CCM kutosimamisha mgombea Arusha Mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kutosimamisha mgombea Arusha Mjini

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Ntemi Kazwile, Apr 5, 2012.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kuna uwezekano mkubwa kuwa CCM hawatasimamisha mgombea Arusha Mjini.
  Wanajua kutakuwa na kura za hasira kwa jinsi kesi ilivyoendeshwa na namna hukumu ilivyotolewa.
  Pili wanajua kuwa chama hakina tena mvuto kwa wananchi hasa hasa mijini na kama uchaguzi utarudiwa yatatokea yale yale ya Arumeru Mashariki.

  Tatu, katika CCM ya sasa hakuna tena kada anayeamika kwa wananchi, Nkapa kachemsha na sidhani yuko tayari kudhalilishwa mara ya pili ndani ya miezi mitatu, Six amejaribu Kirumba kachemsha, Mama Kilango kachemsha Kiwira(vijijini), sijui sasa watamtuma nani akamsaidie mgombea wao. Kwa upande mwingine CHADEMA hata wakinituma mimi, ambaya hata sina cheo, nitawaongoza kushinda.

  Kama wakifanya kosa wakasimamisha mgombea, na kulingana na upepo wa kisiasa wa sasa watapoteza tena uchaguzi, watakuwa wameamua rasimi kurudisha serikali mikononi mwa Wananchi kwani 2015 itakuwa ni kujumlisha kura tu!

  Naona kuna uwezekano mkubwa kimada wa sisiyemu anaweza kuombwa asimamishe mgombea ambaye magamba watamuunga mkono nyuma ya pazia na kujiepusha na aibu ya kushindwa mara mbili ndani ya miezi mitatu.

  Naomba kuwasilisha
   
 2. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  Acha mawazo hayo wewe ccm wanaweza kushinda kama uchaguzi utafanyika kataka ofisi ndogo za lumumba na kama jk atagombea
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kusimamisha mgombea watamsimamisha, we sema hakuna mtu atakayeukubali umeneja wa kampeni.
  Hakuma mtu anataka kupata aibu
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,796
  Likes Received: 36,817
  Trophy Points: 280
  "CCM wanaruka sarakasi na taulo." By dmayola(Jf member)
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hiyo;

  Nilipofuatilia kesi ya Lema yote, sikuona ushahidi wowote wa kufanya ubunge huo utenguliwa. Kwa vile gharama za uchaguzi huwa ni kubwa sana kwa taifa na vile vile kuvuliwa kwa mbunge kunakosesha wananchi wake uwakilishi bungeni, nilitegemea mahakama za uchaguzi ziwe zinafanya maamuzi ya busara sana kuangalia iwapo madai yaliyoko mbele yake yangeweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi kweli kweli kweli badala ya visababu uchwara ambavyo haviwezi kubadilisha matokeo. Hata tume ya uchaguzi wakati wakitangaza kumtawaza Kikwete, walisema kuwa kasoro zilizokuwa zimonekana katika uchaguzi hule zisingeweza kubadili matokeao, na hilo ndilo linalotakiwa kuwa linaangaliwa. Sasa hivi visababu uchwara vya ".... niliambiwa kuwa alisema hivi.." siyo sababu za msingi ambazo zingeweza kubadili matokeo yale. Nina imani kuwa kesi hii ikisikilizwa na mahakimu wasio kuwa na upendelea wataitupilia mbali.
   
 6. luhala

  luhala JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 412
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kinyume kabisa ya baadhi ya wana CCM wanavyotazamia, hukumu hii inaweza kuiharibia zaidi CCM na kuuongeza umaarufu wa CHADEMA Arusha na nchi nzima. Tetesi za mafisadi kupenyeza rupia ili Lema ashindwe zilishaenea ndani na nje ya nchi wiki kadhaa kabla na wengi hawakushangazwa sana na uamuzi wa Jaji pamoja na kwamba ulifanywa kisiasa zaidi.
  Uchaguzi mpya Arusha utaipa fursa CHADEMA ya kuuhamasisha umma wa Tanzania nzima kuikataa CCM katika uchaguzi huo na chaguzi nyingine zitakazojitokeza, na kwa jinsi ilivyo kushindwa tena Arusha kutaashiria mwisho wa utawala mkongwe wa CCM. Sasa CCM wanabakiwa na machaguo mawili tu; wajitose, wasambaratishwe na wapoteze kabisa umaarufu wao nchini au watafute sababu za kujitoa ili wasiaibike zaidi na wawaache wananchi na mashaka kama wanafaa au la.
  Nasema tena, hakuna uwezekano wa CCM kulitwaa jimbo la Arusha mjini hata
  wakimweka nani kwani CHADEMA tayari wana turufu katika kampeni zozote za jimbo hilo kutokana na mauaji ya kijinga yaliyofanywa na Polisi mjini humo kwa maelekezo toka juu na ambayo hadi leo hakuna Tume huru iliyochunguza na kuchukua hatua thabiti juu ya hilo.
   
 7. r

  rimoy Member

  #7
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm imefikia muda wa kusambaratika, na Mungu amesikia sala za watu wake, Sasa nio wakati muafaka tukaizike ccm, Parapanda italia x2
   
 8. T

  Topical JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ikishinda mtafanyaje? nauliza tu

  Mbona chadema mnaonekana madikteta; heshimuni mahakama

  Wananchi wanatakiwa kuelimishwa madhara ya chadema kwa taifa..
   
 9. O

  Original JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nina wasiwasi mkubwa sana kama mwenyekiti wa CCM ana watu makini wa kumshauri.
   
 10. Linyakalumbi

  Linyakalumbi JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Topical ni mmoja wapo!!!!!
   
 11. mbwigule

  mbwigule JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Endapo CHADEMA watakata rufaa kwa kesi hii ushindi uko wazi kwani hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Sheria anaweza kubaini kasoro zilizoko katika hukumu hii. Ndiyo maana wengi wameiita hukumu "Ya kisiasa" Tatizo lililopo ni moja, nalo ni urasimu unaotawala sekta ya sheria unaweza kuchelewesha kesi hii hadi 2014 hivyo kupoteza maana kabisa. Binafsi nashauri CHADEMA wasikate rufaa bali wakubali ili jimbo litangazwe wazi, uitishwe uchaguzi mwingine ambapo CCM itajeruhiwa zaidi katika kampeni na kupoteza umaarufu nchi nzima. Ni katika ushiriki wa kampeni kama hizi CHADEMA imefikia umaarufu inaojivunia na CCM imepoteza umaarufu inaoujutia.

   
 12. k

  kagame Senior Member

  #12
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 6, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  bongolala utaamshwa kaburini!! Vichwa vingine maji kweli kweli......... Napita tu.
   
 13. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi unazungumzia CCM ya magamba? au kuna CCM nyingine? kama ni ccm ya magamba lazima wasimamishe mgombea, hawana aibu hao usoni kubaka haki za raia
   
 14. Mlingwa

  Mlingwa JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  TUMENENA VYEMA SANA, LAKINI akiri ya magamba ni sawa na sikio la kufa...
  Naoma nimnukuu mhadhiri mmoja leo katika jicho letu ndani ya habari star tv (live) alisema
  "CCM Kimezeeka, kinataka kufanya kama chama kipya, hakiweze maana akiri yake imeshazeeka, nakisipositaafu, basi wananchi watakistaafisha"
   
 15. broken ages

  broken ages Senior Member

  #15
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 160
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  kwa hiyo mnatoa ushauri gani kwa ccm katika hili? mimi naishauri serikali na ccm kulitazama kwa makini
  na kuangalia upepo wapi unaelekea kwa kasi kubwa ili kunusuru kutumia mamilioni ya wananchi katika uchaguzi huu basi hao majaji wasikiliza rufaa itakayokatwa na chadema nao waamue katika namna ambayo itaepusha matumizi yasiyokuwa na lazima ili basi hata kama ccm tunaye mgombea tunayemwamini tumweke kama karata yetu ya ushindi tutakayoitumia ktk uchaguzi ujao wa 201.na hapo hapatakuwa na lawama ktk gharama za uchaguzi maana hili ni muhimu na wala hata wapiga kura hatapiga kura za kukomoa kwamba wanaiadhibu ccm lakini kwa sasa katika hili inaonyesha zitapigwa kura za kwamba ccm inapewa adhabu...
   
 16. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  Hongera kwa tathmini nzuri, namna nyingine wanayoweza kufanya ni kufanya kila hila kumuengua mgombea wa CHADEMA kwa namna watakayoona inafaa, haya hivyo hii pia haitawaacha salama endapo CDM wataamua kumuunga mkono mgombea mwingine wa chama cha siasa, chochote hata CHAUSTA, SAU, APP Maendeleo na akishinda watakuwa wameaibishwa kuliko kumwacha Lema ashinde rufaa aliyofungua mahakama ya rufaa.

  Kama kuna mtu ndani anayeweza kuiona aibu hii mapema na awashauri wasiingilie kesi mahakamani itakayolazimisha uchaguzi kurudiwa. Wakicheza mchezo wa kupoteza muda hadi miaka mitano iishe bila Arusha kuwa na mwakilishi, itawaghalimu zaidi kwani wananchi watawaadhibu kwa kura za hasira mwaka 2015!
   
 17. U

  Userne JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 895
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umeshadhurika!
  baba anakuchukulia mkeo wee endelea kumheshimu tu!
   
 18. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  I see ngoja tuone! lakini nijuavyo walichotaka kimekuwa! walitaka a town wasiwe na mbunge mpaka 2015! hiyo rufaa itapigwa kalenda mpaka katiba nzee itakapo anza
   
 19. M

  Murrah Senior Member

  #19
  Apr 15, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 20. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,659
  Likes Received: 21,876
  Trophy Points: 280
  Mungi,hivi katika CCM kuna mtu ana aibu? Umeneja kila mtu katika CCM atautaka kwani unaposho hilo swala la aibu kwao ni msamiati mpya
   
Loading...