CCM kumtenga Makonda inajiharibia

Alikuwa muovu na sasa analipwa uovu wake
 
Yamekuwa hayo! Lakini mbona mlifurahi na kumzawadia ukuu wa wilaya baada ya kumpiga kofi Jaji Warioba? Ccm ni kokoro kweli!
Makonda alikuwa wakati ule anatumiwa na Samuel Sitta na Kikwete kuvuruga majadiliano ya Katiba; kwani walikuwa hawataki ipite!! Hata hivi sasa Samia sio kikwazo cha kupata katiba mpya; Kikwete ameiteka CCM baada ya Mzee mangulla kustaafu na yeye ndiyo kikwazo cha kupata katiba mpya kwani madhambi yake yanaweza kufumuka!!! Ndio maana hivi sasa kwavile Samia ni weak anatumia mwanya huo kuwarudisha watu wake aliokuwa nao awamu ya nne kwenye uongozi kwenye sehemu mbali mbali na ndiyo hao wakina SOPHIA SIMBA!!!
 
Jambazi anapokuja kumuombea jambazi mwenzake apate huruma ya Kinga!
 
Hakuna kitu kama hicho! My word: accountability and strong institutions.
 
Makonda aliumiza hadi KM wa CCM hadharani akimfokea kama mtoto leo aonewe huruma? Kwa kuwa anatofauti gani na wanaccm wengine? Huyu hadi PM alimdhrau achilia mbali Bi. Mdashi

Ngoja tusome namba wote kwanza ili nzi wengine wajifunze heshima
Makonda ni pimbi kabisa!
 
Umesema kweli tupu!
 
Uhuni huo ndiyo umefanya wabunge wengi wa CCM wawepo bungeni. Ndiyo uliowapa madiwani na kushika local goverment nchi nzima. Kifupi inaishi kwa mtindo hui. Wakianza kunyosheana vidole wataanguka.
Eti ccm ilishinda serikali za mitaa zote na uchafuzi Mkuu wabunge wote, takataka hizi! Tuna ushahidi wa mwendazake akiamuru mpinzani asitangazwe hata akishinda. Stupidity! Kuvunja katiba!
 
Unashangaa ya ccm ! uliza Pengo au Bakwata wako wapi ?
 
Sijui ni nani ila ana ushawishi hadi walimpa ukuu wa wilaya na mkoa.

Ukuu wa walaya alipewa na Magufuli na sio CCM . Kwa ccm makonda is a nobody. Hana ushawishi ndio maana aliliwa kichwa Kigamboni.
 
Makonda ni Sabaya mtarajiwa, yaan ni swala la muda tu. Na kwa wanaomjua wanasema ukiunganisha kina Sabaya kadhaa ndo unapata Makonda mmoja. Au vile Sabaya alivyo basi ni mwanafunzi tu kwenye shule ambayo Mwalimu Mkuu ni Makonda.

Mtu wa aina hii ukianza kijihusisha nae unaweza na wewe ukaunganishiwa huko huko so CCM wenzie wako makini nae sana.
 
Ikasimame na Sabaya pia.
 
Tatizo moja la Makonda ni kuwa attention seeker, alipokwenda Moshi kuzindua ukarabati wa magari ya polisi alitembea na ving’ora msafara ukiongozwa na polisi.

Hii attention seeking ndiyo ilimfanya aumize watu kwa kujijenga kwa mkubwa wake. Aumize watu ili aendeshe magari mazuri, nk.
 
CCM kuwa na nguvu haitegemei wananchi bali ushirikiano wao kwa wao na mshikamano wao.
 
Yaani unahamasisha CCM wawalinde watu waovu? Je, CCM ni chama cha uovu? CCM ikitaka iaminike kwa wananvhi tena, ni lazima ijitenge waovu wote kama akina Makonda, Sabaya, Kingai, Goodluck, Jumanne, Mahita, Happy, n.k. Ni hatari kubwa cha cha siasa kujishikamanisha na majambazi, wauaji, watekaji watu na waporaji.
 
Makonda aliumiza hadi KM wa CCM hadharani akimfokea kama mtoto leo aonewe huruma? Kwa kuwa anatofauti gani na wanaccm wengine? Huyu hadi PM alimdhrau achilia mbali Bi. Mdashi

Ngoja tusome namba wote kwanza ili nzi wengine wajifunze heshima
CCM huwa hawajifunzi mkuu. Utawala huu ukipita, unaokuja nao itawavurumsha na kuwanyanyasa hawa waliopo madarakani sasa. Na kwa kuwa wengi ni mazuzu, chawa wanaoshangilia leo na kuusifu huu utawala wa awamu ya sita watauponda na kuunanga kama hawajawahi kuusifu. C.f watu kama johnthebaptist, akina Le Mutuz nk
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…