CCM kitakufa mwaka 2015 na hakitarudi tena

CCM kitakufa mwaka 2015 na hakitarudi tena

ccm ishakufa tayari ebu tazama mtwara na lindi ccm wayafanyayo!!!!!!
 
Hata msibani sitamani kufika kwa jinsi marehem alivyonichefua enzi ya uhai wake,afe tu.
 
Ccm ni taasisi, hakuna siku itakufa labda siku vyama vya siasa vikifutwa na nchi kutawaliwa kijeshi na mwana ccm. Ngo na vyama vya kufa na kuzikana kama chadema ndivyo vitakufa

Kama hujui kufa (ccm) kachungulie kaburi la marehemu (KANU) utapata majibu. Au KANU haikuwa taasisi?
 
pole sana kamanda kwa mawazo mgando na ndoto za kusadikika.nasema hakuna chama kinachoweza kuishinda ccm iwe mwaka 2015 au 2025 au 2035 na kuendelea.badilisha mawazo yako ili mwaka 2015 cdm itakapopoteza majimbo yake mengi iliyonayo sasa na kuwa kama nccr usife kwa presha. Ccm jana-ccm leo -ccm kesho.
hawa wamekwisha magamba wananchi wamechoka na longolongo
 
Naona POLICECCM wameanza kushambulia mwanza hawa mabosiwote wa police CCM 2015 Tunawabadishia kazina kuwa FFU tenawakailinde bank
 
Pole sana kamanda kwa mawazo mgando na ndoto za kusadikika.Nasema hakuna chama kinachoweza kuishinda CCM iwe mwaka 2015 au 2025 au 2035 na kuendelea.Badilisha mawazo yako ili mwaka 2015 CDM itakapopoteza majimbo yake mengi iliyonayo sasa na kuwa kama NCCR usife kwa presha. CCM Jana-CCM Leo -CCM Kesho.

Malizia kwa kusema CCM Milele
Usiogope kufikiri,akili ni yako itumie tu,hujakopa au kuiazima kiasi utatakiwa kuirudisha,
Usiwe muoga wa mabadiliko
Katika maisha ya mwanadamu mabadiliko kwa kitu chochote ni muhimu sana,hata wewe unaeogopa kufikiri umekuwa
ukibadilika kwa muda na nyakati tofauti,ULIKUWA MTOTO UKABADILIKA UKABALEHE/UKAVUNJA UNGO KAMA WEWE NI WA KIKE.
SAUTI YA ALIAE NYIKANI INASIKIKA IKISEMA YANYOOSHENI MAPITO YAKE BWANA ANAKUJA
 
Labda kuna CCM ITASHINDANA HUMUHUMU JF ns chadema. Lakini kwa kura uraiani kule. CCM ITASHINDA NUSU SAA TU BAADA YA VITUO KUFUNGULIWA. VITU AMBAVYO NINAUHAKIKA VITATOKEA 2015
1) CCM ITASHINDA
2) WANA JF wengine hata kura hamtapiga mtakuwa busy kutukana humu wakati wana CCM wakipiga kura
3) Wasio na kazi wataandamana
4) watakaopewa viroba watafanya vurugu na kutakuwa na watu wa kutosha tu kupambana nao walisomea kazi hiyo na wanalipwa kwa kazi hiyo.
UNAYEOTA ENDELEA KUOTA , NJOO NA MIFANO HATA YA KUZIMU. ILA CCM ITASHINDA 2015. HILI SIO LA MJADALA
:bange:Kati ya Wanyiramba wanaoona mwisho wa Pua zao ni pamoja na huyu jamaa Nchemba!!!! Nduguyangu vuvuzela la ccm nchemba, nakushauri uanze kutafuta kazi nyingine ya kufanya kwa vile baada ya 2015 utakuwa kijiweni huna kazi wewe na wenzako wa ccm.Napenda kuku hakikishia kuwa, ndoto ulizoota kushinda ubunge Igunga na Arumeru na bado mkashindwa nakuhakikishia kuwa karata hiyo 2015 ccm itapoteza hivyo hivyo.Ni mara ngapi ulisikika arumeru ukitabiri ccm kushinda na bado utabiri wako ukawa feki.Weka hadharani tujue kuwa wewe ni mganga feki wa ccm unayestahili kunyang'anywa hiyo dili ya kuganga kwa kuwa kila unalolitabiri halitokei!!!! looooooooooo. Achana na hiyo fani ya kucheza na matunguri ina wahusika wake wewe huiwezi.
 
Ccm kufa ni ngumu kwa kuwa hii mijitu ina mbinu nyng co kura pekee, ikikaribia 2015 utackia vitu vyao kwamba Chadema ukanda, udini na vurugu. Mbaya zaidi watu wengi wasioijua ccm vizuri na uchafu wake wanaleweshwa na hoja hewa na kuamua kuwapigia kura.
 
pamoja na kuchukua nchi 2015,tujitahidi kuikaba kila hatua! tuhakikishe kila mtu kwa nafasi yake anaipiga vita ccm na mambo yake yote! juzi magamba wali andaa mkutano pale iringa soko kuu,alienda mwenyekiti wao na wajumbe tu!walijibeba na hapo ni baada ya matangazo kwa mji wote! NAAPA KUICHUKIA ccm(MAGAMBA) NA MAMBO YAKE YOTE!
 
Mbona hili jeneza lao limeshatengenezwa pale Manzese?
View attachment 79022














Ni dhahiri kabisa Kifo kinanukia ndani ya CCM.

Maandiko ya vitabu vitakatifu yanasema kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho. CCM ilianzishwa lazima iwe na mwisho wake. Ni uongo na ujinga kujidanganya kuwa CCM ati itatawala milele. Never ever!

Kina Nepi, Mchembe,Wasiwasihasira(Wassira)na jahazi la waropokaji wa CCM wakae mkao wa kuzika!
Hakuna kitu kitainusuru CCM mwaka 2015. Nasema hivi kwa sababu kuu 7 zifuatazo:

  1. Mwaka 2015 tutakuwa na Katiba Mpya isiyo rafiki wa CCM.
  2. Tutakuwa na Tume Huru ya Uchaguzi(NEC) isiyoteuliwa na Rais wa CCM.
  3. CCM hawatakuwa na mtu mwenye ubavu wa kushindana na mgombea wa CHADEMA maana wote ni mafisadi.
  4. CCM watakuwa hawana pesa za kampeni maana mirija yote ya kuchotea pesa toka BOT(EPA)imeshafungwa.
  5. Watanzania watakuwa wameelimika zaidi kuhusu Raslimali za Taifa kama Gesi,Madini na Hifadhi za Taifa.
  6. Tanzania itakuwa na Vijana wengi zaidi walio wasomi ifikapo 2015 wenye kuchambua mambo kwa kina.
  7. Chuki ya Watanzania dhidi ya CCM itakuwa iko mara dufu kutokana na uonevu inaowafanyia Wananchi.

Poleni sana wana CCM!
 
Labda kuna CCM ITASHINDANA HUMUHUMU JF ns chadema. Lakini kwa kura uraiani kule. CCM ITASHINDA NUSU SAA TU BAADA YA VITUO KUFUNGULIWA. VITU AMBAVYO NINAUHAKIKA VITATOKEA 2015
1) CCM ITASHINDA
2) WANA JF wengine hata kura hamtapiga mtakuwa busy kutukana humu wakati wana CCM wakipiga kura
3) Wasio na kazi wataandamana
4) watakaopewa viroba watafanya vurugu na kutakuwa na watu wa kutosha tu kupambana nao walisomea kazi hiyo na wanalipwa kwa kazi hiyo.
UNAYEOTA ENDELEA KUOTA , NJOO NA MIFANO HATA YA KUZIMU. ILA CCM ITASHINDA 2015. HILI SIO LA MJADALA

Bwana Mwigulu Nchemba,

Wewe ni mmojawapo wa wana-CCM mnaoiharibia CCM credibilty mbele ya Watanzania na mwenzako Nnape Nauye kwasabau ya UROPOKAJI wenu. Mmejitokeza kuwa wasemaji ovyo wa kuongea lolote linalokuja kichwani mwenu bila ya kufikiri madhara yanayoweza kutokana na matamushi yenu. Kauli unazozitoa Bwana Nchemba hakika zinasikitisha na hii inaonekana ni hulka yako uliyozaliwa nayo. Watu husema Tabia haina dawa kwa hiyo Watanzania hawawezi kukusaidia katika hilo.

Juzi nafikiri last week ulinukuliwa na vyombo vya habari ukidai kuwa CHADEMA ni chama cha wauaji na kimepanga kuwaua Watanzania na ukaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa hata ushahidi wa video unao! Mimi nilitegemea siku hiyo baada ya kuongea na media ungelienda moja kwa moja Polisi kupeleka Ushahidi wa video yako ili CDM washtakiwe. Lakini mpaka leo hii kimya!!Sijaskia IGP au Polisi yeyote akihoji tuhuma zako hizo ambazo tunaweza kusema ni nzito!!!

Kwa watu makini wanaweza kuona kabisa kuwa ulichokuwa unaongea na media ni THE COMEDY show. Yaleyale ya Afande Kova na Dr. Ulimboka. Ni vitu planned kati ya CCM, Jeshi la Polisi na UWT-TISS!!!Naweaza kukuhakikishia Bwana Nchemba kwamba huo mpango wa mauaji unaousema ni wa CCM. Najua mna mikakati mliyojiwekea ya kukichafua CDM kwa mbinu chafu ikiwemo MAUAJI yatakayofanywa na CCM,Polisi,UWT na mamluki wa kukodiwa ili baadaye ionekana kuwa mauaji hayo yametekelezwa na CDM!

Nakushauri Bwana Nchemba kuwa hiyo video CD yako ya mauaji toka CDM uiwasilishe Polisi na kama huwezi basi Jeshi la Polisi likukamate na ulazimishwe kukabidhi huo ushahidi kwa Polisi. Failure to which Watanzania wanaona kabisa weye bwana ni mchochezi na ni hatari kwa mstakabali wa amani ya Taifa hili. Watanzania bado wanakumbuka matukio ya mauaji kwenye chaguzi ndogo za Igunga, Arumeru East na huko Ndago kwenye jimbo lako ambako wewe inoanekana kulikuwa na mkono wako na ulishiriki katika mauaji hayo kwa sehemu kama siyo 99.9999%!

Bwana Nchemba nataka ujue kitu kimoja kwamba hii Tanzania si ya kikundi fulani tu au Chama fulani tu. Hii nchi ni yetu sote na Mtanzania yeyote,chama chochote kina haki ya kuongoza nchi hii! Kauli kama ati CCM itatawala milele inaacha maswali mengi sana ndani ya mioyo ya watu! Mtu anayesema hivi inaonyesha tu kwamba swala la DEMOKRASIA halimo kwenye kamusi ya msamiati wake. Kumbuka Wananchi au Watanzania ndiyo wanaoamua nani awaongoze kila baada ya miaka 5. Kuwasemea Watanzania wote kuwa wewe CCM utatawala milele ina maana kuwa wewe ulishapiga kura zako milele na hakuna kitakachobadilisha kura hizo jambo ambalo haliwezekani kwenye nchi yeyote yenye true democracy!!

Inawezekana tu kama CCM muna mbinu chafu ambazo huwa munazitumia kila chaguzi kujihakikishia Ushindi. Na kiukweli ndivyo ilivyo kwa sasa! Lakini naamini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu muumba wa Mbingu na nchi haya mambo yanaenda kumalizwa na KATIBA MPYA. Unless CCM muichakachue hiyo Katiba kwa vile watu husema there is nothing impossible under the sun! Napenda kukuhakikishia kuwa kama Katiba Mpya itakuwa imefuata misingi ya haki ya uundwaji wa hiyo Katiba kwa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi(NEC) ambayo Mwenyekiti na Mkurugenzi wake hawateuliwi na Rais wa CCM basi itakuwa hakuna mlango wa kupitia kwa CCM. Vilevile kama Katiba itakuwa imemwondolea mamlaka makubwa aliyo nayo Rais ya kuteua wakuu wa Idara nyeti kama TISS na Jeshi la Polisi kama ilivyo sasa basi hakutakuwa na kimbilio la CCM kama ilivokuwa 2010.

Naishia hapa kwa sasa.
 
:bange:Kati ya Wanyiramba wanaoona mwisho wa Pua zao ni pamoja na huyu jamaa Nchemba!!!! Nduguyangu vuvuzela la ccm nchemba, nakushauri uanze kutafuta kazi nyingine ya kufanya kwa vile baada ya 2015 utakuwa kijiweni huna kazi wewe na wenzako wa ccm.Napenda kuku hakikishia kuwa, ndoto ulizoota kushinda ubunge Igunga na Arumeru na bado mkashindwa nakuhakikishia kuwa karata hiyo 2015 ccm itapoteza hivyo hivyo.Ni mara ngapi ulisikika arumeru ukitabiri ccm kushinda na bado utabiri wako ukawa feki.Weka hadharani tujue kuwa wewe ni mganga feki wa ccm unayestahili kunyang'anywa hiyo dili ya kuganga kwa kuwa kila unalolitabiri halitokei!!!! looooooooooo. Achana na hiyo fani ya kucheza na matunguri ina wahusika wake wewe huiwezi.

NCHEMBA FANYA MPANGO URUDI BOT ULIPOKUWA,.....NAPE ANZA HARAKATI ZA KURUDI INDIA.....2015 ni mwaka wa mapinduzi halisi...
 
Pole sana kamanda kwa mawazo mgando na ndoto za kusadikika.Nasema hakuna chama kinachoweza kuishinda CCM iwe mwaka 2015 au 2025 au 2035 na kuendelea.Badilisha mawazo yako ili mwaka 2015 CDM itakapopoteza majimbo yake mengi iliyonayo sasa na kuwa kama NCCR usife kwa presha. CCM Jana-CCM Leo -CCM Kesho.

kwa lililotokea jana kweli ccm isife? tazama police ccm walivyo fanya kwa waendesha bodaboda?
 
Ndio kweli kamanda,
CCM IMESHAKUFA TAYARI NA MRATIBU WA MAZISHI NI NDUGU MWIGURU NCHEMBA
 
Ziko dola duniani zilizokuwa na nguvu za kutisha duniani zilianguka na mara zote ni kwa nguzu za makosa yanayofanyika ndani. Ona Mtwara na lindi walivyokuwa royal kwa CCM lakini wamefika mahali wameona CCm haina huruma nao, huruma ya CCM ni wana DSM ambao inawalimbikizia kila kitu hata makao makuu ya nchi ambayo yenyewe iliwahi kusema kuwa ni DOM. Nguvu ya uovu inayopikwa ndani ya CCM huku wana CCM wenyewe wakion ni sawa itaifanya CCM kufunga historia ya vyama Afrika vilivyatafuta uhuru. Hata ganda la karanga litaisukuma CCM na kuanguka nje. Hakuna mwana CCM atakeyokubali ukweli huu kwa hata mgonjwa mahtuti huwa anatazamia maisha ingawa kila kipimo kinaruhusu kufa
 
Mwigulu nchemba jiandae kuwa mpiga kura tu na si mbunge wa wanasingida tena hapo mwaka 2015.
Lipo jembe Dr kitila Mkumbo ndoa atakuwa mbunge wa jimbo hilo
 
Back
Top Bottom