CCM kuibuka kidedea uchaguzi Arusha

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
2,009
1,607
Ndugu wana jamvi,hatimaye siku na saa watanzania tulikuwa tunasubili kwa hamu ili kuweza kujua nani ataibuka kidedea katika kata nne zinazofanya uchaguzi leo jijini Arusha kwa maana ya kata ya Erelai, Kimandolu, Themi na Kaloleni.

Wana jamvi waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu ,na hofu ni ishara ya woga wa kushindwa,ni wazi chadema wameingiwa na hofu kubwa baada yakuona kuna uwezekano mkubwa wakupoteza kata nne za jiji la Arusha mkoa ambao wamekuwa wakijinasibu kuwa ndiko kiliko kitovu cha chadema.

Hofu hiyo inatokana na kugundua kwamba wananchi wa Arusha wamechoka kuona mkoa wao ukigeuzwa kuwa uwanja wa mapambano na umwagaji damu kwa ajili ya maslahi ya watu wachache.

Hivyo basi ni wazi sasa chadema wamejichimbia kabuli wenyewe kwakutokujali misingi ya utawala bora inayosema kiongozi ni mali ya wananchi ila mwanachama ni mali ya chama wao wakakiuka misingi hiyo na kuamua kufukuza madiwani wao kwa maslahi ya watu wachache.

Ni wazi sasa CCM inaenda kuibuka kidedea na kushinda kwa kishindo katika kata zote nne kwa namna ilivyojipambanua kwa sera zake kipindi cha kampeni na wananchi hasa vijana kuanza kuelewa tofauti iliyopo kati ya chama maslahi jamii(CCM)na chama maslahi binafsi(chadema)

Viva ccm,umoja ni ushindi.
 
Kweli akili ni nywele kila mtu ana Zake aise hivi unajua maana ya breaking NEWZ
 
Juliana naheshimu utabiri Wako uliyatabiri haya na yakatokea,Big up binti mrembo na mchapa kazi nakukubali sana,ningekua sijaoa ningekupa zawadi kwa kukuoa hahahahahah
 
Duh ndugu zangu mshaanza kuporomosha matusi tayali.kuweni wavumilivu kipindi hiki japo najua kitaenda kuwa kigumu sana kwenu.
 
...karoreni,... kabuli,... Nani alikufundisha kiswahili?!!!
 
Hivyo basi ni wazi sasa chadema wamejichimbia kabuli wenyewe kwakutokujali misingi ya utawala bora inayosema kiongozi ni mali ya wananchi ila mwanachama ni mali ya chama wao wakakiuka misingi hiyo na kuamua kufukuza madiwani wao kwa maslahi ya watu wachache.
Hivi chadema mlikosa watu wa kuwapa uongozi hadi mkampaga huyu mtu nafasi ya uongozi kwenye chama chenu kabla hamja mtimua? jamani jamani jamani,hata kuandika imekua tabu? hata jipendekeze vipi kwenye chama chetu haupati nafasi yoyote ya uongozi,kwanza wewe ni mamluki wa chadema
 
Umwekewa ki2 kwenye sehemu yoyote ya mwili wako? it must be disturbing you!!!get it out faster!!!
 
Chadema ni chama cha demokrasia. Kinaamini katika demokrasia na maamuzi ya watu. Kwahiyo kama CCM watashinda kwa haki, chadema haina tatizo na wala haihitaji kulalamika. Lakini kama ushindi wenyewe unaoitwa breaking news ni huu wa kununua shahada za kura kutoka kwa wanachama wa CHADEMA, nina uhakika matokeo hayo yatapingwa mahakamani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom