CCM kumng’oa Mukama; Wabunge walioipinga bajeti kukiona | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kumng’oa Mukama; Wabunge walioipinga bajeti kukiona

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 24, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  MKAKATI wa kumng'oa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, anayedaiwa kushindwa kukiendesha chama umeshika kasi, Tanzania Daima Jumapili limebaini.

  Mbali na Mukama, baadhi ya wabunge pia wanataka wenzao waliogoma kuipitisha bajeti ya serikali nao kushughulikiwa kwa kukisaliti chama.

  Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa baadhi ya wabunge na wanachama wanataka Mukama aachie ngazi au afukuzwe.


  Duru za kisiasa kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa matumaini ya wanachama wengi wakiwamo vigogo wa chama hicho waliyokuwa nayo kwa Mukama wakati anaingia madarakani yamefifia.


  Katibu mkuu huyo aliyeingia madarakani kwa mbwembwe ndani ya CCM miaka miwili iliyopita, anadaiwa kushindwa kabisa kukijenga chama kama ilivyotarajiwa na badala yake ametengeneza mpasuko mkubwa ndani ya chama.


  CCM kwa sasa inakabiliwa na makundi makubwa mawili yenye wafuasi wengi, moja ni lile linaloongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, ambaye amebaki na kundi linalojinadi kama wapinga ufisadi na kundi jingine ni lile linaloongozwa na hasimu wake kisiasa, Edward Lowassa, linalopingana na dhana ya kujivua gamba.


  Mukama pia anadaiwa kushindwa kukiimarisha chama na kuruhusu wanachama wengi kukihama chama hicho kwa kile kilichoelezwa kutoridhishwa na mwenendo wa mambo ndani ya CCM.


  Kiongozi huyo anabebeshwa lawama kuwa ameshindwa kusimamia dhana ya kujivua gamba wakati yeye ndiye aliyeanzisha hoja hiyo kupitia tume aliyoiongoza kufanya utafiti kubaini sababu za CCM kupata kura chache za urais na kupokwa majimbo mengi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.


  "Unajua, Mukama ndiye aliyekuja na matokeo ya utafiti kwenye Kamati Kuu na Halmashauri Kuu. Alibainisha sababu kadhaa za chama kushindwa, lakini sababu kubwa tume yake ilibaini ni pamoja na chama kukosa mvuto kutokana na baadhi ya makada wake, Edward Lowassa, Andrew Chenge na Rostam Aziz kuhusishwa na ufisadi.

  Akaja na mapendekezo kwamba makada hao wavuliwe nyadhifa zao.


  "Leo ameshindwa kusimamia kile alichokiamini, badala yake chama kimekuwa kikipiga vita ya maneno tu, mara kutoa siku 90, mara tumeongeza, mara haijulikani. Matokeo yake tumezalisha makundi yanayokitafuna chama," alisema kada mmoja ambaye ni mjumbe wa NEC.


  Kada huyo anasema kuwa baadhi ya makada wanaotuhumiwa kwa ufisadi waliandaliwa barua za kutakiwa kuachia nyadhifa zao lakini hilo lilishindikana kutokana na utendaji mbovu wa Mukama.


  Makada wengine wanamlinganisha Katibu Mkuu Mukama na mtangulizi wake, mzee Yusuf Makamba, kwamba licha ya kuwa na elimu ndogo ya darasani, amemzidi Mukama kiutendaji.


  Dalili za CCM kumchoka Mukama zimejionyesha hivi karibuni katika moja ya vikao vya wabunge wa CCM ambapo baadhi walifikia hatua ya kusema katibu mkuu wao amechoka kimawazo, bora aachie ngazi sasa.


  Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mjini Dodoma zilisema wabunge walikuja juu wakati walipokuwa wakijadili hali ya kisiasa ndani ya chama chao na kuwekeana msimamo wa kuiunga mkono Bajeti ya mwaka 2012/2013.


  Mmoja wa viongozi waandamizi wa CCM, aliliambia gazeti hili kuwa katibu mkuu sasa hashirikishwi katika baadhi ya mambo baada ya kubaini kuwa hana uwezo wa kukiimarisha chama.


  "Angalia katika mikutano yote inayofanywa na chama kwa sasa hata ule wa Jangwani ulikuwa na watu wengi, Mukama hakuwepo. Ingawa alikuwa nje ya nchi, lakini hata kama angekuwapo, asingepata nafasi ya kuhutubia kwani hana uwezo wa kuongea hadharani.


  Kada mwingine wa CCM alimshmabulia Mukama kwa madai kuwa amekuwa akiropoka vitu ambavyo wakati mwingine hana utafiti navyo.


  " Mfano ni wakati wa kumuaga marehemu Bob Makani. Alitoa historia ya ajabu kuhusu waasisi wa CHADEMA, matokeo yake, Freeman Mbowe, alimuumbua pale alipotoa ufafanuzi kupinga kauli yake," alisema.


  Wabunge walioipinga bajeti kukiona

  Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa kuna mpango wa kutaka kuwawajibisha baadhi ya wabunge waliokiuka msimamo wa pamoja wa wabunge wa CCM juu ya kuipitisha bajeti.

  Bajeti hiyo ya serikali iliyopitishwa Ijumaa wiki hii kwa kura 225 za ndiyo huku kura 72 zikiikataa, kwa kupiga kura za hapana, zaidi ya wabunge 54 hawakuhudhuria mkutano huo.


  Kuna taarifa kuwa wabunge waliogoma kuhudhuria kikao hicho bila taarifa na wengine waliokataa kuipitisha bajeti hiyo huenda wakakumbana na mkono wa chama ambacho katika siku za hivi karibuni kimekuwa kikihaha kujinusuru kutoka katika minyukano ya makundi yanayohasimiana.


  Inasemekana baadhi ya wabunge wanataka wenzao wajadiliwe na ikiwezekana wawajibishwe ili kujenga nidhamu chamani pamoja na kudumisha uwajibikaji wa pamoja.


  Wabunge hao wanatarajiwa kujadiliwa na kikao cha wabunge wa CCM ambacho kinatarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo mara baada ya kuwasilishwa kwa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.


  Wabunge wanaoonekana kuwasaliti wenzao ni Luhaga Mpina (Kisesa), Deo Filikunjombe (Ludewa) na Kangi Lugola (Mwibara).
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Chama chenye mipango kina deal na kutekeleza sera zake. Chama chenye siasa mbovumbovu kina deal na wanachama wake wanaokikosoa kiendapo vivyo sivyo
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi tatizo ni Mukama au chama?
   
 4. W

  Welu JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 815
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Hawawezi kuwafanya chochote wabunge hao. Kwani ukiwa mbunge unazuiliwa kuwa na maamuzi binafsi. Oo tutavua magamba sasa tena wanaanza ngonjera zingine. Another silly season!
   
 5. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,314
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Ccm ni simba wasiyo na meno hawawezi kuwafanya chochote ni kerere za chura.
   
 6. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  CCM msitafute mchawi, haya ndiyo baadhi ya makosa yanayokiangamiza Chama kwa sassa, mnahangaika na individual members ndani ya chama ina wa-cost a lot, wakati kuna millions of potential members and voters particularly young people wanataka wasikie matumaini mliyonayo kwao katika kuelekea maisha bora.

  Wake up party, mnapaswa ku-start thinking positive, na seriously smpeaking, Mukama is among those leaders who have often spekoen negatively about the oposition (except kwenye Misiba) fashion ambayo inafuata na makada wengi wa CCM. How can we measure your maturity if you behave tipically like a growing up teenagers whom we can excuse them for thier transitional attitude?

  Kuwa atractive is only one thing, kuwa pisitive about every person and all people so that people can motivetly be atracted and support the party as this generate hope. People often change their mind based on convinsing power, not by insulting them simply because they have today, a differing opinion, what about tomrow? They may stick to their bad situation simply because you have defined them as enemies, and do not wait until this situation turns up, it will be very expensive.
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Chama Cha Mapenzi ina uwezo wa kumwajibisha Mukama, lakini haina uwezo wa kuwawajibisha Wabunge
   
 8. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Kukuza mada kama za Ufisadi, na kuidentify few individuals ambao both you and the public spend a lot of time, it a serious questionable act. I do not beleive this can in any wasy solve our overwhelming problems and challenges we face as a Developing solution. You are simply using simple solutions to complex situation.

  Viongozi wa CCM mnatafuta mchawi? haya ndiyo baadhi ya makosa yanayokiangamiza Chama kwa sassa, mnahangaika na individual members ndani ya chama ina wa-cost a lot, wakati kuna millions of potential members and voters particularly young people wanataka wasikie matumaini mliyonayo kwao katika kuelekea maisha bora.

  Wake up party, mnapaswa ku-start thinking positive, na seriously smpeaking, Mukama is among those leaders who have often spekoen negatively about the oposition (except kwenye Misiba) fashion ambayo inafuata na makada wengi wa CCM. How can we measure your maturity if you behave tipically like a growing up teenagers whom we can excuse them for thier transitional attitude?

  Kuwa atractive is only one thing, kuwa pisitive about every person and all people so that people can motivetly be atracted and support the party as this generate hope. People often change their mind based on convinsing power, not by insulting them simply because they have today, a differing opinion, what about tomrow? They may stick to their bad situation simply because you have defined them as enemies, and do not wait until this situation turns up, it will be very expensive.

  Be positive, let children, young peole, youth, adult of various age be involved in defining the future Tanzania, let the media play part, let the musicians start talking about the development issues, let them talk about the beauty of the country, let young people start making it a fassion feeling Tanzanian, and do somthing to make the Tanzania you want it tomorrow! Lets not talk about Education, Health, Water, Sevurity but also quality of it, and equality as well as iquity to all of that. Achaneni na kusifiaq vitu ambavyo mnajua kabisa ni bomu la kesho. Mfano, Kwa ujinga wa wengi wa viongozi kutokuwa wabunifu katika miradi binafsi, wametumia udhaifu wa Huduma hizi kujinufaisha, kama watoto wako wanasoma kwenye shule zenu mlizopanzisha wenyewe na marafiki zenu, na kutibiwa katika mahospitali yenu na marafiki zenu, na kuletewa maji na magari yenu na ya marafiki zenu mpaka wenye matanki yenu nyumbani, ni lini mtafikiria shida wanazopata wananchi? Ili wawapigie kura, ni lazima muwadanganye na kuwa manipulate na kuwa brainwash, ili wawashangilie, utasema lolote tu ili mradi wakupigie kura hata kama sio kweli. Ni lazima CCM muamke muteteee kile kilichoanzisha CCM tangu mwanzo, Uhuru, Usawa, Ujamaa (hapa kuna tatizo kubwa), na Kujitegemea (na hapa pia).

  Na niko convinced kabisa, tatizo haliko kwa Mwenyekiti, ila mfumo mzima wa Chama. Kuna watu wako tayari kufa au kuua, kulinda maslahi yao binafsi na hawako tayari hata kwa adhabu ya kifo kulinda maslahi ya Taifa hili bila kuona maslahi yao binasi kwanza. Mimi nilidhani maslahi ya Taifa hili kwanza na yanapokuwa unaweza kuona maslahi yakop na yatatiririka kwa urahisi bila shida, kutokana na heshima na mazingira unayojijengea? na ukiendlea kuimarisha nchi na watu wake, hutaishi kwa shida. Na hili ndilo CCM inapaswa kufanya.
   
 9. M

  Makupa JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  profesa umetumwa na nani wewe
   
 10. p

  petrol JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Gazeti la Tanzania Daima linaeleza Wabunge wa ccm wanataka Mukama ang'olewe. Kwa nini? ameshindwa kutengua kitendawili cha makundi mawili hasimu ndani cha chama. kundi la mwenyekiti wa chama Rais Kikwete (wapinga ufisadi) na kundi la Mhe. Lowassa (wakumbatia ufisadi). Je ni kweli matatizo ya ccm ni bwana mukama? Mie nadhani wabunge wa ccm wanaendelea kukosa ujasiri wa kueleza kiini cha mtatizo ya chama chao. wanajamii jaribuni kujadili hili bila ushabiki wa chadema au ccm.
   
 11. t

  tupak Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku wakiweza kumtosa cheamen wao taifa tatizo kwisha shida ni jinsi ya kumnyemelea hadi umfunge kengele
   
 12. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,812
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  gazeti la Uhuru la chadema,mwe!
   
 13. S

  Satanic_Verses Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtabadili makatibu kila leo kwa sababu zilezile labda muombe CHADEMA ife kabla ya 2015.

  Kuhusu wabunge, je wabunge waliopinga bajeti ni akina nani?

  Kujibu swali hili inabidi CCM wachukue idadi ya wabunge waliopinga bajeti zote tangu 2011 na hii ya 2012 ndipo wapate ukweli kamili.
   
 14. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Tanzania Daima ni gazeti makini lenye waandishi wasomi wanaoandika habari zenyn maslahi ya taifa. Gazeeeeetiiii pawa.
   
 15. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mukama alikidhalilisha sana CCM kwenye msiba wa Bob Makani jambo lilomfanya hata Kikwete mwenyewe kupingana na risala yake wazi wazi!
   
 16. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,015
  Likes Received: 2,663
  Trophy Points: 280
  Tumia japo ubogo wewe.
   
 17. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mkama nadhani huwa anatumia bluetooth maana huyo mzee haeleweki vile.Aliukwaa ukatibu kwa sabab chama cha magamba hakina watu wa kukiongoza hata kichaa anaweza kuwa kiongozi
   
 18. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Issue sio kumng'oa, issue ni kureview job descrption yake. Lakini CCM imeshachelewa, Unakumbuka wakati uleeeee, Jembe Kolomba aliwaambia nini. Suala lake halikufanyiwa kazi. Mwalimu wangu alisema mnachukua mabaya aliyowafundisha, katika Azimio la Arusha, na kuacha mazuri. Hili nalo hamkulifanyia kazi. Mna Kiburi sana nyinyi. Sasa nawaambia, kama hamjui, mmeshalaanika na mtatazama lakini hamtaelewa, mtaangalia wala hataona. Na mtakaa nje ya utawala kwa miaka zaidi ya 50. Shauri yenu. Tatizo sio Mkama, hata Mkama anaogopa kibri chenu.
   
 19. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Mukama wanaweza kumg'oa lakini lowasa baba lao hawana uthubutu wa kumgusa kabisa maana ana waweka mjini.
   
 20. NG'OMBE

  NG'OMBE JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 362
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Waanze na Nepi.
   
Loading...