Kwani walitoa tamko dhidi ya mbakaji Kapuya? Waache wafu wazike wafu wenzao
Umewachoma wakuda hao, Ngoja tumskie Nape a.k.a GAMBA MROPOKAJI
Wanajamvi heshima kwenu,
Katika hali isiyo ya kawaida chama tawala kimekuwa kimya sana tangu kifo cha kada wake, diwani wa Kisesa, Clement Mabina. Wanajamvi kuna yeyote ameshatoa tamko rasmi (msemaji wa chama) kuhusiana na hili? Tumezoea sana kupata taarifa rasmi kupitia kwa Katibu Mwenezi kwenye vyombo vya habari, kupitia kwenye mitandao na blog mbalimbali hususan ya Michuzi kila mara kunapokuwa na jambo linalohusu viongozi wa chama tawala. Mmepata kigugumizi gani? Ama mnafikiri kwa kukaa kimya tutasahau?
Bwana mdogo Kiwi,
Hayo si mambo madogo kama weye ulivyo mdogo. Aliye kufa ni diwani, aliyeuawa na wananchi wake kwa hasira zao juu ya ufisadi wake.
Tayari hilo pekee linatosha kuonesha kuwa kata hiyo sio ya ccm tena. Sasa, kupokwa kata mchana peupe, uongeze na sile za Arusha ambapo kidonda bado kibichi kabisa!!! Yataka moyo atii kuamini.
CCM bado hawaja amini. Nape hajaamini kuwa aibu nyingine inamngoja ya kupoteza tena kata hiyo.
Poleni sana wafiwa wa mtoto asiyestahili bali amenyang'anywa uhai wake mapema mno. Mungu ampokee tu na amlipe aliyemtuma huko kabla.
Duu,
Mkuu nimekuwa bwana mdogo?
Ninafikiri kiumri ni mmoja wa wanajamvi wenye umri mkubwa humu JF.
Shahada yangu ya kwanza niliipata mwaka 1981 UDSM, sina haja ya kueleza nina shahada ngapi mpaka sasa wala wasifu wangu hauna haja ya kuanikwa humu jamvini. Mahali panapohusika na kwa wanaonifahamu wanajua hayo.
Nimekusamehe bure mkuu...