CCM: Kufikia Disemba 2022 Vijiji vyote nchini lazima viwe na umeme

Kiturilo

JF-Expert Member
Sep 27, 2021
709
2,858
Katibu mkuu wa CCM bwana Chongolo leo akiwa anazungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya CCM kwa miaka 60 amesema kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ya 2020 - 2025 imeelekeza kuwa kufikia mwezi wa 12 mwaka 2022 vijiji vyote nchini Tanzania lazima viwe na umeme na waziri atakayeshindwa kufikia hilo lengo atawajibishwa mara moja.

Chongolo amebainisha kuwa mpaka sasa hakuna mkoa wala wilaya ambayo haina mkandarasi wa kupeleka umeme maeneo husika.
 
Umeme au wiring za umeme?

Sababu acha vijinini hata huku mijini siku kadhaa zilizopita umeme ulikuwa ni wa kugawana
 
Katibu mkuu wa CCM bwana Chongolo leo akiwa anazungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya CCM kwa miaka 60 amesema kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ya 2020 - 2025 imeelekeza kuwa kufikia mwezi wa 12 mwaka 2022 vijiji vyote nchini Tanzania lazima viwe na umeme na waziri atakayeshindwa kufikia hilo lengo atawajibishwa mara moja.

Chongolo amebainisha kuwa mpaka sasa hakuna mkoa wala wilaya ambayo haina mkandarasi wa kupeleka umeme maeneo husika.
Watatumbua wengi.

Waanze kutatua matatizo ya upatikanaji wa umeme jikoni. Kwani Stglers G itakuwa imeshaanza ufanisi wakati huo Dec 22?

Hapana, haina maana kwa ukatikaji wa umeme uliopo leo, kudhani kuwa ukisambaza vijiji vyote umeme ndio utatosha. Umeme wa namna hii, kaeni nao huko mijini.
 
Miaka 60 ya Uhuru Mapinduzi makubwa ya maendeleo tumepiga. Political development tumefanikiwa. Mfano, transition ya uongozi kwa amani kabisa baada ya kifo cha Rais wetu mpendwa JPM.

#Social development tupo. Elimu bure, mikopo elimu ya juu, huduma za afya, maji. #Uchumi tunaenda vizuri ingawa tunahitaji kufanya MAPINDUZI YA KILIMO ili kukata mnyororo wa umasikini. #Nchi ina amani na usalama wa kutosha na kuwa miongoni mwa nchi chache duniani zenye amani na usalama wa hali ya juu.

#Miundombinu mikubwa ya uchumi, JNHP, SGR, Barabara kuunganisha mikoa. Tunayo mengi ya kujivunia kama Taifa.

Viva Tanzania. Viva CCM. CCM NI NGOME YA CHUMA. #Hongera ndugu KM Comrade Chongolo.
 
Wewe unaishi Tanzania hii au Tanzania nyingine!
Transition ya uongozi kwa amani - kumbuka unazungumzia miaka 60 ya uhuru hivyo usichukulie kuingia kwa Samia tu
Elimu bure -sawa ila ubora je? Mikopo ya elimu ya juu (Rais alisema wote wapewe kwa kuwa ni mkopo, na kodi zikaongezwa kwa ajili hiyo) Unajua kilichotokea?
Nchi ina amani na usalama - wako wapi Azori, Mwangosi, Saanane, nk. Hivi hizo familia zao unawaambia kuna amani na usalama! Sema watanzania tuko wapole
 
Concept ya amani na usalama wa nchi sidhani kama inatafsiriwi hivyo. Hata Marekani vitisho vya usalama wa mtu mmoja mmoja vipo. Na kuna factors nyingi; labda chuki binafsi za kibiashara, uhusiano wa hali ya ndoa na mpenzi au usaliti kwa Taifa.

Nazungumzia mfumo wa ulinzi na usalama wa nchi unaotabirika. Na usiseme Watanzania ni wapole; mosi, Watanzania wengi wana akili sana huwezi kuwashawishi wavuruge amani na usalama wa nchi yao wakati wanajua hawana nchi nyingine kukimbilia.

Pili, amani na usalama kwa Tanzania ni matunda mazuri ya vyombo vyetu vya dola. Usidhani ipo tu nchi inalindwa. Wapo waliotamani, wanaotamani na watakaotamani kuivuruga nchi lakini walizimwa na wataendelea kuzimwa.

Miaka 60 ya Uhuru tuonyeshe ukomavu wa kutafuta suluhu ya changamoto zetu kwa mazungumzo ya upendo na amani. Tuache NONGWA.
 
Mwaka 1990 ccm walisema,kufika mwaka 2000,shida ya maji TANZANIA itakuwa ni historia.
 
Shida siyo umeme kufika vijiji vyote bali wazungumzie idadi ya watanzania kuunganishwa na umeme huko vijijini.

Umeme unapelekwa kwenye taasis za serikali tu huko vijijini halafu unajisifu kuunganisha vijiji vyote!
 
Katibu mkuu wa CCM bwana Chongolo leo akiwa anazungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya CCM kwa miaka 60 amesema kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ya 2020 - 2025 imeelekeza kuwa kufikia mwezi wa 12 mwaka 2022 vijiji vyote nchini Tanzania lazima viwe na umeme na waziri atakayeshindwa kufikia hilo lengo atawajibishwa mara moja.

Chongolo amebainisha kuwa mpaka sasa hakuna mkoa wala wilaya ambayo haina mkandarasi wa kupeleka umeme maeneo husika.
Tanesco yenyewe hii yakuuliza mteja utanunua nguzo au usubiri wa rea, au tanesco mpya🤔.
 
Back
Top Bottom