Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,387
- 38,662
Mnataka kurudisha zama za Chama kushika Hatamu ambapo wakubwa wakisema watu wengine wote mnatakiwa mfunge vinywa vyenu. Kila siku Hapa JF lazima muanzishe thread dhidi ya Lowassa, lakini mtu akiuliza swali tu kuhusu Magufuli inakuwa Nongwa. Lowassa siyo Kiongozi wa serikali iliyoko Madarakani, lakini Magufuli ni Rais wa nchi. Kumzungumzia Magufuli kwa sasa ni muhimu zaidi kuliko Lowassa, na sisi kama raia tuna haki hiyo.
Bomoa bomoa ya kikandamizaji imefanyika Dar Mbunge wa Kinondoni kaenda Mahakamani, mnahoji kwa nini anapingana na serikali. Mnataka kutujengea picha kwamba serikali inajua kila kitu na iko sahihi wakati wote. Sisi ndiyo wenye serikali bila ya kujali kama tulimchagua Magufuli au la.
Wale mnaodhani kwamba ambao hawakumuunga mkono Magufuli hawana haki ya kumkosoa, jiulizeni hao ambao hawakumchagua huwa hawatozwi kodi? Kama wanatozwa kodi mnawaondowaje kwenye haki ya kuwakosoa wale wanaokusanya kodi toka kwao. Kama vipi Kodi isikusanywe toka kwa wapinzani. Kama wewe ni UKAWA basi usilipe kodi kwa kuwa hukumchagua Magufuli. Hiyo imekaaje ndugu zangu wa CCM?