CCM: Mambo si mambo

CCM: Mambo si mambo

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Mambo si mambo ndani ya CCM.Kunafukuta.Yasome malalamiko ya Makada waandamizi wa CCM Ofisi Ndogo Lumumba,Dar es Salaam:

1. Viongozi wakuu wote wana makundi ya Urais ndani ya chama,sisi tunakatazwa tukiambiwa tusubiri taratibu za chama.Zipi?

2.Wanakula kuku sisi makombo.

3. Wanasafiri wao sisi tupo tu kama nyumba za NHC.

4.Tenda za vifaa vya uchaguzi kila mwaka wa uchaguzi wanapewa wale wale.

5.Wao wameshawapata wagombea wao kwenye majimbo halafu sisi tunasubiri kwenda kuigiza Kura za Maoni ndani ya chama.

6.Wao wanafanya biashara kubwa,sisi wanatuuzisha mashati na fulana za chama hapo nje-Lumumba.

Hapo 'nimesamaraizi' malalamiko yanayokandamizwa na miiko mikutanoni. Hali si shwari. Viongozi mpo?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Ngoja waje wadogo zako wa Lumumba! Wakianza kuporomosha matusi usikimbie!
 
Waache tamaa.

Mbona nao wanalipwa elfu sabasaba za kutetea chama kwa kutoa taarifa za uwongo na kuwanenea uwongo na matusi Wapinzani hasa wale wenye nguvu, ili kuwachafulia sura?

Hawajui kwamba Uwongo na propaganda ya ccm nayo ni maradi mzuri unawapa book 7 kwa siku?

Wakajifunze mgawanyo wa kazi na madaraka.
 
Mambo si mambo ndani ya CCM.Kunafukuta.Yasome malalamiko ya Makada waandamizi wa CCM Ofisi Ndogo Lumumba,Dar es Salaam:

1. Viongozi wakuu wote wana makundi ya Urais ndani ya chama,sisi tunakatazwa tukiambiwa tusubiri taratibu za chama.Zipi?

2.Wanakula kuku sisi makombo.

3. Wanasafiri wao sisi tupo tu kama nyumba za NHC.

4.Tenda za vifaa vya uchaguzi kila mwaka wa uchaguzi wanapewa wale wale.

5.Wao wameshawapata wagombea wao kwenye majimbo halafu sisi tunasubiri kwenda kuigiza Kura za Maoni ndani ya chama.

6.Wao wanafanya biashara kubwa,sisi wanatuuzisha mashati na fulana za chama hapo nje-Lumumba.

Hapo 'nimesamaraizi' malalamiko yanayokandamizwa na miiko mikutanoni. Hali si shwari. Viongozi mpo?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Moderator nyuzi kama hizi za kizushi zisizo na ushahidi wowote hazifai kuachwa hapa jamvini.
 
Last edited by a moderator:

Ndugu MUSSA ALLAN,wewe haupo Lumumba.Huko nako mna malalamiko yenu. Tulia ili chama kipate utatuzi wa mambo haya.Acha ushabiki na mihemko ndugu. Kada gani wewe usiye na uchungu na wenzako?

Mzee Tupatupa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom