PostGE2025 CCM wamemwachia Samia jumba bovu limwangukie?

PostGE2025 CCM wamemwachia Samia jumba bovu limwangukie?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,173
Reaction score
60,538
Baada ya ushindi wa kishindo tofauti na chaguzi zilizopita, siwaoni wana CCM wakisherehekea ushindi wala simuoni Mkiti wao akizunguka mikoani kuwashukuru wana CCM na wapigakura.

Ni yeye tu na msemaji wa serikali ndio wanasikika sioni wengine wakihangaika kumtetea.

Simuoni Makamu Mwenyekiti akimpongeza wala akimusaidia Mkiti wake kujibu au kutoa pole kwa wahanga.

Sijawasikia wastaafu, Kinana, Majaliwa, Makamba hata swahiba wake Kikwete.

Sijamsikia Katibu Mkuu akizungumza chochote kuhusu ushindi au kilichotokea baada ya uchanguzi.

Siwaoni wabunge kwenye majimbo yao wakiwashukuru wapiga kura wao kwa kuwapa ushindi wa kishindo.

Huku mitaani siwaoni wana CCM kindakindaki wakitamba ma pikipiki na baiskeli zilizomwagwa kabla ya uchaguzi sizioni labda huko kwenu.

Si Wenyeviti wa matawi, si Wenyeviti wa Wilaya wa CCM wala Wenyeviti wa Mikoa walioandaa mikutano ya kumpongeza Mwenyekiti wao.

Je, kawazuia, wanamuogopa, wanawaogopa wananchi au wamemsusia wasionekane na wao wamehusika na mauaji ya ndugu zao Watanganyika.
 
Tenga la samaki limeshakubali hakuna kiteweo maana waliacha samaki mmoja kuoza walijua ni salama Sasa inabidi watupe Tenga
 
Mwenyekiti wangu wa kitongoji Kahama mtaa wa Muhungula vijana walimfanyia mbaya 29 mpaka sasa akili hazijamkaa sawa familia yote imekimbia yeye wamevunja miguu yote na nyumba ikachomwa.

unafikiri nani wa kujitokeza tena ashangilie
 
Mwenyekiti wangu wa kitongoji Kahama mtaa wa Muhungula vijana walimfanyia mbaya 29 mpaka sasa akili hazijamkaa sawa familia yote imekimbia yeye wamevunja miguu yote na nyumba ikachomwa.

unafikiri nani wa kujitokeza tena ashangilie
Mtaani kwetu tangu siku ya kupiga kura hajaonekana.
 
Back
Top Bottom