CCM kufa baada ya 2015?

we ulipata ngapi Kiswahili kwenye mitihani yako? Au unadhani hatujui kama ulikua unakua wa pili kutoka mwisho? Ama kweli nyani haoni kundule.

Mie ni lugha mama kwangu ukienda kunipa hii mitihani yenu utanifelisha kwa sababu mnafanya kila hila kuchakachuwa Kiswahili kiondoke kwenye asili yake.

Unapokosea matamshi ni lazima nikurekebishe.
 
Hivi mazishi maana yake ni nini hasa; Je, ni kupoteza uchaguzi 2015 au Kusamsambaratika baada ya kupoteza uchaguzi 2015? Kama suala ni kupoteza uchaguzi 2015, wengi wetu tumeshakomaa na tupo tayari kwa demokrasia ya kupokezana vijiti; kama ni kusambaratika baada ya kushindwa 2015, wataondoka waliokuwa wachumia tumbo na kuacha wenye nia ya dhati na chama wakijenge upya, kwani kwa sasa ni mchanganyiko wa wenye mapenzi ya dhati moyoni na wale wenye mapenzi ya tumboni; Vinginevyo, Tanzania bila CCM haiwezekani - na hii sio sawa na kusema Tanzania bila CCM ikulu haiwezekani, kwani hilo linawezekana;

CCM walivyo na njaa za matumbo yao? Sijui?
 
Kila dalili zinaonyesha umaarufu wa CCM unazidi kutokomea. Pamoja na mipesa wanayomwaga kununua Tshirt, kufia na Kanga, wananchi tunazidi kuwakimbia. Walitumia jeshi la Police kuwatisha wananchi kuhudhulia mikutano ya Wapinzani, wapi ndio kwanza wamekoleza moto. Sasa wanakata umeme, kuhujumu mukutano, wamesahau generators zipo kusaidia.
Je CCM ikishindwa (ohh sorry)itakaposhindwa 2015, ni mkoa gani tuuchague kubeba kaburi lake?

mkuu Fitinamwiko kwanza jifunze how to spell kabla hujatupia thread jukwaa la great thinkers and 2nd aim sorry to disappoint you ! ndoto zako ni far from reality ..! but sio mbaya keep on dreaming
 
ukiwa shabiki wa vyama utaamini kuwa ccm inakufa lakini ukiwa mpembuzi na mchambuzi wa mambo huwezi amini hiyo kitu.

hakuna dalili yoyote kwa CCM kufa.tusidanganyane,ukweli ni kitu muhimu sana katika maisha ya mwanadam
 
CCM ina wabunge zaidi ya 250 hivi sasa na walichaguliwa hivi majuzi.waliopiga kura juzi watapiga kura 2015.kipi kipya kinachowafanya wasiwape wale wale kura waliowapa 2010???
TUACHE USHABIKI badala ya kuambizana ukweli.
 
ukiwa shabiki wa vyama utaamini kuwa ccm inakufa lakini ukiwa mpembuzi na mchambuzi wa mambo huwezi amini hiyo kitu.

hakuna dalili yoyote kwa CCM kufa.tusidanganyane,ukweli ni kitu muhimu sana katika maisha ya mwanadam
Walking while dreaming is very dangerous.
 
kwa sasa hakuna chama mbadala cha siasa kinachofaa kushika dola.viendelee kujijenga kwanza
 
vyama vya siasa vya upinzani vina dosari za ukanda,udini na ukabila.vikiondoa hizo kasoro vikajipambanua kama ni vya kitaifa zaidi ndio watanzania wataanza kuwafikiria kuingia ikulu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom