CCM kwaiva: Kama si Salim ni Mwandosya

CCM kwaiva: Kama si Salim ni Mwandosya

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Ingawa nipo Arusha,naendelea kudokezwa yanayochomoza vikaoni (ndani ya CCM) na katikati ya makada wa haja. Nimedokezwa kuwa CCM inaelekea kugeukia kwa wanachama wawili ambao kura zao hazikutosha mwaka 2005 na 2010, Dr. Salim Ahmed Salim na Profesa Mark Mwandosya. Nikaambiwa kuwa makada hawa wawili wana kila sifa za kuwa Rais wa Tanzania na hawana makuu wala makundi. Pia,wako mbali na kashfa ya aina yoyote iliyoitafuna taifa.

Ninaaminishwa kuwa ripoti mpya ya CAG imempiga mweleka Dr John Pombe Magufuli kwakuwa Wizara yake ililidanganya Bunge na kufisidi mamilioni ya fedha (bilioni 262). Dr. Salim na Prof. Mwandosya sasa wanatazamwa kama dawa pekee ya kuiponya CCM katika kipindi ambacho chama na Serikali yake kimeandamwa na kashfa za kifisadi za kila aina na rangi. Nikaambiwa kuwa Salim na Mwandosya watashawishiwa kuchukua fomu za kugombea kipenga kitakapopulizwa.

Hatimaye CCM yetu imepata pakutokea. Walionidokeza na kuniambia ni wabobezi wenzangu chamani na nawaamini. Afadhali papoe jamani!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
 
Huu ndo mwaka wa mwisho kwa utawala ccm .
 
Ma rais wa ccm sio Tanzania.Tukutane October .

swissme
 
Umetumwa wewe, hao vikongwe wa nini! Kuna hazina kubwa CCM zaidi ya hawa ajuza..... tunawaka viongozi sio makapi!
 
CCM inawataka hao. Je, wapiga kura wanahitaji hao au...?

Could that serve as a prelude to the beginning of the end of ruling party...?

I bet not.
 
wameona watashindwa oktoba,sasa wameanza figisufigisu kwenye uandikishaji wapiga kura,...nahisi maccm yanaandikishwa kwa siri usiku wa manane...
 
Ingawa nipo Arusha,naendelea kudokezwa yanayochomoza vikaoni (ndani ya CCM) na katikati ya makada wa haja. Nimedokezwa kuwa CCM inaelekea kugeukia kwa wanachama wawili ambao kura zao hazikutosha mwaka 2005 na 2010, Dr. Salim Ahmed Salim na Profesa Mark Mwandosya. Nikaambiwa kuwa makada hawa wawili wana kila sifa za kuwa Rais wa Tanzania na hawana makuu wala makundi. Pia,wako mbali na kashfa ya aina yoyote iliyoitafuna taifa.

Ninaaminishwa kuwa ripoti mpya ya CAG imempiga mweleka Dr John Pombe Magufuli kwakuwa Wizara yake ililidanganya Bunge na kufisidi mamilioni ya fedha (bilioni 262). Dr. Salim na Prof. Mwandosya sasa wanatazamwa kama dawa pekee ya kuiponya CCM katika kipin ambacho chama na Serikali yake kimeandamwa na kashfa za kifisadi za kila aina na rangi. Nikaambiwa kuwa Salim na Mwandosya watashawishiwa kuchukua fomu za kugombea kipenga kitakapopulizwa.

Hatimaye CCM yetu imepata pakutokea. Walionidokeza na kuniambia ni wabobezi wenzangu chamani na nawaamini. Afadhali papoe jamani!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
@VUTA NikuVUTE wabobezi wote wa chama wako Idodomya, we unafanya nini Arusha? Nitilia shaka ubobezi wako
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom