MUIKOMA
Member
- Nov 1, 2011
- 35
- 8
Ndugu wana jamvi leo nalazimika kutoa rai kwa rais wangu mh. Dk. J Kikwete atuepushe na vita au fujo za kudumu pindi chama chake cha mapinduzi kitakapo ondolewa madarakani kwa ridhaa ya watanzania 2015. Natumia busara sana kumuomba jk kwani sina shaka na upande wa dk. W Slaa hasa ukizingatia kuwa amekuwa mpenda amani siku zote na alishawahi kutamka kuwa "sitaki kuingia ikulu huku damu ya watanzania ikiwa imemwagika". Katika hili nina imani kabisa na mh. Kikwete kwamba nae hatataka kuona anakuwa chanzo cha kuwagawa watz na kuzua machafuko. Nakumbuka kauli yake ya kuanza upya si ujinga wakati wa mnyukano wa urais 2005, ningependa kauli yake hii iwaongoze wana CCM wote ili wakijenge chama chetu (CCM) upya. Najua wapambe wa jk hawatataka kukubaliana na hali halisi itakayojitokeza bali kwa Kikwete kukubali japo hatakuwa mgombea nahisi itatuondolea vita kati yetu wenyewe hasa ikizingatiwa kuwa atakuwa bado ni mwenyekiti wa ccm
Si lazima uchangie bali unaweza kutuma salaam hizi kwa mh rais kwa namna utayoona inafaa.
CHONDE CHONDE KUANZA UPYA SI UJINGA.
Si lazima uchangie bali unaweza kutuma salaam hizi kwa mh rais kwa namna utayoona inafaa.
CHONDE CHONDE KUANZA UPYA SI UJINGA.