VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Chama cha Mapinduzi kimedhamiria kujisafisha kwa kutimua mafisadi wote chamani kuanzia mwezi Juni mwaka huu. Nyaraka za ndani ya chama zinaonesha kuwa mwezi Juni ni mwezi unaotazamiwa kuwa mwezi wa 'mabadiliko makubwa chamani'. Rais Magufuli anatazamiwa kukabidhiwa Uenyekiti wa CCM mwezi huo wa Juni.
Nyaraka za kimaandalizi zinaonesha kuwa CCM imepania kujisafisha kwa kuwatimua mafisadi wote chamani ili kuendana na dhamira ya Rais na Mwenyekiti mtarajiwa wa CCM, Rais Magufuli, katika vita dhidi ya ufisadi. Nyaraka nzitonzito zinaendelea kuandaliwa na kuwabaini wanaofaa kutimuliwa chamani.
CCM inataka kuwa na sura mpya. CCM inataka kuwa mpya. Nyaraka za kichama zinaonesha kuwa huo utakuwa ni muendelezo wa Operesheni ya Kujivua Gamba, ambayo sasa itaitwa Operesheni ya Kutumbua Majipu,iliyoasisiwa wakati Mukama akiwa Katibu Mkuu wa CCM.
Safishasafisha hiyo ya kichama, kama ikifanyika kweli, itawakumba Wabunge na vigogo mbalimbali chamani ambao kwa miaka nenda rudi wamekuwa wakisemwa kuwa ni mafisadi. CCM isirudi nyuma. Ifanye kweli. Isije ikawa kama vile ambapo 'Gamba liliishia kiunoni'. Ukifika muda wa kutaja na kutoa ushahidi wa ufisadi, nitafutwe!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam