CCM mnawakomoa wananchi, sio UKAWA!

CCM mnawakomoa wananchi, sio UKAWA!

Tpaul kubishana na kizibo kama hiki ni kujivunjia heshima! Lina macho lakini halioni! zezeta kabisa hili

mkuu MTENGETI kuna baadhi ya watu humu utadhani vichwani mwao kumejaa gongo badala ya ubongo. anyway, tutazidi kuwaelimisha ipo siku wataelewa na kuuishi ukweli ghairi ya propaganda wanazolishwa na CCM.
 
Last edited by a moderator:
.....nchi imegawanyika,sio majimbo tu hata sehemu wanakoona sera za ccm hazipandi basi hakuna mradi wala nini,cha kushangaza fedha zote zinaishia halmashauri,mfano fedha za ukimwi huku rorya hatupati.
 
mkuu, tutajie basi matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo

kwanza niambie pesa za mfuko wa jimbo ni sh ngapi na zinaweza kufanya miradi mingapi kwenye jimbo. Pia naomba unitajie kazi za fedha za bajeti ya serikali zinazotengwa kila mwaka.
 
mwambieni mnyika tunataka maji ubungo alisema ndani ya mwezi mmoja akichaguliwa ataleta maji ubungo yako wapi sasa hayo maji aliyosema mnyika.

hivi kikwete alishatekeleza ahadi zake zote alizoahidi mwaka 2005 na 2010? kama serikali inalitenga jimbo la ubungo ikidhani litarejea CCM mwaka huu, endelea kusubiri~~utasubiri mpaka Yesu arudi na jimbo hamjalipata. mbinu zenu ni za kitoto sana na zinalenga kuwaumiza walipakodi.
 
mwambieni mnyika tunataka maji ubungo alisema ndani ya mwezi mmoja akichaguliwa ataleta maji ubungo yako wapi sasa hayo maji aliyosema mnyika.

Watanzania mmezoa shida ................................ CCM wanajlijua hilo!!
 
Fedha za mfuko wa jimbo ndizo zinajenga barabara, miundombinu ya maji, kujenga maabara na kila kitu? kama kazi yake ni hiyo, sasa kuna haja gani ya wananchi kuchangishwa fedha za maabara? ama kweli humu jf kuna mimburura mingi sana. wakuu BAK lusungo Mamndenyi, Elli, et al hebu piteni huku mnisaidie kutoa elimu ya uraia. kuna watu huku hawajui jinsi serikali inavyopata mapato yake na matumizi yake.

Wengine wanajitoa ufahamu tu sio kwamba ni kweli hawayajui haya mambo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, kuna fedha za mfuko wa jimbo ambazo zinasimamiwa na mbunge. Je wanazitumiaje?

Siko hapa kuwatetea wabunge wa upinzani niko hapa kutetea kila mtu/idara/mamlaka kuwajibika kwa eneo lake na kwa haki. Mmbuge awe wa ccm/upinzani atapaswa kutoa taarifa za miradi ya maendeleo ya jimbo lake na ni kiasi gani kapata na katumiaje kiasi alichopata kwa ajili ya maendeleo ya eneo lake. Na kama anakwamishwa na serekali ya ccm kwa makusudi atoe ufafanuzi sisi wananchi tutachukua hatua.
 
mwambieni mnyika tunataka maji ubungo alisema ndani ya mwezi mmoja akichaguliwa ataleta maji ubungo yako wapi sasa hayo maji aliyosema mnyika.

Nyumba yenyewe uliyopanga haina bomba maji yatatokaje sasa?
 
Nawashauri wabunge wote wanaonyimwa miradi ya maendeleo kwa hila wawaeleze wananchi wao kinagaubaga na ikibidi wawatake wasilipe kodi, full stop. Kodi wanalipa wananchi wote na sio wanachama wa ccm tu.Tena ni lazima watoe hela ya maendeleo na wala sio ombi vinginevyo hakuna kulipa kodi.

Hilo hakuna hadi uwe na ushahidi kamili, si porojo tu. Sasa hivi wananchi wa vijijini wanafurahia umeme unaosambazwa, hatujasikia kuna jimbo la mbunge yeyote aliyenyimwa huo umeme.
 
Siko hapa kuwatetea wabunge wa upinzani niko hapa kutetea kila mtu/idara/mamlaka kuwajibika kwa eneo lake na kwa haki. Mmbuge awe wa ccm/upinzani atapaswa kutoa taarifa za miradi ya maendeleo ya jimbo lake na ni kiasi gani kapata na katumiaje kiasi alichopata kwa ajili ya maendeleo ya eneo lake. Na kama anakwamishwa na serekali ya ccm kwa makusudi atoe ufafanuzi sisi wananchi tutachukua hatua.

mkuu tindo hujuma za CCM dhidi ya majimbo yanayoongozwa na wabunge wa UKAWA ziko wazi. kuna waziri mmoja alitishia kuwanyima wananchi maendeleo ikiwa watawachagua wenyeviti wa serikali za mtaa kwa tiketi ya UKAWA lakini wananchi wakampuuza na kuwachagua wanaUKAWA kwa kishindo. chezea wananchi wewe!
 
Last edited by a moderator:
Hilo hakuna hadi uwe na ushahidi kamili, si porojo tu. Sasa hivi wananchi wa vijijini wanafurahia umeme unaosambazwa, hatujasikia kuna jimbo la mbunge yeyote aliyenyimwa huo umeme.

utajuaje wakati umejitoa akili na kumkabidhi bosi wako Nape Nnauye? hili suala liko wazi na wala halihitaji utafiti. ni watu wanaojitoa akili kama wewe ndio wanaoweza kubisha tu.
 
Last edited by a moderator:
Fedha za mfuko wa jimbo ndizo zinajenga barabara, miundombinu ya maji, kujenga maabara na kila kitu? kama kazi yake ni hiyo, sasa kuna haja gani ya wananchi kuchangishwa fedha za maabara? ama kweli humu jf kuna mimburura mingi sana. wakuu BAK lusungo Mamndenyi, Elli, et al hebu piteni huku mnisaidie kutoa elimu ya uraia. kuna watu huku hawajui jinsi serikali inavyopata mapato yake na matumizi yake.

Usishangae hao tu mkuu maana yawezekana hawafahamu hata nini wanachangia.....

Nchi vituko ni vingi kuanzia kwa watu Wa chini mpaka juu nimemsikia yule bolizozo Mwigullu akisema anashangaa kwanini serikali inatenga PESA nyingi kwaajili ya maadhimisho kuliko mambo ya msingi wakati hazina inayotoa fedha IPO chini yake......

kuna tatizo kubwa Sana juu ya uwezo Wa hawa watu kiakili ndio maana serikali imedorora na maendeleo yamedorora.....
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, kuna fedha za mfuko wa jimbo ambazo zinasimamiwa na mbunge. Je wanazitumiaje?
Mkuu, tutajie basi matumizi ya fedha za mfuko wa Jimbo
Wewe usijitoe ufahamu, pesa za mfuko wa Jimbo ni kidogo sana. Mfano ni huu hapa toka kwa Bwana wako Zitto:

photo.jpg

Soma hapo pekundu. Pesa hizo ziliwe na mafisadi halafu msingizie pesa za mfuko wa maendeleo wa Jimbo?

Ama kweli.
16 Julai, 2014 Na Abdallah Khamis

MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amemnusuru Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala asiendelee kuzomewa na wananchi wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miundombinu ya maji jimboni humo.

Mapema wanachama wa CCM wakiwa na bendera zao, walionekana kupangwa ili kumzomea Mnyika ambaye hata hivyo hakuwajali, badala yake aliendelea kuhutubia mkutano huku Makala akionekana kufurahishwa na hali hiyo.

Mnyika alieleza jinsi alivyowapigania wakazi wa Kimara Mavurunza na maeneo mbalimbali ya jiji kupata maji pasipo kujali itikadi zao za vyama.
Alisema ziara hiyo ya naibu waziri ni matokeo yake ya kumbana Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, pamoja na watendaji wa Kampuni ya kusambaza maji ya Dawasa kuhakikisha maji yanapatikana kwa wakazi wa Dar es Salaam.

Alisema kama si kushindwa kwa Serikali ya CCM kuzuia wizi wa maji unaofanywa na watu wanaoyauza, hususan viongozi wa serikali, tatizo hilo lisingekuwa kwa kiasi kinachotisha kama ilivyo sasa.

Alimtaka Naibu Waziri Makala ahakikishe wakazi wa Ubungo na maeneo mengine ya jiji wanapata maji kwa kuwa ni haki yao ya msingi, na kwamba wawabane watu wanaouza maji.
Baada ya Mnyika kumaliza, Makala alisimama na kabla hajaanza kuzungumza wananchi walimueleza kuwa hawataki porojo zaidi ya maji.

"Kiongozi hapa tunataka maji, hizo porojo zako za kisiasa peleka huko huko kwa kuwa tumechoka na ahadi zisizotekelezeka kwa muda wa miaka hamsini," alisema mwananchi ambaye hakufahamika jina.

Makala badala ya kutulia, alimueleza mwananchi huyo kuwa kama hataki porojo aondoke katika mkutano hali iliyozua zomea zomea kutoka kwa wananchi.
Akiwa amekasirika, Makala aliwatishia wananchi kuwa atawakamata kwa kuwaita polisi, lakini kitisho hicho hakikufua dafu.

Katika jitihada zake za kuendelea kuwatisha wananchi, Makala aliinuka mithili ya kutaka kuwafuata, lakini Mnyika alimzuia na kumueleza hali hiyo isingekuwepo kama CCM wasingeingiza siasa katika masuala ya kiserikali.

Mnyika aliwasihi wananchi wampe nafasi kiongozi huyo aweze kuwaeleza mipango ya serikali. Baada ya ombi hilo, wananchi walitulia na Makala akaeleza kuwa
serikali imeshatenga sh. bilioni 362 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Ruvu Juu na Chini na kwamba miradi hiyo itakamilika ifikapo Septemba mwakani.

attachment.php

Attachments

  • The Water Sector.jpg
    The Water Sector.jpg
    203.3 KB · Views: 3,082
Hilo hakuna hadi uwe na ushahidi kamili, si porojo tu. Sasa hivi wananchi wa vijijini wanafurahia umeme unaosambazwa, hatujasikia kuna jimbo la mbunge yeyote aliyenyimwa huo umeme.

We kigagula unazani kila mtu mjinga mimi naishi ubungo yanayosemwa nayaona na kuyashuhudia
 
attachment.php

Mnyika fuatiliea tu, pesa zipo. CCM mkifanya mchezo, hii itakuwa ni MCC scam kama EPA na Escrow.
 
We kigagula unazani kila mtu mjinga mimi naishi ubungo yanayosemwa nayaona na kuyashuhudia

Ukiwa unaishi Ubungo ndiyo nini? Jionee:
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mkasi Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Mhe John Mnyika ili na yeye akate utepe na viongozi wengine kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila mkoa wa Pwani leo April 24, 2014.
 
utajuaje wakati umejitoa akili na kumkabidhi bosi wako Nape Nnauye? hili suala liko wazi na wala halihitaji utafiti. ni watu wanaojitoa akili kama wewe ndio wanaoweza kubisha tu.

"nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

h4.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe L:eonidas Gama na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo.
 
Hilo hakuna hadi uwe na ushahidi kamili, si porojo tu. Sasa hivi wananchi wa vijijini wanafurahia umeme unaosambazwa, hatujasikia kuna jimbo la mbunge yeyote aliyenyimwa huo umeme.

Labda uniambie kama ni porojo, maana tunalipa kodi tena kwa uzalendo hatutaki kusikia upuuzi wa maamuzi ya kichama kwenye kodi zetu. Anayetaka kuweka maamuzi ya kichama mbele kwenye kodi zetu hatutaelewana kabisa. Halafu dada FF hebu waambie chama chako waache mambo yaliyopitwa na wakati kila maendleleo wanapeleka Dar. Hivi hamuoni aibu jiji limejaa msongamano wa watu tena wengi hawana ajira za kueleweka mpaka mmezalisha panya road!? Wanashindwa nini kujenga bandari ya Mtwara na kuanzisha viwanda pamoja na kujenga reli. Pia Tanga kuna bandari na reli ya kufufua tu na viwanda lukuki vilivyouliwa na wasomi wetu uchwara. Halafu kuna mtu ambaye nikimtaja hapa unapata hisia zile za imani zetu anataka kujenga bandari hapo bagamoyo pua na mdomo na Dar, wakati Tanga na Mtwara zingetosha kuondoa huo msongamano hapo Dar kwenye chemba cha maji machafu. Ama dada wewe huwa husikii hizo harufu za choo hapo mjini. Na kama unasikia huoni aibu?
 
Usishangae hao tu mkuu maana yawezekana hawafahamu hata nini wanachangia.....

Nchi vituko ni vingi kuanzia kwa watu Wa chini mpaka juu nimemsikia yule bolizozo Mwigullu akisema anashangaa kwanini serikali inatenga PESA nyingi kwaajili ya maadhimisho kuliko mambo ya msingi wakati hazina inayotoa fedha IPO chini yake......

kuna tatizo kubwa Sana juu ya uwezo Wa hawa watu kiakili ndio maana serikali imedorora na maendeleo yamedorora.....

umeona eeh? hii nchi ni ya ajabu sana huwezi kuamini i see! nchi imelaaniwa na aliyeilaani kafa.
 
Back
Top Bottom