Uchaguzi 2020 CCM kuangukia pua Tarime Vijijini

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,821
11,527
Nimefanya utafiti wangu binafsi ndani jimbo la Tarime Vijijini, jimbo hili linaenda kurudi Chadema chini ya kamanda John Heche, kama haitawezekana basi watamtanganza mbunge wa ccm kibabe, hali itakayoleta uvunjifu mkubwa wa amani hasa katika mji wa Sirari.

Sababu za ccm kuangukia pua Tarime ni hizi hapa;

1. Mkuu wa wilaya ya Tarime.
Huyu bwana anaitawala Tarime kibabe na kijeshi, amekuwa na hulka ya kutembea na wanajeshi toka kambi ya Nyandoto na akienda sehemu yeye na wanajeshi hushirikiana nao kupiga raia mfano mzuri amepiga raia sana katika viijiji Nyantira, Itiryo na hata hivi karibuni katika kijijini cha Komarera karibu na mgodini, kitendo hiki kinaifanya wananchi waichukie ccm na wengi kuapa kutoipigia kura tena.

2.Makundi ya wagombea ndani ya Chama,
Kuna wagombea wengi ndani ya ccm waliotia nia ya kugombea ubunge, baadhi ni kama Mwita Waitara, Eliakim Maswi, John Gimunta, Nyerere Mwera, Bwire Marwa(Alliance) na wengine wengi, watia nia wote wametengeneza makundi hasimu ndani Chama, na hata sehemu nyingi makundi haya hugombana wao kwa wao, na kila kundi huapa kuwa endapo mgombea wao asiposhinda basi watahamia kumsapoti mgombea wa chadema tena.

3.Koo
Ndani ya jimbo la Tarime vijijini Kuna koo zipatazo 8 ambazo ni wairege, wanyabasi, wakira, watimbaru, wakenye, walenchoka,waanchari,wanyamongo, nje ya vyama vya siasa, koo hizi hupiga kura kwa kuangalia mtu wa koo yao halafu Chama hufuata, lakini pia koo hizi zimekuwa na migogoro ya mara kwa mara iliyofanya wasiaminiane, hivyo kama ikitokea kwa mfano akachaguliwa Maswi ambae anatoka koo ya wanyabasi kama ilivyokuwa kwa Kangoye ambayo ni wachache ni ngumu apate kura toka koo ya wairege na wanyamongo ambazo ni koo hasimu.
Nimemtolea Maswi mfano kwa sababu anapewa nafasi kubwa ya kushinda, ndani ya koo yake hana mshindani mkubwa hivyo kura za wajumbe atanyakuwa zote, tofauti na koo ya wairege ambayo ina wagombea wengi hivyo rahisi kugawana kura, lakini pia tetesi zinasema Maswi ni chaguo lao.

Ili CCM ishinde kwenye jimbo hili ipate mgombea toka koo kubwa ya wairege ambayo nayo watia nia wake wapo kwenye mgogoro mfano Waitara na Bwire(rahisi kusalitiana)

4.Udhaifu wa wagombea wa ccm.
Ccm ina wagombea dhaifu wasiojua kujieleza na kumudu jukwaa,hawajulikani nje mpaka ya nyumbani kwao, wagombea wa ccm karibia wote hawana uwezo mzuri wa kujieleza, na wengine wamekuwa wakitoa ahadi hewa, hali inaweza fanya wananchi wasiwapigie kura nikianza na
#Waitara hajui kujenga, ametoa ahadi nyingi ambazo hazitekelezeki. Wengi wanamuona kama mbabaishaji tu hasa kutokana na rekodi yake ya kutelekeza jimbo lake la Ukonga.
#Bwire(Alliance) huyu nje kijiji chake na vijana wanaoshabikia mpira hakuna anaemfahamu.
#Maswi rekodi zake chafu akiwa mtumishi wa umma,
# Nyerere, hajulikani jimbo, nje kijiji chake na kata ya Muriba hakuna anaemfahamu.

5.Kukubalika kwa mgombea wa chadema hasa kwa vijana,
Vijana wa Tarime wanamkubali mbunge anayemaliza muda wake hasa kutokana na ule ujasiri wake, uwasilishaji mzuri wa hoja zake, kujiamini kwake, kifupi wanamuona jembe, kama vijana watashiriki kupiga kura basi jimbo hili litarudi tena upinzani.

Waswahili husema, "Vita ya panzi, furaha ya kunguru"
Nawasilisha.
 
Hilo jimbo lipi kwenye list ya bashiru mkuu most wanted
Mwambieni heche atafute kazi ingine
 
Namtakia heri Mh.Heche, ni mwanaume hodari kama ilivyo watu wa kanda maalumu.Kapambana anamsimamo matunda mchakato fidia Nyamongo nk tunayaona.
 
Nimefanya utafiti wangu binafsi ndani jimbo la Tarime vijijini, jimbo hili linaenda kurudi Chadema chini ya kamanda John Heche, kama haitawezekana basi watamtanganza mbunge wa ccm kibabe, hali itakayoleta uvunjifu mkubwa wa amani hasa katika mji wa Sirari.

Waswahili husema, "Vita ya panzi, furaha ya kunguru"
Nawasilisha.
Duh...!.
P
 
Nimefanya utafiti wangu binafsi ndani jimbo la Tarime Vijijini, jimbo hili linaenda kurudi Chadema chini ya kamanda John Heche, kama haitawezekana basi watamtanganza mbunge wa ccm kibabe, hali itakayoleta uvunjifu mkubwa wa amani hasa katika mji wa Sirari.

Sababu za ccm kuangukia pua Tarime ni hizi hapa;

1. Mkuu wa wilaya ya Tarime.
Huyu bwana anaitawala Tarime kibabe na kijeshi, amekuwa na hulka ya kutembea na wanajeshi toka kambi ya Nyandoto na akienda sehemu yeye na wanajeshi hushirikiana nao kupiga raia mfano mzuri amepiga raia sana katika viijiji Nyantira, Itiryo na hata hivi karibuni katika kijijini cha Komarera karibu na mgodini, kitendo hiki kinaifanya wananchi waichukie ccm na wengi kuapa kutoipigia kura tena.

2.Makundi ya wagombea ndani ya Chama,
Kuna wagombea wengi ndani ya ccm waliotia nia ya kugombea ubunge, baadhi ni kama Mwita Waitara, Eliakim Maswi, John Gimunta, Nyerere Mwera, Bwire Marwa(Alliance) na wengine wengi, watia nia wote wametengeneza makundi hasimu ndani Chama, na hata sehemu nyingi makundi haya hugombana wao kwa wao, na kila kundi huapa kuwa endapo mgombea wao asiposhinda basi watahamia kumsapoti mgombea wa chadema tena.

3.Koo
Ndani ya jimbo la Tarime vijijini Kuna koo zipatazo 8 ambazo ni wairege, wanyabasi, wakira, watimbaru, wakenye, walenchoka,waanchari,wanyamongo, nje ya vyama vya siasa, koo hizi hupiga kura kwa kuangalia mtu wa koo yao halafu Chama hufuata, lakini pia koo hizi zimekuwa na migogoro ya mara kwa mara iliyofanya wasiaminiane, hivyo kama ikitokea kwa mfano akachaguliwa Maswi ambae anatoka koo ya wanyabasi kama ilivyokuwa kwa Kangoye ambayo ni wachache ni ngumu apate kura toka koo ya wairege na wanyamongo ambazo ni koo hasimu.
Nimemtolea Maswi mfano kwa sababu anapewa nafasi kubwa ya kushinda, ndani ya koo yake hana mshindani mkubwa hivyo kura za wajumbe atanyakuwa zote, tofauti na koo ya wairege ambayo ina wagombea wengi hivyo rahisi kugawana kura, lakini pia tetesi zinasema Maswi ni chaguo lao.

Ili CCM ishinde kwenye jimbo hili ipate mgombea toka koo kubwa ya wairege ambayo nayo watia nia wake wapo kwenye mgogoro mfano Waitara na Bwire(rahisi kusalitiana)

4.Udhaifu wa wagombea wa ccm.
Ccm ina wagombea dhaifu wasiojua kujieleza na kumudu jukwaa,hawajulikani nje mpaka ya nyumbani kwao, wagombea wa ccm karibia wote hawana uwezo mzuri wa kujieleza, na wengine wamekuwa wakitoa ahadi hewa, hali inaweza fanya wananchi wasiwapigie kura nikianza na
#Waitara hajui kujenga, ametoa ahadi nyingi ambazo hazitekelezeki. Wengi wanamuona kama mbabaishaji tu hasa kutokana na rekodi yake ya kutelekeza jimbo lake la Ukonga.
#Bwire(Alliance) huyu nje kijiji chake na vijana wanaoshabikia mpira hakuna anaemfahamu.
#Maswi rekodi zake chafu akiwa mtumishi wa umma,
# Nyerere, hajulikani jimbo, nje kijiji chake na kata ya Muriba hakuna anaemfahamu.

5.Kukubalika kwa mgombea wa chadema hasa kwa vijana,
Vijana wa Tarime wanamkubali mbunge anayemaliza muda wake hasa kutokana na ule ujasiri wake, uwasilishaji mzuri wa hoja zake, kujiamini kwake, kifupi wanamuona jembe, kama vijana watashiriki kupiga kura basi jimbo hili litarudi tena upinzani.

Waswahili husema, "Vita ya panzi, furaha ya kunguru"
Nawasilisha.
TUNAENDA NA HECHE
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom