CCM kukata rufaa Ubunge Igunga...

hawana jipya,majimbo mengi sana walipigwa ila kwasababu wagombea wa upinzani hawakuwa na fedha ya dhamana ya kesi na kulipa mawakili wakaamua kuachana na kesi. Jamaa wamepwaya sana.
 
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya C.C.M-Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
imesema kuwa hawakuridhishwa na hukumu iliyotolewa hapo jana ya kumsimamisha ubunge mbunge wao Dr. Kafumu na hivyo watakata rufaa.

Yawezekana hiyo hukumu ilikuwa kiini macho tu ili kuusafisha Mhimili huu wa dola ambao kwa hivi karibuni Unakumbwa na kashfa ya kubeba majaji vihiyo. Yawezekana baada ya kukata rufaa wakashinda na kurudishiwa kiti chao. Tunaweza tukaisifu sana mahakama lakini mwishoe ikala kwa sisi!
 
SOURCE: Michuzi Blog
Lazima wafanye hivyo kama njia ya kupunguza aibu waliyovuna kutokana ubabe walioufanya kwa wapiga kura wa Jimbo la Igunga.
 
Those are necessary stages of justice. CCM go for that referal its your right any way.
 
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya C.C.M-Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
imesema kuwa hawakuridhishwa na hukumu iliyotolewa hapo jana ya kumsimamisha ubunge mbunge wao Dr. Kafumu na hivyo watakata rufaa.

Yawezekana hiyo hukumu ilikuwa kiini macho tu ili kuusafisha Mhimili huu wa dola ambao kwa hivi karibuni Unakumbwa na kashfa ya kubeba majaji vihiyo. Yawezekana baada ya kukata rufaa wakashinda na kurudishiwa kiti chao. Tunaweza tukaisifu sana mahakama lakini mwishoe ikala kwa sisi!
Wanapoteza Muda Tu.!
 
Mwanzo kafumu alitaka kujitoa kugombea mkamlazimisha, jana katamka na kasema hataki tena siasa na ataki mawasiliano yeyoye na kiongozi yeyote wa CCM na anakwenda zake nje kufanya kazi aliyosomea. na hii imetokana na CCM kushindwa kusaidia katika kesi hiyo kwa upande wa gharama sasa leo mnakata Rufaa ya kumtetea nani? kafumu hataki tena Ubunge!
 
Hii sikuisikia. Nilichosikia nape akisema ni wanasubiri judgement copy waiangalie watoe uamzi.
 
hivi mnagawa mapilaua wazi wazi watu wanapanda jukwaani na ma pisto bado mnasema mmeonewa?kweli nyie kiboko
 
Rufaa ni haki yao, hivyo sio jambo la ajabu.

Binafsi kama bush Lawyer sioni nafasi ya Ccm kushinda rufani hiyo kwa hoja.

Jaji aliyetengua ushindi wa CCM ametoa facts ambazo kila mtu aliyekuwa anafuatilia uchaguzi wa Igunga aliziona wazi.
 
Demokrasia na utawala
wa sheria uheshimiwe. Rafani ni haki ya msingi ya kila mtu. CCM isibezwe
kwa kutumia haki yake ya msingi.
Haki ya CCM kukata rufaa kwenye kesi hii inatoka wapi? CCM si mmoja wa washtakiwa katika kesi ya msing, itakata rufaa kwa misingi gani kisheria? nadhani wenye haki ya kukata rufaa nui aidha Dalali, mwanasheria mkuu au msimamizi wa uchaguzi ambao ndio walioshtakiwa. inachoweza kufanya ccm ni kumshauri au kumwelekeza mgombea wake akate rufaa
 
Back
Top Bottom