CCM kwa hili tunamkosea sana Rais Magufuli

Kwa nature ya serikali hii, iko tayari kuruhusu mijadala? Toka umemjua Magufuli umewahi kumuona kwenye mjadala wowote? Usipendekeze kisichowezekana. Sasa hivi ni mwendo wa shuruti, hayo ya mjadala ni kama kutaka kuhalalisha tu matakwa ya mtu.

Haina haja ya wasiwasi ndivyo inavotupasa, uoga na kukosa uthubutu ni mwiko, Ni lazima na wajibu wetu kujadili, na forums si kama hii jamii forum. We are all state officers and men, kama itahitajika vinginevyo kwa namna inayofaa tutajadili pia kwa nyakati zijazo. Nawasilisha.
 
P.
Mtoa mada ameongea Ukweli na Uzaoendo mtupu.
Tatizo ni hawa wenzetu wa CCM kujifanya WANAMPENDA MAGUFULI KULIKO TANZANIA....!!!Huu ni wendawazimu na wehu!!

Ushauri kwa Rais Magufuli:
RAIS MAGUFULI ATALIVUNJA BUNGE LA JMT TAREHE 19.06.2020 NINAOMBA AFANYE YAFUATAYO;
  1. AMKEMEE SPIKA NDUGAI NA WABUNGE WOTE WANAOTAKA RAIS AONGEZEWE MUDA.
  2. ATANGAZE RASMI MTU YEYOTE ATAKAYE SIKIKA ANATAKA RAIS MAGUFULI AONGEZEWE MUDA ASHTAKIWE KWA UCHOCHEZI.
Kama Magufuli hatafanya Kati ya hayo 2 au yote basi Watanzania wajue na Yeye yuko nyuma na Ni sehemu ya Mpango huo OVU.
Mzalendo2015
Umeliongelea vizuri sana jambo hili, kuwa unampa "ultimatum" Rais aliongelee hili kwa ukali jambo hili, pale anapovunja Bunge letu na amkemee vikali Spika Ndugai na genge lake la akina Kessy..........

Kama Rais asipoliongelea hili katika hotuba yake ya kulivunja Bunge, basi wananchi tutakuwa na "doubt" kuwa na yeye yupo sambamba na mpango huo muovu.......

Kwa kuwa tushaanza kumwelewa vizuri sana Rais Magufuli, kuwa jambo lolote asilolipenda ni lazima aliongelee mapema iwezekanavyo anapopata nafasi ya kulihutubia Taifa
 
Haina haja ya wasiwasi ndivyo inavotupasa, uoga na kukosa uthubutu ni mwiko, Ni lazima na wajibu wetu kujadili, na forums si kama hii jamii forum. We are all state officers and men, kama itahitajika vinginevyo kwa namna inayofaa tutajadili pia kwa nyakati zijazo. Nawasilisha.

Tatizo hapo sio woga au kukosa uthubutu, ni wapi kitatoka kibali cha kukutana na kujadili hilo kwa utaratibu unaokubalika?
 
Uko sahihi sana Mkuu, kwa mujibu wa Katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977 na mabadiliko yake inasema na nainukuu..

____
98.-(1) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kubadilisha
masharti yoyote ya Katiba hii kwa kufuata Kanuni zifuatazo:-
(a) Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti
yoyote ya Katiba hii (isipokuwa yale yanayohusika na
aya ya (b) ya ibara hii ndogo) au masharti yoyote ya
sheria yoyote iliyotajwa katika Orodha ya Kwanza
kwenye Nyongeza ya Pili utaungwa mkono kwa kura
za Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili
ya Wabunge wote;
(b) Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti

Mwisho wa kunukuu.

Kama Mhe Kessy akirudi bungeni, atapeleka hilo Azimio lake Bungeni...Bunge litajadili na kupiga kura kama ilivyoelekezwa na Katiba baadae kura zikitosha kama ilivyoelekezwa kwenye aya hapo basi Bunge litaruhusiwa kutunga sheria ya kubadilisha masharti ya katiba (likiwemo sharti la ukomo wa urais )

Wakimaliza wataleta huku chini kwa wananchi kwa ajili ya referendum.

Hatuogopi kuingia kwenye majadiliano kuhusu Ukomo wa Urais, kuongeza au kupunguza bali Tunaetaka Kumuongezea muda ameshasema mara nyingi hataki .

Kwa nini tunafosi?

Kama tunaetaka abaki hataki, basi tuache hizi habari.....

Kama mbeleni huko tukiona kama Taifa tuna haja ya kufanya extension ya muda wa Urais basi tukae tuzungumze.

Lakini kwa Rais Magufuli kashatuambia hataki na tunamkwaza.

Then we should stop...kama ambavyo Katibu Mkuu alisema "Amefunga" huu mjadala kwa Rais Magufuli.

Umma na mmoja mmoja wakiwa na kiu ya jambo lolote la kizalendo ni ruksa kusema na mhusika pia ruksa kuendeleza kukataa kwa kadri anavyopata wasaa wa kusema, kwa uchanya wake inaweza kumtia moyo wa kuenenda namna ipasavyo kwa watu wake, kumtia nguvu na ari ya kazi na kuyashinda majaribu ya kukengeuka. Tuendelee kuunga mkono kwa hoja au kupinga kwa hoja, tufungue mirija ya kuyasikia mengi, ebu tufikirie kwamba upo wigo wa mawazo mengi yaliyo bora na tuendelee kuyasoma.
 
Tatizo hapo sio woga au kukosa uthubutu, ni wapi kitatoka kibali cha kukutana na kujadili hilo kwa utaratibu unaokubalika?

Well said chukua mtazamo chanya ainisha huo utaratibu, haina haja ya kuwa na wasiwasi kbsa. Rejea ujumbe wangu umebeba options zote katika misingi ya viapo, utii na unyenyekevu. Tanzania ni yetu na tutailinda wenyewe, tuwape fursa waseme hoja zao wala haina shida, wakitushawishi tunaungana na nao wakishindwa ushawishi tunaungana pia nchi inasonga. Raia nchi ni yenu ondoeni shaka let's live freedom to expression and opinion ifanye kazi kwa Sasa.
 
Mnaongea Mambo mengi Sana yasio kuwa na faida yeyote kwa nchi,
✓kwanza mkasome tabia za udikteta kwa undani
✓ukishamaliza kusoma uje apa utuambie tutumie njia gani kuzuia udikteta Tanzania
✓tusiwe walalamikaji wa mitandaoni bila matendo kwani tukiendelea ivi ipo siku vyama vya upinzani vitafutwa kabisa, cc tukiendelea kutafuta democracy kwa kujificha,,,
 
Well said chukua mtazamo chanya ainisha huo utaratibu, haina haja ya kuwa na wasiwasi kbsa. Rejea ujumbe wangu umebeba options zote katika misingi ya viapo, utii na unyenyekevu. Tanzania ni yetu na tutailinda wenyewe, tuwape fursa waseme hoja zao wala haina shida, wakitushawishi tunaungana na nao wakishindwa ushawishi tunaungana pia nchi inasonga. Raia nchi ni yenu ondoeni shaka let's live freedom to expression and opinion ifanye kazi kwa Sasa.

Wao tayari wana platform ya kusemea maoni yao, na kwakuwa wao wana platform, wakishasema wanatulisha maneno kuwa wote tumekubali! Lakini hawako tayari sisi wenye mitazamo tofauti tuongee, maana wanajua fika nia yao ovu itapata vikwazo.
 
Wanabodi...

Niwasabahi kwa kuwatakia asubuhi njema na natumai mko fresh kabisa.
Kabla sijaenda mbali Mwalimu wangu wa Sheria pale chuo kikuu aliwahi nifundisha kuhusu "ku-declare interest", naomba ifahamike kwamba mimi ni Mwanachama Hai wa Chama Cha Mapinduzi na Mzalendo nambari moja kwa Taifa hili.

Naomba Wana CCM na Watanzania tuwekane sawa kwenye hili sababu linatuhusu wote, nashangaa sana wasomi , wanazuoni na wanachama wa CCM tunafanya kama hatukumbuki, au tumepoteza kumbukumbu sijui .

Mhe Kessy, mbunge wa Nkasi juzi alinukuliwa na vyombo vya habari Bungeni akisema Rais Magufuli aongezewe muda " Atake Asitake", akanukuliwa pia akisema "Asiachiwe huyu, alazimishwe" akaendelea kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye janga la Corona mataifa yote ya nnje yamemkubali.

Na Mhe Spika Ndugai akajibu, ngoja twende kwenye uchaguzi mkuu, tukirudi Mhe Kessy utaleta hili hili Azimio la Rais kuongezewa muda na naamini wote tutarudi, na lazima tutamuongezea muda."

Kiukweli, Binafsi nimesikitishwa sana na hii kauli ya Mhe Kessy kwa hoja zifuatazo,

Mosi, ikumbukwe tarehe 14 januari 2018, Rais Magufuli alikutana Ikulu na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndugu Humprey Polepole na hiki ndiko Rais John Magufuli amesema ANASIKITISHWA na HAFURAISHWI na mjadala ambao unaoendelea wa rais kuongezewa kipindi cha kutumikia kutoka miaka mitano hadi saba.

Amesema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na Katiba ya nchi na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hii ni kufuatia Mhe Juma Nkamia mbunge wa Chemba kuibua Hoja ya Kuongezewa Muda wa Urais toka Mitano mpaka saba.

Pia Rais Magufuli alitaka wananchi KUPUUZA mjadala huo.

Ndugu Humprey Polepole nae wakati anaongea baada ya kutoka Kwenye Mkutano na Rais alisema Magufuli aliwataka wana CCM na umma wa Watanzania kutokubali kuyumbishwa ama kupotoshwa na mambo yasiyokuwa ya msingi, badala yake wajielekeze katika ajenda muhimu ya kujenga uchumi na kutekeleza Ilani ya CCM iliyonadiwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Kupitia kitabu chake cha "Uongozi Bora ba Hatima ya Nchi yetu", Mwalimu Nyerere alishatoa Angalizo kuhusu kuongeza kipindi cha Urais , namnukuu Mwalimu na anaendelea kuonya tena, "Suala hili lilikwishakuamuliwa zamani, na sasa ni sehemu ya Katiba yetu. Uamuzi huo inafaa uheshimiwe. Rais Mwinyi ndiye Rais wa kwanza kuchaguliwa kwa mujibu wa katiba hiyo. Yeye akisema kuwa vipindi viwili havitoshi, na akataka viwe vitatu; Rais wa pili atasema vipindi vitatu havitoshi, na atataka viwe vinne na kadhalika mpaka tufikie Ngwazi (rais wa milele) wa Tanzania," (uk.10).

Kwa hii kauli ya Mwalimu Nyerere wabunge tunakwama wapi?

Ina mana hatujui tunachokisema?

Je, ni kweli hatuna uhakika wa kurudi kwenye Bunge la 12 kwa hiyo tunatamka chochote huku mwishoni ili tupate "Political Empathy"?

Wana CCM wenzangu, lazima ifike mahali tukubaliane na msemo wetu tunaosema kila siku " TUNASIMAMA NA RAIS MAGUFULI,", basi hata kwa hili analosema "Hafikirii hata siku moja kuongeza siku hata moja baada ya kipindi chake kuisha,", " Rais akasema ANAKWAZWA na hafuraishwi na mjadala wa kuongezwa muhula wa uongozi"

Rais Magufuli amenukuliwa mara mbili tofauti akiwajibu wale wote wanaomlazimisha aongeze muda, na Rais wetu hajazunguka kimaneno, kasema plain black and white "SITOONGEZA MUDA HATA WA SIKU MOJA BAADA YA KIPINDI CHANGU KUISHA", nakumbuka hii ilikua disemba 2019 alikua anatoa hotuba mahali.

Katibu Mkuu wa CCM ndugu Dr Bashiru nae alipokua pale Chemba akimtumbua Katibu wa CCM mkoani Chemba kwa kukosa Kujiongeza kuiva na viongozi wenzake alilisemea hili jambo, akasema " Rais Magufuli atamaliza miaka yake kumi, hiyo tutampa ridhaa badala ya Hapo atafata utaratibu wetu wa kikatiba wa kuachiana vijiti"...

Hivi wabunge wanataka KUTUAMINISHA wana nguvu zaidi ya wananchi waliowachagua?

Hivi Spika wa bunge Ndugu Ndugai anaposema BUNGE TUTAMUONGEZEA muda anaelewa kweli?

Hivi Spika hakumbuki TUME YA JAJI NYALALI(NYALALI'S COMISSION), miaka ya 1998 9 na ile kazi ya kukusanya maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba?

Kwamba lazima wanachi wafanye kitu tunaita Referendum .,

Kukawa kuna kitu kinapita mtaani kwa jina la "WHITE PAPER"? Chenye lengo la kutaka kujua maoni ya watanzania kuhusu jambo husika la kurekebisha kwenye katiba yetu.

Kwa nini Spika useme " TUTAMUONGEZEA MUDA" maana yake unasahau sisi wananchi wa kawaida na nguvu yetu kwenye maamuzi.

Hivi Mhe Kessy kweli anataka tuamini hajasikia maneno ya Katibu Mkuu wetu Dr Bashiru kuhusu mjadala wa ukomo wa Urais.?, Katibu Mkuu alitamka ameufunga Rasmi disemba 2019 au Mhe Kessy ana nguvu zaidi ya Dr Bashiru??, kitu akishasema Katibu Mkuu wa Chama wewe mwanachama wa kawaida una comply nacho..Hauna haja ya kuropoka tena maana Msimamo wa Katibu Mkuu ni msimamo wa Chama.

Waziri Kabudi nae alishatolea ufafanuzi hili jambo wakati akiwa Katiba na Sheria , akasema vipindi vya Urais ni VIWILI tu vyenye miaka Kumi Kumi ndanu yake.

Simlaumu Waziri Mkuu mstaafu Ndugu Mizengo Pinda siku ile aliposema "Anatamani Rais Magufuli aongezewe muda wa Urais"..

Mhe Pinda alikua anatoa maoni yake kama mtanzania wa kawaida, kama mimi na wewe, lakini baada ya Rais Magufuli kutoa msimamo wake kuhusu hilo ombi , binafsi sijamsikia Tena ndugu Pinda anakuja kwenye media na kuanza kumbembeleza Rais.

Hii sio mara ya kwanza kwa watu kutoa maoni, hata wakati Rais Kikwete anamalizia uongozi wake 2009 kulikua na watu wakimtaka Rais Mstaafu Kikwete aongeze muda wa kukaa kwenye Urais..

Waziri wa katiba na sheria mhe Chikawe wakati huo akatoa msimamo kwamba Rais Mstaafu Kikwete hatoongeza tena muda wa Urais.

Narudia tena, Ndugu Juma Nkamia alikua amepeleka hoja yake binafsi ya kuongeza Kipindi cha Urais toka miaka mitano mpaka saba lakini baadae aliitoa hii hoja yake akasema " Ameshauriwa na viongozi wake wa juu wa Chama cha Mapunduzi aitoe na asiendelee na hoja yake japo Nkamia aliileta hoja yake mara mbili lakini alivyoambiwa aitoe, ALIITOA", na hii inaitwa UTII kwa viongozi wako wa CHAMA.

Pia Mhe Mizengo Pinda hakuendelea na hoja yake mara baada ya msimamo wa Rais Magufuli, kwa nini Mhe Kessy anakomaa?, unaweza kuona "countance" (mwonekano) wa Mhe kessy pale Spika Ndugai alipomwambia "Utarudi kwenye Bunge lijalo la 12 na utakua ni wewe mletaji wa Azimio hili".

Ukiisoma Body Language ya Mhe Kessy unaona kabisa anafurahi kusikia atarudi kwenye Bunge lijalo!

Anafurahi kuambiwa atakua mletaji hoja ya Azimio la Bunge kuhusu Kuongeza ukomo wa Kipindi cha Urais!.

Kifupi mhe Kessy anataka kurudi bungeni, which is okay lakini rudi bungeni with your own expense!, sio unarudi bungeni with expense' of the Nation.

Leo kila mbunge atake Katiba ibadilishwe ili apate debe/upendeleo wa kurudi bungeni toka kwenye Kamati Kuu ya CCM si kila siku tutakua tunabadilisha katiba yetu .

Nkamia alikua anataka ku-copy paste Katiba ya Rwanda ambayo toka 1994 ilikua inasema Kipindi (tenure) ya uongozi wa Urais ni miaka saba saba , lakini Rwanda wamefanya mabadiliko kwenye Katiba yao na kuanzia Mwaka 2024 Rwanda wanarudi kwenye tenure ya miaka mitano mitano, , Rais akae miaka kumi tu madarakani ampishe Mwenzie.

Kifupi Rwanda wanatamani kuwa kama sisi lakini Sisi ndo kwanza Tunataka Rais Aongezewe miaka 10 zaidi kutoka 2025 yaani Rais Magufuli atumikie mpaka 2035.

Mi nampenda sana Rais wangu kwa kazi alizofanya na anazoendelea kufanya.

Naipenda spirit yake ya kujitegemea na "will power" yake kwenye kufanya mambo na maamuzi kama Taifa hakuna sehemu nam-doubt Rais Magufuli.

Ni will-power yake na roho yake ya kizalendo kwa Taifa hili imetufikisha hapa tulipo, maofisi ya serikali yana nidhamu, wanyonge wanasikilizwa na kupewa HAKI.

Rais Magufuli amefanya Maamuzi ya kipekee sana kwenye kushughulikia suala la Corona, ametujengea Roho ya kipekee kwenye Kipindi hiki Taifa limepitia kwenye Huu ugonjwa.

Rais Magufuli kawajibisha wakuu wa mikoa, wakuu wa idara mbalimbali za serikali pale Rais anapobaini mambo hayaendi!...unakumbuka kuvunjika kwa Daraja pale Morogoro?, unakumbuka Waziri Kamwele alivyochanwa Live kwa kutomuajibisha Meneja wa TANROADS wa mkoa?

Unakumbuka Rais alivyowachana Magereza na TBA pale Ukonga kwenye mradi wa nyumba za jeshi la magereza?

Na akawaambia live atawaletea Kamishina wa MAGEREZA toka JWTZ?

Unakumbuka JKT walivyoendeleza ujenzi wa zile Nyumba na Ukaisha?

Hii ni mifano michache ya Rais Magufuli, bado uthubutu wake wa Kufufua Mashirika ya UMMA kama ATCL .

Sitozungumzia ujenzi wa madaraja, barabara, vituo vya Afya kila kata, Elimu Bure, Mikopo ya Elimu ya Juu n.k maana hivyo kila mtu anavizungumzia.

Binafsi naungana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ndugu Dr Bashiru , Naungana na Rais Magufuli na Msimamo wa Chama kwa Pamoja Kumruhusu Rais Magufuli apate kipindi cha Pili cha Uongozi kwa miaka mingine mitano mpaka 2025.

Vivaa Magufuli....

Mzee Pius Msekwa alikua mmoja wa wazee walioshughulikia mabadiliko anuwai' yaliyokua yanafanyika kwenye Katiba ya Tanzania toka ile ya 1921 .

Anajua tulikotoka na mabadiliko yote tuliyofanya zaidi ya mabadiliko 12 na alisema wazi kabisa "Toka enzi za Mwalimu tulishazungumzia kuhusu kuongeza muda wa Urais".

Wana CCM na hasa vijana wenzangu wa UVCCM tusimkwaze Mhe mwenyekiti wetu Dr Magufuli, kashasema HAPENDEZWI, ANASIKITISHWA na HAFURAISHWI na hizi kauli zetu huku kwenye mitandao tunapiga kelele za kuongeza muda wa Urais.

Rais Magufuli nae ana maisha yake ya kifamilia, tumuache apumzike na tumshukuru kwa Mchango wake mkubwa kwenye Taifa hili la Tanzania na alishasema Mara Nyingi " Urais ni KAZI NGUMU".

Alishasema analala na mafaili pale IKULU wakati mwingine tafadhali tuheshimu maamuzi yake.

Tuachane na wanasiasa walio tayari kusema lolote mradi mradi tu warudi bungeni hata ikibidi kurudi "in expense" (kwa gharama) ya kubadilisha katiba....

Laiti Rais mstaafu Jakaya Kikwete angesema aongeze muda basi leo hii tusingempata Rais Magufuli, haijalishi kapatikanaje lakini kapatikana na kwa Miaka hii mitano kalinyanyua hili Taifa akiwa na Timu yake aliyoichagua na Kuiamini.

Sasa akisimama Mbunge kama Mhe Kessy akasema "Haoni mtu mwingine wa kutuvusha baada ya Magufuli", mi namshangaa Mhe kessy..sijui alikua anawaza nini.

Nafunga kwa Maneno ya Rais Magufuli anasema " MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU"...

Na ameshasema zaidi ya mara moja, na viongozi wa Chama na serikali wameshaongea kuhusu kuongeza muda basi TUSIMKWAZE mpendwa wetu Rais Magufuli.

Tutashinda Uchaguzi huu Mkuu wa oktoba na Chaguzi zingine Miaka mingine sababu tunaaminika na wananchi.

Ndugu Humprey Polepole aliulizwa siku swali kwenye redio unadhani siku CCM ikiondoka madarakani tatizo litakua nini?

Na napenda jibu alilotoa, "Kwa sasa CCM haitotoka madarakani kwa mabadiliko haya tuliyofanya", Lakini huko baadae CCM ikianza kudharau wananchi basi itaanguka na kuondoka madarakani"

Tueshimu Msimamo wa Rais Magufuli kuhusu kutokuongeza muda wa Urais na tumshukuru Kwanza yeye na serikali yake kwa kazi nzuri waliyofanya ndani ya miaka mitano na tusimame nae kwenye hii miaka mingine mitano mpaka 2025.

Nimeona Niliseme hili wazi na tafadhali moderators msiunganishe huu uzi na nyuzi zingine maana haufanani na nyuzi zingine maana hamkawii kunikwaza asubuhi

"MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU MBARIKI RAIS MAGUFULI NA SERIKALI YAKE YA AWAMU YA TANO".

NB: Kwa maoni au ushauri usisite kumuandikia muandishi kwenye barua pepe : godjohn8@gmail.com
Tuchukue fursa hii kumpongeza sana Dr kwa kukufanya uwe mzalendo hakika atatawala milele[emoji16]
 
Kwa mtazamo wangu finyu wengi wanaohamasisha hii ajenda wao binafsi wamefilisika kisiasa na ni nguvu ya dola na CCM ndio inawabakisha katika nafasi walizokua nazo. Hivyo kwa kupenyeza hili pendekezo nao wanajitengenezea mazingira ya kubaki katika nafasi walizonazo kupitia mgongo wa CCM na Mh Rais na laiti kama katika chama kungekua na transparency au tume huru ya uchaguzi ingefanya kazi yake kwa weledi huu mjadala usingekuwepo.
 
sasa mbona maandiko yako yapo kama ally kessy?
Tujifunze kukubali na kuheshimu mawazo ya wengine hata kama mnatofautiana.

Hili la kufuta mihula ya urais, angalia mimi nilianza kushauri lini...
Wanabodi hili ni bandiko la 2015

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
4. Na hiyo 2025 tukimuona Magufuli bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili hiyo katiba yetu ili tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.

5. Kwani katiba ni nini?, si ni kipande tuu cha karatasi?!, ingekuwa katiba ni muhimu kihivyo kama ambavyo watu wanataka kutuaminisha humu, nini muhimu zaidi kwa taifa letu Tanzania, kati ya katiba ambayo ni kipande tuu cha karatasi na maamuzi ya rais Magufuli ambaye ni rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu, katika uchaguzi huru na wa haki?.

6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, hivyo kama sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua tunamtaka Magufuli aendelee tuu idefinately, si tunaweza kuiweka tuu pembeni hiyo katiba, na tukaendelea na Magufuli wetu mpaka tutosheke naye?!.

7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana kuliko hata katiba na ndio maana anaweza hata kuikanyaga, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu, na kumwacha aendelee tuu kama Kagame, Museveni na Mugabe?.

8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Kama katiba inakanywa na hakuna kinachofanyika, Jee kuna ubaya kama tutaibadili katiba na Magufuli akapatiwa muda wa kutosha kabisa wa kuinyoosha nchi yetu kama Kagame anainyoosha Rwanda, , Museveni anavyoinyoosha Uganda na Mugabe anavyoinyoosha Zimbabwe?.

Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.

Paskali
Wanabodi, kwanza angalieni tarehe ya bandiko hili, kisha angalia hoja No. 4, 5, 6, 7 na 8 za bandiko hili, kisha sikiliza kilichozungumzwa jana Bungeni Dodoma kuhusu hoja hii.

P
 
Tujifunze kukubali na kuheshimu mawazo ya wengine hata kama mnatofautiana.

Hili la kufuta mihula ya urais, angalia mimi nilianza kushauri lini...
Wanabodi hili ni bandiko la 2015

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Wanabodi, kwanza angalieni tarehe ya bandiko hili, kisha angalia hoja No. 4, 5, 6, 7 na 8 za bandiko hili, kisha sikiliza kilichozungumzwa jana Bungeni Dodoma kuhusu hoja hii.

P
Mbona unampongeza tena huyu anaelipinga hapa?

kama sio umalaya wa kisiasa ni nini?
 
Uko sahihi sana Mkuu, kwa mujibu wa Katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977 na mabadiliko yake inasema na nainukuu..

____
98.-(1) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kubadilisha
masharti yoyote ya Katiba hii kwa kufuata Kanuni zifuatazo:-
(a) Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti
yoyote ya Katiba hii (isipokuwa yale yanayohusika na
aya ya (b) ya ibara hii ndogo) au masharti yoyote ya
sheria yoyote iliyotajwa katika Orodha ya Kwanza
kwenye Nyongeza ya Pili utaungwa mkono kwa kura
za Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili
ya Wabunge wote;
(b) Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti

Mwisho wa kunukuu.

Kama Mhe Kessy akirudi bungeni, atapeleka hilo Azimio lake Bungeni...Bunge litajadili na kupiga kura kama ilivyoelekezwa na Katiba baadae kura zikitosha kama ilivyoelekezwa kwenye aya hapo basi Bunge litaruhusiwa kutunga sheria ya kubadilisha masharti ya katiba (likiwemo sharti la ukomo wa urais )

Wakimaliza wataleta huku chini kwa wananchi kwa ajili ya referendum.

Hatuogopi kuingia kwenye majadiliano kuhusu Ukomo wa Urais, kuongeza au kupunguza bali Tunaetaka Kumuongezea muda ameshasema mara nyingi hataki .

Kwa nini tunafosi?

Kama tunaetaka abaki hataki, basi tuache hizi habari.....

Kama mbeleni huko tukiona kama Taifa tuna haja ya kufanya extension ya muda wa Urais basi tukae tuzungumze.

Lakini kwa Rais Magufuli kashatuambia hataki na tunamkwaza.

Then we should stop...kama ambavyo Katibu Mkuu alisema "Amefunga" huu mjadala kwa Rais Magufuli.

Kama box la kura haliheshimiwi na yeye akiwa kinara wa hilo, usitegemee kupata matakwa halisi ya wananchi, zaidi ya matakwa ya kundi linalomtegemea ili kuboresha maisha yao.
 
Tujifunze kukubali na kuheshimu mawazo ya wengine hata kama mnatofautiana.

Hili la kufuta mihula ya urais, angalia mimi nilianza kushauri lini...
Wanabodi hili ni bandiko la 2015

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Wanabodi, kwanza angalieni tarehe ya bandiko hili, kisha angalia hoja No. 4, 5, 6, 7 na 8 za bandiko hili, kisha sikiliza kilichozungumzwa jana Bungeni Dodoma kuhusu hoja hii.

P

Paskali hakuna mtu anakataa utabiri au maoni yako. Lakini huko kukaa kuwe kwa ridhaa ya wananchi, na sio kwa kunajisi box la kura. Ni nani asiyejua kinachoendelea kwenye chaguzi zetu? Huenda utabiri wako uliongozwa kwa kufahamu mwenendo wake kwenye kuchezea box la kura, na sio kinyume chake.

Nakuhakikishia iwapo kutakuwa na uchaguzi huru na haki, yeye binafsi na chama chake hawana uwezo tena wa kushinda zaidi ya 50% kihalali. Sababu kubwa ni kuwa zama zimebadilika, na kizazi hiki sio cha ccm. Hiyo ni kanuni ya maisha, kwamba watu huchoka kitu baada ya muda fulani au kizazi fulani. Hata hizi figisu unazoziona hivi sasa ili ccm iendelee kukaa madarakani, ni kwa kwakuwa ccm inalazimisha kuvunja kanuni ya maisha. Sio kwamba ccm haijafanya kitu, bali kizazi ndio sio cha ccm tena.
 
Wanabodi...

Niwasabahi kwa kuwatakia asubuhi njema na natumai mko fresh kabisa.
Kabla sijaenda mbali Mwalimu wangu wa Sheria pale chuo kikuu aliwahi nifundisha kuhusu "ku-declare interest", naomba ifahamike kwamba mimi ni Mwanachama Hai wa Chama Cha Mapinduzi na Mzalendo nambari moja kwa Taifa hili.

Naomba Wana CCM na Watanzania tuwekane sawa kwenye hili sababu linatuhusu wote, nashangaa sana wasomi , wanazuoni na wanachama wa CCM tunafanya kama hatukumbuki, au tumepoteza kumbukumbu sijui .

Mhe Kessy, mbunge wa Nkasi juzi alinukuliwa na vyombo vya habari Bungeni akisema Rais Magufuli aongezewe muda " Atake Asitake", akanukuliwa pia akisema "Asiachiwe huyu, alazimishwe" akaendelea kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye janga la Corona mataifa yote ya nnje yamemkubali.

Na Mhe Spika Ndugai akajibu, ngoja twende kwenye uchaguzi mkuu, tukirudi Mhe Kessy utaleta hili hili Azimio la Rais kuongezewa muda na naamini wote tutarudi, na lazima tutamuongezea muda."

Kiukweli, Binafsi nimesikitishwa sana na hii kauli ya Mhe Kessy kwa hoja zifuatazo,

Mosi, ikumbukwe tarehe 14 januari 2018, Rais Magufuli alikutana Ikulu na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndugu Humprey Polepole na hiki ndiko Rais John Magufuli amesema ANASIKITISHWA na HAFURAISHWI na mjadala ambao unaoendelea wa rais kuongezewa kipindi cha kutumikia kutoka miaka mitano hadi saba.

Amesema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na Katiba ya nchi na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hii ni kufuatia Mhe Juma Nkamia mbunge wa Chemba kuibua Hoja ya Kuongezewa Muda wa Urais toka Mitano mpaka saba.

Pia Rais Magufuli alitaka wananchi KUPUUZA mjadala huo.

Ndugu Humprey Polepole nae wakati anaongea baada ya kutoka Kwenye Mkutano na Rais alisema Magufuli aliwataka wana CCM na umma wa Watanzania kutokubali kuyumbishwa ama kupotoshwa na mambo yasiyokuwa ya msingi, badala yake wajielekeze katika ajenda muhimu ya kujenga uchumi na kutekeleza Ilani ya CCM iliyonadiwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Kupitia kitabu chake cha "Uongozi Bora ba Hatima ya Nchi yetu", Mwalimu Nyerere alishatoa Angalizo kuhusu kuongeza kipindi cha Urais , namnukuu Mwalimu na anaendelea kuonya tena, "Suala hili lilikwishakuamuliwa zamani, na sasa ni sehemu ya Katiba yetu. Uamuzi huo inafaa uheshimiwe. Rais Mwinyi ndiye Rais wa kwanza kuchaguliwa kwa mujibu wa katiba hiyo. Yeye akisema kuwa vipindi viwili havitoshi, na akataka viwe vitatu; Rais wa pili atasema vipindi vitatu havitoshi, na atataka viwe vinne na kadhalika mpaka tufikie Ngwazi (rais wa milele) wa Tanzania," (uk.10).

Kwa hii kauli ya Mwalimu Nyerere wabunge tunakwama wapi?

Ina mana hatujui tunachokisema?

Je, ni kweli hatuna uhakika wa kurudi kwenye Bunge la 12 kwa hiyo tunatamka chochote huku mwishoni ili tupate "Political Empathy"?

Wana CCM wenzangu, lazima ifike mahali tukubaliane na msemo wetu tunaosema kila siku " TUNASIMAMA NA RAIS MAGUFULI,", basi hata kwa hili analosema "Hafikirii hata siku moja kuongeza siku hata moja baada ya kipindi chake kuisha,", " Rais akasema ANAKWAZWA na hafuraishwi na mjadala wa kuongezwa muhula wa uongozi"

Rais Magufuli amenukuliwa mara mbili tofauti akiwajibu wale wote wanaomlazimisha aongeze muda, na Rais wetu hajazunguka kimaneno, kasema plain black and white "SITOONGEZA MUDA HATA WA SIKU MOJA BAADA YA KIPINDI CHANGU KUISHA", nakumbuka hii ilikua disemba 2019 alikua anatoa hotuba mahali.

Katibu Mkuu wa CCM ndugu Dr Bashiru nae alipokua pale Chemba akimtumbua Katibu wa CCM mkoani Chemba kwa kukosa Kujiongeza kuiva na viongozi wenzake alilisemea hili jambo, akasema " Rais Magufuli atamaliza miaka yake kumi, hiyo tutampa ridhaa badala ya Hapo atafata utaratibu wetu wa kikatiba wa kuachiana vijiti"...

Hivi wabunge wanataka KUTUAMINISHA wana nguvu zaidi ya wananchi waliowachagua?

Hivi Spika wa bunge Ndugu Ndugai anaposema BUNGE TUTAMUONGEZEA muda anaelewa kweli?

Hivi Spika hakumbuki TUME YA JAJI NYALALI(NYALALI'S COMISSION), miaka ya 1998 9 na ile kazi ya kukusanya maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba?

Kwamba lazima wanachi wafanye kitu tunaita Referendum .,

Kukawa kuna kitu kinapita mtaani kwa jina la "WHITE PAPER"? Chenye lengo la kutaka kujua maoni ya watanzania kuhusu jambo husika la kurekebisha kwenye katiba yetu.

Kwa nini Spika useme " TUTAMUONGEZEA MUDA" maana yake unasahau sisi wananchi wa kawaida na nguvu yetu kwenye maamuzi.

Hivi Mhe Kessy kweli anataka tuamini hajasikia maneno ya Katibu Mkuu wetu Dr Bashiru kuhusu mjadala wa ukomo wa Urais.?, Katibu Mkuu alitamka ameufunga Rasmi disemba 2019 au Mhe Kessy ana nguvu zaidi ya Dr Bashiru??, kitu akishasema Katibu Mkuu wa Chama wewe mwanachama wa kawaida una comply nacho..Hauna haja ya kuropoka tena maana Msimamo wa Katibu Mkuu ni msimamo wa Chama.

Waziri Kabudi nae alishatolea ufafanuzi hili jambo wakati akiwa Katiba na Sheria , akasema vipindi vya Urais ni VIWILI tu vyenye miaka Kumi Kumi ndanu yake.

Simlaumu Waziri Mkuu mstaafu Ndugu Mizengo Pinda siku ile aliposema "Anatamani Rais Magufuli aongezewe muda wa Urais"..

Mhe Pinda alikua anatoa maoni yake kama mtanzania wa kawaida, kama mimi na wewe, lakini baada ya Rais Magufuli kutoa msimamo wake kuhusu hilo ombi , binafsi sijamsikia Tena ndugu Pinda anakuja kwenye media na kuanza kumbembeleza Rais.

Hii sio mara ya kwanza kwa watu kutoa maoni, hata wakati Rais Kikwete anamalizia uongozi wake 2009 kulikua na watu wakimtaka Rais Mstaafu Kikwete aongeze muda wa kukaa kwenye Urais..

Waziri wa katiba na sheria mhe Chikawe wakati huo akatoa msimamo kwamba Rais Mstaafu Kikwete hatoongeza tena muda wa Urais.

Narudia tena, Ndugu Juma Nkamia alikua amepeleka hoja yake binafsi ya kuongeza Kipindi cha Urais toka miaka mitano mpaka saba lakini baadae aliitoa hii hoja yake akasema " Ameshauriwa na viongozi wake wa juu wa Chama cha Mapunduzi aitoe na asiendelee na hoja yake japo Nkamia aliileta hoja yake mara mbili lakini alivyoambiwa aitoe, ALIITOA", na hii inaitwa UTII kwa viongozi wako wa CHAMA.

Pia Mhe Mizengo Pinda hakuendelea na hoja yake mara baada ya msimamo wa Rais Magufuli, kwa nini Mhe Kessy anakomaa?, unaweza kuona "countance" (mwonekano) wa Mhe kessy pale Spika Ndugai alipomwambia "Utarudi kwenye Bunge lijalo la 12 na utakua ni wewe mletaji wa Azimio hili".

Ukiisoma Body Language ya Mhe Kessy unaona kabisa anafurahi kusikia atarudi kwenye Bunge lijalo!

Anafurahi kuambiwa atakua mletaji hoja ya Azimio la Bunge kuhusu Kuongeza ukomo wa Kipindi cha Urais!.

Kifupi mhe Kessy anataka kurudi bungeni, which is okay lakini rudi bungeni with your own expense!, sio unarudi bungeni with expense' of the Nation.

Leo kila mbunge atake Katiba ibadilishwe ili apate debe/upendeleo wa kurudi bungeni toka kwenye Kamati Kuu ya CCM si kila siku tutakua tunabadilisha katiba yetu .

Nkamia alikua anataka ku-copy paste Katiba ya Rwanda ambayo toka 1994 ilikua inasema Kipindi (tenure) ya uongozi wa Urais ni miaka saba saba , lakini Rwanda wamefanya mabadiliko kwenye Katiba yao na kuanzia Mwaka 2024 Rwanda wanarudi kwenye tenure ya miaka mitano mitano, , Rais akae miaka kumi tu madarakani ampishe Mwenzie.

Kifupi Rwanda wanatamani kuwa kama sisi lakini Sisi ndo kwanza Tunataka Rais Aongezewe miaka 10 zaidi kutoka 2025 yaani Rais Magufuli atumikie mpaka 2035.

Mi nampenda sana Rais wangu kwa kazi alizofanya na anazoendelea kufanya.

Naipenda spirit yake ya kujitegemea na "will power" yake kwenye kufanya mambo na maamuzi kama Taifa hakuna sehemu nam-doubt Rais Magufuli.

Ni will-power yake na roho yake ya kizalendo kwa Taifa hili imetufikisha hapa tulipo, maofisi ya serikali yana nidhamu, wanyonge wanasikilizwa na kupewa HAKI.

Rais Magufuli amefanya Maamuzi ya kipekee sana kwenye kushughulikia suala la Corona, ametujengea Roho ya kipekee kwenye Kipindi hiki Taifa limepitia kwenye Huu ugonjwa.

Rais Magufuli kawajibisha wakuu wa mikoa, wakuu wa idara mbalimbali za serikali pale Rais anapobaini mambo hayaendi!...unakumbuka kuvunjika kwa Daraja pale Morogoro?, unakumbuka Waziri Kamwele alivyochanwa Live kwa kutomuajibisha Meneja wa TANROADS wa mkoa?

Unakumbuka Rais alivyowachana Magereza na TBA pale Ukonga kwenye mradi wa nyumba za jeshi la magereza?

Na akawaambia live atawaletea Kamishina wa MAGEREZA toka JWTZ?

Unakumbuka JKT walivyoendeleza ujenzi wa zile Nyumba na Ukaisha?

Hii ni mifano michache ya Rais Magufuli, bado uthubutu wake wa Kufufua Mashirika ya UMMA kama ATCL .

Sitozungumzia ujenzi wa madaraja, barabara, vituo vya Afya kila kata, Elimu Bure, Mikopo ya Elimu ya Juu n.k maana hivyo kila mtu anavizungumzia.

Binafsi naungana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ndugu Dr Bashiru , Naungana na Rais Magufuli na Msimamo wa Chama kwa Pamoja Kumruhusu Rais Magufuli apate kipindi cha Pili cha Uongozi kwa miaka mingine mitano mpaka 2025.

Vivaa Magufuli....

Mzee Pius Msekwa alikua mmoja wa wazee walioshughulikia mabadiliko anuwai' yaliyokua yanafanyika kwenye Katiba ya Tanzania toka ile ya 1921 .

Anajua tulikotoka na mabadiliko yote tuliyofanya zaidi ya mabadiliko 12 na alisema wazi kabisa "Toka enzi za Mwalimu tulishazungumzia kuhusu kuongeza muda wa Urais".

Wana CCM na hasa vijana wenzangu wa UVCCM tusimkwaze Mhe mwenyekiti wetu Dr Magufuli, kashasema HAPENDEZWI, ANASIKITISHWA na HAFURAISHWI na hizi kauli zetu huku kwenye mitandao tunapiga kelele za kuongeza muda wa Urais.

Rais Magufuli nae ana maisha yake ya kifamilia, tumuache apumzike na tumshukuru kwa Mchango wake mkubwa kwenye Taifa hili la Tanzania na alishasema Mara Nyingi " Urais ni KAZI NGUMU".

Alishasema analala na mafaili pale IKULU wakati mwingine tafadhali tuheshimu maamuzi yake.

Tuachane na wanasiasa walio tayari kusema lolote mradi mradi tu warudi bungeni hata ikibidi kurudi "in expense" (kwa gharama) ya kubadilisha katiba....

Laiti Rais mstaafu Jakaya Kikwete angesema aongeze muda basi leo hii tusingempata Rais Magufuli, haijalishi kapatikanaje lakini kapatikana na kwa Miaka hii mitano kalinyanyua hili Taifa akiwa na Timu yake aliyoichagua na Kuiamini.

Sasa akisimama Mbunge kama Mhe Kessy akasema "Haoni mtu mwingine wa kutuvusha baada ya Magufuli", mi namshangaa Mhe kessy..sijui alikua anawaza nini.

Nafunga kwa Maneno ya Rais Magufuli anasema " MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU"...

Na ameshasema zaidi ya mara moja, na viongozi wa Chama na serikali wameshaongea kuhusu kuongeza muda basi TUSIMKWAZE mpendwa wetu Rais Magufuli.

Tutashinda Uchaguzi huu Mkuu wa oktoba na Chaguzi zingine Miaka mingine sababu tunaaminika na wananchi.

Ndugu Humprey Polepole aliulizwa siku swali kwenye redio unadhani siku CCM ikiondoka madarakani tatizo litakua nini?

Na napenda jibu alilotoa, "Kwa sasa CCM haitotoka madarakani kwa mabadiliko haya tuliyofanya", Lakini huko baadae CCM ikianza kudharau wananchi basi itaanguka na kuondoka madarakani"

Tueshimu Msimamo wa Rais Magufuli kuhusu kutokuongeza muda wa Urais na tumshukuru Kwanza yeye na serikali yake kwa kazi nzuri waliyofanya ndani ya miaka mitano na tusimame nae kwenye hii miaka mingine mitano mpaka 2025.

Nimeona Niliseme hili wazi na tafadhali moderators msiunganishe huu uzi na nyuzi zingine maana haufanani na nyuzi zingine maana hamkawii kunikwaza asubuhi

"MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU MBARIKI RAIS MAGUFULI NA SERIKALI YAKE YA AWAMU YA TANO".

NB: Kwa maoni au ushauri usisite kumuandikia muandishi kwenye barua pepe : godjohn8@gmail.com
Kwa Mara ya kwanza nampongeza mwanaccm .... kiukweli naweza sema huenda wewe ni mwanachama wa zamani sana ambaye bado una upeo mkubwa sana wa kuona Mambo ..Ila Kama mh Rais hataki haya basi akiwa anavunja bunge naomba awakemee wale wapuuzi wote wakiongozwa n Ndugai ili iwe fundisho
 
Nadhani kuna baraka kutoka muhusika mwenyewe kwenye hizi nia OVU.

Angekua anakereka angetoka hadharani akafoka na kukemea pamoja na kutishia.

Tusingesikia huu ujinga wa akina Ndugai na Keso cjui nani nani hko.
 
Too late,Bunge la CCM limezika demokrasia.Kuna haja gani ya kupiga kura?
 
Safi sana!
 
Back
Top Bottom