CCM kitakufa mwaka 2015 na hakitarudi tena

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2011
Posts
789
Reaction score
293
Mwaka 2015 ni mwaka wa CHADEMA kuongoza Nchi hii, Nasema hivo baada ya kufanya tafiti za maeneao mbalimbali hapa Nchini na kugundua wengi wanaunga mkono jitihada za CHADEMA!

CHADEMA ni wembe wa kunyolea tena aina ya wembe unyoleao karatasi Ambao hupatikana viwandani tu na ambao huwa na Makari zaidi ya vipindi vi 4 baada ya kunyoa.

CHADEMA tuna jembe letu Dr SLAA.
CCM MTAMPA NANI? kwani wote wamechafuka na Richmond, Epa, Kagoda,Mapesa ya Uswis, Kutaka kuchakachua Gasi na kuileta Dar es salaam na Bagamoyo. Kwa nini Mnataka kupeleka Gasi Bagamoyo kwa Kikwete? je hao wananchi walopewa neema hiyo baada ya CCM kuaacha bila Barabara, Umeme, Maji na Afya hawafai? Hadi mtake Gasi iende Bagamoyo kwa Kikwete?

CCM mwisho wake ni 2015
Angalia wamepandisha Mafuta ya Taa ili wananchi washindwe kupika vyakula!!!!
Ndio maana nasema mwisho wa Kutawara kwa CCM ni 2015
 
Ccm ni taasisi, hakuna siku itakufa labda siku vyama vya siasa vikifutwa na nchi kutawaliwa kijeshi na mwana ccm. Ngo na vyama vya kufa na kuzikana kama chadema ndivyo vitakufa
 
Pole sana kamanda kwa mawazo mgando na ndoto za kusadikika.Nasema hakuna chama kinachoweza kuishinda CCM iwe mwaka 2015 au 2025 au 2035 na kuendelea.Badilisha mawazo yako ili mwaka 2015 CDM itakapopoteza majimbo yake mengi iliyonayo sasa na kuwa kama NCCR usife kwa presha. CCM Jana-CCM Leo -CCM Kesho.
 
Hakika wewe ni mbumbumbu, hujui usemalo. Nakujibu hivi: Iwapo UNIP ya Kaunda (Zambia), KANU ya Kenyatta/Moi (Kenya), UPC ya Obote (Uganda), kile cha Nkrumah (Ghana), UPRONA cha Rwagasore/Micombero (Burundi) na kile cha Habyarimana(Rwanda) vilirudi kutawala, basi na CCM nayo inaweza ikarudi kutawala. Ni kitu kisichowezekana kutokana na siasa za Kiafrika. Vyama vinapoondoka madarakani huwa vinatokomea nyikani.
 
Ni vizuri kuota lakini isiishie kuota, imarisheni chama hicho mnachodai kinatakiwa kuirithi CCM. Acheni magomvi ya kitoto kila kukicha, jinoeni kwenye itikadi na sera kwani wimbo ufisadi unaanza kupoteza umaarufu. Safisheni chembe za udini, ukanda na unyanyasaji. Bila shaka hapo CCM itakufa lakini kwa sasa tuendelee kupiga soga hapa JF maana naona bado kuna wanonufaika na mifarakano ndani ya CDM hasa babu na demu wake.
 
Mwigulu Nchemba ni suala la muda tu,mkubali mkae ukweli utabaki kuwa huo,baada ya
2015 hii kitu inaitwa ccm itakuwa historia kwenye hii nchi.
 
Hakika wewe ni mbumbumbu, hujui usemalo. Nakujibu hivi: Iwapo UNIP ya Kaunda (Zambia), KANU ya Kenyatta/Moi (Kenya), UPC ya Obote (Uganda), kile cha Nkrumah (Ghana), UPRONA cha Rwagasore/Micombero (Burundi) na kile cha Habyarimana(Rwanda) vilirudi kutawala, basi na CCM nayo inaweza ikarudi kutawala. Ni kitu kisichowezekana kutokana na siasa za Kiafrika. Vyama vinapoondoka madarakani huwa vinatokomea nyikani.

Umewaweza hao magambas kwa mifano hai kabisa. mimi nawachallenji wataje hata chama kimoja hapa barani Afrika kilichoondolewa madarakani na baadaye kikarudi kushika dola -- kwa njia ya kura. Qakitaje ni chama gani. Vyama vya wezi huwa havirudi.
 
Nakwambia kwamba Kama hamuamini subiri 2015.
Wembe ulomnyoa Dr Batrida Burian, Geturda mongera,Hawa Gh"umbi,Antony Dialo Sioi Sumari na wote walokuwa wagombea wa CCM,
Upo:Je mwaujua?
Wembe ni wananchi walochoka na Uchafu wa CCM.Binadamu wamechoka na Danganya toto, Mliwaambia kwamba maisha bora kwa kila Mtanzania , kumbe ni Maisha Bora kwa kira Fisadi? ama ?
Tazameni Gasi mnataka kuileta Dar kufanyaje? wakati wananchi wa Mikoa ya Mtwara na Lindi ni Maskini wa kutupwa
Hivi Lindi na Mtwara hamna wabunge wa kuwatetea? Wabunge wa Mtwara na Lindi Hamwoni GOD BLESS LEMA? anavyo watetea wananchi wa Jimbo la ARUSHA? Ndo maana nasema Mwisho wa CCM ni 2015.
 
Ccm ni taasisi, hakuna siku itakufa labda siku vyama vya siasa vikifutwa na nchi kutawaliwa kijeshi na mwana ccm. Ngo na vyama vya kufa na kuzikana kama chadema ndivyo vitakufa

Majua unatetea tumbo na najua wewe si moja kati ya watu wanaoipenda CCM mawazo yako siku zote unawaza kutumia majeshi kufanya siasa badilika wewe dunia imebadilka (Digital=CDM)
 
Hakika wewe ni mbumbumbu, hujui usemalo. Nakujibu hivi: Iwapo UNIP ya Kaunda (Zambia), KANU ya Kenyatta/Moi (Kenya), UPC ya Obote (Uganda), kile cha Nkrumah (Ghana), UPRONA cha Rwagasore/Micombero (Burundi) na kile cha Habyarimana(Rwanda) vilirudi kutawala, basi na CCM nayo inaweza ikarudi kutawala. Ni kitu kisichowezekana kutokana na siasa za Kiafrika. Vyama vinapoondoka madarakani huwa vinatokomea nyikani.

Ni kweli Na ccm haitakuwa tofauti
 
Kweli Mkuu Zak; Nitaongeza orodha hiyo. Kile chama cha Felix Houphet Boigny (Ivory Coast), chama cha Dawda Jawara (Gambia), cha siaka Stevens (Sierra Leone), cha Mobutu (DRC/Zaire), cha Jaafar Nimeiry (Sudan), cha Sekeu Toure (Guinea), cha Francois Tombalbay (Chad) cha Tafawa balewa (Nigeria)...vyooooote hivyo vilitokomea nyikani kama unavyosema. WHAT IS CCM?
 
Umewaweza hao magambas kwa mifano hai kabisa. mimi nawachallenji wataje hata chama kimoja hapa barani Afrika kilichoondolewa madarakani na baadaye kikarudi kushika dola -- kwa njia ya kura. Qakitaje ni chama gani. Vyama vya wezi huwa havirudi.

Kwa logic hiyo hiyo, akina Wassira wanasema CDM itakufa. Wao pia wanatoa ushahidi wao wakitumia mifano ya NCCR. Ila ukweli unabaki pale pale, CCM haiwezi kujiua yenyewe inahitaji chama madhubuti kuiua na kwa mwendo wa migogoro inayoibuka kila uchwao sioni CCM ikifa ila CDM.
 
Ukweli ni kwamba CCM wenyewe wanalifahamu hilo, na ndiyo maana wanatumia kila mbinu, wizi wa kura, mbeleko ya polisi nk nk kuhakikisha kinabaki madarakani. Lakini iko siku......
 
Kwa logic hiyo hiyo, akina Wassira wanasema CDM itakufa. Wao pia wanatoa ushahidi wao wakitumia mifano ya NCCR. Ila ukweli unabaki pale pale, CCM haiwezi kujiua yenyewe inahitaji chama madhubuti kuiua na kwa mwendo wa migogoro inayoibuka kila uchwao sioni CCM ikifa ila CDM.

Mungu wa Mbinguni atuhuhurumie sana Watanzania 2014/2015, tuondokane na ccm Madikteta.

Amina
 
Ccm ni taasisi, hakuna siku itakufa labda siku vyama vya siasa vikifutwa na nchi kutawaliwa kijeshi na mwana ccm. Ngo na vyama vya kufa na kuzikana kama chadema ndivyo vitakufa
ndio wewe mh mbunge?au hiyo comment haifanani na nyadhifa ulizo nazo,macho yamefunikwa na ukungu na tongotongo nzito mheshimiwa
 
Kwa logic hiyo hiyo, akina Wassira wanasema CDM itakufa. Wao pia wanatoa ushahidi wao wakitumia mifano ya NCCR. Ila ukweli unabaki pale pale, CCM haiwezi kujiua yenyewe inahitaji chama madhubuti kuiua na kwa mwendo wa migogoro inayoibuka kila uchwao sioni CCM ikifa ila CDM.

Wacha porojo: NCCR ilinunuliwa na CCM kwani huoni kiongozi wake aliyeitetemesha CCM sasa anamkampenia JK? Siyo kila chama kinaweza kununuliwa na CCM, mark my words. Mobutu wa Zaire alikuwa anawanunua viongozi wengi wa vyama, na vingine alikuwa anavianzisha mwenyewe. Kiko wapi chama chake sasa?

Bado haujamjibu mtoa mada kwa kutaja chama kilichokuwa madarakani, kikaondolewa na baadaye kikarudi madarakani.
 
Ccm ni taasisi, hakuna siku itakufa labda siku vyama vya siasa vikifutwa na nchi kutawaliwa kijeshi na mwana ccm. Ngo na vyama vya kufa na kuzikana kama chadema ndivyo vitakufa
Nchema unaudhi sana, unadiriki kusema chadema ni chama cha kufa na kuzikana? Kwa hoja zako inaonyesha elimu ya Tz imeshuka sana, kama wewe una first class una argue hivyo, sijui wenye pass wata argue vipi. Huna hoja una argue kama mtu wa mtaani, eti wewe ndie naibu katibu mkuu, kama viongozi ndio nyie sioni kwanini ccm isife
 
Kwa logic hiyo hiyo, akina Wassira wanasema CDM itakufa. Wao pia wanatoa ushahidi wao wakitumia mifano ya NCCR. Ila ukweli unabaki pale pale, CCM haiwezi kujiua yenyewe inahitaji chama madhubuti kuiua na kwa mwendo wa migogoro inayoibuka kila uchwao sioni CCM ikifa ila CDM.
Kuna watu mnaota. Mbona chadema haina mgogoro? Kumfukuza mamluki tena ambaye hana effect yeyote kwenye chama unasema ni mgohoro?
 
Wacha porojo: NCCR ilinunuliwa na CCM kwani huoni kiongozi wake aliyeitetemesha CCM sasa anamkampenia JK? Siyo kila chama kinaweza kununuliwa na CCM, mark my words. Mobutu wa Zaire alikuwa anawanunua viongozi wengi wa vyama, na vingine alikuwa anavianzisha mwenyewe. Kiko wapi chama chake sasa?

Bado haujamjibu mtoa mada kwa kutaja chama kilichokuwa madarakani, kikaondolewa na baadaye kikarudi madarakani.
Mkuu mabadiliko ni kama mafuriko,kamwe hayawezi kuzuiwa na binadamu!
 
Back
Top Bottom