ccm lazima itoe tafrisi ya neno fisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ccm lazima itoe tafrisi ya neno fisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Apr 17, 2011.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  nimefuatilia kwa umakini swala la ccm kujivua gamba. nimegundua kwa mara nyingine washauri wa jk wamempotosha kweli. na safari hii wamemtumbukiza shimoni. katika kuwaondoka mafisadi katika uongozi lazima kwanza uwe na tafrisi ya neno fisadi kwa minajili ya kuwaondoa kwenye chama. kila kiongozi wa ccm ni potential fisadi, sasa je ni yupi fisadi? na kama tuhuma ni za kweli kwanini wasiwapeleke mahakamani? kwa mtindo huu wengi wataona wameonewa na itakigharimu zaidi chama. sioni ccm itasimama vipi. vita hivi
  http://www.google.com
   
 2. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tafsiri ya ufisadi ilishatolewa mwembeyanga na Dr. Slaa, hivyo CCM haina haja ya kutoa ufafanuzi. Pia katika barua zitakazoandikwa na Komredi Mukama ataeleza sababu za mhusika kuomba ajitoe katika uongozi ndani ya CCM wakikataa itakuwa fursa kwa CCM kutoa RED CARD. Kimsingi CCM inafunga goli la kisigino kwa kuwatosa mafisadi wakati CDM wanapoteza uelekeo kwani hoja yao ya CCM na ufisadi itakuwa haina meno baada ya siku 83 zijazo. TZ inaelekea pazuri kutokana na kuzaliwa upya kwa CCM!
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Una imani sana na gamba eh? Subiri uje ushuhudie hizo sarakasi zenu! Ni vigumu kumtosa mtu ambaye ndiyo life support tube yenu, dili zote za survival ya familia zenu na zingine zote za kimkakati za kichama mmekuwa mkiwategemea ati leo muwatose, thubutuuuu! Hata ascendancy to power ya the existing govt imetokana nao, eti leo muimbe kuwatosa, sidhani kama itawezekana, this kujivua gamba is a shallow slogan aimed at camouflaging wajinga wachache lakini wenye akili wanajua sio rahisi kama mnavyoimba. Mfano ni maazimio ya bunge kuhusu richmond, epa na mengineyo mengi ambayo yamekuwa kwenye top10 ya political billboard ya hapa bongo kwa zaidi ya miaka 5 sasa, hatua zilizochukuliwa zimekua friendly kulinda magamba yenu yasikwaruzwe!
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kinachoendelea ni siasa, siyo vita ya kisayansi; kwenye vita ya kisayansi mtu anatakiwa amjue kwanza adui wake ni nani kabla ya kuanza kupigana, lakini katika vita ya hivi sasa inayoendeshwa na ccm lengo lake ni kuteka nyoyo za watu kwa njia ya kupotosha mambo. Katika hali hiyo, kuacha kila kitu kwenye utata ni sehemu ya mbinu iliyobuniwa kufanikisha vita hiyo.
   
Loading...