CCM mchezo mnaoufanya ni hatari

CCM mchezo mnaoufanya ni hatari

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,946
Reaction score
38,657
  1. Kila mtu anafahamu wazi kwamba mchezo mnaoufanya mlishaupanga kitambo na sasa mmeanza kuutekeleza kwa awamu Kutumia dola ISIYOJITAMBUA kubambikiza kesi kwa viongozi wa upinzani hasa CHADEMA.
  2. Mnajua wazi kwamba hampo tena kwenye mioyo ya Watanzania na hivyo mmeamua kutumia nguvu kujithibitishia kuitawala nchi hata kama mkishindwa kupitia sanduku la kura kama ilivyowatukia 2010.
  3. Mmeshiindwa kudhibiti mfumuko wa bei kiasi kwamba mlipoamua kupandisha nauli za vyombo vya usafiri mkatafuta kigezo kwa kupandisha bei ya mafuta usiku usiku ili iendane na ongezeko la nauli, na inajulikana wazi kwamba mnawategemea wafanyabiashara wawabebe kugharimia 2015 baada ya mipango yenu ya kuiba kuanza kugundulika mianya kuzibwa kila kona.
  4. Mnaelewa fika kwamba upinzani una nafasi kubwa ya kuchukua hatamu za uongozi kuanzia 2015 na sasa mmeamua kutumia kampeni za udini kwa vitendo kuwagawanya Watanzania ili nchi isitawalike na muweze kuendelea kuwepo madarakani kwa kigezo cha vurugu za kidini.
  5. Viongozi wenu wa juu wameridhia uteswaji, udhalilishwaji na hata kunyofolewa uhai kwa yeyote ambaye anaonekana ni kikwazo kwa chama na hususani anayewaamsha raia kujitambua.

Hii ni hatari kwenu maana kama hatutawaswaga ninyi kwenye mahakama za uhalifu basi wajukuu zenu watasimama kwa niaba.
 
Kwa kweli hizi propaganda zinazofanywa na ccm zinaangalia faida ya leo tu bila kufikiria madhara ya kesho na vizazi vijavyo. Walianza kwa kuwaaminisha wakristo kuwa CUF ni chama cha waislam na kwa kiasi kikubwa walifanikiwa, wakristo wengi walipoteza imani nacho na kikapoteza umaarufu.

Wamegukia upande wa pili na kuwaaminisha waislamu kuwa CDM ni chama cha wakristo na pia kwa kiwango flani wamefanikiwa maana kwa sasa ata waislam wapenda mabadiriko wanaitazama CDM kwa jicho la tahadhari tofauti na mwanzo lakini ubaya uliojitokeza ni kuwa wakristo wengi nao wameshawishika kuamini kuwa CCM ni chama ama cha kiislamu au kinawapendelea na hivyo kukichukia.

Huu mnyukano tunaouona sasa kwa kisingizio cha "haki ya kuchinja" ni matokeo ya chuki baina ya wana dini wa CCM na CDM ndio maana maeneo ambayo yana wafuasi wengi wa CDM ndio hali inakuwa mbaya zaidi na itakuwa vigumu sana kwa kiongozi wa dini au Serikali kujitokeza kusuluhisha na kupokelewa vizuri bila ya kuonekana anapendelea dini ya chama flani.

Kabla ya huu moto wa udini haujapoa wanawasha chuki zingine baina ya wananchi na polisi kwa kuwatengenezea au kubambikia watu kesi za utekaji na ugaidi na kuwaziba midomo wanaodai au kuhoji haki. Mbinu hizi ovu zinaweza kuwasaidia lengo lao la kutugawa ili watutawale lakini watatawala nchi yenye makovu makubwa na chuki mbaya kwa wananchi na kurudisha nyuma sana maendeleo ya kiuchumi maana hata makazini hatutoaminiana.
 
Leo nchi imewashinda kutawala wanakesha kutafuta visingizio.

Rais analalamika,
PM analalamika
Waziri analalamika
Raia analalamika.

Hatuwezi kuongozwa na jamii ya watu wasio na majibu ya madhila yetu, wao wapo wapo tu wala hawajui kwa nini wapo
 
Kila mtanzania anyeishi tanzania na anayeishi kwa kipato chake halali hawezi kuiunga mkono ccm.
Ndugu zangu watanzania,hii nchi ni ya kwetu sote,vyombo vya mamlaka vimetokana na sisi,rais hawez kuwa rais bila kura zetu wananchi.
Mleta mada ameandika kwa hisi na yote aliyosema kila mwenye kuipenda nchi hii angeyatafakari na kuchukua hatua mifumo yote ya utawala ingebadilika na pengine matatizo tunayopata kwa sasa yangeisha,hima watanzania wenzangu tuamke na tuchukue hatua.
 
Ccm ilishakufa kitambo hii iliyopo ni uvundo wa mzoga wa ccm,shime kwa pamoja tuukusanye tuuzike kabla haujatuletea maradhi ya matumbo tukaangamia sote.😛ainkiller:😛ainkiller::A S-cry:
 
Kila mtanzania anyeishi tanzania na anayeishi kwa kipato chake halali hawezi kuiunga mkono ccm.
Ndugu zangu watanzania,hii nchi ni ya kwetu sote,vyombo vya mamlaka vimetokana na sisi,rais hawez kuwa rais bila kura zetu wananchi.
Mleta mada ameandika kwa hisi na yote aliyosema kila mwenye kuipenda nchi hii angeyatafakari na kuchukua hatua mifumo yote ya utawala ingebadilika na pengine matatizo tunayopata kwa sasa yangeisha,hima watanzania wenzangu tuamke na tuchukue hatua.

Hapo kwenye red mkuu, don't forget the fact that in most African countries vote don't count, the one who count the vote is the one who matters the most. Hawa jamaa wako tayari kushinda hata kwa magoli ya mkono as long as referee ashawekwa sawa.
 
Leo nchi imewashinda kutawala wanakesha kutafuta visingizio.

Rais analalamika,
PM analalamika
Waziri analalamika
Raia analalamika.

Hatuwezi kuongozwa na jamii ya watu wasio na majibu ya madhila yetu, wao wapo wapo tu wala hawajui kwa nini wapo

shiiii! Taratibu! Rais pia anaogopa itifaki, no, itikafu! Sijuhi ndio laana gani hiyo?
 
shiiii! Taratibu! Rais pia anaogopa itifaki, no, itikafu! Sijuhi ndio laana gani hiyo?
Kwa kuweka sawa historia.
hakuna msikiti Dar uliomsomea Itikafu rais. Amedanganya kama alivyotudanganya kwenye kampeni zake 2010.

Anapoongea maneno kumi chuja mawili ndo ya ukweli
 
kuna wimbo aliuimba abiudi akiombea uchaguzi mwaka 2005 ni nani anaujua ulikuwa na message nzuri sana
 
Nashauri sektretarieti mpya ya CCM imemshawishi Professor Boaz anafundisha Wahington University agombee nafasi ya Urais. Hawa waliojitokeza mapema kuutaka Urais wameonekana hawafai machoni pa Watanzania walio wengi na hii ndiyo njia pekee ya kukabiliana na upinzani mkali unaoonyeshwa na CHADEMA.
 
Back
Top Bottom