CCM mkwepa kodi mkubwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM mkwepa kodi mkubwa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Jul 5, 2011.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Chama cha Mapinduzi aka chama cha magamba kimekwepa kulipa mabilioni ya kodi (withholding tax) tangu ilipovitwa viwanja vya michezo nchi zaidi ya miaka arobaini iliyopita.Chama cha Mapinduzi baada ya kujimilikisha mali mbali eg Viwanja vya michezo CCM Kirumba - Mwanza,Sheikh Amri Abeid - Arusha,Sokoine Mbeya na vinginevyo vingi vimekuwa vikikwepa kulipa kodi withholding tax.

  Inashangaza sana Bwana Mdogo Nape anaposhupalia suala la Dr Slaa kulipa kodi toka kwenye posho anazolipwa na CHADEMA huku chama chake kikikwepa kulipa kodi kwa zaidi ya miaka arobaini.Wakuu wa TRA wamekuwa waoga kudai kodi iliyoweka na kupitishwa kwa sheria ya bunge.Ikumbukwe uhalali wa umiliki wa viwanja hivyo umekuwa ukipigikwa kelele muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi.Viwanja vyote vilijengwa na wananchi kipindi cha mfumo wa chama kimoja.

  Withholding tax ni asilimia 3 ya kodi wanazolipa wapangaji wote.kodi ya chumba ni tsh 200,000/= kwa mwezi.Ebu fikiria muda na wingi wa vyumba vya biashara vilivyotapakaa Tanzania nzima TRA wangepata shilingi ngapi ?.Ukipiga hesabu za haraka haraka pengine CCM wanaweza kushika namaba mbili aua tatu nyuma ya migodi ya dhahabu na makampuni yanayobadili majina kila kukicha ili kukwepa kulipa kodi.
   
 2. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nyani haoni kundule..... wameyachokonoa sio hayo tu, tunakusanya data wewe subiri watakimbia wenyewe humu.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280

  Nashangaa Kitlya anafanya nini ?.
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Wao wanadhani sheria inang'ata upande mmoja tuu haya ngoja waje wenye data waanike hapa
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Bila shaka watakujibu kwamba nao ni wawekezaji wa ndani, wanahitaji tax holiday ili kuongeza kiwango cha uwekezaji.

  Viwanja tumejenga wote lakini CCM wamevipora na kujibinafsishia, ila siku tukiikamata hii nchi basi wajue viwanja vimerudi kwa wenyewe wananchi.
   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Duh Tax holiday ya miaka arubaini CCM ni wezi na wakwepaji wakubwa wa kodi
   
 7. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Tax holiday ya CCM ktk umiliki wa viwanja na majengo ilishapita miaka mingi, therefore i hope this time around watawajibika kulipa billions za kodi.
   
 8. e

  ebrah JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani kuna wenye ushahidi na hili jambo tulipandishe juu? hawa watu wamezidi kunyonya vya uma! na pia nashauri mikataba ya umiliki wa hivyo viwanja na pia majengo yote ya MAGAMBA ipitiwe upyaaaa!
   
 9. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Ohoo, wameshamkanyaga nyoka mkia, kazi kwao magamba, TRA wachukuwe kodi yetu, then uje mjadala wa kuvichukua viwanja na mali zote walizojilimbikizia enzi ya chama kimoja.Ukila na kipofu usimshike mkono sasa Nape kasha likoroga hilo.
   
 10. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Yaani wao wana viwanja vingi kuliko serikali!
   
 11. MANI

  MANI Platinum Member

  #11
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,413
  Likes Received: 1,872
  Trophy Points: 280
  Ebra unataka ushahidi wa aina gani? Kumbuka kipindi cha kampeni 2010 CDM walivyokuwa wanapata taabu ya nafasi ya kuhutubia wananchi kisa viwanja ni mali ya chama tawala. Any how nafikiri ni wajibu wetu kufuatilia kama hizo kodi husika zinalipwa maana sheria haina ubaguzi ni matarajio yetu tutajua ukweli hivi karibuni !
   
 12. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  wamewekwza au wamejimilikisha maeneo hili ni swala muhimu sana mkuu tena linapashwa kuvaliwa njuga na kama ni slaa basi ni la tija..
   
 13. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Withholding tax ya 3% iko kwenye sheria gani ya mapato? Sheria ya mapato ya mwaka 2004 inasema 10%. Pili nani anayetakiwa kukata na kuwasilisha hii kodi; kwa mujibu wa sheria ya mapato mpangaji ndiye anayetakiwa kuzuia 10% na kuwasilisha TRA.


  BTW ukichukulia wingi a properties walizonazo kodi wanayokusanywa inazidi TShs. 40 million hivyo kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wanatakiwa wajiandikishe na kulipa 18% ya mapato yao kama VAT
   
Loading...