CCM: Kufikia Disemba 2022 Vijiji vyote nchini lazima viwe na umeme

Umeme upi sasa? kama mijini tu huo umeme haupo,huko vijijini utafikaje?
 
Vitakuwa na umeme au miundombinu ya umeme?
 
Usaliti kwa taifa ni tafsiri iliyoko kwa viongozi wa CCM dhidi ya viongozi wa upinzani. Lakini mikataba yote mibovu ambayo ni hatari ya kweli kwa taifa wameingia viongozi wa CCM, na hakuna wa kuwagusa. Uza ubongo huo kaka.
 
Usaliti kwa taifa ni tafsiri iliyoko kwa viongozi wa CCM dhidi ya viongozi wa upinzani. Lakini mikataba yote mibovu ambayo ni hatari ya kweli kwa taifa wameingia viongozi wa CCM, na hakuna wa kuwagusa. Uza ubongo huo kaka.
Maana ya usaliti umeielewa. Hizo nyingine zako ni porojo tu.
 
Miaka ya uhuru bado kuna vijiji havina umeme?
 
Hiyo siyo hoja, atwambie walau kila kitongoji kitakuwa na umeme ila kusema kila kijiji ni ngonjera ambazo tumezizoea
 
Shida siyo umeme kufika vijiji vyote bali wazungumzie idadi ya watanzania kuunganishwa na umeme huko vijijini.

Umeme unapelekwa kwenye taasis za serikali tu huko vijijini halafu unajisifu kuunganisha vijiji vyote!
Yaani hii ni kero kubwa sana, sijui rais hajui kuwa watu huko vijijini watu hawana umeme bali ni kwenye sehemu chache tuu
 
Ccm huwa wanatufanya mazuzu sana, kipindi cha uchaguzi walituambia umeme ipo vijiji vyote Tanzani, sasa hii ya kutuambia kufika 2022 umeme utakua vijiji vyote, labda kama kuna vijiji vipya
 
Your browser is not able to display this video.

Ataamini huyu na wengineo wengi..
 
Bwawa la Mwl Nyerere limeshaanza kujazwa maji kama ilivyoahidiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…