CCM kwaiva: Kama si Salim ni Mwandosya

CCM kwaiva: Kama si Salim ni Mwandosya

hakuna msafi ndani ya ccm , hao unaodhania ni wasafi subiri wachukue fomu uone mambo !
 
Mzee Tupatupa,ngoja nikupe pole maana huyo mumtakaye hatakubali........Ama nimeamini ile methali ya BANIANI MBAYA KATOKA INDIA
 
Mbona Mwandosya na EL wamesha wekeana MOU?? DR Salim nae ni muumini wa serikali tatu. Hapo imekaaje?? Mzee Tupatupanaamini sanatetesi zako ila hapo ufafanuzi kidogo plz
 
huku ni sawa na kuishi kwa matumaini.

Mkuu usibishane na Lumumba fc, wanasema wana mbinu zaidi ya 100 za kushinda uchaguzi na bado hawajaanza kutumia hata mbinu moja. Unadhani kuna mbinu gani nyingine zaidi ya sanduku la kura? Sasa hizo mbinu 100 wamezitoa wapi? Nadhani miongoni mwa hizo mbinu ni kuiba kura, kuua wagombea hodari wa upinzani, kuhonga waandishi wa habari, kutumia jeshi... Na nyingine kibao
 
Mzee Tupatupa,ngoja nikupe pole maana huyo mumtakaye hatakubali........Ama nimeamini ile methali ya BANIANI MBAYA KATOKA INDIA

Tatizo wakongwe wa chama wanazidiwa nguvu na vijana wapenda pesa chamani.Wanapelekeshwa tu. Inauma sana

Mzee Tupatupa
 
Mbona Mwandosya na EL wamesha wekeana MOU?? DR Salim nae ni muumini wa serikali tatu. Hapo imekaaje?? Mzee Tupatupanaamini sanatetesi zako ila hapo ufafanuzi kidogo plz

Usihofu. Dawa ni Salim au Mwandosya.Lowassa na wenzake tupa kule#

Mzee Tupatupa
 
yaani CCM ya Mwaka huu ni kama chama cha ADC, chama kichanga. haiingii akilini kwa hofu ya uchaguzi waliyonayo utafikiri sio chama kikongwe.
kinafanya mambo kwa kificho na kwa hofu kuu.
 
VUTA-NKUVUTE

Kati ya hao Salim afadhali ana sifa za kuwa rais toka 2005 basi walimwengu walifanya yao na kashfa lukuki mzee wa watu kimya, Vipi ile kashfa ya Karume watamsafisha kwa dodoki au maana hao hao wanao taka achukue fomu ndo waliomchafua.
 
Last edited by a moderator:
Huu ndo mwaka wa mwisho kwa utawala ccm .

Mkuu, kwa bahati mbaya sana, haitakuwa hivyo! Licha ya HALI HALISI, wagombea flani hawatapenyeza, watakataliwa. Mambo ya chama chao hayatakataliwa. Mipango ya kuhakikisha hilo haipingiki kwa nguvu za soda.
Kwa mwenenendo wa kipinzani uliopo ambao ni more VERBAL than else, kukamata dola itabaki ndoto. Nasema hivi kwa kigezo kidogo tu. Pale inaposemekana waTanzania wa leo hawadanganyiki tena na sio wale wa 1995 hao hao wakienda kwenye ballot box wanamchagua nani? Licha ya wizi wa kura, matokeo ya uchaguzi wa serikali ya mitaa uliopita ulirejesha picha ya ajabu sana. Ile muvi ya chopa tatu na kata tatu. Zile takwimu hazidanganyi. Katika nchi nzima distribution ya takwimu zile inakita kwenye CONVERGENCY ambayo anayeibuka kidedea sio upinzani. Hili halitabadilika hadi pale watu watakapobadilika kikweli, kuanzia Dar es Salaam. Pale watakapokataa watu wa CCM na mambo yao. Tofauti na hapo, 2015 sio mwisho wa utawala wa CCM.
 
kwa salimu sina pingamizi tuache kumwongelea lowassa.
 
yaani CCM ya Mwaka huu ni kama chama cha ADC, chama kichanga. haiingii akilini kwa hofu ya uchaguzi waliyonayo utafikiri sio chama kikongwe.
kinafanya mambo kwa kificho na kwa hofu kuu.
Wanasema nyani akikaribia kufa basi miti haishikiki.
 
Mwandosya anayo ya kwake labda umesahau! Ile SA umesahau!!???
Watanzania wengine ni rahisi kusahau madhara ya Mwandosya kuhusu ttcl mpaka sasa tunayaona isitoshe alipokuwa mgonjwa hakujiuzulu bali aliendelea kupokea mshahara wakati akijua fika hakuwa na mchango wowote kwa kifupi hafai
 
Tatizo wakongwe wa chama wanazidiwa nguvu na vijana wapenda pesa chamani.Wanapelekeshwa tu. Inauma sana

Mzee Tupatupa

Ninakuone huruma Mzee wangu,lakini mliyataka mlishindwa kabisa kusema NO wakati ule.Hakika mngemchukua Dr.Salim leo taifa letu lisingefika hapa lilipofika.LAkini CHUKI,PESA,na UROHO WA MADARAKA ndivyo vilivyopelekea haya yote.

Mzee Tupatupa naona huruma sana maana kati ya wale wachache waliosoma ile KATIBA YA TANU na KATIBA YA CCM,mimi ni mmoja wapo.Mzee wangu hata mafunzo yale ya mwaka mzima ili kuwa Mwanachama wa CCM pia hayapo kwa sasa...........

Ingekuwa chama kina sera zile zile za kwenye KATIBA zile ninauhakika hakuna CUF,CDM wala NCCR ingepenyeza....

Hakika ninaona maumivu yako,pole Mzee wangu,labda yule Shemeji yangu WWMN labda kidogo naona msafi kidogo anaweza kulibeba hilo dubwasha,lakini huyu mh! Sidhani kama atakubali........
 
Watanzania wengine ni rahisi kusahau madhara ya Mwandosya kuhusu ttcl mpaka sasa tunayaona isitoshe alipokuwa mgonjwa hakujiuzulu bali aliendelea kupokea mshahara wakati akijua fika hakuwa na mchango wowote kwa kifupi hafai
Salimu naye 2005 tuliambiwa sio raia na alihusika sijui katika nini miaka hiyo ya nyuma......
 
Back
Top Bottom