Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,558
- 113,751
Wanabodi,
Baada ya vyama vya upinzani kupata ushindi wa matumaini na CCM kuporwa mitaa na vijiji kadhaa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kumefufua matumaini ya uwezekano wa CCM kushindwa jumla katika uchaguzi mkuu ujao, hivyo kuweka possibility ya CCM kuwa ni chama cha upinzani Tanzania ama baada ya 2015 au 2020!.
Wengi tunajua kuwa CCM huwa inashinda chaguzi mbalimbali, sio tuu kwa sababu inapendwa, au imewatendea mema Watanzania, bali katika baadhi ya maeneo CCM inapendwa mpaka basi, huku baadhi ya maeneo imechokwa!, ila bado huwa inashinda kwa mbinu mbali, ambazo some ni hooks & crooks!, kunakopelekea wengi wa wapiga kura kujikuta, hata wafanye nini, CCM ni lazima tuu itashinda!, hali iliyopelekea watu kujikatia tamaa na any possibility ya CCM kushindwa, hivyo kuamua kuliko kupoteza muda wao kupiga kura, bora wajilalie tuu majumbani mwao, ndio maana tumeshuhudia watu milioni 22 wakijiandikisha, kisha ni watu milioni 8 tuu wakijitokeza!, hivyo msindi wa urais kushinda kwa kura milioni 5 tuu, ambayo ni asilimia 9% tuu ya watu milioni 45!.
Pia kuna maeneo CCM imechokwa ila bado inaendelea kushinda kwa mazoea tuu, watu hawana elimu ya uraia ya kutosha, hivyo kuamini kuwa chama kinachopaswa kuongoza Tanzania milele ni Chama cha Mapinduzi CCM!.
Kwa vile CCM imezoea kushinda kwa mbinu, kuna mwanajf alisema humu, kuwa hufikia wakati, hata "the greatest magicians runs out of tricks!" hivyo CCM waliishiwa mbinu, wakashindwa huko walikoshindwa!.
Wengi wanajipa matumaini kuwa kushindwa huko, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM!, lakini inawezakana pia isiwe hivyo, inawezekana sasa ni faru amejeruhiwa!, faru ni mnyama mpole sana, ila akijeruhiwa, atakuwa ni myama wa hatari sana, huisimamisha ile pembe yake na kukimbia hovyo chochote atakachokutana nacho mbele yake, anatoboa na pembe hiyo!.
Hivyyo kuna uwezekano sasa CCM ikaja na mbinu mpya za faru aliyejeruhiwa hivyo uchaguzi wa 2015 ikakomba kila kilicho mbele yake!, jee unajua ni kwa nini, CCM lazima ilazimishe kushinda ili kubakia madarakani?!.
Nimekuwa inspired kuandika uzi huu na thread ya mwana jf huyu
Sipati picha bendera za Chadema kwenye majengo ya CCM!.
Wakati wa chama kimoja, CCM ilichangiwa kwa lazima na wafanyakazi wote!, ile siku tunaanza vyama vingi, kiuhaki na kiuhalali, ilibidi mali zote CCM iliyomiliki kwa michango ya lazima, zilipaswa kurudishwa serikali, zikiwemo zile mali CCM iliyozivuna kama chama dola, mfano uwanja wa CCM, Kirumba, ukumbi wa CCM, Kizota, Jengo la Makao Makuu ya CCM, Dodoma, Jengo la Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba, na mali zote za jumuiya za CCM, likiwemo jengo la Umoja wa Vijana, lile jengo la Airtel etc, yalipaswa kurudishwa serikalini, yaani kutaifishwa kuwa mali ya umma!.
Kitendo cha CCM kuendelea kuzishikilia hizo mali, ni wizi, ujambazi na uharamia kwa jasho la Watanzania!. Nilishauri, kama kweli itakuja kufika siku, CCM ikawa ni chama cha upinzani, huo ndio utakuwa mwisho wa CCM, milele, maana kazi ya kwanza ya chama kingine kikitawala, itakuwa ni kuipoka, na kuipurura CCM, malizo zote ilizojitwalia kwa uporaji (looting), na kuzigeuza ni mali ya umma!.
CCM ikiishaporwa kila kitu!, kamwe haiwezi kuamka tena!, that will be the end of it jumla, ndio maana kwenye chaguzi mbali mbali CCM does all it can to remain in power, maana naamini hili CCM hili wanalijua, hivyo nawaombeni sana msiendelee kuishangaa CCM inapotumia all the means, by hooks and crooks to remain in power, ni pamoja the fear of unknown!, on what will happen, if CCM looses, ndio maana mnaona hakuna any preparations kwa serikali na vyombo vya dola, kuitumikia serikali ya chama kingine!.
Kama ilivyo kanuni ya the law of the jungle ni "struggle for existence, survival for the fittest", bila kujali ni mbinu gani zitatumika kushinda uchaguzi, kwa sababu mwisho wa siku, uhalali wa mshindi, unapatikana kwa "the end, justify the means!", "The winner takes it all!, the looser standing small!.
Mnaondani kuwa baada ya kipigo hiki cha serikali za mitaa, CCM will just sit and watch!, they might be wrong!.
Tangu tuanze mfumo wa vyama vingi, kuna baadhi ya maeneo ambayo watu wake wanajitambua, yamekuwa yakiwachagua wapinzani, maeneo hayo ni pamoja na jimbo la Moshi mjini, Arusha Mjini na Jimbo la Kigoma Mjini, tangu kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi, majimbo haya yamekuwa ni chachu ya upinzani, hivyo huku ndiko CCM itaweka concentration kubwa ya mbinu na crooks kwasababu kutumia hooks kwa watu wanaojitambua, hakuwezi kuzaa matunda. Hivyo majimbo stronghold za upinzani jiandaeni kivita kuzuia hizo crooks vinginevyo majimbo haya yatarejeshwa CCM.
Namalizia kwa swali, kama CCM imekuwa ikitumia mbinu za Hooks & Crooks kushinda chaguzi mbali mbali, ili kuhakikisha inabakia madarakani, kwa sababu inajua ikishindwa, ndio itakufa jumla, jee unadhani CCM itakubali kujikalia na kujiangalia tuu huku ikijifia kibudu, au itaendelea kutawala hadi milele na milele ?.
Jumapili Njema,
Pasco.

Baada ya kushinda vijiji vingi katika jimbo la Moshi vijijini changamoto mpya imezuka. Majengo mengi ambayo ofisi za vijiji zipo ni ofisi pia za CCM.
Katika vijiji vya Okaseni na Kimanganuni ofisi za vijiji zilijengwa wakati wa chama kimoja, na kwa kuwa CCM ndo walikuwa viongozi wa serikali za mtaa hii haiukuwa changamoo.
Sasa hatujui itakuwaje kwa kuwa CHADEMA nao wamepandisha bendera zao kwenye haya majengo, hivyo CCM sasa hawana tena ofisi katika vijiji hivi ambayo wameichagua CHADEMA 100%.