ni kwamba, suala hili linagusa sera ya chama kwa mujibu wa katiba ya chama. Kwa hali hii, itakuwa ni vigumu sana kwa kamati ya wabunge wa CCM kufanya maamuzi kinyume na sera rasmi ya chama chao (CCM), vinginevyo watarajie kukivunja chama. Katiba ya CCM haiwapi wajumbe wa CCM katika bunge hilo mamlaka ya kubadili sera za chama, badala yake wanatarajiwa kwenda katika bunge hilo kutetea muungano wa serikali mbili. Mamlaka ya kubadili sera lazima yapitie NEC (CCM) na kubarikiwa na Mkutano Mkuu wa Taifa, vikao ambavyo ni dhahiri kwamba CCM ilishaamua kutouviitisha kuelekea bunge la Katiba.

Hivyo basi, chini ya scenario hii ya kwanza, iwapo wajumbe wa CCM wataamua kuunga mkono muungano wa serikali tatu, basi hiyo itakuwa ni hatua ya kwanza kwa CCM kuvunjika vipande vipande kuelekea uchaguzi mkuu (2015).

Scenario ya pili ni kwamba:


Bila ya kujalisha wajumbe wa CCM watajenga hoja gani juu ya haja ya nchi kuendelea kuwa chini ya Katiba ya sasa mpaka hapo baadae kwa vile ni Katiba ya JMT (1977) bado ni halali, ukweli utaendelea kubakia kwamba, ili taifa lisonge mbele kwa amani na utulivu, suala la katiba mpya haliwezi kwepeka tena. Umuhimu wa taifa kuhitaji Katiba mpya haraka upo katika maeneo makuu matatu ya hoja kama ifuatavyo:

Kwanza – on the practical level (KIVITENDO), Katiba ya JMT (1977) kwa sasa "is no longer irrelevant". Na hii ni kwa sababu, msingi wa Katiba ya JMT (1977) ulijengwa juu ya nguzo kuu mbili ambazo ni:
· Nguzo ya kwanza ni Mfumo wa Chama Kimoja Cha Siasa (CCM).
· Nguzo ya pili ni Mfumo wa Muungano wa Serikali Mbili.

Hakuna mjadala kwamba nguzo zote mbili kwa sasa zimesha momonyoka. Ama tutakavyoona, kilichokuwa kinaupa muungano pamoja na sera husika ya CCM uhalali ilikuwa ni masuala mengine. Vinginevyo, katika kipindi chote cha miaka 50 ya muungano, umma haukuwahi shirikishwa juu ya mfumo wanaopendelea, na pia umma haukuruhusiwa kujadili suala la muungano. Matokeo yake ni kwamba, Mlinzi wa muungano huu ikawa ni ‘vyombo vya ulinzi na usalama' badala ya wananchi ambao, katka hali ya kawaida, ndio hutakiwa kuwa walinzi wa muungano. Hata Mwalimu aliwahi jadili kwamba hatowapiga mabomu wananchi ambao wataukataa muungano. Miaka 50 baadae, kwa mujibu wa rasimu ya katiba, hatimaye wananchi wamepara fursa ya kutoa maoni yao juu ya muungano, na walio wengi wameonyesha jinsi gani hawaridhiki na mfumo wa sasa wa serikali mbili.

Hoja ya pili juu ya umuhimu wa taifa kupata katiba mpya ipo ‘on a very basic principle'. Inaonekana kwamba Viongozi wa CCM wanaopinga mfumo wa serikali tatu ambao ni matakwa ya wananchi walio wengi wanashindwa kuelewa kwamba Katiba sio tu ni nyaraka ya kisheria au kitaalamu (it is not simply a legal or/and technical document), bali muhimu Zaidi ni kwamba Katiba ni nyaraka ya kisiasa (a political document). Ili Katiba ipate uhalali wa kisiasa (political legitimacy) na kustahili utiifu na uaminifu (obedience and loyalty) kwa pande zote mbili za jamii – (rulers) watawala na (the ruled) watawaliwa, ni lazima katiba ya nchi iwe na maridhiano kitaifa (national consensus). Ndani ya Katiba kwa kawaida huwa kuna kanuni za msingi ambazo kwa ujumla wake, hutoa mwongozo juu ya jinsi gani jamii inataka kuji ‘organize' naku ‘behave', relative to the use of political power ndani ya taifa. Vile vile katiba ya nchi kwa kawaida huwa ina ‘determine' na kutoa taswira ya jinsi gani mahusiano baina ya serikali (state) na jamii (society) yanatakiwa yawe. Ni kwa misingi hii, kuna ulazima wa maridhiano mapana (broad consensus) ndani ya taifa ili Katiba ya nchi iweze kupata uhalali (legitimacy) mbele ya umma.

Katiba isiyotokana na ‘national consensus' pia huwa inakosa uhalali wa kisiasa (political legitimacy). Katiba ya namna hii huwa ni Katiba ambayo hulazimishwa kwa wananchi, na matokeo yake huwa - sio watawala (rulers) wala watawaliwa (ruled) ambao huijali na kuiheshimu. Baada ya kusema hayo, niseme pia kwamba - haina maana kwamba serikali inayoongoza chini ya katiba ya namna hii huwa haina uhalali wa kuongoza nchi/taifa. Serikali husika inaweza kupata ‘uhalali' wa kuliongoza taifa, lakini UHALALI huo hutokana na vyanzo vingine, na SIO KATIBA YA NCHI, na katika hili ningependa wajumbe wa bunge la Katiba (hasa CCM) waelewe kwamba:

Iwapo bunge la Katiba litavunjika bila ya muafaka juu ya katiba mpya, na iwapo uamuzi utakaofuatia utakuwa kwamba taifa liendelee kutumia Katiba iliyopo (1977) kwa vile ni Katiba "HALALI", ni muhimu kwa wajumbe husika kuelewa kwamba Serikali ya awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere chini ya mfumo wa chama kimoja, serikali ambayo ndio iliyotunga Katiba ya sasa JMT (1977), chanzo (source) cha Uhalali wake haikuwa ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) bali chanzo cha uhalali huo ilikuwa ni haya yafuatayo:

· Kwanza - Historia ya TANU (na ASP) ya kupambana kutokomeza ukoloni na kutetea wanyonge.
· Pili – Uwepo wa ‘a popular and Charismatic Leaders', hasa Baba wa Taifa, J.K Nyerere.
· Tatu - itikadi ya Ujamaa chini ya Azimio La Arusha.

Katika mazingira haya, wananchi wengi hawakujali sana kuhusu "content and practice" ya Katiba ya JMT (1977). Pia hawakujali sana iwapo Katiba ya nchi ilikuwa inafuatwa au inakiukwa. Badala yake wananchi walio wengi waliona serikali yao ni serikali halali kutokana na sources tajwa hapo juu. Uhalali wake haukutokana na Katiba ya JMT (1977). Lakini katika mazingira ya sasa, hali imebadilika, kwani:

· Uhalali wa kihistoria wa TANU/ASP/CCM kama vyama vilivyopigania uhuru na kutetea wanyonge walio wengi, uhalali huu umeshafifia.
· Taifa (na CCM) haina tena charismatic leaders wa mifano ya Mwalimu Nyerere, Karume na wengine wanaofanana nao.
· Itikadi ya Ujamaa haipo tena, na hata rasimu ya Katiba imeifuta ingawa CCM inaenda kwenye bunge la katiba kama chama cha ‘kijamaa'.

Maswali yanayofuatia ni kwamba - iwapo haya matatu yote yametoweka, Je:

· Maridhiano ya kitaifa (national consensus) yatajengwa na kitu gani?
· Ni kitu gani kitafanya pawepo na "loyalty na obedience" miongoni mwa "watawala" (rulers) na "watawaliwa" (ruled) bila ya kujalisha itikadi za vyama vya siasa?

Jibu dhahiri ni "KATIBA MPYA" ambayo itatokana na umma/wananchi.

Umuhimu wa Taifa kupata Katiba mpya unazidi kuwa na nguvu kwa kuzingatia kwamba katika nyakazi za sasa, taifa halipo tena chini ya mfumo wa chama kimoja bali vyama vingi vya siasa, na kwa hoja hii peke yake, umuhimu wa Katiba yenye uhalali wa kisiasa bila ya kujalisha itikadi za vyama unazidi kuwa mkubwa. Vinginevyo tukiendelea kuwa na katiba inayopendelea chama kimoja cha siasa, basi chama chochote kitakachoingia madarakani baada ya CCM kitashawishika kubadilisha katiba itakayokuwepo ili kukidhi mahitaji ya chama husika. Hali hii itatupeleka kwenye machafuko makubwa. Njia pekee ya kuepusha balaa hili ni kwa vyama vilivyopo kuweka mbali itikadi zao pembeni na kujadili katiba yenye maslahi ya taifa.

Scenario ya tatu na mwisho ni kwamba:


Ø Tukianza na hoja juu ya amani na utulivu:
Masuala yanayopelekea taifa lolote lile kuingia katika vurugu ni pamoja na ukandamizaji wa haki na demokrasia, ubadhirifu wa fedha za walipa kodi (ufisadi) na matumizi mabaya ya rasilimali za taifa. Katika muktadha wa muungano wetu, vurugu za upande wa Zanzibar zimetokana na wazanzibari kupigania haki ‘autonomy' na ‘identity' ya kama moja ya nchi shiriki za muungano. Hoja kwamba chanzo cha machafuko husika ni udini ni hoja za kisiasa zenye mapengo maalum to justify mambo Fulani Fulani. Kwa upande wa "Tanzania Bara", wengi walikuwa wamefumbwa macho na "kiini macho". Na isitoshe wananchi walizuiwa kujadili suala la muungano, na matokeo yake ikawa kwamba – walinzi wa Muungano ikawa ni "vyombo vya ulinzi na usalama" badala ya "wananchi". Katika muungano wowote ule duniani, Walinzi wa kweli na wa Kuaminika wa muungano inatakiwa kuwa ni WANANCHI, sio vyombo vya ulinzi na usalama. Sasa kwa vile wananchi walio wengi wamependelea muungano wa serikali tatu, basi ni dhahiri kwamba ni wananchi hao hao ndio watakaoulinda muungano wanaoupenda kwa hali na mali. Nje ya hapo, tutaendelea na mfumo wa kulazimisha, ambao utachochea machafuko ndani ya taifa letu. Kwa mantiki hii, hoja kwamba Serikali Tatu zitapelekea uvunjifu wa amani na utulivu ' goes straight to the dustbin'.

Ø Tukija kwenye hoja ya pili kwamba "serikali tatu" zitavunja muungano:
Viongozi wa CCM ambao wanapinga serikali tatu, wengi wao ni wale wale ambao wana msimamo na na maoni ambayo yanavunja badala ya kuimarisha. Kwa mfano, kwa mujibu wa taarifa zilizopo, baadhi ya viongozi wa CCM waliotoa maoni yao mbele ya tume huku wakisimamia serikali mbili, pia walitaka kuwepo na mabadiliko makubwa kwenye katiba ambayo kimsingi yanadhoofisha muungano. Kwa mfano:

· Viongozi hawa wanaopendelea mfumo wa serikali mbili, pia wanataka Zanzibar iwe na kiti chake Umoja wa Mataifa, mabadiliko ambayo ni dhahiri yatapelekea kuvunjika kwa muungano. Lakini kwa mtazamo wao, haya yataimarisha muungano wa serikali mbili. Ni vigumu kuelewa nia yao kwa Tanganyika ni nini hasa. Hakuna lengo lingine hapa Zaidi ya ulafi wa madaraka. Pia:
· Viongozi hawa wa CCM pia wanataka Zanzibar iwe na Benki Kuu yake, Sarafu yake, Usalama wa taifa, Jeshi, Polisi na rais wake kutambulika kama amiri jeshi mkuu. Kwa mtazamo wao, haya yataimarisha muungano wa serikali mbili. Katika hili, pia ni vigumu kuelewa nia ya kwa Tanganyika ni nini hasa. Hakuna lengo lingine hapa Zaidi ya ulafi wa madaraka.

Muungano ambao unampa mshirika mmoja (Zanzibar) ‘autonomy na identity' anayostahili huku mshirika mwingine (Tanganyika) akinyimwa haya, ni dhahiri kwamba muungano wa ain ahiyo hautadumu. Kwa maana nyingine, viongozi wa aina hii ndani ya CCM ndio watakawa ni sababu ya kuvunjika kwa muungano.

Ø Tukija kwenye hoja kwamba serikali tatu itakuwa ni mzigo kwa walipa kodi:
Hoja hii tumeshaifafanua vya kutosha, lakini pia tume ya warioba imefanya kazi nzuri katika hilo. Pamoja na hayo, bado wapo viongozi ndani ya CCM na wafuasi wao waliendeleza ‘hoja za kisiasa' kuwatishia wananchi. Lakini habari njema ni kwamba wananchi wengi wanazidi kuwa waelewa na wameangalia suala la muungano "over and above politics", na ndio maana juhudi za baadhi ya viongozi wa CCM kuwashawishi waendelee kuishi chni ya kiini macho, juhudi hizo zimegonga mwamba kwani 34% ndio wameitikia wito wa viongozi hawa huku 61% wakipinga hoja za viongozi hawa wa CCM.

Na mwisho ni hoja mpya ya "kisiasa" kwamba wananchi waliofikiwa na tume ya warioba kutoa mapendekezo ya serikali tatu ni wachache mno ikilinganishwa na jumla ya watanzania ambao ni karibia milioni 45. Hoja hii ni mufilisi, na mjumbe yoyote wa bunge la katiba ambae ni msomi na mwelewa hawezi thubutu kusimamia hoja hii. Mimi sio "statician" lakini kwa upeo wangu mdogo katika hili (wataalam wengine watanisaidia Zaidi):

Idadi ya watanzania waliosikilizwa na tume ya warioba ni ‘sample' kati ya watanzania Zaidi ya milioni 40. Ni muhimu wanasiasa wa CCM watakaoenda kujadili hoja hii kwenye bunge la katiba wakafahamu kwamba hata kama idadi ya watanzania wote ingekuwa haijulikani, kuchukua sample ya 37,00 bado isingekuwa tatizo kwani "Mathematics of probability" zina prove for us kwamba size of population doesn't matter unless size ya sample yako exceeds a few percentage ya total population unayoitafiti. Kwa mantiki hii, hata sample ya watu (500) mia tano tu is equally useful kutafiti maoni katika idadi ya watu hata milioni kumi na tano, as it would kwa population ya watu laki moja. Na ndio maana ni kawaida kwa ‘survey systems' ku ‘ignore' the population size, kama size ya population ni kubwa sana au kama haijulikani. Population size becomes a factor only if unahusisha idadi ndogo sana ya watu au una ‘deal' na idadi ya wanachama au wajumbe wa chombo Fulani ambao wajulikana wapo wangapi, kwa mfano "idadi ya wanachama wa CCM ambao inaodaiwa kwamba wapo "milioni sita".
Ni matumaini yetu kwamba tutawakilishwa na wajumbe wenye uelewa wa "mathematics of probability", ili wanasiasa uchwara wasiende bungeni kupotosha umma kwa kukejeli matokeo ya utafiti wa tume ya jaji warioba.

Bila Tanganyika, Tanzania Haiwezekani. Tusemezane.

Cc Nguruvi3, Mag3, Candid Scope, Jasusi, Pasco, Mzee Mwanakijiji, JokaKuu, Zinedine, MTAZAMO, zumbemkuu, Mkandara, Kichuguu, Bongolander, Nape Nnauye, ZeMarcopolo, zomba, chama, Ritz, MwanaDiwani, Kimbunga, JingalaFalsafa, Kobello, EMT, Ngongo


Kama ulivyosaidia kufafanua scenarios tatu katika muelekeo wa nini kinachowakabili Wabunge wa CCM, ingekuwa jambo la busara kuwaeleza scenario ipi itakuwa bora kwao.


Kwa upande wangu nahisi scenario ya kwanza ndio itakayoisaidia CCM. Uzoefu unatuonyesha kuwa CCM hawajawa wakweli katika nyoyo zao badala yake wamekuwa wakisimamia masilahi yao tu hasa viongozi. Mara ngapi wamekuwa wakiweka ahadi na kuzivunja wao wenyewe, hawajawahi kutekeleza ahadi yoyote katika wanayodai kuyafanya kusafisha chama chao. CCM toka imeundwa imekuwa ikiendeshwa kwa makundi hivyo suwala kuwa kuitupa sera yao ya serikali mbili mbele ya maslahi ya kura za wananchi halitowazuia CCM kubadilika.
Bado nahisi CCM watapima upepo na kuingia kundini na kujilabu kuwa wao ndio vinara wa mageuzi.

Ukweli ni kuwa naombea kwa mola CCM ichague scenario ya kwanza kwani ni hiyo tu ndiyo itakayowapa nafasi ya usawa na vyama vya upinzani kugombea uwakilishi wa wananchi na kuongoza dola. Vyama vya upinzani bado havijaonyesha imani kwa wananchi wengi lakini CCM ikikosea hesabu itawafanya wengi waamuwe kutoshiriki uchaguzi na hilo maana yake kuwa CCM itaanguka vibaya.
 
Nakuunga mkono mchambuzi. CCM kwa ukaidi tu, hawatakubaliana na uhitaji wa Katiba mpya yenye mfumo wa serikali tatu na yawezekana wakavuruga kabisa bunge hilo. Swali tu ni kuwa hali hiyo itakapotokea WaTZ unashauri wachukue hatua gani? Kuna uwezekano mkubwa wa hilo kutokea!!
 
Jambo la msingi ambalo naona katika bunge la katiba ambalo wengi wa wajumbe ni kutoka CCM wakiwa na itikadi na sera pengine zinazotofautiana na matakwa ya wananchi walio wengi kuhusu muundo wa Muungano, hali kadhalika mfumo wa serikali ya Muungano ambayo katika rasimu hii inaonyesha uwepo wa serikali tatu, mbili za serikali shiriki katika Muungano na moja serikali kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa vile mtazamo wa baadhi ya wajumbe ni itikadi za kichama badala ya kitaifa, kuna haja ya kufanyiwa semina ili kuwajengea uelewa wa kujali utaifa zaidi kwa kuangalia mbali badala itikadi za kichama zenye mlengo wa upande mmoja usio na mtazamo wa kina kitaifa.

Pengine mmoja wa wafanyiza semina wangekuwa kati ya wajumbe wa tume, bila hivyo kuachia hali ilivyo kwa mtazamo wa kichama kutakuwa na haja ya kufanyiwa marekebisho yasiyoepukika siku za karibuni tu katika katiba mpya.
 

Kwa vile mtazamo wa baadhi ya wajumbe ni itikadi za kichama badala ya kitaifa, kuna haja ya kufanyiwa semina ili kuwajengea uelewa wa kujali utaifa zaidi kwa kuangalia mbali badala itikadi za kichama zenye mlengo wa upande mmoja usio na mtazamo wa kina kitaifa.


Tatizo ni kwamba katiba ya JMT (1977) ilijengwa kwa nguzo kuu mbili - one party state (CCM) na muungano wa serikali mbili (sera rasmi ya ccm). Pamoja na amendments za hapa na pale za Katiba kufuatia mageuzi ya kisiasa nchini, kimsingi katiba ya sasa ya JMT bado ni katiba partisan na ndio maana mvutano mkubwa bado umekuwa ukiendelea katika mchakato wa katiba mpya. Katika mazingira haya, upinzani unashawishika kuja na agenda za kisiasa katika kujadili katiba mpya kwa imani kwamba hivyo ndivyo wataweza kufanikisha kutengua uccm katika katiba ya JMT ili kuweka a level playing field. Haina maana kuvihimiza vyama vya siasa kuweka itikadi zao pembeni katika kujadili katiba mpya huku chama kilichopo madarakani kinaendelea kuchambua mchakato wa katiba in a partisan fashion na kinaendelea kujipanga kwenda kwenye bunge la katiba kusimamia partisan issues.

Tatizo lingine ni kwamba viongozi wengi wa ccm wana amini kwamba maslahi ya ccm ndio maslahi ya taifa. Pia wana imani kwamba ccm is the only legitimate political expression of the state. Bila ya imani na mitazamo hii kubadilika, unachosema, pamoja na umuhimu wake, itakuwa ni vigumu kutekelezeka.

Pengine mmoja wa wafanyiza semina wangekuwa kati ya wajumbe wa tume, bila hivyo kuachia hali ilivyo kwa mtazamo wa kichama kutakuwa na haja ya kufanyiwa marekebisho yasiyoepukika siku za karibuni tu katika katiba mpya.

Suala la semina ni muhimu sana kama unavyojadili lakini litakuwa na maana pale tu wajumbe walio wengi watakapoacha ukaidi kama nilivyojadili, vinginevyo itakuwa ni kazi bure. Isitoshe, wengi hawana imani na tume ya katiba na walisha jaribu sana kuifuta kabla ya bunge la katiba kuanza. Njia pekee ya wajumbe hawa kuamka ni kwa asasi za kiraia kutoa elimu kwa umma ambapo sasa umma huko majimboni and elsewhere utawaeleza wawakilishi wao their hopes, aspirations and dreams katika katiba mpya. Wajumbe watakuwa hawana jinsi but to comply.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu Mchambuzi
Ahsante kwa bandiko lako. Ningeomba nitoke nje kidogo ili kuweza kueleweka.
Kauli ya Rais kuwa kutakapokuwa hakuna muafaka katiba itakayotumika ni hii iliyopo linaonyesha uwepo wa tatizo.

Tatizo lililopo limetokana na Rais na washauri wake walioshindwa kusoma alama za nyakati. Kitendo cha kuteka mchakato kuanzia mwanzo kililenga kulinda muungano wa serikali 2.
Hilo limeshindikana na sasa inaonekana Rais amepoteza control ya serikali 2 na haelewi hizo 3 zitakuwaje na kama kutakuwa na muafaka. Anachokifanya ni kuzuia kuvunjika kwa muungano.

Makosa aliyafanya kwasababu, kwanza alitakiwa apate mwafaka kama wananchi bado wanataka muungano. Halafu wananchi kama Tanzania au Tanganyika pekee (Zanzibar wana katiba) wakae na kuamua iwapo muungano utakuwepo ni wa aina gani. Kama haupo Tanganyika ijenge taifa lenye mwelekeo gani.

Baada ya hapo waitwe watu wa makundi mbali mbali kutegemeana na matokeo niliyoyasema hapo juu ili waamue katiba iandikweje, nini kiwemo na kwasababu gani na nini kiondolewe na sababu gani. Na mwisho waunde chombo cha kusimamia utaratibu.
Rais hakuliona tatizo hilo na mchakato mzima umekuwa wa katiba nusu ya wananchi nusu ya serikali. Hilo ni tatizo kwasababu haitakuwa katiba ya wananchi kwa ukamilifu.

Bunge la katiba litakuwa na wabunge wa Zanzibar na wa JMT. Hakuna wabunge wa kuitetea Tanganyika. Hivyo wabunge wa JMT kutoka bara watageuga kuitetea Tanganyika isiyokuwepo kwa sasa. Hili ni kosa kubwa kwasababu hatua zingefuatwa lingeshaonekana mapema.

Scenario yangu ya kwanza
Wabunge wa Tanganyika(bara) wataungana kama wa znz na kila mmoja akivutia ngozi kwake.
Theluthi mbili haitapatikana. Tunaweza kubaki na katiba iliyopo.

Scenario ya pili
Baadhi ya wabunge wa CCM(wa bara na Unguja tu) watatumia mwanya wa kutokuwepo kwa wajumbe wa tume ya Warioba kupotosha hoja za serikali 3 ili wabaki na 2 kwa manufaa yao
Theluthi mbili itakuwa matatani, tunaweza kubaki na katiba iliyopo.

Scenario ya tatu
Wajumbe wa ZNZ kushinikiza waondoe uraia katika masuala 7. Hili litawaunganisha wajumbe wa Tanganyika kwa kuangalia yale znz inayoyataka yawe ya muungano yatakuwa na faida gani kwa Tanganyika. Ikifika hapo 2/3 itapatikana Tanganyika na znz itagawanyik na 2/3 haitakuwepo.
Tutabaki na katiba iliyopo.

Scenario ya nne
Kutatumika vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia mwamvuli wa Spika ambaye atatoka CCM kwa jinsi ilivyo ili kushinikiza baadhi ya hoja kutoka serikalini zipite kwa nguvu.
Suala hili litawagawa wajumbe na 2/3 haitapatikana.

Scenario ya tano
Kwasababu ya uzanzibar na uwepo wa SMZ na BLW ambalo lina nguvu kuamua mambo ya muungano kuliko Bunge la JMT, wajumbe wa bara watakwenda katika bunge kama wajumbe wa Tanganyika. Uwezekano wa kupata 2/3 ya Tanganyika kwa mambo yanayoigusa Tanganyikaupo kwasababu watanganyika wameshakuwa 'sensitized' na uzanzibar.

Wao watakuwa tayari kusimamia masilahi ya Tanganyika kwa kutambua kuwa hawana cha kupoteza kwa matokeo ya aina yoyote.

Mzigo utarudi kwa znz ambayo licha ya kelele tunazosikia bado wanauhitaji muungano. Pressure itawagawa kati ya Unguja na Upemba. 2/3 inaweza kupatikana na serikali 3 zikawepo.

Kwa kuangalia scenario 1-4 matokeo ya kushindwa kwa bunge lawama zitamwendea rais na si bunge. Kama nilivyoeleza awali Rais hakuzingatia kanuni za uandishi wa katiba kwa mazingira tuliyo nayo. Muungano ulipaswa kujadiliwa kwa kura ya maoni endapo bado unahitajika kabla ya mchakato.Kilichotokea ni rais kuweka mkokoteni mbele ya farasi na sasa anataka kuurudisha nyuma.

Badala ya kuwa na wabunge wa Tanganyika watakaoridhiana na wenzao wa znz, sasa hivi kuna wabunge wa JMT ambao ni waWatanganyika watakaoihami nchi yao isiyo na uwakilishi.

Prssure ni kwa znz wenye kila kitu isipokuwa namna ya kubaki na Tanganyika salama wakitambua mkataba haupo na wanahitaji mahusiano na Tanganyika kwa namna yoyote.
Kama muungano utavunjika watakouvunja ni wznz though unlikely vinginevyo wangeshatumia option hiyo badala ya mkataba n.k.

Mtazamo wangu
 
Last edited by a moderator:
Naweza part kuungana na Nguruvi,kuwa kabla hata ya Rasmu au mchakato wa katiba mpya kuanza tungepewa nafasi ya kuamua watanzania kwa wingi wetu bila kuingiliwa na wanasiasa tunataka nini?Je ,tunauhitaji Muungano wa serikali mbili au wa serikali tatu. Au hatuuhitaji Muungano kabisa kwa kila mtu kuhitaji Nchi yake?

Wengi wa wanasiasa wanajali zaidi matumbo yao na familia zao,wanaogopa sana mabadiliko na mwisho wa siku ndiyo mara nyingi waanzishaji wa machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa kuogopa tu mabadiliko ya nyakati.Wengi wanadhani bila madaraka waliyonayo hawawezi kuishi.

Nategemea wabunge wa kutoka bara wataweka UZALENDO kwanza kwa jali kinachohitajika sasa kwa kuirudisha serikali ya Tanganyika baada ya kuona wenzetu Zanzibar wameshaamua wanataka nini,na hatuna sababu ya kuwalzimisha.
 
Mkuu Mchambuzi, kabla sijaanza kusoma post yako, la muhimu, haraka, na dharura zaidi, wanaohusika waboreshe daftari la kudumu la wapiga kura. Hii kitu ni muhimu kuliko hilo Bunge la Katiba au hata Katiba yenyewe. Bila watu (wapiga kura) Bunge na Katiba havina maana yoyote.

.... naanza sasa kusoma huu uzi.
Jaji Lubuva, kaishalitolea ufafanuzi suala hilo wataboresha daftari la wapiga kura, alisema watatumia teknolojia ya kisasa (biometric registration) kwa sasa hivi wapo kwenye mchakato wa zoezi hilo.

Jaji John Mkwawa alisema kukubali vitambulisho vya taifa kutumika katika uchaguzi ni hatari kwani Tanzania ina raia ambao siyo wazawa hivyo siyo jambo jema kukubali wakapiga kura.

Sasa na mimi namsoma Mchambuzi
 
Last edited by a moderator:
Kuhusu muundo wa Muungano tuombe na tusali CCM ikubali maoni ya wengi au wenye nchi yao (wananchi). Katiba tuliokuwa nayo ilikuwa ilikuwa na kila matakwa ("influence") ya CCM lakini ikaonekana kuwa na kasoro ya msingi kwamba haikuwahi kupata ridhaa ya wananchi. Sasa, baada ya wananchi kwa uhuru wao kusema wanataka serikali tatu (pamoja na CCM kuwa na nafasi ya juu ya ku-influence matokeo) sharti tukubali vinginevyo itakuwa muungano wa "as we were" na wananchi watarudi tena kudai katiba yenye ridhaa ya wananchi kwa tena gharama nyingine. Je tutafika? Ni nani adai ana akili kuliko akili zote zilizotumika (hasa kutoka wananchi wenyewe) katika mchakato wa kupata maoni ya wananchi hadi rasimu ya pili. Kwangu mimi kazi ya Bunge la Katiba ni kuboresha utekelezaji wa rasimu na siyo kamwe kubadili maoni ya wananchi. Matakwa binafsi yasituyumbishe. Ingawa nataka nchi moja Tanzania ninaheshimu matakwa ya wengi ya serikali tatu. La kuboresha napendekeza rais awe ni wa muungano tu. Viongozi wa Tanganyika na Zanzibar watafutiwe jina lingine na hii itakuwa na maandalizi mazuri baadaye kuwa na seriali moja.
 
· Kwanza - Historia ya TANU (na ASP) ya kupambana kutokomeza ukoloni na kutetea wanyonge.
· Pili – Uwepo wa ‘a popular and Charismatic Leaders', hasa Baba wa Taifa, J.K Nyerere.
·Tatu - itikadi ya Ujamaa chini ya Azimio La Arusha.


Mkuu mchambuzi Tanzania kimsingi imejengwa kwenye matofali hayo matatu, na legitimacy ya CCM naweza kusema huo ndio msingi wake.

Lakini tukianza kuziangalia CCM za sasa, hii ya bara na ile ya visiwani, unaweza kuona kuwa hakuna element hata moja ya TANU. CCM ya sasa si ya kumtetea mnyonge, kuna evidence nyingi zinazoonesha kuwa kwa sasa hii ni nchi ambayo haki ya myonge inategemea hisani ya mwenye nguvu. Kote bara na visiwani.

Kwa sasa hapa Tanzania hatuna mtu kama Nyerere anaweza kuikemea serikali na ikasikia. Sasa hivi JK does as he wish na mawaziri wanafanya wanayopenda as long as JK hachukii. Chama kwa sasa sio chama kama kilivyokuwa na katibu mkuu Rashid Kawawa. Hata mwenyekiti, katibu toka ngazi ya taifa, mkoa hadi wilaya naweza kutajwa kuwa hana moral authority ya kumnyooshe kidole mtu wa chini.

sasa hivi sidhani kama mtu anaweza kuzungumzia itikadi ya CCM, kwa sasa ipo tu kwenye vitabu, kinachozungumzwa ni sera ya chama au manifesto. Lakini zote mbili hazitekelezwi ispokuwa kuna vitu tofauti kabisa.


Lakini hata watanzania wenyewe tumeanza kubadilika, tukiangalia kijani ya siku hizi haifanani kabisa na ile ya enzi wa Mwalimu. Kijani ya sasa ni ya kisanii.

Issue ya katiba inaweza kuwa mile stone ya kubadillika kwa Tanzania, na inaweza kuwa chanzo cha mgogoro mkubwa baadaye. CCM watajitahidi kuibanaga ili kulinda masli yao na mambo yaliyomo kwenye documents zao, lakini inaelekea kuwa kazi hiyo itakuwa ngumu.

Kwa sasa nikiangalia bunge la katiba bado naona usanii fulani. Still CCM ina-dominate, kitakachopatikana ni documentes itakayolinda interest za CCM, unless will ya watanzania ifuatwe.

 
Mkuu Mchambuzi asante kwa bandiko lako lenye shule ya kutosha.Nitarejea baadae kuchangia mawili matatu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom