CCM na CHADEMA watambiana kushinda uchaguzi mdogo Arumeru mashariki

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Vyama vya CCM na CHADEMA vimetambiana kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru mashariki. Kwa upande wa CCM, Katibu wa itikadi na uenezi NAPE NAUYE amesema kuwa watani zao (akimaanisha CHADEMA) ni wasindikizaji tu katika uchaguzi huo kama ilivyokuwa katika chaguzi ndogo za Igunga na Uzini Zanzibar.

Aidha kwa upande wa CHADEMA mkurugenzi wa kampeni MSAFIRI MTEMENWA amesema anao uhakika kwa asilimia mia moja kwamba CHADEMA italichukua Jimbo hilo bila kutumia nguvu kubwa.


Vyama vyote vimeshaanza mchakato wa kuliwania jimbo hilo ambalo uchaguzi wake umepangwa kufanyika April 1, 2012.


Source: Taarifa ya habari Mlimani TV.

Nawasilisha.
 
Lakini Nape amesahau kuwa hawa wasindikizaji ni balaa! walihamishia serikali yote igunga!
 
Back
Top Bottom