CCM,Mbio za Sakafuni huishia Ukingoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM,Mbio za Sakafuni huishia Ukingoni

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by kasitile, Mar 13, 2011.

 1. kasitile

  kasitile Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa maoni yangu kama CCM itaendelea kuwepo madarakani daima dumu basi kuna maandishi ukutani yasomekayo, "TANZANIA HAITAENDELEA KAMWE", nasema hivyo baada ya kutaathimini kwa makini sana mwenendo wa mambo serikalini na kwenye chama hiki kikongwe Afrika.

  Inawezekana kuna mazuri yanayofanywa na CCM, lakini sintajikita katika hilo
  , maana naamini wapo watu walioajiliwa na chama kwa ajili ya kueneza uzuri wake kama vile akina TAMBWE, hii ni kazi ya akina Makamba ambao CCM kwa kiasi kikubwa inawaweka mjini.

  CCM kamwe haijakwepa kasumba ya ukoloni ya kuwatukuza watu wachache na kuwasahau watu walio wengi.CCM ile ya mwaka 1967 si ya sasa, CCM ya Nyerere si hii ya Kikwete.CCM kimeendelea kuwa chama chama cha matajiri na kuwasahau wakulima na wafanyakazi ambao ndio msingi wa chama hiki kisichokuwa na mpango wowote wa kuwaletea maendeleo wananchi.

  Sasa hivi kila mwenye ukwasi anakimbilia CCM maana anajua mali zake zitaendelea kuwa salama,matokeo yake serikali inashindwa kufanya maamuzi mazito,maana kuingia kwao madarakani ni matokeo ya ufisadi wa wakwasi hao ambao ndio wafadhili wakubwa wa chama.Chama kinabeba kila aina ya uchafu,kiasi kwamba ndani ya chama na serikali haonekani nani msafi na nani mchafu.


  Wakulima ambao ndio msingi mkubwa wa CCM sasa hawathaminiwi tena,wao wamekuwa mtaji wa chama wakati wa uchaguzi baada ya hapo hawakumbukwi tena wanabaki wanatajwa tu kwenye hoja,lakini maisha yao ni yaleyale zaidi yanazidi kudidimia,hakuna matumaini yoyote kwa wakulima waliotapakaa kila pembe ya nchi hii.

  CCM kimebaki kuwa chama cha kwenye makaratasi,na hata ukiwaangalia usoni wana CCM hawaonekani kama wanafanana.Wanatofautiana sana kimawazo na kimatendo,kila mtu na lwake.Hebu watazame kwa makini utangundua kuwa hakuna chochote kinachowaunganisha,wanashinda wanaparuana.Hata wale wanaonekana waadilifu kwa kiasi Fulani,hawaonekani,wamemezwa na uozo wa chama hiki,hakuna ambaye anaweza kunyoshea kidole mwanzake.

  Ukitaka kugombea cheo chochote ndani ya CCM sharti uwe mkwasi,si mkulima na mfanyakazi kama awali,makundi haya hayana chao ndani ya chama hiki,wao ni daraja la kupandia kwa wenye nazo.Tangu Azimio la Arusha lizikwe huko Zanzibar,CCM ina wenyewe,wafanyabiashara ndio msingi mkubwa wa chama.Mchakato wa kugombea cheo chochote ndani ya chama hiki ni mzito mno kuliko ninavyoweza kusema.Aliyekuwa katibu mkuu wa CCM enzi za kibabe za Mkapa,bwana Philip Mangula amewahi kusema kuwa itafika muda kwenye uchaguzi ndani ya CCM itakuwa inatangazwa tenda ya kupata viongozi maana pesa ndio inayoamua nani wa kushinda.

  Baadhi ya watu wanaosema ukweli ndani ya chama wanatengwa na hata kuadhibiwa kisirisiri mfano Samwel Sitta ambaye alianguliwa kwa mizengwe katika kinyangÂ’anyiro za uspika.Hawataki utofauti wa mawazo,wanataka sauti za ndio mzee au zidumu fikra za mwenyekiti,kuna baadhi ya watu ni wamiliki wa chama na serikali.CCM wanaamini kuwa wao ndio wanaostahili kuongoza nchi,wana akili sana na ndio wanaojua sana matatizo yetu na masuluhisho yake.Wakijitokeza watu wengine wenye mwono tofauti wanapewa majina tofauti yanayochefua sana,wanasahau kuwa hii ni nchi yetu wote,hakuna anayeweza kusema yeye ni zaidi ya watu wengine.

  Pengine hili ni suala la wakati,kama CCM wanaamini watabaki madarakani kwa sarakasi wanazofanya bila kushughulika na matatizo ya msingi ya wananchi wanajidanganya.Hawataki kusoma maandishi ukutani,ulevi wa madaraka umewatawala.Watanzania wengi wamechoka na maisha haya ya maigizo,pengine kinachosubiriwa ni mtu wa kuanzisha na kuongoza mapinduzi kama nchi za Kiarabu.Ole wenu CCM msipobadilika,kiama chenu kinakuja upesi,na hakuna atakayesalia,na kamwe hamtarudi tena,itabaki simulizi tu.   
 2. kasitile

  kasitile Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika uchaguzi wa mwaka jana,Dr Slaa ambaye alikuwa anapambana na J.Kikwete katika kinyang'anyiro na urais amewahi kusema Kuirudisha CCM madarakani ni kuleta maafa katika nchi hii.Ukweli wa kauli sasa unaonekana,kwani tayari makali ya maisha tunaushuhudia,huku nishati ya umeme ikibaki kuwa anasa miaka 50 ya uhuru.Serikali imeendeleza maigizo,hasa kwa suala la Dowans,yote haya wananchi wanayajua.Kwa upande wa bungeni,CCM kupitia kwa Anne Makinda,inafanya kila liwezalo kunyamazisha sauti ya umma,sasa ni mpambano mkali kati ya CCM na CHADEMA.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mimi nadhani tuseme kwamba wananchi wa tanzania wasipobadilika, "TANZANIA HAITAENDELEA KAMWE". Wananchi wa Tanzania wamekuwa wakiwapa ccm a '' collateral advantage'' ya kuonekana kukubali kila kitu, kibaya au kizuri kinachowaathiri maisha yao! Iwe ni kudanganywa na viongozi waliokosa uoni na matarajio ya baadaye, watanzania wapo wapo tu. Kwa kweli pamoja na elimu wanayopewa na vyama vya upinzani lakini bado wengi bado wanaona kwamba umasikini wao ni natural kama wanavyolaghaiwa na watawala wao huku section fulani kwenye jamii ikipaa kama uchumi aliouona mh. lowasa miaka ile alipokuwa pm, teh!
   
 4. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Siyo kweli kwamaba wananchi tunaipa CCM kura , tume ya uchaguzi na usalama wa taifa ndiyo waliochakachua kura zetu, nani asiyejuwa kuwa slaa alishinda na Philipo Shelembi alishinda Shinyanga mjini na ushindi kuporwa kwa nguvu zote,kazi naapa na kukuhakikishia ndugu msomaji 2015 hatufiki kabla hawajatuulia barabarani, kama ambavyo ndugu yao gadafi anafanya, maana kuna mwanafalsafa mmoja humu jamii forum aliwahi kusema nakukuru"

  Tabaka la watawala Tanzania ni sawasawa na Gaddafi kwa sababu zifuatazo:

  1. Wote wanaimani potofu kuwa serikali yao inapendwa sana na wananchi
  2. Wote wanaamini kuwa maandamano yanachochewa na serikali/taasisi/wafadhili wa nje
  3. Wote wanaamini kuwa wananchi wanapewa kitu ili kushiriki maandamano, eg pesa/madawa ya kulevya
  4. Wote wanaamini kuwa wananchi hawana shida yoyote (eg Sophia akisema "kama kuna matatizo."
  5. Wote wametawala kwa muda mrefu sana (CCM miaka 50 na Gadaffi miaka 42)
  6. Wananchi wa nchi zote wamechoka umasikini, ufisadi, manyanyaso, ukosefu wa ajira, uporaji wa pesa za umma, etc
  7. Chama tawala Tanzania/Libya miaka yote kimekuwa kikishinda uchaguzi wa Urais na wabunge kwa kuiba kura
  8. Need I say more?
   
 5. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  inachfanya sisiem ni kuwafanya wananchi watazame pasipo kuona na wasikie pasipo kuelewa.
   
 6. kasitile

  kasitile Member

  #6
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM imegeuka kuwa chama jiwe,hawaambiliki wala hawashauriki,wao ni wao.Ukiwakosoa na kuwashauri watakuambia una wivu wa kike na mambo mengine ya hovyo.Hapo walipofikia CCM hawawezi kubadilika,wanatakiwa kubadilishwa na wananchi.
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kilishakuwa CCW/K - Chama cha Washenzi/Kishenzi.
  Mshenzi siku zote hajali wengine.
   
Loading...