CCM mnataka mkisema wengine wasiseme, Haiwezekani!

CCM mnataka mkisema wengine wasiseme, Haiwezekani!

Wakati hao wachafuzi wanamchafua Lowasa,ccm walikuwa wanamsafisha na wakwanza ni mwenyekiti wa ccm Jk,2010 alimpigia kampeni monduli na kumsifia kuwa ni jembe na hakuhusika na ufisadi wowote,ni upepo wa kisiasa tu.
sasa leo chadema wamekubali kuwa siyo fisadi baada ya yeye mwenyewe {Lowasa} kueleza kuwa muhusika ni Bosi wake{JK} upande wa pili {ccm}nao wamebadilika kuwa eti fisadi,loh.
Sitaki kusikia habari za CCM maana tulishawachoka ....nazungumzia chama chetu....je kilikuwa kinapiga kelele juu ya EL miaka tisa bila ushahidi? Kama wameweza kufanya hivyo kwa miaka tisa kupiga kelele na kumchafua mtu bila uhakika kwanini tuwaamini mengine?
 
Mkuu nakuonea huruma hawa unaojadiliana nao hapa,wataishia kukutukana tu.Siasa imewafanya watu wamekuwa vipofu,ukiangalia trend huyo bwana kila siku lazima afungue mada kumponda Magufuli cha kusikitisha now imefikia steji kuna watu wanadiriki kumsifia JK na kumponda JPM
 
Mnataka kurudisha zama za Chama kushika Hatamu ambapo wakubwa wakisema watu wengine wote mnatakiwa mfunge vinywa vyenu. Kila siku Hapa JF lazima muanzishe thread dhidi ya Lowassa, lakini mtu akiuliza swali tu kuhusu Magufuli inakuwa Nongwa. Lowassa siyo Kiongozi wa serikali iliyoko Madarakani, lakini Magufuli ni Rais wa nchi. Kumzungumzia Magufuli kwa sasa ni muhimu zaidi kuliko Lowassa, na sisi kama raia tuna haki hiyo.

Bomoa bomoa ya kikandamizaji imefanyika Dar Mbunge wa Kinondoni kaenda Mahakamani, mnahoji kwa nini anapingana na serikali. Mnataka kutujengea picha kwamba serikali inajua kila kitu na iko sahihi wakati wote. Sisi ndiyo wenye serikali bila ya kujali kama tulimchagua Magufuli au la.

Wale mnaodhani kwamba ambao hawakumuunga mkono Magufuli hawana haki ya kumkosoa, jiulizeni hao ambao hawakumchagua huwa hawatozwi kodi? Kama wanatozwa kodi mnawaondowaje kwenye haki ya kuwakosoa wale wanaokusanya kodi toka kwao. Kama vipi Kodi isikusanywe toka kwa wapinzani. Kama wewe ni UKAWA basi usilipe kodi kwa kuwa hukumchagua Magufuli. Hiyo imekaaje ndugu zangu wa CCM?
Mkuu nilikushauri uache kuvuta Bangi haukusikia. Naona madhara yake yamekuwa dhahiri sasa.
 
Sitaki kusikia habari za CCM maana tulishawachoka ....nazungumzia chama chetu....je kilikuwa kinapiga kelele juu ya EL miaka tisa bila ushahidi? Kama wameweza kufanya hivyo kwa miaka tisa kupiga kelele na kumchafua mtu bila uhakika kwanini tuwaamini mengine?
Hoja hapa ule uliokuwa unaitwa ufisadi wa Lowassa na CHADEMA kwa hiyo inayoitwa miaka 9 ilihusu kwa nini hafikishwi mahakamani? Na wala hakuna mahali CHADEMA wao walisema kuwa ushahidi wao unatokana na wao wenyewe bali unatokana na taarifa za serikali. Kwa mfano suala la Richmond CHADEMA kwa muda mrefu wamekuwa wakisema kuwa Mwakyembe aseme hicho alichosema kwamba "walikificha" ili serikali isianguke. Lakini wakati anasema hayo tayari mapendekezo ya kumtaka Waziri Mkuu "ajipime mwenyewe" yalikuwa yameshatolewa. Kwa maana nyingine hoja ya kina Mwakyembe kwamba waliyoyaficha waliyaficha kwa kuhofia Serikali kuanguka hayakumhusu Lowassa bali aliyekuwa juu Lowassa ambaye ni Kikwete!

Makosa kutokea haiwezekani ikawa ni adhabu kwa taasisi nzima. CCM walikuwa wanaimba "CCM ni ile ile" Lakini leo tunaambiwa kwamba "CCM ya Magufuli na ya Kikwete ni tofauti". Maana yake wanajaribu kuyatenganisha mambo ya ovyo yaliyotokea wakati wa Kikwete na yale anayoyafanya Mafuguli hivi sasa. CHADEMA ilisema kwa mujibu wa taarifa ya Mwakyembe Lowassa ni fisadi kwa nini hafikishwi Mahakamani? CCM wakasema Lowassa ni Gamba dawa yake kumtoa kwenye chama chao, lakini kama kuna hasara Lowassa kalisababishia Taifa inatosha tu kumtoa kwenye chama? Hapo ndipo CHADEMA ilikuwa imesimamia!
 
Mkuu nilikushauri uache kuvuta Bangi haukusikia. Naona madhara yake yamekuwa dhahiri sasa.
Wakati tunabeba mizigo ya waarabu bangi ilikuwa inatupa burudisho na uwezo wa kutoka bara mpaka pwani bila ya kuchoka. Au unadhani kwamba Wakwere ile methali yao ya "Mzigo mzito mpe Mnyamwezi" waliitunga tu bila ya kuwa na ulinganisho na hali halisi?
 
Hii

Mada ni kituko Mkuu
Majaliwa keshawaambia mambo ya Siasa iwe mwisho fanyeni kazi
itakapofika 2020 mtaaarifiwa kipindi cha Kampeni ni lini kianze

Mnashindwa kuelewa Majukumu ya Diwani na Mtendaji wake wa Kata
Leo Meya naye anakuwa Mtendaji je huyo Mkurugenzi atafanya kazi gani basi
Iringa Manispaa inaweza kuwa zaidi ya Arusha ya Godbless Lema kwani km na DC yumo basi RC atawabeba mpaka na ma RPC,RCO nk
 
Hii

Majaliwa keshawaambia mambo ya Siasa iwe mwisho fanyeni kazi
Kama yeye hafanyi siasa anafanya nini sasa? Kwani Waziri Mkuu siyo cheo cha kisiasa? Sifa za kuwa Waziri Mkuu ni lazima uwe ni mbunge wa kuchaguliwa kwenye jimbo, na ili uwe na sifa za kugombea ubunge ni lazima upitishwe na chama cha siasa, sasa majaaliwa wa CCM anatumia kivuli cha "Serikali" kuzuia wanasiasa wa vyama vingine vya siasa kufanya siasa eti kwa kuwa uchaguzi umepita, nani kamwambia vya vya siasa hufanya kazi wakati wa uchaguzi pekee? Wao wanazunguka nchi nzima wanajitapa wanatekeleza Ilani ya chama chao, wenzao kushukuru kwa wapiga kura inakuwa Nongwa. Asiyependa kushukuru, ana roho ya shetani!!
 
Hapa Iringa kuna mvutano mkubwa sana kati ya Meya wa Manispaa ya Iringa anayetokana na a CHADEMA. Mkuu wa Mkoa anadai inayotekelezwa ni Ilani ya CCM na Meya ni alama tu ila mwenye serikali ni yeye na DC!! Meya anapanga vitu vya mabasi ya daladala yeye anatumia askari kuzuia vituo hivyo kutumika.
Hawajui kuwa wote ni watanzania
 
1) Nini kinakufanya uamini hayo yanafanywa na wanaccm?
2) Kwanini unafikiri wananchi waliojitoa kuunga mkono mabadiliko ya kweli miaka mingi hawana haki kuhoji kwanini viongozi wao waliongoza mapambano ya kumchafua EL miaka zaidi ya tisa bila ushahidi kama leo wao wanasema aliye na ushahidi apeleke Mahakamani?
3) Haki ya kumkosoa Magufuli anayo kila mtu lakini hapa ukimkosoa Lowasa unashukiwa the same to JPM ...hizi ndio siasa za humu sijui unalalamika nini ....
umefikia umri wa kukeketwa
 
Mnataka kurudisha zama za Chama kushika Hatamu ambapo wakubwa wakisema watu wengine wote mnatakiwa mfunge vinywa vyenu. Kila siku Hapa JF lazima muanzishe thread dhidi ya Lowassa, lakini mtu akiuliza swali tu kuhusu Magufuli inakuwa Nongwa. Lowassa siyo Kiongozi wa serikali iliyoko Madarakani, lakini Magufuli ni Rais wa nchi. Kumzungumzia Magufuli kwa sasa ni muhimu zaidi kuliko Lowassa, na sisi kama raia tuna haki hiyo.

Bomoa bomoa ya kikandamizaji imefanyika Dar Mbunge wa Kinondoni kaenda Mahakamani, mnahoji kwa nini anapingana na serikali. Mnataka kutujengea picha kwamba serikali inajua kila kitu na iko sahihi wakati wote. Sisi ndiyo wenye serikali bila ya kujali kama tulimchagua Magufuli au la.

Wale mnaodhani kwamba ambao hawakumuunga mkono Magufuli hawana haki ya kumkosoa, jiulizeni hao ambao hawakumchagua huwa hawatozwi kodi? Kama wanatozwa kodi mnawaondowaje kwenye haki ya kuwakosoa wale wanaokusanya kodi toka kwao. Kama vipi Kodi isikusanywe toka kwa wapinzani. Kama wewe ni UKAWA basi usilipe kodi kwa kuwa hukumchagua Magufuli. Hiyo imekaaje ndugu zangu wa CCM?

CCM WANAISHI KWA KUJIHAMI MAANA WANAJUA WAZI KWAMBA HAWAKUPATA RIDHAHA YA WANANCHI WAMELAZIMISHA KWA MABAVU KAMA ALIVYOWAHI KUSEMA KIKWETE WANAZO MBINU NYINGI ZA KURUDI IKULU PIA ALITANGAZA WAZIWAZI KAMA AMIRI JESHI MKUU NA RAIS WA NCHI KWAMBA MAGUFULI WEWE NDIYE RAIS WA AWAMU YA TANO SIKU 3 KABLA YA UCHAGUZI. UKIDHULUMU HUWEZI KUACHA KUJITILIA MASHAKA
 
Sitaki kusikia habari za CCM maana tulishawachoka ....nazungumzia chama chetu....je kilikuwa kinapiga kelele juu ya EL miaka tisa bila ushahidi? Kama wameweza kufanya hivyo kwa miaka tisa kupiga kelele na kumchafua mtu bila uhakika kwanini tuwaamini mengine?
Chama chenu kipi?
Angalia humo nilimoweka nyekundu kunathibitisha unafiki wako na maccm wenzio,.
 
Back
Top Bottom