Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,603
- 29,748
Mungu nakuomba uniongoze niandike kinachoeleweka
Tanzania sasa inapitia wakati mzito na mgumu sana kama Taifa. Wananchi wamepoteza matumaini lakini kinachowazuia kufanya maamuzi ni hofu ya kuuawa kinyama na vyombo vya dola ambavyo vimeshikamana na mirija inayoitafuna nchi yetu.
Hali ya tabianchi imekuwa negative sana kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, lakini pamoja na utajiri wa mito na maziwa hatujaweza kuwekeza kwenye kilimo chenye tija. Watanzania walio wengi vijijini wanalima vibustani vya mazao ya vyakula na biashara lakini kilimo hiko hakijakidhi mahitaji ya nchi kuikabili njaa iliyobisha hodi maeneo mengi nchini.
Viongozi wetu ambao wanatumia mbinu zote chafu kujihakikishia wanabaki madarakani wamekuwa ndiyo majinamizi yanayohakikisha hatusongi mbele kwa sababu wanatumia madaraka yao kujinufaisha na mkwamo wa kiuchumi wa nchi yetu. tukianzia bandarini, unaweza kuziona zile CILOS ambazo hapo awali tulikuwa tunaaminishwa kuwa ni hifadhi za nafaka zinazotoka Tanzania kwenda ng'ambo lakini yale maghala kiuhalisia nni kwa matumizi ya goods arrivals za nafaka kutoka nje ya nchi. Mnajua ni kiasi gani cha dola za Kimarekani zinatumika kuagiza chakula kutoka nje? imefikia mahala tunaimport mpaka mchele.
Viongozi wa serikali yetu tukufu wamehakikisha sheria kali zinazodhibiti uwezekano wa mapinduzi ya kilimo zinapitishwa na Bunge ambalo kimsingi halijawahi kutunga sheria bali kuzipitisha tu na watunzi wa sheria ndo wanaenda kuzipitisha. Unapoweka bodi za mazao ambazo hadidu zake kubwa ni kupanga bei za mazao na kudhibiti masoko ni juhudi tukuka za serikali kuwahujumu wananchi wake ambao ndiyo wamiliki halali wa serikali hiyo. Taifa limefanya makosa mengi sana ambayo suluhu yake ni kuwaomba radhi wananchi ama CCM ikubali uwepo wa mazingira chanya ya chaguzi kuu ili kuleta ushindani wenye tija kwenye maongozi ya nchi yetu.
Leo bidhaa ya unga wa mahindi imeshuka bei nchini Kenya ambapo mahindi yake yanatoka Tanzania kwa sehemu kubwa. Ni rahidi kwa mfanyabiashara kufuata unga kutoka Kenya na kuja kuuza hapa nchini kwa bei ya chini. Viongozi wetu wanajua hilo na wanahakikisha wananchi wasijue lolote.
Hivi kuna kiongozi gani wa nchi tukianza na mawaziri hasa Waziri wa elimu au Tamisemi ambaye wanae wanasoma shule za msingi za umma? kama wao wanatunga sera za elimu na wanazisimamia huku wakikwepa zisitumike kwa watoto wao, je ni haramu gani wanayowapelekea wananchi? Hatuwezi kuendelea kama Taifa kwa aina hii ya viongozi ambao wao wanaamini na kuishi kwenye MATAMKO na FIGISUFIGISU.
Niwajulishe tu Watanzania wenzangu kwamba, siasa ina sehemu kubwa kwenye maongozi ya nchi hii lakini tunaweza kuiendeleza nchi yetu nje ya hizi siasa za kimizimu ambazo tunalazimimshwa kuishi nazo na CCM. Endapo Chama Cha Mapinduzi kinaendeleza madudu yake ya miaka mingi ya kujimilikisha utashi na akili za Watanzania kimabavu, basi kijiandae kuwa historia kadiri tunavyosogelea sanduku la kura.
Wananchi wanalalamikia tozo na mazingira adui ya kipato nchini, lakini anatoka Waziri anang'aka NENDENI BURUNDI.... kauli hii na Mfalme wa Ufaransa alipowajibu watu wenye njaa kuwa wale mikate... ni kauli ya kishetani iliyojaa shibe ya jasho la Watanzania kupitia tozo mbalimbali.
CCM mnapaswa kulileleza Taifa ukweli kwamba tupo kwenye mkwamo kama nchi. tumekwama kwa sababu sera na ilani zenu havitekelezeki. mzunguko wa fedha umekuwa mgumu kwa wananchi wengi. nchi inategemea wachuuzi wanaoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi ili kutunisha mapato ya taifa. Serikali inawaibia wananchi wake vipato vyao viduchu tena inajilinda kwa kutunga sheria kulinda ujambazi huo. Hakuna mahala ambapo wananchi wamekataa kulipa kodi, lakini aina ya kodi mnazozitaka kutoka kwa wananchi maskini ni sawa na kuwasainisha hati zao za vifo kwa kukosa madawa, huduma na pensheni zao huku mkiwazuia kufanya biashara kwenye mazingira rafiki.
Tanzania sasa ipo kwenye autopilot mode, nchi ina viongozi lakini haina maongozi. tumewajaza wananchi uongo kwamba uchumi upo stable lakini uhalisia nin kwamba tumeshauzwa kama alivyosema Job Ndugai (ingawa naye ni mule mule walioshiriki madhila yetu)
Itaendelea.....