CCM kiboko; Mafuta yameshuka bei:

Serikali yashusha bei ya mafuta Send to a friend
Tuesday, 02 August 2011 20:19
0diggsdigg

Mussa Juma, Dodoma
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeshusha bei za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kunzia leo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Chuo cha VETA mjini hapa, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Haruna Masebu alisema bei ya petroli imeshuka kwa Sh202.37 kwa lita ambayo ni sawa na asilimia 9.17. Dizeli imeshuka kwa Sh173.49 ambayo ni sawa na asilimia 8.32 na mafuta ya taa yameshuka bei kwa 181.37 sawa na asilimia 8.70.

Masebu alisema kutokana na viwango hivyo vipya, bei ya kikomo ya petroli katika jiji la Dar es Salaam itakuwa Sh2,004 kwa lita moja, dizeli Sh1,911 na mafuta ya taa Sh1,905. Jijini Arusha bei ya kikomo itakuwa 2,088 kwa petroli, Sh1,989 kwa mafuta ya taa na Sh1,995 kwa dizeli. Dodoma mjini bei itakuwa Sh2,062 kwa lita moja ya petroli, mafuta ya taa 1,963 na dizeli 1,960.

Alisema kushuka kwa bei hizo kumetokana na kukamilika kwa mchakato wa kuandaa kanuni mpya ya ukokotoaji wa bei za bidhaa za mafuta hasa kutokana na maagizo ya Serikali na pia kubadilika kwa viwango vya kodi katika bidhaa za mafuta.

"Kwa ujumla tozo hizi ni asilimia 2.6 na ilipendekezwa zipunguzwe kwa asilimia 50 lakini sisi baada ya kukokotoa tumepunguza kwa asilimia 51.44," alisema Masebu.

Hata hivyo, alisema kupanda kwa bei ya mafuta kwa kiasi kikubwa, hakutokani na tozo hizo, bali kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na pia kuendelea kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani.

Alisema baada ya kuanza kwa mchakato wa kupitia mabadiliko ya tozo, petroli imeshuka kutoka Sh54 hadi Sh27 kwa lita, mafuta ya taa kutoka Sh54 hadi Sh28 kwa lita na dizeli kutoka Sh55 hadi Sh24 kwa lita.

"Bei hizi zimepungua kwa nchi nzima kuanzia leo na kituo kitakachokutwa kimepandisha bei tofauti na ile ya kikomo faini yake ni Sh3 milioni kwa kila shilingi moja ambayo itakuwa imeongezwa,"alisema Masebu.

Aliwataka watu wanaopata huduma za mafuta kuhakikisha wanapewa risiti katika vituo ili iwe rahisi kuwabana wamiliki wa vituo wenye bei za juu na ambao watabainika.

Kushuka kwa bei hizo kumekuja baada ya serikali kupokea malalamiko mengi ya wananchi kuhusiana na bei za mafuta kuendelea kupanda tofauti na nchi jirani.
HTML:

Bullshit, sasa hapo imeshuka nini. just 100 bob!!!
 
Mchezo huu umenifanya nitafakari mara mbili, CCM wameagiza serikali itafute njia kushusha bei ya Mafuta hasa ya taa, SIKU moja BAADA ya agizo hilo EWURA WAMETANGAZA KUSHUSHA BEI. HUU MCHEZO UNAENDA WAPI?

I beg to differ, CCM waliitaka serekali iangalie upya na kushusha bei ya MAFUTA YA TAA kwakuwa yanatumiwa na watanzania wengi na sio vinginevyo. Haya ya Disel na Petroli yalitakiwa kushushwa tangu Julai 1 baada ya kupunguzwa ka kodi. EWURA walikuwa wakiendelea na mchakato na taarifa yake ndio imetoka. Ni mambo mawili ambayo hayana ushusiano.
 
Mchezo huu umenifanya nitafakari mara mbili, CCM wameagiza serikali itafute njia kushusha bei ya Mafuta hasa ya taa, SIKU moja BAADA ya agizo hilo EWURA WAMETANGAZA KUSHUSHA BEI. HUU MCHEZO UNAENDA WAPI?
<br />
<br />
Hebu tuambie kabla ya kuwakilishwa budget bungeni mafuta yalikuwa yanauzwa bei gani halafu linganisha na hii bei unayosema imeshushwa. Utagundua kwamba mafuta yamepanda hasa ya taa sii kupanda ila yamepaa.
Sii wote tunaoweza kuzugwa na usanii wa serikali ya ccm.
.
 
Mchezo huu umenifanya nitafakari mara mbili, CCM wameagiza serikali itafute njia kushusha bei ya Mafuta hasa ya taa, SIKU moja BAADA ya agizo hilo EWURA WAMETANGAZA KUSHUSHA BEI. HUU MCHEZO UNAENDA WAPI?

CCM nikibokoooooo jamani mpaka mpigiwe kelele na kudokezwa kuwa tuna mpago wa kushusha bei ndio mtoke huko kwenye vikao ndio mseme mbona hamuishinikizi serikali yenu vitu vingine?

Kushuka kwa bei ya mafuta basi ishinikizeni serikali ishushe bei ya bidhaa mbali mbali huko mikoani basi chumvi kwamfano, nauli za mabasi, mkitaka CCM ionekane ni kioboko ishinikize serikali bidhaa nyingi zishuke basi kwa punguzo lililo tolewa jana la mafuta
 
Mbona naona upuuzi tu hapa, yaani huyu anatuambia tangazo la ewura badala ya hali halisi vituoni halafu eti ccm kiboko!, kwanza ewura mi sioni haja yao kuwepo, bei wanazozitoa eti ni elekezi siku zote huwa juu ya hali halisi, hawafanyi udhibiti wa bei hata kidogo. kazi bado tunayo hapa mpaka tutakapopata viongozi wakali
<br />
<br />
Serikali legelege haiwezi kusimamia bei hata siku moja.
 
Hawa ccm wanatuchezea mno, walikaa wataalam wa serikali ya ccm wakaona njia bora ya kuondoa tatizo la uchakachuaji wa mafuta ni kuongeza ushuru wa mafuta ya taa ili bei ipande, halafu walala usingizi wao wakapitisha bungeni wakizani uchaguzi uko mbali. Sasa baada ya Rostam kuachana na siasa uchwara za ccm, wanataka kurusha changa la macho kwa wanaigunga maana wanajua idadi kubwa ya wananchi hao ni watumiaji wa vibatari hivyo kupanda kwa mafuta kumewasababishia maumivu ambayo yatasababisha kura za hasira dhidi ya ccm
 
Bei ya mafuta ya taa ilikuwa 1690, huwezi kuniaminsha kuwa kwa kuwa kati ya tshs 1879-2040 ndo imeshuka, hakuna kitu hapo ni usanii tu na ninashangaa wanahabari kuipa habari hii kichwa cha bei kupungua
 
Kama bei imeshuka mbona wauzaji wamegoma na hakuna anayeweza kusema fyoko!!
 
CCM wanachofanya ni kiini macho; kwa kuwa kuna uchaguzi mdogo wa Igunga itabidi washushe bei ya mafuta ya taa ili wawadanganye wanyamwezi wenzangu wa vijijini ili wawapigie kura. Wao ndo wenye dhamana ya uongozi kupitia chama chao. Kwani nani aliongeza kodi kwenye mafuta hasa ya taa yanayotumiwa na maskini wengi vijijini?
 
Back
Top Bottom