CCM kufa baada ya 2015? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kufa baada ya 2015?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Fitinamwiko, Aug 16, 2012.

 1. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Kila dalili zinaonyesha umaarufu wa CCM unazidi kutokomea. Pamoja na mipesa wanayomwaga kununua Tshirt, kufia na Kanga, wananchi tunazidi kuwakimbia. Walitumia jeshi la Police kuwatisha wananchi kuhudhulia mikutano ya Wapinzani, wapi ndio kwanza wamekoleza moto. Sasa wanakata umeme, kuhujumu mukutano, wamesahau generators zipo kusaidia.
  Je CCM ikishindwa (ohh sorry)itakaposhindwa 2015, ni mkoa gani tuuchague kubeba kaburi lake?
   
 2. b

  bdo JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  CCM ina negative perception kila kona ya nchi hii, kwa mila zetu Watz msiba hufanyika kwa mwenyeji na wakati mwingine mazishi yanaweza fanyika kwake, nadhani kama haitazikwa mkoa wa Pwani Bagamoyo, basi kaburi litakuwa dodoma
   
 3. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kwanini ife? Hakuna chama cha upinzani ambacho kimejipanga sawasawa.
  Huwezi kuleta mabaadiliko only by criticizing the ones holding power
  We are still to see a realistic program from wapinzani that takes into account
  our needs, our resources, our allies, our partners, our people na mengine
  Kwa sasa sijaona chama kinacho niridhisha. Better the devil we know...
   
 4. m

  majebere JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  CCM ikifa basi Tanzania inakufa, CCM ndio roho ya hii nchi. Bila CCM kila kitu kinazimika. UN itabidi waje waweke serikali yao ili Tanzania ifufuke tena.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,671
  Likes Received: 82,493
  Trophy Points: 280
  Magamba mbona ilishakufa siku nyingi..... Tunasubiri mazishi yake tu.
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kuhudhuria, wewe ni Mtanzania au ndio wale mnajifundisha Kiswahili mkianza shule?
   
 7. Taz

  Taz JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 305
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii ilikua ni point kubwa sana kule jukwaa la lugha, ila bahati mbaya hapa ni siasa. Mkuu, goal lako offside!
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Siku mkipata mbunge kutoka Zanzibar.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,671
  Likes Received: 82,493
  Trophy Points: 280
  Siku Mwalimu alipotamka, "CCM si mama yangu" ndio siku rasmi CCM ilipokutana na umauti wake sasa tunasubiri mazishi tu ili ipotee kabisa kwenye anga za siasa za Tanzania.

   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Imekufa TAA, TANU, AFRO SHIRAZI PARTY, itakuwa CCM? unafikiri nini kitabaki? wewe? Huyo Mwalimu wako mwenyewe yuko wapi?
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  Ndugu Siasa wa Tanzania, anasikitika kutangaza kifo cha bwana CCM, aliyeuawa kwa ufisadi. Mazishi yatafanyika 2015, hukohuko Tanzania. Mipango ya mazishi inafanywa na bwana Chadema. Habari ziwafikie wazalendo wote popote walipo. Ukisikia tangazo hili, mjulishe na mwenzako
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,671
  Likes Received: 82,493
  Trophy Points: 280
  lol! Bujibuji......Ubwabwa utaliwa wapi?
   
 13. t

  tenende JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mazishi ya CCM Yataliwa makande!... Majonzi makuu ya umaskini mkubwa waliotutwisha.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,671
  Likes Received: 82,493
  Trophy Points: 280
  Hahahaha lol! :)

   
 15. JJB

  JJB JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  we ulitaka wapinzani wajipange vipi? Au mpaka waingie magogoni ndio utaamini CCM imekufa? Think great!
   
 16. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Hivi mazishi maana yake ni nini hasa; Je, ni kupoteza uchaguzi 2015 au Kusamsambaratika baada ya kupoteza uchaguzi 2015? Kama suala ni kupoteza uchaguzi 2015, wengi wetu tumeshakomaa na tupo tayari kwa demokrasia ya kupokezana vijiti; kama ni kusambaratika baada ya kushindwa 2015, wataondoka waliokuwa wachumia tumbo na kuacha wenye nia ya dhati na chama wakijenge upya, kwani kwa sasa ni mchanganyiko wa wenye mapenzi ya dhati moyoni na wale wenye mapenzi ya tumboni; Vinginevyo, Tanzania bila CCM haiwezekani - na hii sio sawa na kusema Tanzania bila CCM ikulu haiwezekani, kwani hilo linawezekana;
   
 17. JJB

  JJB JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimegundua hata elimu yako ya msingi ulioipata kwa kubahatisha haijakukomboa. Yani wewe CCM unaiona kama mzazi wako? Kweli mapenzi ya mbwa ni kituko kwa watazamaji.
   
 18. JJB

  JJB JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  we ulipata ngapi Kiswahili kwenye mitihani yako? Au unadhani hatujui kama ulikua unakua wa pili kutoka mwisho? Ama kweli nyani haoni kundule.
   
 19. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Una hoja lakini kidogo imechanganyika na ushabiki. Vinginevyo ni kweli kwamba CCM haiwezi kutoweka kwenye ramani ya siasa Tanzania, ina mizizi mirefu sana na kwa kiasi fulani ni sehemu ya utamaduni wa nchi kwa both, wanaoipenda na wanaoichukia; hii ndio maana ya kauli ya nyerere kwamba CCM ikiyumba, nchi itayumba; vinginevyo nchi haiwezi kuanguka kutokana na anguko la CCM, labda juhudi za binafsi zifanyike - aidha wanachama wa CCM wasio na uelewa wa demokrasia ya vyama vingi walete vurugu au wanasiasa wenye uwoga wa kufikishwa mahakamani Chadema ikiingia Ikulu walete vurugu; au wanachama na viongozi wa chama kitakachoshinda uchaguzi waanzishe vurugu (jambo ambalo sioni likitokea) na kutumia nguvu yao mpya ya dola kukifanyia CCM kila aina ya hujuma kipotee kwenye ramani ya siasa;

  Kushindwa kwa CCM iwapo itatokea 2015, haitakuwa mwisho wa dunia bali ukomavu wa demokrasia na Chama kitaendelea kujijenga vizuri zaidi kwa chaguzi za baadae; kuna mifano mingi nchi za wenzetu:


  • CCM ya Zambia (UNIP) iliangushwa na Chadema za Zambia (MMD) baada ya kutawala miaka 27; Chadema ya Zambia (MMD) ikaja angushwa na chama kingine kipya kabisa cha satta - Patriotic Front (PF) baada ya kutawala kwa miaka 20;
  • Nchini Ghana, chama Cha NDC kilipoteza madaraka 1992, na kikaja kushinda tena 2008;
  • Nchini Uingereza, chama cha Labour kilikaa benchi kwa miaka 17 (wakati wa Thatcher akiwa Waziri Mkuu) na kuja kushinda uchaguzi chini ya blair mwaka 1997;
  • Nchini Japan, Democratic Party (DP) Japan kilitawala kwa miaka 50 mfululizo hadi juzi juzi kilipokuja angushwa, na kinajipanga vizuri sana na kuna chances kubwa sana kinarudi next elections;

  Hata sisi Tanzania pia tunaweza; tusidanganyike na kutumiwa kuingiza nchi katika machafuko;
   
 20. M

  Magesi JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  r.i.p ccm
   
Loading...